CHADEMA yatangaza kutomtambua John Tendwa

CHADEMA yatangaza kutomtambua John Tendwa

Hivi ni kwamba Dr Slaa ajitambui? au ni hurka tu ndio zinamfanya afanye hayo maamuzi?

Kwa hali tu ya kawaida, huwezi kusema unaitambua ofisi pasipo kumtambua mwenye mamlaka na ofisi husika.

Mbona sheria ipo wazi na imesema kutakuwapo na msajili wa vyama vya siasa, na hili liko wazi kwa sasa ni jaji Tendwa.

Dr Slaa usinifanye niamini kuwa ni ubabu ndio unakupereka puta!
Ni kama HAMY-D inavyotambulika pale Lumumba. Mw...lu ni kama Registrar tu, HAMY-D ni taasisi na sio Mwi..lu
 
anamtambua josephine mshumbuz shemeji yako

Wewe tahira hivi unajua kwamjibu wa taratibu tendwa mkataba wa kuikalia ofisi ya msajiri wa vyama vya siasa ulishaisha kitambo sana...
 
CDM mwaka huu imedhamiria kuwachezesha tikiri ccm,kila kiongoxi ccm atarukaruku kuhusu chadema dahhh cdm daima
 
Wewe tahira hivi unajua kwamjibu wa taratibu tendwa mkataba wa kuikalia ofisi ya msajiri wa vyama vya siasa ulishaisha kitambo sana...

kwani uchaguzi wa cdm ulitishwa lini,huoni na slaa ni yale yale nyani haon ....
 
Chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA kimetangaza kutomtambua msajili wa vyama vya siasa nchini John Tendwa na kusema wao walishamfuta kabla ya yeye hajakifuta chama hicho.

Katibu mkuu wa CHADEMA, Dr. Willbroad Slaa amesema wao hawatishwi na kauli ya msajili John Tendwa ya kukifuta chama hicho maana wao wanaitambua ofisi ya msajili wa vyama vya siasa tu na si John Tendwa.

Amezungumza hayo hii leo jijini Dsm wakati wa uzinduzi wa kongamano la kimataifa la vijana kuhusu demokrasia.



Source: Mimi mwenyewe!

For more info: Tazama HotMix ya EATV!

Tendwa ameshajivua nguo na kudhihirisha alivyo Punguani. HIVI HUYU MTENDWA HATA MKATABA WAKE HUWA HAUISHI, MAANA KAMA MIAKA 60 TAYARI, SI AENDE KUCHUKUA NSSF.

AFRICANS CAANOT RULE THEMSELVES, GIVE THEM A GUN AND THEY WILL KILL EACH OTHER-PW BOTHA-1985
 
Kwasababu Chadema hawamshiriki tena Tendwa katika mambo mengi yanayohusiana na ofisi yake badala yake wanafanya mawasiliano au hata kutuma barua,kupata go-ahead kupitia maofisa ya ofisi ya msajili na sio Tendwa tena.CHADEMA haihitaji tena baraka za Tendwa kufanya mambo yao ikiwemo suala la Red Brigade ila ofisi yake ina taarifa nayo na ilishatoa baraka.Swali lingine?
ukweli ni kuwa Tendwa hapaswi kuendelea kuwepo pale kama msajiri wa vyama vya siasa kwani muda wake ulisha isha siku nyingi sana, ndiyo maana anajikomba komba aendelee kuwepo pale apate pesa ya ulabu...
 
kwani uchaguzi wa cdm ulitishwa lini,huoni na slaa ni yale yale nyani haon ....

wewe huna ruhusa ya kuhoji mambo ya chadema kwa kuwa wewe si mwanachama lakini mtanzania yoyote anayo haki ya kuhoji utendaji wa -------- wenu Tendwa....
 
Dr Yuko sawa.
Tendwa anatumika vibaya.
Alipata aibu sn kule Arumeru alipotumiwa na Lowassa na ccm, pale walipojaribu kuitumia ofisi yake kupandikiza chuki kati ya Wameru na Lema.
Inasikitisha sana kwa umri ule kukosa uamuzi na kupewa maagizo na wanaume wengine.

Khaaaa kwamba Chadema imekuwa appointing authority siku hizi? Nahisi huyu Slaa akili zinamruka. Kichaa kinaanza kupanda. Hajui hata anachoongea. Hili ni janga la taifa.
 
Hivi ni kwamba Dr Slaa ajitambui? au ni hurka tu ndio zinamfanya afanye hayo maamuzi?

Kwa hali tu ya kawaida, huwezi kusema unaitambua ofisi pasipo kumtambua mwenye mamlaka na ofisi husika.

Mbona sheria ipo wazi na imesema kutakuwapo na msajili wa vyama vya siasa, na hili liko wazi kwa sasa ni jaji Tendwa.

Dr Slaa usinifanye niamini kuwa ni ubabu ndio unakupereka puta!
Jaji wa BSS au Maisha Plus? Tendwa amepata lini ujaji?
 
hahahahaha dr slaa kwa kutupa jiwe penyewe lakini na kuhakikishia hili jiwe litawatoa wezi wengi pangoni ni swala la muda tuu, Jiwe amerushiwa Tendwa lakini lazima sisiemu wapige kelele.

Kwakweli hii trick ni nzuri sana
 
Dr Yuko sawa.
Tendwa anatumika vibaya.
Alipata aibu sn kule Arumeru alipotumiwa na Lowassa na ccm, pale walipojaribu kuitumia ofisi yake kupandikiza chuki kati ya Wameru na Lema.
Inasikitisha sana kwa umri ule kukosa uamuzi na kupewa maagizo na wanaume wengine.

Hapooo penye RED. ifike wakati hata kama mtu unalipwa ili uwe na msimamo fulani, basi nawewe uoneshe msimamo wako halisi. naamini kabisa kwamba TENDWA kama angetumia akili yake ya kuzaliwa na elimu yake na busara yake, asingekuwa anafanya na kusema hivyo asemavyo. hivi ni nini bei au gharama ya kuonekana -------- MCHANA KWEUPE, wakati anaonekana kabisa kuwa mtu na heshima zake na familia yake na wajukuu pengine...
 
polisi wameshindwa kuzuwia speed ya mabadiliko tendwa hataweza kamwe speed 120 mpaka kieleweke
 
Tanzania Daima said:
"Kumuendekeza Tendwa kwa kauli zake ni kuliandaa taifa na maafa makubwa kwa kuwa anachoongea hakilingani na hadhi yake ya kuwa mlezi wa vyama vya siasa na katika hili tumeamua kutoshirikiana nae kwa namna yoyote mpaka atakapoomba msamaha na awe amejirekebisha."

Na Abdallah Khamis
KAMATI Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), iliyokutana kwa dharura juzi jijini Dar es Salaam, imeazimia kwa kauli moja kutokufanya kazi na Msajili wa Vyama vya Siasa Nchini, John Tendwa, hadi hapo atakapojirekebisha katika utendaji kazi wake.

Mbali ya Tendwa, kamati hiyo pia imewataka Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk. Emmanuel Nchimbi, Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Saidi Mwema, Mkuu wa Oparesheni wa jeshi hilo, Paul Chagonja, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Faustine Shilogile, na Iringa, Michael Kamuhanda, wachukue hatua ya kuwajibika.
Akisoma tamko la Kamati Kuu lenye maazimio nane mbele ya waandishi wa habari jana, Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, alisema kuwa wamemwandikia barua Rais Jakaya Kikwete juu ya maazimio saba kati ya nane, ambayo yapo katika mamlaka yake ili viongozi hao wakishindwa kuchukua hatua, aingilie kati na kuwafukuza kazi.
Mbowe alisema, kama hali hiyo itashindikana, CHADEMA itawaongoza wananchi kwa njia ya kidemokrasia ikiwemo maandamano ya amani kwa nchi nzima kushinikiza hatua za haraka kuchukuliwa kwa ajili ya kuiokoa nchi.
Aliongeza kuwa katika mfumo wa vyama vingi, viongozi wenye mamlaka ya kiserikali wasipokuwa makini katika kutoa matamko yao wanaweza kuhatarisha usalama wa nchi na kuelezea kauli za Tendwa kuwa haziwezi kuvumiliwa na watu wanaoitakia mema Tanzania.
"Kumuendekeza Tendwa kwa kauli zake ni kuliandaa taifa na maafa makubwa kwa kuwa anachoongea hakilingani na hadhi yake ya kuwa mlezi wa vyama vya siasa na katika hili tumeamua kutoshirikiana naye kwa namna yoyote mpaka atakapoomba msamaha na awe amejirekebisha," alisema Mbowe.
Alisema CHADEMA itaendelea kufuata sheria na iko tayari kukutana na karani katika ofisi ya msajili kuliko kuhudhuria kikao kitakachoitishwa na Tendwa ambaye alimuelezea kuwa anatumiwa au anajipendekeza kwa watawala na kusahau majukumu yake kama mlezi wa vyama vyote.
Alisisitiza kuwa kwa udhaifu unaoonyeshwa na msajili huyo, Kamati Kuu ya CHADEMA imemtangaza kuwa adui namba moja wa demokrasia nchini na kwamba hafai kuwa katika nafasi aliyo nayo.
Kuhusu Dk. Nchimbi, IGP Mwema, Chagonja, Kamuhanda na Shilogile, Mbowe alisema wao wanapaswa kuachia nafasi zao v kwa kuwa mauaji ya mwandishi wa habari, Daudi Mwangosi, na Ally Singano (Nzona) yametokea mikononi mwa jeshi hilo.
Alibainisha kuwa Kamanda Kamuhanda, mkuu wa kikosi cha kutuliza ghasia Morogoro na askari waliohusika katika matukio ya kusababisha vifo katika mikoa ya Iringa na Morogoro, wanapaswa kukamatwa na kufikishwa mahakamani kujibu mashtaka ya mauaji.
Aidha Mbowe, alisema Kamati Kuu imemtaka Rais Kikwete aunde tume huru ya kiuchunguzi ya kimahakama kuchunguza vifo tata vilivyotokea katika mazingira ya kutatanisha katika mikoa ya Tabora (Igunga), Arusha (Mjini na Arumeru), Singida, Morogoro na Iringa.
Alisema Kamati Kuu inalihimiza Jeshi la Polisi kusimamia haki, kufuata na kuheshimu sheria zinazoongoza shughuli za vyama vya siasa ikiwemo kifungu cha 11 cha sheria ya vyama vya siasa inayotoa fursa kamili kwa vyama vyote kufanya mikutano na maandamano kama sehemu ya ujenzi na uenezi wa kazi za siasa.
Kuhusu Shirika la Utangazi la Taifa (TBC) lenye vituo vya redio na televisheni, Mbowe alisema Kamati Kuu imetangaza mgogoro na taasisi hiyo na kuwataka wanachama wake na wapenda haki kuvisusia kwa kutotazama vipindi vyake na kuvipa matangazo akisema vimeshindwa kutenda haki licha ya kutumia kodi ya Watanzania wote.
Alisema vyombo vya umma vinapaswa kutenda haki kwa kuripoti taarifa bila upendeleo wowote kwa kutumia weledi wa kiuandishi na kwamba TBC imeshindwa kazi hiyo kwa kuwa mpiga kinanda wa shughuli za CCM.
Watimua Madiwani
Wakati huo huo, Kamati Kuu hiyo imewavua uanachama madiwani wawili wa chama hicho mkoani Mwanza kwa tuhuma za kujihusisha na vitendo vya ufisadi.
Madiwani waliovuliwa uanachama ni Adams Chagulani wa Kata ya Igoma na Henry Mattaka wa Kata ya Kitangiri, wakidaiwa kukiuka katiba, kanuni na maadili ya chama.
Mbowe alisema, baada ya Kamati Kuu kupokea taarifa ya kamati iliyoundwa kuchunguza chanzo cha mgogoro mkoani Mwanza, wamejiridhisha kuwa wanachama hao wanastahili kuondolewa katika chama.
"Wahusika walishapewa onyo kabla ya hatua za jana na walikuwa chini ya uangalizi kabla ya hatua kuchukuliwa na tuliwapa nafasi ya kujieleza," alisema Mbowe.
Alifafanua kuwa kamati ya uongozi ya mkoa wa Mwanza nayo imevunjwa kutokana na kushindwa kutimiza wajibu wake ipasavyo na kwamba itaundwa nyingine kadiri ya mahitaji.
Aliongeza kuwa kutimuliwa kwa wanachama hao iwe ni onyo kwa wanachama na viongozi wengine wa CHADEMA kuwa hawataweza kuvumiliwa wakikiuka maadili.
M4C kuendelea
Katika hatua nyingine, Mbowe alisema kuwa operesheni yao ya M4C haitasitishwa bali itaendelea nchi nzima licha ya kudaiwa kuwa kuna mkakati wa makusudi wa kuikwamisha.
Alisema yaliyotokea katika mikoa ya Morogoro na Iringa ni sehemu ya mikakati hiyo na kwamba wamejizatiti kuhakikisha hilo haliwakwazi kwa kufanya kazi ya ujenzi wa chama zaidi.
Mzee wa upako anena
Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC), Ubungo Kibangu, Antony Lusekelo, maarufu kama Mzee wa Upako, amesema kuwa umwagaji damu unaoendelea unatokana na shinikizo kutoka kwa baadhi ya wanasiasaa nchini kushindwa kujenga hoja dhidi ya CHADEMA.
Akizungumza na Tanzania Daima jana jijini Dar es Salaam, Lusekelo alisema kuwa anaamini kuwa polisi hao hawafanyi kazi hiyo kwa utashi wao bali wanatumiwa na wanasiasa.
Alisema kuwa wanasiasa hao baada ya kubaini kuwa wameishiwa hoja sasa wamedhamiria kutumia jeshi hilo ili kuhakikisha CHADEMA inafutika katika ulimwengu wa siasa kama ilivyotokea kwa vyama vingine.
"Nina imani kuwa polisi hawafanyi mauaji hayo kwa matakwa yao, bali inawezekana kabisa kuna shinikizo la wanasiasa ambao wameishiwa hoja na sasa wameamua kulitumia jeshi hilo pasipo kujua kuwa hiyo ni hatari kwa mustakabali wa nchi," alisema.
Lusekelo alisema kuwa damu ya Mwangosi haiwezi kuwaacha salama kwani kuna uwezekano mkubwa wa CCM kuondoka madarakani mwaka 2015.
Alinukuu maandiko matakatifu akisema kuwa katika amri 10 za Mungu inakatazwa kuua, hivyo hatua ya kumuua Mwangosi ni kwenda kinyume na maandiko hayo.
Aliongeza kuwa iwapo viongozi wetu wangekuwa wanafuata masuala ya uwajibikaji, Waziri Nchimbi na IGP Mwema wangeweza kujiuzulu.
Jamani tendwa alisha tendwa siku nyingi na chadema, mwacheni ajifie kimya kimya...
 
khaaaa kwamba chadema imekuwa appointing authority siku hizi? Nahisi huyu slaa akili zinamruka. kichaa kinaanza kupanda. hajui hata anachoongea. Hili ni janga la taifa.

hahaha sasa hapa nani kichaa? Jiwe limerushwa kwa tendwa wewe unahamaki nini? Tendwa amefutwa rasmi
 
Back
Top Bottom