CHADEMA vs CCM: Nani Mbabaishaji?

Eh!!! Kumbe CHADEMA mkwara wote huo chadema ni CCM B!!! nimwage data?

Waridi, je hiki ni kisasi baada ya NCCR kuitwa CCM B? Mbona walioita hivyo si washabiki wa CHADEMA? Je, chama chenye msimamo kama huu kinaweza kuwa CCM B? naona ukieendelea kuitetea NCCR juu ya kashfa yake ya kupewa fedha za EPA badala ya kuanza kuishambulia CHADEMA. Nakumbuka NCCR mliwahi kuja Zanzibar kuiwekea pingamizi CUF naona mmefanya hivyo tena Tarime lakini mkaumbuka.

CHADEMA: Hatutakoma
na Mwandishi Wetu

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesema kamwe hakitaacha kumkosoa Rais Jakaya Kikwete na serikali yake katika mambo ambayo hafanyi vizuri, sambamba na kuwataka Watanzania wasimchague kuwa rais katika uchaguzi wa mwaka 2010, kwa sababu zipo dalili za wazi zinazoonyeha kuwa utawala umemshinda.

Kimesema kauli ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) iliyotangazwa juzi na Katibu wa Itikadi na Uenezi, John Chiligati, kuwa kauli zinazotolewa na Mwenyekiti wa Taifa wa CHADEMA, Freeman Mbowe, kuhusu uwezo wa Rais Kikwete kuongoza nchi zinalenga kumdhalilisha, haikubaliki kwa sababu inapingana na wosia wa muasisi wa chama hicho, hayati Mwalimu Julius Nyerere, ambaye chama hicho kimekuwa kikihubiri kumuenzi.

Msimamo huo wa CHADEMA dhidi ya kauli ya CCM ulitolewa jana na viongozi wawili wa chama hicho.

Wa kwanza kueleza msimamo huo alikuwa Mbowe wakati akihutubia mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Kibara uliofanyika jana kwenye mfululizo wa mikutano ya CHADEMA.

Mbowe alisema amefikia uamuzi huo baada ya kauli ya kejeli iliyotolewa juzi na John Chiligati kuwa anawapotosha Watanzania.

"Napenda kumwambia Rais Jakaya Kikwete kwamba simuogopi, nitaendelea kumkosa hadi siku ya mwisho ya utawala wake, lakini namheshimu kama rais wangu wa nchi… hatukubali kuona taifa linapotea huku tukiwa kimya, hiyo itakuwa si kazi ya vyama vya upinzani," alisema Mbowe.

Alisema kutokana na dhamira yake ya kuwakomboa Watanzania, hatakuwa tayari kucheka na kiongozi yeyote wa chama tawala huku wananchi wakiendelea kutaabika bila msaada kutoka serikalini.

"Siko tayari kuchekea kiongozi yeyote wakati hali za wananchi wetu zinazidi kuwa mbaya kila kukicha, kila kona unayopita wananchi wanalia hali ngumu ya umaskini," alisema Mbowe.

Alisema moto uliowashwa na chama chake utaendelea kuwaka hadi kieleweke na kuridhika kuwa nchi inabadilika na kurudi kama ilivyokuwa kwa muasisi wa taifa, hayati Mwalimu Julius Nyerere.

Mbowe alitumia fursa hiyo pia kuwatumia salamu, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, John Chiligati kwamba atabanana nao hadi mwaka 2010 wakati wa uchaguzi mkuu.

"Natumia nafasi hii kuwatumia salamu, Waziri Mkuu, Pinda, Makamba na Chiligati kwamba nitaendelea kupambana nao tu.... nasema kwamba hawa ninao tu ndugu zangu," alisema Mbowe.

Aliishutumu CCM kuwa kipindi kirefu imekuwa haitaki kuambiwa ukweli kutokana na makosa mengi inayofanya tangu taifa lilipojipatia uhuru mwaka 1961.

"CCM imekuwa bingwa wa kukutaa kukosolewa pale inapofanya makosa...imegeuza Watanzania kuwa kitega uchumi chao huku wakibaki maskini wa kutupwa, angalieni leo hapa Mwibara mmeshindwa hata kuvua samaki," alisema.

Kwamba hali ya umaskini imesababisha wananchi wengi wa Kanda ya Ziwa kula mabaki ya samaki, maarufu kwa jina la ‘mapanki' huku minofu yake ikisafirishwa kwenda nchi za Ulaya.

Akisisitiza msimamo wake wa kuendelea kuwakosoa viongozi walioko madarakani, alisema kutokana na serikali kupoteza mwelekeo, wafanyakazi wa serikali wakiwemo walimu wana haki ya kugoma na kudai masilahi yao kwa nguvu zote kwasababu ni haki yao ya msingi.

Wa pili alikuwa Mkurugenzi wa Vijana wa chama hicho, John Mnyika, alipozungumza na Tanzania Daima Jumapili kupitia simu yake ya kiganjani kuhusu msimamo wa chama hicho baada ya Mwenyekiti wake, Mbowe kushambuliwa na CCM kwa kauli zake dhidi ya Rais Kikwete.

Akiongea kwa sauti kali, Mnyika alisema kamwe CHADEMA haitaacha kutoa kilio cha umma na kwamba viongozi wa chama hicho wako tayari kukamatwa na hata kufungwa gerezani kwa ajili ya kutetea wanyonge.

Alisema kauli za CCM hazitawatikisa CHADEMA wala kuwanyamazisha kwa vile wanatambua kuwa mara nyingi viongozi wanaoshindwa kujibu hoja hutumia mamlaka yao kuwanyamazisha wananchi wenye hoja za msingi za kukosoa watawala.

Alitoa mfano kuwa hata Rais wa Kwanza wa Tanzania, hayati Julius Nyerere aliwahi kushitakiwa na serikali ya kikoloni kwa kusema ukweli ambao ulitafsiriwa na watawala hao kuwa ni uchochezi.

Mnyika, alisema kauli zinazotolewa na Mbowe kuhusu uongozi wa Rais Kikwete ni kauli za umma na kwamba zina ukweli ambao unasemwa na wananchi walioelemewa na ugumu wa maisha, wakiwemo wasomi, wanaharakati na viongozi wa dini.

"Heshima ya kiongozi inalindwa na matendo yake, wapo Watanzania wanaoona kwamba Rais Kikwete anashindwa kuchukua hatua dhidi ya mafisadi na kutekeleza ahadi alizotoa, ndiyo maana wanamsema.

"CCM wameanza kutaharuki kutokana na Operesheni Sangara kwa kuwa ufisadi unaotajwa unaigusa CCM na baadhi ya viongozi wake. Wananchi wameanza kupinga hali hiyo, jambo ambalo halikutarajiwa na viongozi wa CCM, ndiyo maana wameanza kuhaha," alisema Mnyika.

Mnyika alimtaka Chiligati kuacha kutoa kauli zinazolenga kumpotosha Rais Kikwete na kwenda katika mwenendo anaoutaka rais, wa kukosolewa na kushauriwa kila inapobidi.

Alisema kauli ya Chiligati ya kumpamba Rais Kikwete hata katika mambo anayoonekana hajafanya vizuri na Watanzania anaowaongoza wananung'unika, zinaweza kuzaa udikteta wa kukwepa kubadilika.

"CCM inaelekea kwenye kuminya fikra mbadala; ililifungia gazeti la MwanaHalisi kwa sababu ambazo hadi sasa zinatia shaka miongoni mwa Watanzania na sasa imemkemea Mbowe ambaye anazungumza kile kilichopo. Hali ikiendelea hivi, itageuka kwa wakosoaji wengine. CHADEMA tunasema CCM, na hasa Chiligati, wasome wosia wa Julius Nyerere ‘tujirekebishe' utawasaidia kukubali kukosolewa," alisema Mnyika.

Alimtaka Chiligati aache kupoteza muda kufanya propanda za kisiasa, badala yake aeleze hatua alizowachukulia watu walio katika orodha ya mafisadi katika Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, anayoingoza, ambayo alikabidhiwa na mtangulizi wake.

Kauli hiyo ya Mnyika imetolewa siku moja baada ya CCM kueleza kukasirishwa, kukerwa na kusikitishwa na kauli ya hivi karibu ya Mbowe ya kumshutumu Rais Kikwete kuhusu uwezo wake wa kuongoza kuwa zinaonyesha kumdhalilisha na kumkosea adabu na heshima mkuu wa nchi.

Tamko hilo la CCM lilionekana kama kujibu mapigo dhidi ya kauli ya Mbowe kwa Rais Kikwete; lilikwenda mbali zaidi kwa kumkejeli na kumdharau Mbowe, kwa kumhusisha na upigaji disko na uchezaji wa kamari.
 
Waridi, je hiki ni kisasi baada ya NCCR kuitwa CCM B? Mbona walioita hivyo si washabiki wa CHADEMA? Je, chama chenye msimamo kama huu kinaweza kuwa CCM B? naona ukieendelea kuitetea NCCR juu ya kashfa yake ya kupewa fedha za EPA badala ya kuanza kuishambulia CHADEMA. Nakumbuka NCCR mliwahi kuja Zanzibar kuiwekea pingamizi CUF naona mmefanya hivyo tena Tarime lakini mkaumbuka.

Asha,
Nikimwaga data utaujua ukweli nao ukweli utakuweka huru. kasirikeni kisawasawa kwanza kabla sijalipua bomu
 
Eh!!! Kumbe CHADEMA mkwara wote huo chadema ni CCM B!!! nimwage data?
Dada Waridi,

Itapendeza ukiandika hoja moja kwa moja kuliko hivi unavyofanya. Kama ni joke basi naomba topic ihamie sehemu husika. Lete data acha utani!
 
Waridi, je hiki ni kisasi baada ya NCCR kuitwa CCM B? Mbona walioita hivyo si washabiki wa CHADEMA? Je, chama chenye msimamo kama huu kinaweza kuwa CCM B? naona ukieendelea kuitetea NCCR juu ya kashfa yake ya kupewa fedha za EPA badala ya kuanza kuishambulia CHADEMA. Nakumbuka NCCR mliwahi kuja Zanzibar kuiwekea pingamizi CUF naona mmefanya hivyo tena Tarime lakini mkaumbuka.

alaa, kumbe huyu waridi ndio wale wale mamluki wa demokrasia!!!
ahsante sana bi.asha, mi nilikuwa sijamfahamu ati!!!!
sasa nimemgundua, hana data yoyote isipokuwa anataka kuanzisha majungu, maana hawa NCCR ni kawaida yao kupika majungu na fitna dhidi ya vyama mbadala.wao wamechoka sana kiasi kwamba kadri siku zinavyosogea ndivyo wanazidi kufutika kwenye ramani.
hebu waridi badala ya kupoteza muda kupiga majungu,jipangeni upya ili muweze angalau kurudisha heshima na hadhi ya chama chenu.
 
Dada Waridi,

Itapendeza ukiandika hoja moja kwa moja kuliko hivi unavyofanya. Kama ni joke basi naomba topic ihamie sehemu husika. Lete data acha utani!

Invisible,
Una haki ya kunidai data, get ready.. lakini wakati huo huo nakuomba utafakari ni kwa nini hata kabla sijaleta data watu washarukia eti ni NCCR inataka kulipa kisasi. Hapa JF kama kweli kuna watetezi wa haki basi idaini CHADEMA nayo ilete ushahidi wa madai yake kwamba NCCR ni CCM B. za kwangu naleta, wala usihofu,ila nina maana yangu kuwaulizeni kwanza
 
Dada waridi,

Mimi sina ubaya na allegations wanazorushiana vyama, ila topic ikianza ikiwa fupi hivi inakuwa inachanganya sana. Aidha, hata majibu ya Asha ya kuihusisha NCCR na CCM inanifanya nicheke tu, yani mnaifanya topic ionekane ya kidaku kwani uthibitisho wa kauli unakuwa mdogo. Topic hii naiunganisha na nyingine ambayo pia inaihusisha CHADEMA na CCM.

Ahsante mamangu
 
alaa, kumbe huyu waridi ndio wale wale mamluki wa demokrasia!!!
ahsante sana bi.asha, mi nilikuwa sijamfahamu ati!!!!
sasa nimemgundua, hana data yoyote isipokuwa anataka kuanzisha majungu, maana hawa NCCR ni kawaida yao kupika majungu na fitna dhidi ya vyama mbadala.wao wamechoka sana kiasi kwamba kadri siku zinavyosogea ndivyo wanazidi kufutika kwenye ramani.
hebu waridi badala ya kupoteza muda kupiga majungu,jipangeni upya ili muweze angalau kurudisha heshima na hadhi ya chama chenu.

Mwitaaa!
safi sana kwa kuonesha unalalia upande gani, harakaharaka umemwamini bi Asha kuliko waridi, hujui hapa JF juma aweza kuwa ndiye Joseph, shauri lo
 
Nimekuwa msomaji wa JF karibia miezi 4 sasa, nimechogundua, watu humu, sina uhakika kama ni wote ila asilimia kubwa ni wanachadema, ona tu likiletwa neno lolote kuhusu chadema itakavyo tetewa, arafu iletwe kuhusu ccm inavyo unngwa mkono. nadhni mtuweke wazi hapa je JF ni ya wanachama wa chadema au?
 
Hata wewe uliyeandika utakuwa CHADEMA sio? Sikulaumu, umeandika mara moja na kutoweka haraka! Jiamini, simamia hoja mkuu. Usihame katika hoja ya msingi. Topic inayoongelea ulichoandika ipo.

Kwa post yako ya kwanza napenda kukukaribisha JF, ni ukweli na uwazi tu.

Wenye hasira huwa tunawatuliza wakienda mrama!
 
Nimekuwa msomaji wa JF karibia miezi 4 sasa, nimechogundua, watu humu, sina uhakika kama ni wote ila asilimia kubwa ni wanachadema, ona tu likiletwa neno lolote kuhusu chadema itakavyo tetewa, arafu iletwe kuhusu ccm inavyo unngwa mkono. nadhni mtuweke wazi hapa je JF ni ya wanachama wa chadema au?

Mhe.Gosheni,
unasema ukweli, hii JF imeingiliwa sana na CHADEMA. Ona thread inayopasua jipu ilivyozua mambo hapa hadi ikaamishwa.Vile vile mtu akiweka hoja yoyote inayohusu chama kingine inapondwa utadhani ni wananchi wenye hasira wanamponda kibaka.

Lakini ukweli ni kwamba;
Freeman Mbowe na Wilbroad Slaa ni wanachama hai wa CCM, sasa hivi wanahaha kwa sababu kuna mswada wa marekebisho ya sheria ya vyama unapelekwa bungeni, mswada huo unapiga marufuku mtu kuwa mwanachama wa vyama viwili tofauti, waheshimiwa hao wanalengwa hapo.

Aidha katika ishu ya Tarime, Chambiri kada wa CCM alikuwa financier mkuu wa kambi ya CHADEMA. unajua nini, ndani ya CCM wakikorofishana, wanashindana kwa kuitumia chadema, CCM B yao
kanusheni basi wanachadema
 
Hata mwanangu akija kusoma hapo atashangaa sana maana ni udaku tu!lete Data na kadi zao za CCM!
 
Nimekuwa msomaji wa JF karibia miezi 4 sasa, nimechogundua, watu humu, sina uhakika kama ni wote ila asilimia kubwa ni wanachadema, ona tu likiletwa neno lolote kuhusu chadema itakavyo tetewa, arafu iletwe kuhusu ccm inavyo unngwa mkono. nadhni mtuweke wazi hapa je JF ni ya wanachama wa chadema au?

JF is open to everyone, kila anayeingia humu ni lazima ana itikadi yake hiyo hakuna mtu awezaye kubisha, Sasa kuna kosa gani wana CHADEMA wengi wakiwa humu? Nani amekataza TLP, UDPP, UDM, PONA, CCM humu? Wewe kama unahisi kuna wanachama wa CHAMA Fulani wamejazana humu hilo sio kosa la JF, Nimesoma kwa umakini rules za JF sijaona hata moja ambayo inavutia Wanachama wa Chama Fulani.
USHAURI WANGU!
Kama wewe ni PONA nk, nenda kahamasishe wenzako waje wajoin cha msingi waje kujenga HOJA na si VIOJA
 
mhe.gosheni,
unasema ukweli, hii jf imeingiliwa sana na chadema. Ona thread inayopasua jipu ilivyozua mambo hapa hadi ikaamishwa.vile vile mtu akiweka hoja yoyote inayohusu chama kingine inapondwa utadhani ni wananchi wenye hasira wanamponda kibaka.

Lakini ukweli ni kwamba;
freeman mbowe na wilbroad slaa ni wanachama hai wa ccm, sasa hivi wanahaha kwa sababu kuna mswada wa marekebisho ya sheria ya vyama unapelekwa bungeni, mswada huo unapiga marufuku mtu kuwa mwanachama wa vyama viwili tofauti, waheshimiwa hao wanalengwa hapo.

aidha katika ishu ya tarime, chambiri kada wa ccm alikuwa financier mkuu wa kambi ya chadema. Unajua nini, ndani ya ccm wakikorofishana, wanashindana kwa kuitumia chadema, ccm b yao
kanusheni basi wanachadema

thibitisheni
 
CCM wasipokuwa makini na majibu yao ya kihuni yatawaponza sana kwani wenzao wa CHADEMA huwa wanafanya utafit kwanza ndippo wanaibuka sasa wao wanleta mambo ya ya ajabu na kujibu vitu ambavyo havikuulizwa wao wanasema rais hawezi kuambiwa na wapinzani utadhani wapinzani sio raia wa taifa hili.

wajue kuwa rais ni mtumishi wetu na sio mwajiri wetu sisi watanzania ndio tumempa kazi hivyo hana budi kujibu maswali yetu kwa kina.

Pamoja na kutumia mabavu yote na mapesa ya kuwashangaza hata wao wenyewe (Rejea kauli ya M/Mwenyekiti wao P. Msekwa) Tarime ni mfano wa karibuni zaidi, and its likely to happen in Biharamulo nad Mwibara if the elections are to be done.
 
Mhe.Gosheni,
unasema ukweli, hii JF imeingiliwa sana na CHADEMA. Ona thread inayopasua jipu ilivyozua mambo hapa hadi ikaamishwa.Vile vile mtu akiweka hoja yoyote inayohusu chama kingine inapondwa utadhani ni wananchi wenye hasira wanamponda kibaka.

Lakini ukweli ni kwamba;
Freeman Mbowe na Wilbroad Slaa ni wanachama hai wa CCM, sasa hivi wanahaha kwa sababu kuna mswada wa marekebisho ya sheria ya vyama unapelekwa bungeni, mswada huo unapiga marufuku mtu kuwa mwanachama wa vyama viwili tofauti, waheshimiwa hao wanalengwa hapo.

Aidha katika ishu ya Tarime, Chambiri kada wa CCM alikuwa financier mkuu wa kambi ya CHADEMA. unajua nini, ndani ya CCM wakikorofishana, wanashindana kwa kuitumia chadema, CCM B yao
kanusheni basi wanachadema

Wala huna haja ya kulalamika.....waalike watu wako wa NCCR wajae hapa nao, halafu mupambanishe hoja tu na CHADEMA, CCM n.k .Tupo wengi ni neutral tutapambanua tu yupi mwenye hoja kuliko mwenzake na kuamua.

Kuhusu mods ....kuna jukwaa la malalamiko,advice etc ....wewe post lalamiko lako hapo ukiona unafanyiwa isivyo haki.
 
Ona thread inayopasua jipu ilivyozua mambo hapa hadi ikaamishwa.Vile vile mtu akiweka hoja yoyote inayohusu chama kingine inapondwa utadhani ni wananchi wenye hasira wanamponda kibaka.
Waridi wala haijahamishwa kwa sababu ya eti inaigusia CHADEMA, hoja ya CCM vs CHADEMA ilikuwa ipo hivyo MIMI nikaonelea ni vema tukiiendeleza hapahapa. Wenye jazba hawajui siasa, lakini penye wengi pana mengi pia!

Freeman Mbowe na Wilbroad Slaa ni wanachama hai wa CCM, sasa hivi wanahaha kwa sababu kuna mswada wa marekebisho ya sheria ya vyama unapelekwa bungeni, mswada huo unapiga marufuku mtu kuwa mwanachama wa vyama viwili tofauti, waheshimiwa hao wanalengwa hapo.
Waridi, dadangu hapo umegonga patamu haswa. Hii inaweza kuibomoa CHADEMA endapo unaweza kunisaidia kitu kimoja dadangu, kama una vivuli vya kadi zao za uanachama ama uthibitisho wa kauli hii utakuwa umewasaidia wengi haswa wale waliokuwa wakitizamia kuwa wanachama wa chama hiki kujinasua kabla ya kutumbukia!

Binafsi nitafurahi sana kuona mambo yako exposed hapahapa! Bring em dataz mama...

Aidha katika ishu ya Tarime, Chambiri kada wa CCM alikuwa financier mkuu wa kambi ya CHADEMA. unajua nini, ndani ya CCM wakikorofishana, wanashindana kwa kuitumia chadema, CCM B yao
kanusheni basi wanachadema
Dada ndizo data hizi? Please kama kuna proof ya haya ya Chambiri naomba tupe nyeti hizo hata kwa picha au vivuli (scanned copies) mambo haya. Wanafiki wa siasa hawafai kuvumiliwa, kama umedhamiria kuwaumbua basi toa na uthibitisho mkuu waridi.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom