Sio kosa lako kushidwa kujibizana nami kwa sababu unashindwa kusoma hoja unanitazama mimi. Hujibizani na mimi bali unauliza ama kujibu hoja..Wewe uliyefungwa na chama ndio unashindwa kutazama nje ya sanduku la Uchama ulofungiwa. Huyo huyo Lowassa angekwenda ACT usingeyasema haya ilihali mimi ningewatupia wao makombora kama kawa.Nguruvi3, huyo ndiye Mkandara, wakati mwingine nashindwa hata kujibizana naye maanake unajikuta uko katika level yake. Nakiri ninatofautiana na wengi tu humu ndani kuhusu ujio wa Lowassa Chadema na kuteuliwa kuwa mgombea chini ya UKAWA lakini mimi nasema na narudia, ikiwa Lowassa atatuwezesha kuliondoa hili zimwi madarakani, so be it. Kama Lowassa angeteuliwa kupeperusha bendera ya CCM, nisingemuunga mkono, nisingemtetea kwa sababu vita yangu ni dhidi ya mfumo unaotuzalishia na kuwalea ninaowaita maadui wa taifa hili, period. Wakiachana na CCM kama alivyofanya Dr. Slaa miaka mitatu baada ya kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi, sina sababu tena ya kutowapokea.