CHADEMA vs CCM: Nani Mbabaishaji?

Mpaka Kieleweke

JF-Expert Member
Feb 27, 2007
4,132
1,571
Naona wandugu hapa kwetu bongo siasa zinaelekea kuwashinda watatwala wetu kwani sasa hawajibu hoja badala yake wanajibu vioja.

Pili nimeshangazwa na CCM kujibu tamko lililoelekezwa kwa rais na CHADEMA badala ya habari maelezo kufanya hivyo je?hii ni kulinda mzee asiumbuliwe?

Naweka tamko la CHADEMA hapa na mwenye la CCM tafadhali aliweke hapa pia ili tuweze kujadili kwa kina.
TAMKO LA KAMATI KUU YA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA) KUHUSU KUUNDWA KWA KAMATI YA RAIS YA UCHUNGUZI WA SHERIA NA MIKATABA YA MADINI.

Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) katika Kikao chake cha Dharura kilichofanyika Keys Hotel, Dar es Salaam leo hii tarehe 24 Novemba 2007, imejadili na kutafakari kwa kina uamuzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa kuunda Kamati ya Rais ya Uchunguzi wa Sheria na Mikataba ya Madini na uteuzi wa Mheshimiwa Zitto Zuberi Kabwe(Mbunge) kama mjumbe wa kamati hiyo na kufikia maazimio yafuatayo:

1. Kamati Kuu inamtaka Rais asitishe na/au kufuta uteuzi wa wajumbe wa Kamati hiyo ambao wanatuhumiwa kwa ufisadi na/au kwa kuwa na mgongano wa maslahi;

2. Kamati Kuu inamtaka Rais atimize ahadi yake ya kuipa Kamati "uwakilishi mpana zaidi" kwa kuteua wawakilishi wa taasisi zisizokuwa za kiserikali ,mashirika ya dini na taasisi za kitaaluma kama wajumbe katika kamati hiyo;

3. Kamati Kuu inamshauri Rais aongeze masuala yafuatayo kwa ajili ya kuchunguzwa na Kamati katika hadidu za rejea za Kamati:

(i) Tuhuma za ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu dhidi wa wananchi waishio katika maeneo yenye migodi mikubwa ya madini;

(ii) Tuhuma za kuwepo kwa uchafuzi wa mazingira unaotishia afya za wananchi, viumbe hai na rasilimali za maeneo yenye migodi mikubwa ya madini kutokana na shughuli za uchimbaji unaofanywa na makampuni makubwa ya madini nchini;

(iii) Tuhuma za ufisadi na/au rushwa zinazohusiana na uandaaji na/au upitishwaji wa mikataba ya madini kati ya makampuni makubwa ya madini na viongozi na/au watendaji wa ngazi za juu wa serikali;

(iv) Mchango wa sekta ya madini kwa uchumi na maendeleo ya jamii ya wananchi waishio kwenye maeneo yenye migodi mikubwa ya madini.

4. Kamati Kuu inamtaka Rais kutoa hadharani na/au kwa wawakilishi wa kuchaguliwa wa wananchi Ripoti za Kamati za Uchunguzi zilizokwisha kuundwa na serikali kuchunguza matatizo mbalimbali ya madini ikiwemo Kamati ya Jenerali Mboma (2001), Kamati ya Brigedia Jenerali Mang'enya (2003), Kamati ya Dr. Kipokola (2004) na Kamati ya Masha (2006), ili wananchi wafahamu matokeo na mapendekezo ya Kamati hizo;

5. Kamati kuu inamtaka rais kuelekeza kwamba mikataba yote ya madini iliyoingiwa kati ya serikali na makampuni ya madini itolewe hadharani ili wananchi na wawakilishi wao wa kuchaguliwa waweze kufahamu yaliyomo katika mikataba hiyo;

6. Kamati Kuu inaridhia uteuzi na ushiriki wa Mheshimiwa Zitto Zuberi Kabwe katika Kamati ya Rais ya Uchunguzi wa Sheria na Mikataba ya Madini na inaahidi kufuatilia kwa karibu utekelezaji wa majukumu ya kamati hiyo;

7. Kamati Kuu inamtaka Rais atoe ahadi kwa Watanzania kwamba serikali yake itaitoa Ripoti ya Kamati ya Rais ya Uchunguzi wa Sheria na Mikataba ya Madini na kuyafanyia kazi mapendekezo yake;

8. Kamati Kuu inaagiza Sekretariati ya Makao Makuu ya Chama Taifa kuhakikisha kwamba Tamko hili linasambazwa kwa wananchi wa Tanzania kupitia vyombo vya habari na nakala zake kusambazwa katika ngazi zote za chama.

TAMKO HILI limetolewa kwa pamoja na Wajumbe wa Kamati Kuu na kusainiwa na Mwenyekiti wa Chama Taifa na Katibu Mkuu hapa Dar es Salaam leo hii tarehe 24 Novemba , 2007.
------------------------------------------------- ----------------------------------------
Freeman Aikaeli Mbowe
MWENYEKITI
 
CCM wasipokuwa makini na majibu yao ya kihuni yatawaponza sana kwani wenzao wa CHADEMA huwa wanafanya utafit kwanza ndippo wanaibuka sasa wao wanleta mambo ya ya ajabu na kujibu vitu ambavyo havikuulizwa wao wanasema rais hawezi kuambiwa na wapinzani utadhani wapinzani sio raia wa taifa hili.

wajue kuwa rais ni mtumishi wetu na sio mwajiri wetu sisi watanzania ndio tumempa kazi hivyo hana budi kujibu maswali yetu kwa kina.
 
7. Kamati Kuu inamtaka Rais atoe ahadi kwa Watanzania kwamba serikali yake itaitoa Ripoti ya Kamati ya Rais ya Uchunguzi wa Sheria na Mikataba ya Madini na kuyafanyia kazi mapendekezo yake;

Hii hapa imekosa aidha umakini wa uandishi au CHADEMA na RAIS kila mmoja ana uelewa tofauti,,, Rais huwa anasisitiza kwamba inaitwa Kamati ya Madini, sio ya kamati ya uchunguzi/investigation!!!

Aidha hoja ya ku-include mazingira, haki za binadamu kwa kweli ni ya kuungwa mkono kama Mh. Rais alikuwa hana nia ya kuiweka.

Kuhusu uwakilishi,,, well mambo ya uwakilishi wa wanamazingira na Haki za Binadamu ingekuwa poa, Lakini kwa mambo ya dini kwa jinsi nilivyo msikia alikuwa akibwagiza tu!
 
CCM they are worse, dirty and stink chama. However CHADEMA sound like high school girls who are recommend about wear make up in school. CHADEMA can't be trusted, neither CCM. We need a party with strong strategic plan, well educated candidates, and action party.
 
Do you mean you are looking for a party which has this leaders.

Chairman :-Mzee Mwanakijiji,
Assist. Chairman :- Mpaka kieleweke
Secretary General :- Mwafrika wa Kike,
Assistant Sec. General :- Mugongo Mugongo
Public Relations :- KadaMpinzani
Assistant :- John Mnyika
Treasury :- Kichwa Maji
Assist. Treasury :- FD.

Member of CC:
Several Guys,

Kwi kwi kwi ...
je hiki chama kitaenda? au watu wote wataishia kila mmoja anajua?

just joking guys.
 
CCM they are worse, dirty and stink chama. However CHADEMA sound like high school girls who are recommend about wear make up in school. CHADEMA can't be trusted, neither CCM. We need a party with strong strategic plan, well educated candidates, and action party.

CHADEMA are more strategic than CCM by far.You cant compare CHADEMA with CCM,the party which dump us in a massive poverty for nearly 5 decades.

I dont give damn to this tank of "MAFISADI".CHADEMA are more strategic than CCM by far

Iam out!
 
Nadhani CC ya chadema ina sahau majukumu yake ya msingi kama chama cha siasa .

Napenda kutumia fursa hii kuwashauri chadema yafuatayo.

1; Nikiwa mkulima anaetoka eneo la madini ya Dhahabu na pamba nawashauri achane siasa za magazetini na Habari maelezo.
2;Kauli zenu hazionyeshi ni kiasi gani mu wazalendo nchi yetu 80%ni wakulima dhahabu,ufasadi wa BOT zito kushiriki au kuto shiriki kamati kutpatia taarifa au kuto toa Taarifa kamwe haitusaidii watanzania tulio wengi Agenda yetu kama TAIFA ni kilimo na si DHAHABU,wala mabomu ya SLAA.Jengeni hoja ili sisi wakulima tuone uwezo wenu wakuwasemea wanyonge au iachene CCM ifanye kazi ya kutusaidia sisi wakulima kwani hivi sasa wametupatia matrekta angalau.

3;Hivi nyie ni chama cha DAR au watanzania bcs hatujui hata ofisi zenu huku vijijini mpaka mfukuzwe bungeni ndo mje kwetu kututembelea fungueni ofisi na mtueleze mtatufanyia nini si porojo za DAR.

4;WAPELEKENI SHULE JOHN MYIKA NA MREMA nakumbuka hawakumaliza chuo hapo mlimani angalau tuone mnawajali.

MTOTO WA MKULIMA
 
CHADEMA yapingwa

na Agnes Yamo

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimeyapinga maazimio yote manane yaliyotolewa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), yanayopinga muundo wa Kamati ya Rais ya Kuchunguza Mikataba ya Madini.

Msimamo huo wa CCM ulitangazwa kwa nyakati tofauti jana na Katibu wa Itikadi na Uenezi, Kapteni John Chiligati na Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa chama hicho tawala (UV-CCM, Amos Makala.

Uamuzi huo wa CCM unaendeleza malumbano ya miezi ya hivi karibuni kati ya vyama hivyo viwili, kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu uendeshaji wa serikali na maamuzi mbalimbali ya kiutendaji.

Kabla ya suala hili la kamati ya madini, viongozi wa juu wa CCM na Chadema wamekuwa wakilumbana kuhusu kashfa ya ubadhirifu wa fedha katika Benki Kuu (BoT), utiwaji wa saini wa mkataba wa Buzwagi na kabla ya hapo matamko mbalimbali ya viongozi wa Chadema yanayohusu uwezo wa serikali kiutendaji na maamuzi ya kisera na kisiasa serikalini.

Katika suala hili la sasa, Chiligati ambaye alizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, alisema ni jambo la ajabu kwamba Chadema waliupokea vibaya uamuzi wa Rais Kikwete kuunda kamati hiyo ya madini, hali ambayo ilizaa malumbano miongoni mwa viongozi wa chama hicho cha upinzani.

Kwa mujibu wa Chiligati, mapokeo mabaya ya Chadema yalisababisha malumbano miongoni mwa chama hicho cha upinzani ambayo kwa kiwango kikubwa yalionyesha kushindwa kwao kuelewa dhamira ya rais kuunda kamati hiyo.

"Jambo la kusikitisha ni kwamba Chadema walipokea vibaya uteuzi huo…Chama Cha Mapinduzi kinayaona maazimio hayo ya Chadema kama kushindwa kuelewa dhamira njema ya rais na mantiki ya kuunda kamati hiyo," alisema Chiligati. Akisoma tamko rasmi la chama hicho lenye kurasa nne, Chiligati alieleza kushangazwa na namna maazimio hayo ya Chadema yalivyoshindwa kutofautisha kuhusu haja ya kuundwa kwa tume au kamati ya madini.

"Ni vema ikaeleweka kuwa tume huundwa pale ambapo imethibitika kuwa kuna kosa lililotendeka au athari za wazi zimeonekana kwenye utendaji wa chombo cha serikali, lakini kamati huundwa pale ambapo mwelekeo mpya unahitajika katika utendaji wa chombo cha serikali,

"Tunapenda wananchi waelewe kuwa, alichounda rais ni kamati ya kuangalia upya sera, sheria na mikataba ya uchimbaji madini na si tume ya kuchunguza mikataba ya uchimbaji madini," alisema Chiligati akipinga pendekezo la chadema ambalo pamoja na mambo mengine lilitaka rais aunde tume badala ya kamati.

Mbali ya hilo, Chiligati katika tamko lake hilo alisema iwapo Chadema ilikuwa na mtazamo huo, basi walipaswa kumpa Kabwe Zitto ambaye ni mjumbe wa kamati, maoni yao kuhusu suala hilo badala ya kukimbilia kwenye vyombo vya habari.

Akizungumzia suala la kumtaka Rais Kikwete kufuta uteuzi wa baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo, Chiligati alisema madai hayo ni sawa na mbio za sakafuni ambazo lazima zitaishia ukingoni, na kuwa Chadema wanapaswa kuelewa kuwa uteuzi wa rais haufanywi kwa shinikizo la mtu wala taasisi yoyote.

"Hakuna migongano ya kimasilahi baina ya mjumbe yeyote wa kamati na kamati yenyewe na tuhuma za ufisadi dhidi ya baadhi ya wajumbe walioteuliwa hazina uthibitisho wowote na kuwa ni hisia binafsi za uongozi wa chama hicho," alisema.

Alisema Watanzania wanapaswa kufahamu kazi za kamati ambazo miongoni mwake ni pamoja na kupitia mikataba yote ya madini na nyaraka nyingine zinazohusu migodi mikubwa na kuchambua mfumo wa kodi unaotumika katika sekta hiyo.

Kazi nyingine ni kupitia mifumo ya usimamizi wa shughuli za uchimbaji mkubwa unaofanywa na serikali kuchambua na kuainisha haki na wajibu wa mwekezaji na mwenye rasilimali ambaye ni serikali.

Alisema chama chake kinayaona maazimio hayo kuwa ni matokeo ya kushindwa kuendesha siasa zenye hoja ndani ya jamii ya Kitanzaniaa.

Wakati Chiligati akitoa maoni yake hayo, UVCCM nao walitoa tamko la kurasa mbili wakieleza kushangazwa kwao na maazimio hayo ya Chadema.

Taarifa ya UVCCM iliyotolewa na Makala iliyaelezea maazimio hayo ya Chadema kuwa yaliyojaa upotoshaji, dalili za kutapatapa, uzushi pamoja na ubinafsi na kuwa, hoja hizo zinalenga kudhoofisha jitihada za Rais Kikwete zenye lengo la kulinda rasilimali za nchi.

"UVCCM ina imani na wajumbe wa kamati na tuna imani kamati iliyoundwa itafanya kazi kwa uhuru na zaidi imejaa watu makini na wapenda maendeleo na masilahi ya taifa," ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.

CCM inatoa matamko hayo mawili tofauti siku moja tu baada ya Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema, Freeman Mbowe, kutangaza maazimio manane kuhusu kamati hiyo ya kuchunguza mikataba ya madini.

Chadema katika maazimio yao hayo walimtaka rais afute uteuzi wa baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo ambao wanadaiwa kutuhumiwa kwa ufisadi huku wengine wao wakitajwa kuwa na mgongano wa kimasilahi.

Azimio jingine la chama hicho linamtaka rais kutimiza ahadi yake ya kutoa uwakilishi mpana zaidi kwa kuteua wajumbe wengine kutoka taasisi zisizokuwa za kiserikali (NG'Os), mashirika ya dini na taasisi za kitaaluma.

Chama hicho pia kilipendekeza kuongezwa kwa hadidu za rejea ambazo zilitakiwa kujumuisha masuala yanayohusu ukiukwaji wa haki za binadamu katika maeneo yenye migodi mikubwa ya madini na uchafuzi wa mazingira unaotishia afya za wananchi, viumbe hai na rasilimali katika maeneo hayo.

Kwa mujibu wa Chadema, hoja nyingine zinazotakiwa kufanyiwa kazi ni madai ya kuwapo kwa tuhuma za rushwa wakati wa uandaaji na uchapishaji wa mikataba ya madini kati ya kampuni kubwa za madini na viongozi au watendaji wa serikali.

Nyingine ni mchango wa sekta ya madini kwenye uchumi na maendeleo ya jamii ya wananchi waishio kwenye maeneo yenye migodi mikubwa ya madini.

Azimio jingine linamtaka rais kutoa hadharani ripoti ya kamati za uchunguzi zilizokwisha kuundwa na serikali kuchunguza matatizo mbalimbali yanayohusu sekta ya madini tangu mwaka 2001.

Azimio la tano linamtaka rais kuelekeza mikataba yote iliyoingiwa kati ya serikali na kampuni za madini kuwekwa hadharani, ili wananchi waweze kuelewa yaliyomo katika mikataba hiyo.

Azimio la sita ni kuridhia uteuzi na ushiriki wa Kabwe Zitto katika kamati hiyo ya rais na kuweka kipengele kinachoiagiza Kamati Kuu ya Chadema kufuatilia kwa karibu utekelezaji wa majukumu ya Kamati ya Rais.

Azimio la saba linamtaka rais binafsi au kwa kupitia mwenyekiti wa kamati hiyo atoe ahadi kwa wananchi kuwa utekelezaji wa kamati na ripoti yake vitakuwa hadharani na kuwa ushauri wa kamati hiyo utafanyiwa kazi.

Azimio la mwisho limeiagiza sekretarieti ya chama hicho kusambaza tamko hilo nchi nzima kupitia vyombo vya habari na nakala zake kusambazwa katika ngazi zote za chama.

----------------------------------MWISHO------------------------------------------
My take;

Tangu mwanzo mimi nilikuwa nimeelewa hivi hivi CCM walivyorudia, sasa sijui version ya CHADEMA ilitoka wapi? anyway... ndio siasa hizo tena
 
Ni kweli kabisa hoja za Chadema zina mvuto, zina umakini na ni kwa manufaa ya watanzania wote.

Hoja za CCM ni za kuona aibu kwamba wanatekeleza kile walichoambiwa na upinzani

by the way, ukweli unabaki kuwa hata kuundwa kwa kamati hiyo na Rais ni baada ya shinikizo kutoka kwa wapinzani,

kwa kuwa siku za nyuma viongozi wengi wa 'sirikali' alisikika wakisema kuwa system ya madini na migodi iko safi saaaana.

Mbaya zaidi hata Waziri Mkuu wa CANADA amewaumbua

LEO HII KAMATI IMEUNDWA,
 
Chadema Vs Ccm Nani Mbabaishaji?

Nafikiri wananchi wa Tanzania, walishaamua siku nyingi sasa kuhusiana na hili swali ambalo, sina uhakika kama ni valid argument, isipokuwa in case likiwa, then wananchi wameshajibu mara nyingi sana, kupitia kwenye kura za uchaguzi,

CCM ina miaka karibu 45 sasa, na Chadema ina miaka karibu 20 sasa, hivi kweli within miaka yote hiyo ya uhai wa Chadema, na CCM hili swali halijajibiwa? Kama ni mafisadi ni ishu ya sheria sio siasa it has nothing to do na CCM kwa ujumla,

Swali nafikiri hapa lilipaswa kuwa je Chadema, wanafanya kazi yao waliyopewa na wananchi toka waanzishe chama chao, ya kuisaidia serikali ya CCM katika kuvumbua mapungufu yao ili waweze kutawala vyema? Ukweli ni kwamba so far so good, Chadema wamekuwa wakijitahidi sana kuisaidia serikali ya CCM na hasa kuikumbusha mapungufu yake katika uongozi wake wa kutawala jamhuri, je Chadema inawea kuaminiwa kutawala jamhuri, wananchi wamesema hata udiwani hawawezi kuwaamini nao hii ni kutokana na majibu ya uchaguzi wa majuzi tu.

Heshima kwa Chadema, kwamba angalau wanajitahidi sana kuliko vyama vingine vya siasa huko upande wa pili nchini, na tunawatakia mafanikio mema huko kwenye sidelines, lakini kutawala jamhuri bado sana, maana hatuwezi kuwapa nchi Zitto, Slaaa, na Lisu tu no way, Freeman mpaka amalize shule ndio ajaribu ku-apply kwenye siasa zetu za taifa aliyoyasoma huko shuleni, kwa kweli hatuwezi ku-afford hayo ya experiment na taifa letu, Chadema waongeze bidii na kuwa watu makini wengi zaidi, kama CCM ambayo leo unaweza kuwaondoa wote walioko kwenye uongozi na kuanza na wengine wapya na bado ukawa na timu tano zaidi.

Kukosoa watawala, au kuwakumbusha watawala mapungufu yao, sio dhana ya kuweza kutawala, tumeyaona hayo wazi Kenya, Zambia, Malawi, Poland, na Ukraine.

Ahsanteni Wakuu!
 
Chadema Vs Ccm Nani Mbabaishaji? ...Chadema waongeze bidii na kuwa watu makini wengi zaidi, kama CCM ambayo leo unaweza kuwaondoa wote walioko kwenye uongozi na kuanza na wengine wapya na bado ukawa na timu tano zaidi...

mkuu, kweli tumeona timu makini za ccm tangu izaliwe ambazo kwa umakini wao ndio maana kama nchi tupo tulipo leo. kweli safari bado ndeeefu
 
mkuu, kweli tumeona timu makini za ccm tangu izaliwe ambazo kwa umakini wao ndio maana kama nchi tupo tulipo leo. kweli safari bado ndeeefu

Ni kweli kabisaa mkuu, ndio maana wananchi wame-stick na CCM maana walishagundua siku nyingi kuwa hakuna alternative, na Chadema pamoja na upinzani nzima hawajawapa wananchi sababu ya kuchagua tofauti nani awatawale,

Tupo hapa tulipo sio kutokana na chama cha siasa, au viongozi, hapana ni sisi wenyewe wananchi ndio tulioridhika na hali tuliyonayo, uzembe wa kufikiri na maneno mengi ambayo ni hewa tupu, huku matendo kukiwa hakuna kabisa, Yes! CCM itanednelea kututawala tu maana hakuna mwananchi mjinga atakayetoa taifa kwa watu watatu, Zitto, slaa, na Lisu, na chama cha Dar-es-saaalam tu!
 
Kuwalaumu wananchi pekee kwa maoni yangu si sawa, ni lazima pia tuangalie vyombo vya dola vinavyotumika katika kuwanyima haki wapinzani kufanya kampeni zao bila bughudha zozote na pia wizi wa kura ambao umeshamiri. Vyombo vya dola polisi na FFU wametumika katika chaguzi zote kuwanyanyasa na kuwavurugia wapinzani kampeni zao. Tukumbuke wasimamizi wa uchaguzi wa mwaka 2005 walitamka kwamba uchaguzi ule haukuwa free and fair.
 
Chadema Vs Ccm Nani Mbabaishaji?

Nafikiri wananchi wa Tanzania, walishaamua siku nyingi sasa kuhusiana na hili swali ambalo, sina uhakika kama ni valid argument, isipokuwa in case likiwa, then wananchi wameshajibu mara nyingi sana, kupitia kwenye kura za uchaguzi,

CCM ina miaka karibu 45 sasa, na Chadema ina miaka karibu 20 sasa, hivi kweli within miaka yote hiyo ya uhai wa Chadema, na CCM hili swali halijajibiwa? Kama ni mafisadi ni ishu ya sheria sio siasa it has nothing to do na CCM kwa ujumla,

Swali nafikiri hapa lilipaswa kuwa je Chadema, wanafanya kazi yao waliyopewa na wananchi toka waanzishe chama chao, ya kuisaidia serikali ya CCM katika kuvumbua mapungufu yao ili waweze kutawala vyema? Ukweli ni kwamba so far so good, Chadema wamekuwa wakijitahidi sana kuisaidia serikali ya CCM na hasa kuikumbusha mapungufu yake katika uongozi wake wa kutawala jamhuri, je Chadema inawea kuaminiwa kutawala jamhuri, wananchi wamesema hata udiwani hawawezi kuwaamini nao hii ni kutokana na majibu ya uchaguzi wa majuzi tu.

Heshima kwa Chadema, kwamba angalau wanajitahidi sana kuliko vyama vingine vya siasa huko upande wa pili nchini, na tunawatakia mafanikio mema huko kwenye sidelines, lakini kutawala jamhuri bado sana, maana hatuwezi kuwapa nchi Zitto, Slaaa, na Lisu tu no way, Freeman mpaka amalize shule ndio ajaribu ku-apply kwenye siasa zetu za taifa aliyoyasoma huko shuleni, kwa kweli hatuwezi ku-afford hayo ya experiment na taifa letu, Chadema waongeze bidii na kuwa watu makini wengi zaidi, kama CCM ambayo leo unaweza kuwaondoa wote walioko kwenye uongozi na kuanza na wengine wapya na bado ukawa na timu tano zaidi.

Kukosoa watawala, au kuwakumbusha watawala mapungufu yao, sio dhana ya kuweza kutawala, tumeyaona hayo wazi Kenya, Zambia, Malawi, Poland, na Ukraine.

Ahsanteni Wakuu!Afadhali Mbowe alikuwa anajua chanzo cha umasikini wa watanzania kabla hata ya kwenda kusoma zaidi. Kikwete hata baada ya kusoma na kukulia serikalini bado haielewi kwa nini Tanzania ni masikini. Kuendelea kumuacha pale ikulu ni kuendelea kuwatukuna watu wote wenye akili Tanzania. Kila siku unapigia kelele ushindi wa asilimia 80 kuhalalisha uwepo wake pale ikulu, unachosahau ni kuwa ushindi ule umepatikana kwa mizengwe- hauendani kabisa na uwezo wake wa kiasiasa pale kikwete. Asilimia 80 si kipimo cha imani ya watanzania kuhusu uwezo wa Kikwete, labda matumaini waliyolishwa kwa ahadi hewa tu ambayo sasa yamesalitiwa na wameanza kumnyooshea vidole. Ukipiga kura za maoni huru sasa hata asilimia 20 atapata kwa tabu. Ushindi wa Kikwete=Propanda za Mtandao toka 1995(za kuwabomoa wakina Malecela, Salim, Mwandosya na za kuficha udhaifu wa JK)+ Udhaifu wa upinzani(mara baada ya 1995 hususani kupomoromoka kwa NCCR Mageuzi)+ Kampeni za Rushwa( yeye mwenyewe amekiri+ Mahakama imethibitisha kwa kufuta takrima)+chama Dola(Mkapa alitangaza hadharani+ Tume ya uchaguzi ikatekeleza maeneo mbalimbali). Sasa anza kutoa kimoja hadi kimoja utaona kwamba huyu jamaa kama alikuwa anakubalika kwa asilimia 80 au la.

Kikwete ni mzigo kwa taifa! period

Kama CCM mtaendelea kudhani ni tumaini lilirojea mtandelea kuwakatisha tamaa watanzania na hakika Kikwete ataondoka na kina Rostam na Lowasa wake lakini Tanzania itasimama milele.

FMES, kwani Kikwete na JSM au SAS nani bora?

Asha
 
Chadema Vs Ccm Nani Mbabaishaji?

Nafikiri wananchi wa Tanzania, walishaamua siku nyingi sasa kuhusiana na hili swali ambalo, sina uhakika kama ni valid argument, isipokuwa in case likiwa, then wananchi wameshajibu mara nyingi sana, kupitia kwenye kura za uchaguzi,

CCM ina miaka karibu 45 sasa, na Chadema ina miaka karibu 20 sasa, hivi kweli within miaka yote hiyo ya uhai wa Chadema, na CCM hili swali halijajibiwa? Kama ni mafisadi ni ishu ya sheria sio siasa it has nothing to do na CCM kwa ujumla,

Swali nafikiri hapa lilipaswa kuwa je Chadema, wanafanya kazi yao waliyopewa na wananchi toka waanzishe chama chao, ya kuisaidia serikali ya CCM katika kuvumbua mapungufu yao ili waweze kutawala vyema? Ukweli ni kwamba so far so good, Chadema wamekuwa wakijitahidi sana kuisaidia serikali ya CCM na hasa kuikumbusha mapungufu yake katika uongozi wake wa kutawala jamhuri, je Chadema inawea kuaminiwa kutawala jamhuri, wananchi wamesema hata udiwani hawawezi kuwaamini nao hii ni kutokana na majibu ya uchaguzi wa majuzi tu.

Heshima kwa Chadema, kwamba angalau wanajitahidi sana kuliko vyama vingine vya siasa huko upande wa pili nchini, na tunawatakia mafanikio mema huko kwenye sidelines, lakini kutawala jamhuri bado sana, maana hatuwezi kuwapa nchi Zitto, Slaaa, na Lisu tu no way, Freeman mpaka amalize shule ndio ajaribu ku-apply kwenye siasa zetu za taifa aliyoyasoma huko shuleni, kwa kweli hatuwezi ku-afford hayo ya experiment na taifa letu, Chadema waongeze bidii na kuwa watu makini wengi zaidi, kama CCM ambayo leo unaweza kuwaondoa wote walioko kwenye uongozi na kuanza na wengine wapya na bado ukawa na timu tano zaidi.

Kukosoa watawala, au kuwakumbusha watawala mapungufu yao, sio dhana ya kuweza kutawala, tumeyaona hayo wazi Kenya, Zambia, Malawi, Poland, na Ukraine.
Ahsanteni Wakuu!

FMES,

Nakubaliana na wewe kabisa kwenye hili, huwaga kila nikijiuliza je CHADEMA kwa sasa ilivyo yaweza kupewa na kuongoza nchi? naanza na kuhesabu viongozi ambao iliyonayo sasa, kwa ajili at least kuunda baraza la mawaziri dogo kuliko yote hapa duniani lenye uwiano na nchi yetu... naona haiwezekani maana majina hayafiki kumi (vidole vya mikono yangu miwili) nikishafikiri hivyo narudi nyuma nikisema wajameni tujizatiti vijiji, tujizatiti kupata angau 30% ya wabunge hapa tutake sasa kuongoza nchi hii...

Mawazo tu....
 
Chadema Vs Ccm Nani Mbabaishaji?

Nafikiri wananchi wa Tanzania, walishaamua siku nyingi sasa kuhusiana na hili swali ambalo, sina uhakika kama ni valid argument, isipokuwa in case likiwa, then wananchi wameshajibu mara nyingi sana, kupitia kwenye kura za uchaguzi,

CCM ina miaka karibu 45 sasa, na Chadema ina miaka karibu 20 sasa, hivi kweli within miaka yote hiyo ya uhai wa Chadema, na CCM hili swali halijajibiwa? Kama ni mafisadi ni ishu ya sheria sio siasa it has nothing to do na CCM kwa ujumla,

Swali nafikiri hapa lilipaswa kuwa je Chadema, wanafanya kazi yao waliyopewa na wananchi toka waanzishe chama chao, ya kuisaidia serikali ya CCM katika kuvumbua mapungufu yao ili

waweze kutawala vyema? Ukweli ni kwamba so far so good, Chadema wamekuwa wakijitahidi sana kuisaidia serikali ya CCM na hasa kuikumbusha mapungufu yake katika uongozi wake wa kutawala jamhuri, je Chadema inawea kuaminiwa kutawala jamhuri, wananchi wamesema hata udiwani hawawezi kuwaamini nao hii ni kutokana na majibu ya uchaguzi wa majuzi tu.

Heshima kwa Chadema, kwamba angalau wanajitahidi sana kuliko vyama vingine vya siasa huko upande wa pili nchini, na tunawatakia mafanikio mema huko kwenye sidelines, lakini kutawala jamhuri bado sana, maana hatuwezi kuwapa nchi Zitto, Slaaa, na Lisu tu no way, Freeman mpaka amalize shule ndio ajaribu ku-apply kwenye siasa zetu za taifa aliyoyasoma huko shuleni, kwa kweli hatuwezi ku-afford hayo ya experiment na taifa letu, Chadema waongeze bidii na kuwa watu makini wengi zaidi, kama CCM ambayo leo unaweza kuwaondoa wote walioko kwenye uongozi na kuanza na wengine wapya na bado ukawa na timu tano zaidi.

Kukosoa watawala, au kuwakumbusha watawala mapungufu yao, sio dhana ya kuweza kutawala, tumeyaona hayo wazi Kenya, Zambia, Malawi, Poland, na Ukraine.

Ahsanteni Wakuu!

Heshima yako mkuu,

Umeongea point,lakini NAKATAA unaposema kipimo cha kuonyesha CHADEMA hawawezi kuongoza nchi ni kutumia sanduku la kura la 2005, Je matokeo yaliyotokana na uchaguzi ule nddio kipimo sahii ikiwa watanzania wengi wanajua mfumo wetu wa uchaguzi nchini umekaa kimazingaombe?

Kuhusu mapungufu ya CHADEMA kama chama cha siasa: Je CCM kama chama tawala huoni kimekua kikwazo kikubwa kwa ukuaji wa CHADEMA kama chama cha siasa nakuendelea kuishikilia katiba mbovu, ambayo ina rangi zote za kikoloni? Ni mra ngapi tumelalamika kuhusu katiba mbovu isiyotoa nafasi katika ukuaji wa kidemokrasia na hasa ile ya vyama vya upinzani?

Mkuu,ES kwa mamabo mengi amabyo CHADEMA wamefanya kwa mda huu wa miaka 20 huwezi kulinganisha na mambo ambayo CCM wamefanya kwa miaka 45 hyadi kutufanya tuendelee kuwa katika 'top three' of the poorest countries duniani na tuko hapo kwa muda mrefu.

Je,suala la CHADEMA kufanya ile kazi waliyopewa na wananchi huoni pia CCM wanatakiwa kulaumiwa kwa kutumia hila chafu huku kodi za wananchi zikitumiwa kwa manufaa ya chama chao ili wasikosolewe na CHADEMA? Kwa hili nadhani wananchi wanatakiwa kuelimishwa vizuri zaidi na wazielekeze shutuma na lawama kwa CCM kuliko CHADEMA ambao hata wewe mwenyewe umekiri kwamaba vimejitahidi kuliko vingine.

By,the way thanks for your frankness.

Hata hivyo kumbuka hatuko tena kwenye ubinafsi wa UCHADEMA,tuko katika muungano wa vyma vya upinzani so it is better tukaweka UPINZANI VS CCM.

Ingawa CCM hawataki tufike huko ulikodai 'KUFANYA ILE KAZI TULIYOTUMWA NA WANANCHI'.Nadhani hapa ndipo CCM walitakiwa waonyeshe dhamira yao ya wazi ya kutaka kukosolewa kwa kurahisisha mabo yatakayosaidia upinzani kuungana na hatimae wasimamae sasa kwenye uchaguzi 2010 kama kweli CCM hawastahili lawama.
 
mkuu, kweli tumeona timu makini za ccm tangu izaliwe ambazo kwa umakini wao ndio maana kama nchi tupo tulipo leo. kweli safari bado ndeeefu

Heshima mkuu,
Unamaanisha nini ukisema tuko tulipo?

Yaani unamaanisha kwenye huduma bora za afya,miundombinu imara,ajira nje nje, hakuna ubabaishaji katika mfumo wetu wa elimu na vijana wetu vyuo vikuu wanasoma na wanapata elimu bora katika mazingira mazuri,hatuna kashfa za kijinga kama kwa nchi jirani za kifisadi, sarafu yetu inanguvu kubwa,hakuna watoto wa mitaani,machinga hawakandamizwi, kuna maadili ya kiuongozi,demokrasia imepanuka sana,hakuna ujambazi uliokithiri,mtoto wa tajiri na wa maskini anaweza kukaa sehemu moja bila kuona tofauti,kuna usimamizi mzuri wa raslimali zetu,na bajeti yetu haitegemei wahisani kwa asilimia kubwa kwani hilo haliwezekani kabisa na huwa tunalisikia kwa nji jirani tu.

Kweli tumeshuhudia watu makini ndani ya CCM hasa wanaosaini mikataba ya Madini mahotelini.Kweli hpo kulikua na umakini mkubwa kwani Lihoteli hilo lilikua na ulinzi mkali na mkataba huo ulikua nyeti sana
 
kukosekana kwa alternative sio kigezo cha timu makini kubweteka na kushindwa kutekeleza yale ambayo wananchi "wanaoitwa wajinga" wanatumaini kuyapata pamoja na "ujinga wetu"
 
Heshima mkuu,
Unamaanisha nini ukisema tuko tulipo?

Yaani unamaanisha kwenye huduma bora za afya,miundombinu imara,ajira nje nje, hakuna ubabaishaji katika mfumo wetu wa elimu na vijana wetu vyuo vikuu wanasoma na wanapata elimu bora katika mazingira mazuri,hatuna kashfa za kijinga kama kwa nchi jirani za kifisadi, sarafu yetu inanguvu kubwa,hakuna watoto wa mitaani,machinga hawakandamizwi, kuna maadili ya kiuongozi,demokrasia imepanuka sana,hakuna ujambazi uliokithiri,mtoto wa tajiri na wa maskini anaweza kukaa sehemu moja bila kuona tofauti,kuna usimamizi mzuri wa raslimali zetu,na bajeti yetu haitegemei wahisani kwa asilimia kubwa kwani hilo haliwezekani kabisa na huwa tunalisikia kwa nji jirani tu.

Kweli tumeshuhudia watu makini ndani ya CCM hasa wanaosaini mikataba ya Madini mahotelini.Kweli hpo kulikua na umakini mkubwa kwani Lihoteli hilo lilikua na ulinzi mkali na mkataba huo ulikua nyeti sana

mkuu nisome vizuri. mimi nashangaa hizo timu makini kutuweka hapa tulipo. yaani hizo timu makini zimeshindwa kutukwamua na kutufikisha kwenye neema! oops nimesahau kwamba kapteni wa timu iliyopo hajui kiini cha matatizo yetu. ni mawazo tuu
 
Mkuu wangu,
Hapo sasa nimekupata vizuri.Hata mie nilishangaa ulikua unamanisha nini.sasa tuko pamoja mpaka hapo
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom