Jaji Warioba: Suala la Katiba Mpya limalizike kabla ya uchaguzi mkuu wa 2025

Sir luta

Senior Member
Nov 28, 2022
148
209
Muda huu aliyekuwa Waziri Mkuu Jaji Warioba anafanya mahojiano katika kipindi Cha dk 45 ITV na mapendekezo yake ni kuwa katiba mpya ipatikane kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.

My take; kama tunawaheshimu hawa wazee tuheshimu kwanza maoni na maono Yao. Ikumbukwe ndiye alikusanya maoni ya wananchi kuhusu upatikanaji wa katiba mpya.
---

Ninachoamini, ni kwamba , kuna umuhimu wakufanya mabadiliko kwenye katiba,huo umuhimu upo

La pili ambalo, wananchi walizungumzia sana, ni mgawanyo wa madaraka, kwanza kati ya wananchi na uongozi.

Matatizo tunayafahamu yako wapi katika kubadili Katiba,...tujadiliane tufikie uamuzi, na sio suala rahisi, ni gumu lakini viongozi wakae

Hata hawa viongozi, sio wote wanaijua

Viongozi wakae na kuwaonyesha njia wananchi

Tuwe na kampeni ya miaka mitatu ya maendeleo badala ya kampeni ya katiba, elimu ya katiba ilikwisha tolewa, wananchi wanajua changamoto zao

Kuna sheria nyingi sana zinazowahusu wananchi hata kama hawazijui, hata kwenye uelewa wa katiba ni hivyohivyo, inaweza kupatikana hata kama walio wengi hawaijui lakini wanaweza kuifuata

Wananchi hawana mipaka, wanajua haki za uraia wao, wanashirikiana kila upande, kwa wananchi muungano upo imara, tatizo lipo kwa viongozi wetu

Viongozi wanapaswa kuitazama nchi kwa upana, kuna mambo mengi ambayo wananchi hushirikishwa baada ya viongozi kufanya maamuzi

Kuna mambo ukiyatazama unaona kabisa yataipeleka nchi pabaya hata kama yanafanywa na sisi viongozi

Tume ya Jaji warioba ilitoa elimu kubwa sana, kwanza ilipeleka nakala za katiba nchi nzima,na kila kwenye mkutano wajumbe wa tume walikuwa wanaeleza misingi ya katiba

Viongozi wote wanazijua kero za Muungano, tatizo lipo kwenye utaratibu wa kufikia maamuzi

Wapo viongozi hawapendi mabadiliko, wapo wanaodhani hoja ya katiba mpya ni kwa ajili ya kuiondoa serikali iliyopo madarakani

Tume ya Jaji Warioba ilishatoa mapendekezo yake, viongozi wataona wenyewe wayafanye nini

Tunahitaji mabadiliko ya Katiba mpya

Kupata katiba mpya hakuhitaji idhini ya rais kwasababu katiba ni ya wananchi, wananchi wakiamua wameamua,wala rais hatii saini

Kama tukifika 2025 bila katiba mpya, viongozi wategemee suala la katiba mpya litachukua mjadala mkubwa sana

Hata kama kusingekuwepo na mchakato wa katiba mpya lakini kwa mapungufu tuliyoyaona hivi karibuni suala la katiba mpya halikwepeki ili haki ya wananchi ionekane

Sheria ya uchaguzi nia yake ni kumuwezesha wananchi kupiga kura ili yule waliyemchagua awe kiongozi wao na si vinginevyo

Huwezi kuwa kwenye misingi ya kidemokrasia alafu ukawa na katiba tofauti na nchi zinazofuata misingi ya kidemokrasia

Haya yanayoendelea sasa yana dalili za kutugawa
 
Muda huu aliyekuwa waziri mkuu Jaji Warioba anafanya mahojiano katika kipindi Cha dk 45 ITV na mapendekezo yake ni kuwa katiba mpya ipatikane kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.

My take; kama tunawaheshimu hawa wazee tuheshimu kwanza maoni na maono Yao. Ikumbukwe ndiye alikusanya maoni ya wananchi kuhusu upatikanaji wa katiba mpya.
Mzee ana hoja. Asikilizwe
 
Kwa wasojua uzito wa Mzee Warioba Nchi hii na nafasi aliyonayo mioyoni mwa watz watabisha.

Ila tunaoelewa,

Ndivyo ilivyo na itakuwa hivyo.

Amen
 
Hii iliyopo si aliiandika yeye tena akiwa AG alisahau kipengele gani?
 
Muda huu aliyekuwa waziri mkuu Jaji Warioba anafanya mahojiano katika kipindi Cha dk 45 ITV na mapendekezo yake ni kuwa katiba mpya ipatikane kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.

My take; kama tunawaheshimu hawa wazee tuheshimu kwanza maoni na maono Yao. Ikumbukwe ndiye alikusanya maoni ya wananchi kuhusu upatikanaji wa katiba mpya.
Heshima sana kwa Mzee Warioba, lakini hata yeye anajua wazi kwamba hilo CCM imekwishalikataa, haliwezekani tena.
Hata Mwenyekiti wa chama hicho kishasema "miaka mitatu ya mafunzo ya katiba" ndilo chama hicho kimekwisha liamua liwe.
Mzee shapuuzwa siku nyingi sana ndani ya chama chake; na hana mapendekezo yoyote ya kuwafanya/kuwalazimisha wabadili msimamo wao.

Kwa hiyo hili, aachane nalo. Yeye kuendelea kulishikilia halibadili kitu chochote.

Kama anaweza, sasa hivi ahimize tu kufanyike mabadiliko ya sheria mbalimbali zinazohusu uchaguzi.
Na awaeleze waTanzania wote umuhimu wa kushiriki kwenye chaguzi zote zitakazofuata.
 
Muda huu aliyekuwa waziri mkuu Jaji Warioba anafanya mahojiano katika kipindi Cha dk 45 ITV na mapendekezo yake ni kuwa katiba mpya ipatikane kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.

My take; kama tunawaheshimu hawa wazee tuheshimu kwanza maoni na maono Yao. Ikumbukwe ndiye alikusanya maoni ya wananchi kuhusu upatikanaji wa katiba mpya.
Huyu mzee alindwe , wasije kusema naye kang'atwa na Mbwa kama Kingunge
 
Back
Top Bottom