CHADEMA watashiriki Uchaguzi Mkuu wa 2025 bila katiba mpya

Jibu ktk maelezo yako yapo ktk nukuu yako hii "Ukitaka kuwa masikini nchi hii, danganywa kwenda kulima. Utalima kwa gharama zako lakini wakati wa kuuza utapangiwa bei na anayeishi mjini"

Nami nakazia tu kuwa ukitaka kudanganywa kushinda kiti cha Urais kuwa na wanachama wengi mijini tu, halafu ukose kujulikana na ukose wanachama vijijini. Hata kwa kupata katiba mpya haitasaidia.
Ruzuku za mbolea vijijini utaziita HONGGO NA RUSHWA, ujenzi wa zahanati na madarasa vijijini utaita matope n.k
Hao mliokuwa mnaona ni mtaji wenu huko vijijini walimalizika baada ya TV na internet kuingia. Kizazi hiki sio kile cha zamani kilichokuwa kinaona mbolea na zahanati nyingi hisani ya serikali. Kwa taarifa yako hata ikiingia serikali ya kijeshi, itajenga zahanati, shule, kupeleka mbolea nk maana huo ni wajibu wa serikali inayokusanya kodi.

Mngekuwa mnategemea kura za huko vijijini tusingeona chaguzi za kihayawani vile. Danganyeni wajinga sio werevu.
 
Hahahaaaaa! Si nyie ndio mlikuwa mnapiga picha watoto wa shule msingi wakisomea chini ya miti huku mvua ikinyesha. Hivi kodi zilikuwa hazikusanywi? Mtaji huu kama hoja ya kuwaingiza IKULU hautajitokeza tena. Poleni!
Bwawa la umeme la Nyerere si ni mpango uliokuwepo toka enzi za Nyerere- Hivi wakati wote kodi zilikuwa hazipo. Fly over hizo nazo, Daraja la Busisi, SGR, N.K. Hivi huko nyuma kodi hazikuwepo? Jamani anayestahili, mpeni maua yake! Msiwe na choyo.
TV na internet vijijini bado sana. Simu huko vijijini hutumika sana katika sms, m-pesa, tigo/halo-pesa. Bando la Internet kama mjini mnalalamika unafikiri vijijini wanalo la kusikiliza hotuba ya kuboa ya LISSU, Dr Slaa n.k? Mnajidanganya mchana kweupeeeee!
 
Chadema wanafeli kwenye Suala la Matumizi ya fedha na namna ya kuhamasisha upatikanaji Wa fedha Kwa ajili ya watu Wa Chini yaani wale viongozi Wa matawi ya Chini au mitaa.

Bila fedha hakuna ushindi popote Kwa Karne hii. Hata Vita bila fedha hakuna ushindi. Mbele ya fedha Hata nchi imepigwa Bei.
Pesa ni Kila Kitu. Hata Uzalendo Kwa Sasa unahitaji fedha.

CCM walionufaika sana na kifo cha Ndesamburo mana alikua ndiye nguzo kubwa ya Chadema ukanda Wa Kaskazini. Alikua anauwezo Wa kugharamikia shughuli Zote za chama na kuzuia wasaliti kununuliwa na CCM.

Sasa cha KUFANYA ni Chadema kuwakubali Wazalendo wote popote walipo.
Pili kufanya uhakiki Wa Wanachama wao NDANI na nje ya nchi. Kuwajua Kwa majina na Kwa idadi Yao. Kuwapanga Wanachama Kwa makundi na Kwa Uwezo wao .

Baada ya kuwajua Wanachama Wa Chadema waliopo tayari Kupinga ukiukwaji Wa Sheria za uchaguzi Sasa waanze kuhamasisha michango KUANZIA wenye uwezo Wa kuchangia elfu moja mpaka million Kumi .
Kama Chadema itaweka watu waaminifu kukusanya michango bila tamaa kama zile za CCM basi Kwa Miezi Kumi na moja kufikia uchaguzi wa Serikali za mitaa watakua wamekusanya zaidí ya bil.20.

Pesa hizo zisikae makao makuu mana ni za Wananchi . Zitumike kuwagharamikia wagombea wote Wa Serikali za mitaa nchi Nzima. Hawa wagombea Wa Chini wakipatikana Kwa Wingi basi ni rahisi kuwapanga Wanachama kuelekea uchaguzi mkuu Wa wabunge na madiwani ambao kimsingi wanahitajika kupata hamasa ya kukabiliana na wagombea Katili na wenye fedha wa CCM.

Na KUANZIA Sasa Chadema inapaswa kuwasaidia wale wote wanaopingwa na CCM Kama akina Dr. Slaa, Mwabukusi, Shivj, Mbatia, pia wale waliopo kuwaunga mkono au kuwakaribisha wale wanCCM wachache sana ambao Kwa dhahiri Wanapinga nchi kukabidhiwa Kwa wakoloni Kwa mgongo Wa Nyuma.

Chadema ikiendelea kuangalia uchaguzi Wa wabunge na madiwani tuu watapoteza uchaguzi mkuu Hata kama watashinda. Hakuna watu Wa kuhamasisha maandamano nchi Nzima kuanzia vijijini.

Pia ni vyema wakaanzisha será ya kuwalipa pesa za vikao wenyeviti Wa mitaa Ili kuwapa Nguvu na moyo Wa kujitoa .
Mkuu '1000Digits', nimekusoma kwa uangalifu mkubwa sana hadi mwisho wa andiko lako, na ni nadra sana kwangu kutaka kurudia nilichosoma mara ya kwanza (huwa nasoma kwa spidi kubwa sana), ili niliyoyasoma kwa mara ya kwanza yaniingie vizuri akilini.

Sasa niseme, ninakubaliana nawe kwa ujumla. Kilichonifanya kusita kwa mara ya kwanza ni hayo maswala ya 'Hela'; siyo hela za kuwalipa wanachama huko matawini wanaofanya kazi kubwa sana; ni swala la "HELA" kuifanya kuwa rushwa katika uchaguzi.
Lakini hata hili, kwa wakati huu tuliomo, na hasa baada ya kuona CCM wanavyoitumia njia hiyo kuvuruga chaguzi ndani ya nchi hii, inanilazimu pia nilifumbie macho kama CHADEMA watahitaji kufanya hivyo ili kuwaondoa CCM madarakani.

Ninakubaliana nawe moja kwa moja, kuhusu CHADEMA kutafuta pesa za kuwasaidia katika chaguzi hizi, lakini isiwe ni kwa kuuza hisa za chama kwa wenye uwezo mkubwa wa pesa kwa mategemeo ya kuvuna baada ya CHADEMA kuingia madarakani.

Kwa hiyo, niseme hapa wazi, kwamba ninaungana nawe, na ninawasihi CHADEMA kuanzia sasa watafute vyanzo vya kuingiza pesa ndani ya chama kwa lengo la kufanikisha chaguzi zinazokuja karibuni. Ninakubaliana nawe pia, kwamba, pamoja na kuwahamasisha wanachama wao na viongozi wao huko mashinani, ni muhimu sana kuwapa motisha wafanye kazi zao kwa ufanisi zaidi huko kwenye ngazi za chini, kwa kuwawezesha kulipia mahitaji yao muhimu.

Mawazo haya yote ni sehemu ya mchango kwa chama hiki ili kiweze kufanikiwa zaidi katika shughuli yao kubwa ya kuiondoa madarakani CCM.
 
Hahahaaaaa! Si nyie ndio mlikuwa mnapiga picha watoto wa shule msingi wakisomea chini ya miti huku mvua ikinyesha. Hivi kodi zilikuwa hazikusanywi? Mtaji huu kama hoja ya kuwaingiza IKULU hautajitokeza tena. Poleni!
Bwawa la umeme la Nyerere si ni mpango uliokuwepo toka enzi za Nyerere- Hivi wakati wote kodi zilikuwa hazipo. Fly over hizo nazo, Daraja la Busisi, SGR, N.K. Hivi huko nyuma kodi hazikuwepo? Jamani anayestahili, mpeni maua yake! Msiwe na choyo.
TV na internet vijijini bado sana. Simu huko vijijini hutumika sana katika sms, m-pesa, tigo/halo-pesa. Bando la Internet kama mjini mnalalamika unafikiri vijijini wanalo la kusikiliza hotuba ya kuboa ya LISSU, Dr Slaa n.k? Mnajidanganya mchana kweupeeeee!
Nisikilize boss, haya wanayofanya CCM ni wajibu sio hisani, na yoyote atakayeingia madarakani anapaswa kutekeleza, tena kwa speed kubwa katika kuliko hiyo ya CCM. Kizazi limebadilika na CCM sio chama cha kizazi hiki. Hao wajinga wa kuamini kuwa wajibu wa serikali unaweza kutekelezwa na CCM tu walishazeeka. Kizazi hiki kinataka ladha mpya na sio utawala wa shuruti na mazoea.

Huo ujinga kuwa nchi inaweza kujengwa na chama fulani tu, pia KANU ya Kenya waliaminisha watu hivyo, na kuwaburuza watakavyo, leo hii KANU ni marehemu wa muda mrefu, na bado Kenya ina uchumi mzuri kuliko sisi makondoo wa Tanzania. Zama za CCM zilishapita, chama chochote kinaweza kujenga shule, vituo vya afya, barabara nk. Kama CCM ingekuwa na mtaji huo wa wajinga tusingeshuhudia chaguzi za kihayawani vile ili CCM watangazwe washindi kwa shuruti.
 
Binafsi sioni dalili ya kupata katiba mpya au tume huru ya uchaguzi sioni kabisa muamko wa wananchi kujitokeza kupiga kura kama vyama vya upinzani wataingia kwenye uchaguzi huu wategemee kupatiwa wabunge wa hisani
 
Back
Top Bottom