Faida na Hasara alizosababisha Lowassa akiwa CCM-CHADEMA-CCM

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,591
8,810
Kabla ya ujio wa Edward Lowassa, CHADEMA ilikuwa na viti vya ubunge katika majimbo 23 ya uchaguzi na viti maalumu 26 na hivyo kuwa na idadi ya jumla ya wabunge 49 katika bunge la 10 la 2010-2015,

Ujio wa Edward Lowassa uliongeza wabunge kutoka majimbo 23 mwaka 2010 hadi majimbo 35 mwaka 2015. Viti maalumu kutoka 26 hadi 43 na kufanya jumla ya wabunge CHADEMA 78 bunge la 11

Hii kwetu wafuasi na wanachama was CHADEMA ilikuwa ni rekodi ambayo haijawahi kufikiwa na chama chochote cha upinzani tangu Tanzania ipate uhuru, binafsi, Edward Lowassa alikuwa “Asset”

Kabla kuondoka Edward Lowassa ndani ya CCM, CCM ilikuwa na wabunge wa viti maalumu 79 waliopatikana katika uchaguzi wa mwaka 2010. Mwaka 2015 CCM ikapata wabunge wa viti maalumu 62 tu

Nguvu ya Edward Lowassa iliondoka na viti maalum 17. Waliongezeka CHADEMA, ambayo ilikuwa na viti maalumu 43. Chukua viti 26 vya CHADEMA 2010 + viti 17 alivyokuja navyo Edward Lowassa = 43.

2010-2015, CCM ilikuwa inapokea ruzuku zaidi ya 78% ya ruzuku yote ya vyama vya siasa kutokana na kura za Rais alizopata Jakaya Kikwete, 2015 CCM ikapokea ruzuku isiyozidi 59% ya ruzuku.

Hii ni pungufu ya 20% waliyopoteza CCM, na kwa mara ya kwanza chama cha upinzani kikapokea 40% ya ruzuku yote ya vyama siasa, hii ni kutokana na kura mil 6=39% alizopata Edward Lowassa.

Kabla ya ujio wa Edward Lowassa CHADEMA, katika majiji matano (5), Mbeya, Dar es Salaam, Tanga, Mwanza na Arusha, CHADEMA ilikuwa haiongozi hata jiji moja kati ya hayo kwa mwaka 2010-2015.

Awali, majiji yote yalikuwa chini ya CCM. Ujio wa Edward Lowassa ukaifanya CHADEMA kuongoza majiji 4 (Mbeya, Dar es Salaam, Arusha na Tanga ingawa Tanga ilikuwa chini ya UKAWA).

Halmashauri hizo za majiji zilikuwa chini ya CHADEMA kutokana na ushindi
 
Back
Top Bottom