Heshima Mbele,
Kwa mujibu wa habari nilizozipata toka Nyumbani Tanzania,na zimeandikwa katika moja ya magazeti ya leo huko Nyumbani ni kwamba Marehemu Chacha Wangwe alikuwa na mpango wa kuiacha CHADEMA na kuhamia CCM,na kabla ya kuhama alikuwa amepanga kuanika wazi wazi yale ya CHADEMA na ugomvi wao.
na lengo la kusambazwa kwa waraka ule kwa viongozi wa CCM ilikuwa ni kujiandaa na kumpokea Marehemu chacha Wangwe.
Masikini Chacha wangwe umetutoka kabla ya kueleza ukweli
Hapa ndio maana naamini kuwa kuna umuhimu mkubwa wa kufuatilia nyendo zote za Marehemu Chaha Wangwe kwa muda wa wiki mbili ama hata mwezi kabla ya "ajali" ilipomkuta. Ni muhimu kujua kila aliyeongea naye na kama kuna link na hizi siasa zinazoendelea ni muhimu kuwabana kujua waliyokuwa wakiongelea, ni mantiki ya makutano yao na nini kilijiri baadaye
Vilevile ni muhimu kuangalia account za Mallya na hata za Mheshimiwa....Kwa Mallya ni kudetect fedha zisizoeleweka lakini pia kujua mahusiano yao ya Marehemu yalianza lini na yalikuwa katika hali gani. Maana nasikia kuwa Marehemu alikuwa na tabia ya kuamini sana watu na kuingia nao ubia wa kibiashara. Kwake yeye zaidi ilikuwa kuwawezesha wahangaikaji wenzake.
Vilevile kama CCM walikuwa wameshamshawishi kuingia huko kitu ambacho sikiamini kwa kutambua mazingira ya kisiasa ya TARIME na chuki yao dhidi ya CCM na Serikali na pia msiamamo wa awali wa Marehemu kuamaua kutumia vikao vya chama...lakini pia CCM kuna utamaduni wa kuwapatia wanaoasi vyama vyao TAKRIMA ambayo mara nyingi huwa kuanzia millioni 20 kuenda mbele. Mzee Wassira, Msabaha aliyekuwa CUF, Kaborou ni ushahidi mzuri katika hili.
Kwa wanaohoji ni kuhusu marehemu kuwa hapo zamani alikuwa RASTA ni kweli alikuwa nazo na hata alipkuwa Mbunge alikuwa na tabia ya kutembea na picha akiwa na RASTA na kule Tarime ni maarufu kama CHACHA Rasta. Marehemu alilazimika kuondoa Rasta kwa ushauri ama shinikizo la MWALIMU NYERERE alipokuwa anataka ushauri wake ili yeye ajiunge na harakati za siasa.....Hata hivyo marehemu alibaki kuwa muumini mkubwa wa falsafa za Kirasta wakati wote na hiyo ndiyo naweza kusema kuwa ilikuwa msingi mkubwa wa fikira na matendo yake daima.....Hata wakati wa kifo cha Lucky DUbe alisimama bungeni kuwatakia kuangana na kuwatakia pole maJAH wote duniani.
Kuhusu Prof Wangwe ni kweli yeye ni mwanachama wa CCM na pia aliwahi kugombea ubunge wa Afrika Mashariki kupitia CCM ambapo yeye pamoja na mama KABAKA walikuwa wanamlaumu Marehemu CHACHA kwa kitendo chake cha kuungana na wenzake wa CUF na kina Zitto kususia uchaguzi ule kama sababu ya yeye Prof Wangwe kushindwa. Hivi sasa ni mjumbe wa NEC ya CCM na pia kuna madai kuwa kuingia kwake kwenye siasa kulichangiwa na siasa za Marehemu Wangwe ambaye ni mdogo wake kwa UBINAMU.
Hawakuwa karibu kama watu wanavyodai hapa lakini Prof Wangwe naweza kusema ndio mu pekee aliyeweza kutumia busara zake kupunguza jazba na propaganda zilizokuwa zinaitafuna familia kidogokidogo.
Kuna madai kuwa msimamo wa sasa ni kujitahidi kuendana na muono wa baadhi ya wanafamilia ambao walifikia kumshambulia kuwa amepewa hongo kusema kuwa kifo cha CHACHA RASTA kilikuwa cha ajali ya kawaida. Wapo wafanyao hivyo kwa maslahi ya kisiasa na ya binafsi na wapo wafanyayo hivyo kwa mashaka halisi kabisa yaliyojengeka katika fikira zao ambao mimi pia naungana nao mkono.
Tanzanianjema