CHADEMA/UKAWA: Uwekezaji usiotabirika

Freeland

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2012
Messages
14,506
Points
2,000

Freeland

JF-Expert Member
Joined Jan 24, 2012
14,506 2,000
Hawana mbinu mpya kwasababu zama si zao, na kila zama na kitabu chake
Si suala la mbinu tena ni suala linalohitaji surgical precision right away

The time is up, help Mbowe exit the door with honor. Mbowe must go ab initio

Chadema, it's time you express your gratitude to Hon Mbowe for his tireless effort and immense contributions to your party and country at large, and remind him it's time to pack and go!
Mkuu Nguruvi3 kwa leo umesema Jambo la msingi sana ambalo tumeliona kwa muda mrefu sasa

Nilipigwa na butwaa kubwa sana baada ya kuona yanayotokea...especially hili la wasanii

Huu ni wakati mwafaka wa Mbowe kukaa Pembeni...Chama kimesinyaa....as if hakina watu maridadi na wenye uelewa

Chama kinaenda enda tu

Tulizoea CHADEMA ya hoja.....nzito nzito...Tulizoea CHADEMA ya kutoa Plan B ya matatizo ya nchi yetu

Lakini CHADEMA ya sasa hata haijui inafanya nini

Huu ni wakati mzuri sana wa CHADEMA kupaa kwa sababu magufuli ni anapwaya sana katika nafasi yake

Kutokana na kupwaya kwake anawapa room ya hawa jamaa kupaa

Hivi blunders zote alizofanya magufuli wanashindwa ku capitalize na kuwa chachu ya growth yao

This is 2017...Miaka 2 tu hadi mwaka wa uchaguzi mkuu imebaki.....Ukiuliza CHADEMA wanafanya nini..hakuna kitu

Suluhisho liliopo sasa Mbowe akae Pembeni mwaka 2018........Chama kikae chini kifanye tathimini yakinifu ya 2015....

Chama kiunde upya timu yake....Turudi kwenye chama cha hoja

Tunaenda kwenye uchaguzi mwingine katika mazingirra ya kikatiba yaleyale..Itakuwa ajabu sana kama CHADEMA watakaa kimya siku zote hadi 2020 na kuenda katika uchaguzi mwingine katika mazingira yaleyale
 

Nguruvi3

Platinum Member
Joined
Jun 21, 2010
Messages
13,417
Points
2,000

Nguruvi3

Platinum Member
Joined Jun 21, 2010
13,417 2,000
"Freeland, post: 19861431, member: 67846"]
Nilipigwa na butwaa kubwa sana baada ya kuona yanayotokea...especially hili la wasanii
Yaani recruitment ya wasanii ndilo kipaumbele chao ! it's disgusting

Huu ni wakati mwafaka wa Mbowe kukaa Pembeni...Chama kimesinyaa....as if hakina watu maridadi na wenye uelewa
Kuna mambo mengi sana ya kitaifa yanaendelea. Utashangaa chama kinachopaswa kuiweka serikali mguu sawa kimekaa kimya as if kila kitu ni 'poa' tu. Hawana agenda tena. Mambo chungu nzima hawana habari
Chama kinaenda enda tu
Afadhali kingekuwa kinaenda, nadhani kimesimama kabisa na kimevia. Hakuna kinachofanyika
Tulizoea CHADEMA ya hoja.....nzito nzito...Tulizoea CHADEMA ya kutoa Plan B ya matatizo ya nchi yetu
Hakuna tena hoja nzito ingawa hoja nzito za kujadili zipo
Katibu mkuu ni kama hakuna na huyu ni zao la Mbowe. Ukiangalia timu nzima ya uongozi kila mtu anakwenda kivyake vyake, kana kwamba hakuna strategy
Lakini CHADEMA ya sasa hata haijui inafanya nini
Nitashangaa kama atakayesema kinafanya nini. Real suprised
Huu ni wakati mzuri sana wa CHADEMA kupaa kwa sababu magufuli ni anapwaya sana katika nafasi yake
Hawaoni ukweli huu kwasababu hakuna anayeweza kufikiri zaidi.
Ni kama wameishiwa fikra na sasa jahazi linapelekwa na upepo tu
Hivi blunders zote alizofanya magufuli wanashindwa ku capitalize na kuwa chachu ya growth yao
Hawazioni, wapo bize na bongofleva.
Nani alisema Bongofleva ni tatizo au suluhisho la matatizo ya nchi.
Hawaoni blunders kwasababu wanafanya blunders
This is 2017...Miaka 2 tu hadi mwaka wa uchaguzi mkuu imebaki.....Ukiuliza CHADEMA wanafanya nini..hakuna kitu
Timu zao zinakwenda solo.
Leo utasikia fulani yupo eneo fulani kesho mwingine yupo kule, disorganized completely
Wanasubiri uchaguzi waanzisha agenda ya katiba ambayo ilitakiwa iwe mikononi mwao sasa hivi. Watakwenda katika uchaguzi na katiba, tume n.k. kama vilivyo halafu wanalalamika foul.
Suluhisho liliopo sasa Mbowe akae Pembeni mwaka 2018........Chama kikae chini kifanye tathimini yakinifu ya 2015....
No! akae pembeni right now si 2018 wakati uharibifu umekamilika.
Wasipofanya hivyo watavuna mabua tu.
Kupoteza mwelekeo ni suala la dharura na Mbowe asaidiwe kukaaa pembeni
Chama kiunde upya timu yake....Turudi kwenye chama cha hoja
Timu iliyopo ivunje, iundwe mpya ili kuleta mabadiliko ya kweli yanayokidhi haja na nyakati.

Siasa ni jambo 'fluid'ni kosa walioshindwa ku adapt new environment kuendelea

Kuna kila sababu ya kuamini Mbowe na timu yake wametimiza wajibu wao kwa nyakati zao, sasa ni zama nyingine watoe kijiti haraka
Tunaenda kwenye uchaguzi mwingine katika mazingirra ya kikatiba yaleyale..Itakuwa ajabu sana kama CHADEMA watakaa kimya siku zote hadi 2020 na kuenda katika uchaguzi mwingine katika mazingira yaleyale
Na wataendelea kumtafuta mchawi juu ya paa la nyumba wakifumbia macho joka uvunguni.

Watalalamika kuonewa wakati wanajua CCM imedhamiria hivyo

Ili kuamsha fikra mpya, fikra za nyakati walioshindwa huko nyuma wakae pembeni. Waombwe na ikishindikana wasaidiwe.

Hakuna mahali pa kuanzia isipokuwa kwa mwenye chama au Mwenyekiti ambaye hakuna shaka ima yupo nyuma ya wakati au amekimbia mbele sana.

Vyovote iwavyo endapo Chadema na wanachama wao wanataka kitu tofauti, lazima waanze na utofauti huo ndani ya nyumba yao kwanza

Kwa hili wengine tunasimama na kuwaambia bila haya wala soni, Mbowe akae pembeni
 

Alinda

Platinum Member
Joined
Jun 26, 2008
Messages
1,680
Points
2,000

Alinda

Platinum Member
Joined Jun 26, 2008
1,680 2,000
Mkuu Nguruvi3 kwa leo umesema Jambo la msingi sana ambalo tumeliona kwa muda mrefu sasa

Nilipigwa na butwaa kubwa sana baada ya kuona yanayotokea...especially hili la wasanii
Napingana kidogo na ili swala la wasanii, kwa maono yangu sioni tatizo lolote Wema au wasanii kwa ujumla kujiunga na Chadema. Kwa maana chama hakichagui wanachama. Nafikiri hata katika masharti ya kuwa mwanachama hakuna sehemu yeyote ambayo wanakataza watu wa aina fulani kujiunga na chama kwani kwa kufanya hivyo tiyari unakuwa umeweka ubaguzi wa aina fulani..Tukumbuke"Sugu" pamoja na Pro.Jay ni wasanii lakini pamoja na usanii wao wameweza kuwa wabunge. Sasa kama Sugu alipokelewa kwanini Wema hasipokelewi? Tukirudi nyuma na kusema Wema ana tuhuma ya kutumia madawa ya kulevya, hizo ni tuhuma kwani hata Mh. Mbowe anatuhumiwa kwa kosa hilo hilo na tuhuma au hata mtu akitiwa hatiani si sababu ya kutojiunga na chama chochote cha siasa maana hata katika magereza yetu kuna wanachama wa vyama mbali mbali. Lakini lipokuja katika swala nzima la uongozi ndo tunaweza kuona kuwa hatuwezi kumchagua kiongozi mwenye tuhuma mbali mbali. (ingawaje kwa nchi zetu za kiafrika kila kitu kinawezekana kwani hata Mh. Lwakatare alituhumiwa kuwa gaida ila sasa ni Mbunge, Mh. Magufuli anatuhuma za kivuko kwa sasa ni Rais, Mh. Mbowe na madawa ya kulevya)

Nilipokuja swala la Chadema kukosa muelekeo kwa kweli kwa hilo hata mimi ninakuunga mkono, ni kweli Mh. Mbowe amefanya mambo mengi, kuna mambo ambayo yalikuwa mazuri sana, na kuna mambo ambayo yalikitia chama doa kubwa, Sisi wapenzi wa Chadema tulitegemea kuwa Mh. Mbowe baada ya matokeo ya uchaguzi basi ilikuwa ni lazima yeye na team yake wajihudhuru lakini kama walivyo viongozi wa kiafrika wote swala la kuwajibika ni mwiko... Na matokeo ndo haya tunayoyaona Chadema si Chadema ile iliyobeba umoja na matumaini, si Chadema ya viongozi waliokuwa na ujasiri si Chadema iliyokuwa inamsemea mnyoge bali hii ni Chadema iliyokosa mwelekeo. Leo hii Lema yuko gerezani Mh. Mbowe anaendelea na maisha yake kama kawaida, Ben Saanane hajulikani alipo Mh. kimya kama vile hakuna kinachoendelea.. Tujikumbushe wakati Mh. Lwakatare alivyotuhumiwa na ugaidi jinsi wanachadema na viongozi wao walivyo kuwa wanachacharika kwa umoja leo hii anayejitutumua ni Mh. Lissu tu masikini hata Mnyika haonekani. Ni wakati sasa Mh. Mbowe awaachie vijana wake aliyowandaa zaidi ya miaka 10 kwani huu ni wakati wao na Chadema kinawahitaji sana. Ni wakati wa Mnyika, Mwalimu, Lissu, Lema, kuongoza chama..Mh. Mbowe uliyofanya yanatosha sasa pumzika tuone matunda ya malezi yako.
 

Nguruvi3

Platinum Member
Joined
Jun 21, 2010
Messages
13,417
Points
2,000

Nguruvi3

Platinum Member
Joined Jun 21, 2010
13,417 2,000
Alinda ahasante sana sana kwa kuchagiza mjadala. Ningependa kuchangia kidogo kwa mada uliyoelekeza kwa Freeland ambayo sehemu imebeba maudhui ya hoja nilizotoa jana.

Kuna mambo mawili
Suala la wasanii, sehemu ya pili ya mchango wako umeieleza vizuri sana kwa maana ile ile ambayo Freeland na wengine walioshangazwa na 'wasanii' wameonyesha taharuki

Nikuhakikishie suala si Wema kama msanii wala si Wema mwenye tuhuma
Wema ana haki kabisa ya kufanya mambo ya kisiasa kama mtu mwingine

Hoja ni kwa mujibu wa gazeti moja, Wema alikuwa apokelewe na Mbowe
Na ukitazama picha za mitandao Mbowe kakaa na Wema kama suala muhimu sana

Mbona Mbowe hakuonekana katika sakata la Ben Saanane na wala haionekani kama kuna jambo analofanya ikiwa miezi sasa tangu atoweke?

Yaani picha za Wema ni muhimu kuliko hali ya msaidizi wake asiyejulikana alipo ?

Pili, watu hawakumuona Mbowe wakati Lijualikali anahukumiwa kwenda Jela
Tatu, imechukua muda gani Mbowe kwenda kumuona Lema kule Gerezani
Nne, watu wangapi wa Chadema wanafungwa na wala hatusikii Mbowe akishughulika

Hayo ni mfano tu wa kuonyesha shamra shamra za kumpokea Wema at this critical time kwa Chama chake, demokarasia, na hata mfumo wa sheria halikuwa kipaumbele.

Zile Picha za Wema na Mbowe hazikuwa na maana kutokana na wakati na hali iliyopo

Wema angeweza kupokelewa na kiongozi yoyote wa ngazi ya kawaida.

Kitendo cha M/kiti kutajwa kumpokea wakati kuna burning issues nyingi ni cha dhalili

Kwamba, hakuona kingine katika siasa za nchi bali political stunt na Wema

Hivyo suala si Wema kujiunga, ndiyo maana tumetumia neno Bongoflevakuondoa hisia za personality attack. Suala ni wakati gani Mwenyekiti anafanya nini na kwanini kwa hadi ipi

Fikiri hivi dada yangu, watu wamefukuzwa Msumbiji, serikali haitoi taarifa na wanaopaswa kui hold accountable ni opposition kama kazi yao ya msingi

Nilishangaa ACT-Wazalendo wakatolea statement hata kama ni dhaifu lakini wametoa

Mwenyekiti na Uongozi wake hawajui nini kinaendelea nini kifanyike, ghafla watu wanawasikia katika masham sham na Bongofleva!!

Mhimili wa sheria upo katika wakti mgumu sana, majaji 'wanavyopata' tabu pale state attorney wanaposhindwa ''kutumia vifungu kadhaa'' kana kwamba kazi ya mahakama ni kufunga watu na si kusikiliza mashauri

Mawakili wanaambiwa kazi zao watafanyia mahubusu
Opposition ya Mbowe bukheri wa afya, ghafla nderemo na vifijo ujio wa Bongofleva

Kuna issues nyingi hawana habari, ghafla picha na mlimbwende kana kwamba sasa suluhu itapatikana.

Ukiyaangali hayo kwa upana utaona hoja ya kwanini watu wanakereka

Halafu wangefanya hivyo siku nyingine isingekuwa mbaya saana kama ilivyo.

Mbowe na Chadema wanamsubiri mlimbwende wakati wa kesi.
Inaondoa focus kuhusu kesi 'walizonazo' ambazo kiaini ni zina harufu ya kisiasa

Focus sasa ni Mwenyekiti wa Chadema na mlimbwende anayehamia. Please

Sehemu ya pili ya hoja yako nitaipitia, nilitaka kuchangia hii ya kwanza

Ahsante
 

Mwalimu

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2008
Messages
1,532
Points
1,500

Mwalimu

JF-Expert Member
Joined Aug 21, 2008
1,532 1,500
Mimi binafsi nimeshangazwa na ujio wa Wema CHADEMA kama nilivyoshangazwa na ujio wa Lowasa. Lakini kuna kitu kimoja ambacho tunapaswa kujiuliza na labda tukipata jibu itatusaidia kuelewa kinachoendelea sasa... "Watanzania/wapiga kura wanataka nini?", wanapokwenda kupiga kura wanaangalia nini kutoka kwa mwanasiasa?
Hebu tujikumbushe uchaguzi wa mwaka 2010 ambapo CCM ilikuwa imegubikwa na kashfa za richmond, epa, meremeta, vijisenti n.k. lakini bado wananchi sio tu waliipa kura ccm lakini wagombea wote waliotuhumiwa na kashfa walichaguliwa bungeni (lowasa, chenge...). Hii inatufundisha nini? Watanzania wanataka nini? Hoja nzito pekee zinatosha? Watanzania hawa tunaowasema kweli wako tayari kwa mabadiliko?
Tuangalie uchaguzi wa mwaka 2015 ambapo UKAWA walimsimamisha Lowasa matokeo yalikuwaje upande wa upinzani kulingana na uchaguzi wa mwaka 2010?

Kuna wakati nawaza na kufikiri labda sisi wanazuoni tunaojadiliana humu pia hatuelewi watanzania wanataka nini au wanatafuta nini kutoka kwa wanasiasa. Tunaweza kuwalaumu kwa haki kabisa chadema kwa kwenda kinyume na misimamo yao ya awali kwa kuwapokea kina Wema, Lowasa na wengineo, lakini LABDA narudia LABDA tunapaswa kutathmini upya watanzania wanataka nini.
 

Nguruvi3

Platinum Member
Joined
Jun 21, 2010
Messages
13,417
Points
2,000

Nguruvi3

Platinum Member
Joined Jun 21, 2010
13,417 2,000
Nilipokuja swala la Chadema kukosa muelekeo kwa kweli ninakuunga mkono, ni kweli Mh.

Mbowe amefanya mambo mengi, kuna mambo ambayo yalikuwa mazuri sana, na kuna mambo ambayo yalikitia chama doa kubwa, Mh. Mbowe baada ya matokeo ya uchaguzi basi ilikuwa ni lazima yeye na team yake wajihudhuru lakini kama walivyo viongozi wa kiafrika wote swala la kuwajibika ni mwiko...

Chadema si Chadema ile iliyobeba umoja na matumaini, si Chadema ya viongozi waliokuwa na ujasiri si Chadema iliyokuwa inamsemea mnyoge bali hii ni Chadema iliyokosa mwelekeo.

Ni wakati sasa Mh. Mbowe awaachie vijana wake aliyowandaa zaidi ya miaka 10 kwani huu ni wakati wao na Chadema kinawahitaji sana. Ni wakati wa Mnyika, Mwalimu, Lissu, Lema, kuongoza chama..Mh. Mbowe uliyofanya yanatosha sasa pumzika tuone matunda ya malezi yako.
Nianze ulipomalizia. Moja ya kazi kubwa za Mh Mbowe ni kutoa chama kutoka 'club' ya wastaafu na kuwa chama cha siasa kilichobeba matumaini ya Watanzani. Kazi hiyo ni pamoja na recruitment ya vijana

Vijana wamekuwa chachu iliyoineza Chadema katika maeneo mengi ikiwemo ya vijijini

Tuliona uchaguzi wa serikali za mitaa miaka michache iliyopita ilivyokuwa na nguvu
Kuna picha ya watu kama 20 wakishangilia kutwaa kitongoji huko vijijini kabisa

Tukaona watu wakijitoa na plot zao kule Iringa kujenga ofisi katika sakata la Mwandosya
Chama kikapata wabunge wengi kutoka maeneo ambayo CCM ilikuwa haifikirii

Maeneo salama ya CCM kama Morogoro, Tanga , Lindi ikawa si salama tena
Hayo hayakutokea kwa bahati mbaya ilikuwa ni jitihada za wanachama kufikia matarajio

Tatizo lilianza kuelekea 2015. Tulisema katika uzi huu,kundi lililohamia Chadema kwa muda mfupi na katika taharuki haikuwa jambo jepesi,kama ililazimu busara zilitakiwa kuhakikisha smooth transition

Tatizo la kufanya 'amalgamation' ni kitu kinachohitaji umakini, weledi na maarifa
Tuliposikia 'kanyaga twende' wengine tulifahamu hakukuwa na mipango wala vision

Tatizo hilo linaendelea, ni kama kuna makundi ingawa hayapo wazi.
Kazi alitakiwa kuifanya Mbowe katika amalgamation kupunguza effect ya upungufu wa awali.

Tatizo la pili,katibu mkuu. Dr Slaa alikuwa kama chama na hilo halikuwa utamaduni mzuri.
Kilichopaswa kufanya ni kupata katibu mkuu atakayekuwa na vision ya chama next level

Mbowe kwa mujibu wa katiba kamchagua Katibu mkuu ambaye hakuna sababu ya kutosema kapwaya

Mbowe amejikuta akiwa na wajibu wa KUB. Kama mtakumbuka tuliwahi kusema kazi hiyo anaweza kuifanya mtu mwingine Bungeni ili kumpa nafasi ya kushughulikia mengine, haikuwa hivyo

Ipo hoja dhaifu kuwa katika miaka zaidi ya 15 Mbowe amewezesha chama kuwa na wabunge wengi , kutwaa miji na majiji pamoja na vitongoji.

Ni hoja dhaifu kwasababu si suala la kupigia hatua, ni suala la unapiga hatua kwa kasi gani

Miaka 15 wabunge 30 kutoka 2,wanachama wasubiri mingine 15 kuwa na 60 inaeleza kasi ndogo.
Yes kama ameweza kufikisha hapo sasa atoe kijiti kwa mashine mpya inayoweza kutimua mbio zaidi

Mbio si mikutano tu bali kufanya chama cha upinzani kibeba hadhi yake kama mbadala wa serikali
Katika hayo ni muhimu kikajielekeza katika mambo ya Taifa na kimataifa.

Ni lazima kihakikishe kinagusa maisha ya kawaida ya wananchi na kinakuwa ndiyo 'loud speaker' na ''nyenyere'' wa kuiamsha serikali inapozembea au kulala.

Yapo amkundi ya jamii yenye kuhitaji sauti na sauti hiyo ndiyo ilitegemewa kutoka Chadema

Kwasasa hakuna kinachoendelea zaidi ya kuilamu CCM kwa uonevu.
CCM na serikali wanapofanya hayo ndilo lengo lao,si kuwalaumu kutimiza malengo ya kuua upinzani

Kunahitaji fikra mpya za kukabiliana na tatizo.
Fikra hizo zinaweza kutoka kwa watu nje ya uongozi wa sasa, wawe wazoefu au wenye maono tofauti.

Mbowe haonekani kuwa sahihi tukiangalia anavyoshughulikia mambo ndania ya chama chake.
Na kwa kukosa fikra mpya, sasa Bongofleva inaonekana kama ndiyo njia

Ukitazama madhaifu mengi ikiwemo kuongoza Chadema katika failures nyingi na bado amekuwa excused na ukiangalia anapokipeleka chama, nitashangaa kama kuna mtu atakuwa na matumaini

Katika kuzuia uharibifu unaoendelea hatua za haraka na za dharura zinahitajika
Hii ni pamoja na kumtaka Mbowe atoe nafasi kwa fikra mpya au ashinikizwe kutoa nafasi hiyo

Kusubiri hadi 2018 ni kulea ubovu na pengine kumkabidhi ajaye gari lisilo na taa wala matairi, linaunguruma tu, na abiria wana matumini litaondoka kwasababu kuna dereva mpya

Hapana, kama Chadema wanataka kujirudi na kujitathmini, waache kulalamikia externa factors wa deal na internal factors na hapa pa kuanzia ni kwa Mwenyekiti aliyepelekea chama kudorooora!

Tusemezane
 

Nguruvi3

Platinum Member
Joined
Jun 21, 2010
Messages
13,417
Points
2,000

Nguruvi3

Platinum Member
Joined Jun 21, 2010
13,417 2,000
Mimi binafsi nimeshangazwa na ujio wa Wema CHADEMA.

kitu kimoja ambacho tunapaswa kujiuliza na labda tukipata jibu itatusaidia kuelewa kinachoendelea sasa... "Watanzania/wapiga kura wanataka nini?",

wanapokwenda kupiga kura wanaangalia nini kutoka kwa mwanasiasa?

Uchaguzi wa mwaka 2010 ambapo CCM ilikuwa imegubikwa na kashfa za richmond, epa, meremeta, vijisenti n.k. lakini bado wananchi sio tu waliipa kura ccm lakini wagombea wote waliotuhumiwa na kashfa walichaguliwa bungeni (lowasa, chenge...). Hii inatufundisha nini?

Watanzania wanataka nini? Hoja nzito pekee zinatosha?
Watanzania hawa tunaowasema kweli wako tayari kwa mabadiliko?

Tuangalie uchaguzi wa mwaka 2015 ambapo UKAWA walimsimamisha Lowasa matokeo yalikuwaje upande wa upinzani kulingana na uchaguzi wa mwaka 2010?

Kuna wakati nawaza na kufikiri labda sisi wanazuoni tunaojadiliana humu pia hatuelewi watanzania wanataka nini au wanatafuta nini kutoka kwa wanasiasa. Tunaweza kuwalaumu kwa haki kabisa chadema kwa kwenda kinyume na misimamo yao ya awali kwa kuwapokea kina Wema, Lowasa na wengineo, lakini LABDA narudia LABDA tunapaswa kutathmini upya watanzania wanataka nini.
Mkuu una hoja nzito sana naomba nizipitie kwa maoni yangu binafsi

1. Watanzania wanataka nini? Jibu, si wanataka nini bali wamechoshwa na nini
Wanataka mabadiliko ya kweli katika mfumo wa kuendesha nchi nje ya CCM

CCM wanatambua, kushinda kwao chaguzi si kwasababu wanapendwa au kukubalika
Wenyewe wanatambua ndiyo maana wana program ya kukibadili chama

Katika hili uwepo wao wanatambua ni nafasi ya kuwa na serikali na vyombo vyake

wanatambua bila 'misuli' hawana chao na katika kuhakikisha hilo wameenda mbali zaidi

1. Wamemiliki vyombo vya umma, wakadhibiti taasisi zikiwemo za demokrasia

2. wamefanikiwa kumiliki mhimili mmoja,RC ametukumbusha
Mwingine upo mahututi. Unaweza kujiuliza nafasi za kukaimu nafasi zinaeleza nini.

3. Katika kuhakikisha udhibiti, sasa CCM/serikali yake wameingilia vyama vya kitaaluma
Ni kuhakikisha kama kuna sehemu, basi taasisi au mhimili unakuwa na 'total collapse'

4. Wamedhibiti vyama kwa marufuku ya mikutano. Wanajua hawana uwezo wa kujibu hoja, umma wa leo si wa kudanganyika kwa 'amani na utulivu'

Wanachi hawana uwezo wa kukwepa 'kushindwa' kama tulivyoona kule visiwani
CCM ikitaka 'uwe' unavyotaka utakuwa, wana tools zote za kuwezesha hayo kufanyika

Kwa mtazamo wangu, matokeo hayawezi kuwa kipimo cha wananchi wanataka nini
Tungekuwa na chaguzi katika mazingira halisia, tungeweza kujiuliza.
Kwa haya ya leo, ni ngumu

Hayo nayo yanajibu hoja kuwa wananchi wanapiga kura kitu gani?
Inawezakana wanapiga kura wanachokitaka, lakini si lazima wapate wanachokitaka kama tulivyoonyesha hapo juu

Hoja ya uchaguzi kugubikwa kwa rushwa na watu wakarudishwa Bungeni
Hili nalo linaelezwa vema na yote hapo juu, wakitaka liwe linakuwa, wana tools zote

Hoja kubwa inayohitimisha hayo hapo juu ni kuhusu Katiba.
CCM hawataki kabisa kuzungumzia katiba. Hii iliyopo ndiyo inawapa udhibiti wa kila aina

Mabadiliko yoyote yatakayoweka taasisi, mihimili , na demokrasia huru itawaumiza.

Hawana ushawishi mbele ya wananchi. Kama ni mgonjwa anapumuliwa mashine.
Mgonjwa huyo ukimwambia umeme uzimwe kufanya mabadiliko atakutandika kofi hapo ICU.

Hoja ya Chadema kulaumiwa: Hii haina siri, wakati Chadema inasimama kama opposition party iliweza kufanikisha mengi ikiwemo matumizi mabaya ya vyombo vya dola, mihimili kuwa huru kwa kiasi n.k.

Katika wakati tulio nao, inaonekana kana kwamba hakuna mbinu wala fikra mpya
Ikumbukwe hawa kama CCM wanadhima na wajibu kwa umma ndio maana kuna ruzuku

Tatizo linalojitokeza ni kama vile Chadema hawajui wafanye nini.

Kuna mbinu nyingi ikiwemo kujiweka katika nafasi ya chama mbadala kikiongelea mambo ya kitaifa na kimataifa. Kikiratibu na kuwa semeo la watu wasio na nafasi.

Ikitumia udhaifu unaojitokeza katika kujipambanua

Katika hali hii ya 'bongofleva' kuwa leading news, sidhani kama wapo njia sahihi.

Ndiyo maana tunasisitiza ni wakati wa kukaribisha fikra mpya, na wakati ni sasa

Tusemezane
 

Mwalimu

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2008
Messages
1,532
Points
1,500

Mwalimu

JF-Expert Member
Joined Aug 21, 2008
1,532 1,500
Mkuu una hoja nzito sana naomba nizipitie kwa maoni yangu binafsi

1. Watanzania wanataka nini? Jibu, si wanataka nini bali wamechoshwa na nini
Wanataka mabadiliko ya kweli katika mfumo wa kuendesha nchi nje ya CCM

CCM wanatambua, kushinda kwao chaguzi si kwasababu wanapendwa au kukubalika
Wenyewe wanatambua ndiyo maana wana program ya kukibadili chama

Katika hili uwepo wao wanatambua ni nafasi ya kuwa na serikali na vyombo vyake

wanatambua bila 'misuli' hawana chao na katika kuhakikisha hilo wameenda mbali zaidi

1. Wamemiliki vyombo vya umma, wakadhibiti taasisi zikiwemo za demokrasia

2. wamefanikiwa kumiliki mhimili mmoja,RC ametukumbusha
Mwingine upo mahututi. Unaweza kujiuliza nafasi za kukaimu nafasi zinaeleza nini.

3. Katika kuhakikisha udhibiti, sasa CCM/serikali yake wameingilia vyama vya kitaaluma
Ni kuhakikisha kama kuna sehemu, basi taasisi au mhimili unakuwa na 'total collapse'

4. Wamedhibiti vyama kwa marufuku ya mikutano. Wanajua hawana uwezo wa kujibu hoja, umma wa leo si wa kudanganyika kwa 'amani na utulivu'

Wanachi hawana uwezo wa kukwepa 'kushindwa' kama tulivyoona kule visiwani
CCM ikitaka 'uwe' unavyotaka utakuwa, wana tools zote za kuwezesha hayo kufanyika

Kwa mtazamo wangu, matokeo hayawezi kuwa kipimo cha wananchi wanataka nini
Tungekuwa na chaguzi katika mazingira halisia, tungeweza kujiuliza.
Kwa haya ya leo, ni ngumu

Hayo nayo yanajibu hoja kuwa wananchi wanapiga kura kitu gani?
Inawezakana wanapiga kura wanachokitaka, lakini si lazima wapate wanachokitaka kama tulivyoonyesha hapo juu

Hoja ya uchaguzi kugubikwa kwa rushwa na watu wakarudishwa Bungeni
Hili nalo linaelezwa vema na yote hapo juu, wakitaka liwe linakuwa, wana tools zote

Hoja kubwa inayohitimisha hayo hapo juu ni kuhusu Katiba.
CCM hawataki kabisa kuzungumzia katiba. Hii iliyopo ndiyo inawapa udhibiti wa kila aina

Mabadiliko yoyote yatakayoweka taasisi, mihimili , na demokrasia huru itawaumiza.

Hawana ushawishi mbele ya wananchi. Kama ni mgonjwa anapumuliwa mashine.
Mgonjwa huyo ukimwambia umeme uzimwe kufanya mabadiliko atakutandika kofi hapo ICU.

Hoja ya Chadema kulaumiwa: Hii haina siri, wakati Chadema inasimama kama opposition party iliweza kufanikisha mengi ikiwemo matumizi mabaya ya vyombo vya dola, mihimili kuwa huru kwa kiasi n.k.

Katika wakati tulio nao, inaonekana kana kwamba hakuna mbinu wala fikra mpya
Ikumbukwe hawa kama CCM wanadhima na wajibu kwa umma ndio maana kuna ruzuku

Tatizo linalojitokeza ni kama vile Chadema hawajui wafanye nini.

Kuna mbinu nyingi ikiwemo kujiweka katika nafasi ya chama mbadala kikiongelea mambo ya kitaifa na kimataifa. Kikiratibu na kuwa semeo la watu wasio na nafasi.

Ikitumia udhaifu unaojitokeza katika kujipambanua

Katika hali hii ya 'bongofleva' kuwa leading news, sidhani kama wapo njia sahihi.

Ndiyo maana tunasisitiza ni wakati wa kukaribisha fikra mpya, na wakati ni sasa

Tusemezane
Mkuu, yote uliyosema ni sahihi. Lakini bado kuna jambo moja muhimu sana kuliko hayo yote uliyoyaeleza nalo ni ELIMU NA UELEWA WA WANANCHI.

Kama kuna mahala ambapo utawala wa ccm umefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuchota akili za watu ni hapa... Ujinga wa mtanzania ni mtaji mkubwa wa ccm. Ndio wanatumia mbinu nyingi chafu lakini pia wana mtaji mkubwa wa wananchi wenye uelewa mdogo na uoga wa kufanya maamuzi magumu. Siamini kwamba kina chenge wameendelea kupita kwenye chaguzi zao kwa kutegemea rushwa asilimia 100% la hasha! Bado wana asilimia kubwa tu ya watu wanaowapenda na kuwaamini watu hawa hata usemeje bado wataendelea kuwaunga mkono.

Ndio maana nikatoa mfano wa 2010 ambapo upinzani ulipiga kelele za ufisadi lakini hazikusaidia na wale wale waliotuhumiwa wakarejea nafasi zao za ubunge. Unafikiri walipita kwa rushwa 100%? Sidhani!

Kuna wakati wananchi wakishaamua wanamtaka fulani haijalishi hata kama ana makandokando ya aina gani wataenda nae hivyo hivyo... Kama ikivyokuwa kwa bwana Trump huko marekani!

Kama kuna eneo la kufanyia kazi nchini kwetu ni elimu ya uraia, kuwawezesha raia kujitambua na kutambua na kusimamia haki zao, wajiamini bila woga... Tukifanikiwa hapo tutapiga hatua kubwa kwenye kujenga demokrasia imara.
 

Nguruvi3

Platinum Member
Joined
Jun 21, 2010
Messages
13,417
Points
2,000

Nguruvi3

Platinum Member
Joined Jun 21, 2010
13,417 2,000
Mkuu, yote uliyosema ni sahihi. Lakini bado kuna jambo moja muhimu sana kuliko hayo yote uliyoyaeleza nalo ni ELIMU NA UELEWA WA WANANCHI.

Kama kuna mahala ambapo utawala wa ccm umefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuchota akili za watu

Ujinga wa mtanzania ni mtaji mkubwa wa ccm, wanatumia mbinu nyingi chafu na mtaji mkubwa wa wananchi wenye uelewa mdogo na uoga wa kufanya maamuzi magumu.

Ndio maana nikatoa mfano wa 2010 ambapo upinzani ulipiga kelele za ufisadi lakini hazikusaidia na wale wale waliotuhumiwa wakarejea nafasi zao za ubunge.
Unafikiri walipita kwa rushwa 100%? Sidhani!

Kuna wakati wananchi wakishaamua wanamtaka fulani haijalishi hata kama ana makandokando ya aina gani wataenda nae hivyo hivyo... Kama ikivyokuwa kwa bwana Trump huko marekani!

Kama kuna eneo la kufanyia kazi nchini kwetu ni elimu ya uraia, kuwawezesha raia kujitambua na kutambua na kusimamia haki zao, wajiamini bila woga... Tukifanikiwa hapo tutapiga hatua kubwa kwenye kujenga demokrasia imara.
Mkuu ukirudi nyuma katika bandiko langu, nilisema ili kuhakikisha CCM inabaki madarakani wameamua 'kuua' taasisi zinazoojenga uelewa, na kuhakikisha elimu ya Uraia haiwafikii wananchi. Ndiyo maana halisi ya ''marufuku'' ya mikutano

Hilo nakubaliana nawe kama nilivyolieleza. Katika ujenzi wa uelewa wewe , mimi na yule hatuna platform. Nguvu za dola zitatumika kama nilivyoeleza pia, kuhakikisha tunaingia katika matatizo

Katika kufanikisha hilo unaweza kuona mwenendo mzima taasisi na mihimili ya nchi
Nalo tulilisema hapo juu ''kuingiliwa'' taasisi zinazotoa na kusimamia sheria

Kuna kundi ambalo kisheria lina platform. Hili ni la vyama vya siasa, ndipo hoja ya Chadema inapoingia.
Kwavile vyama vya siasa vina platform kazi ya elimu ya Uraia kwao ni wajibu na haki

Chadema ambao ni official opposition na wana haki za kisheria hawawezi kuliona hilo, kuna tatizo
Ndiyo msingi wa kusema kuna makundi yanayohitaji kuelimishwa na kusaidia kujielewa

Kazi hiyo inapokuwa haifanyiki katika maelfu kama unavyosema, halafu tunaona political stunt za bongofleva ndio msingi wa hoja zetu tangu mwanzo.

Bongofleva ni sehemu ndogo ukilinganisha na kile ulichosema 'Watanzania wengi' kwanini hawafikiwi?

Kwanini hakuna jitihada za kuondoa vikwazo vya kukuza demokrasia na uelewa wa watu?
Of course CCM hawafurahi na hawatakubali, lakini ni kosa kukubaliana nao

Hivyo leading news zinapokuwa bongofleva na ku ignore mamilioni yasiyo na weledi ni dereliction of duty and responsibilities kwa opposition party i.e Chadema

Nini kifanyike, ni ku review kama uongozi uliopo unakidhi haja na matakwa ya nyakati

Kuhusu rushwa 100% kupata watu kama wabunge, hapa uelewe haihitajiki hata 30%

Fikiria kunapokuwa na tofauti ya asilimia 3 unahitaji rushwa 100% au 3% tu kukamilisha zoezi?
Hatusemi rushwa ni 100% bali mfumo mzima unaotengeneza rushwa ni mkubwa sana

Mkuu utuambie katika vyombo vyote vinavyosika na demokrasia nchini ni kipi unachoweza ku single out kwamba kipo 'independent'?

Tusemezane
 

Mwalimu

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2008
Messages
1,532
Points
1,500

Mwalimu

JF-Expert Member
Joined Aug 21, 2008
1,532 1,500
Kuna kundi ambalo kisheria lina platform. Hili ni la vyama vya siasa, ndipo hoja ya Chadema inapoingia.
Kwavile vyama vya siasa vina platform kazi ya elimu ya Uraia kwao ni wajibu na haki
Watatekeleza vipi wajibu huo wa kutoa elimu ya kiraia wakati mikutano ya hadhara imepigwa marufuku? Au katika mazingira ambayo tamko la mwanasiasa linaweza kusababisha kushitakiwa kwa uchochezi? Vipi kuhusu nafasi ya wadau wengine kwenye kutoa elimu ya uraia? Au jukumu hili ni la vyama vya kisiasa pekee? ....na kwa muktadha wa mjadala huu tuseme ni jukumu la vyama vya upinzani? ...manake suala la elimu ya uraia sio kwa maslahi ya chama tawala...

Sio nia yangu kuwatetea chadema la hasha! Lakini najaribu kuangalia upande wa pili juu ya mazingira ya kisiasa kwa ujumla na nafasi yetu sisi kama raia kwenye ushiriki wa kikamilifu. Sisi wote ni mashahidi jinsi mchakato wa katiba mpya ulivyovurugwa kiasi kwamba hakuna matumaini kama utakuja kufufuka tena.

Ndio maana bado naendelea kujiuliza swali hili tena na tena; nini nafasi yetu kama raia kwenye ujenzi wa demokrasia imara? Au tunasubiri ujio wa "messiah" kutoka chama cha upinzani aje kutuokoa? Hivi vyama vya siasa vitafanya juhudi kwa kadiri ya uwezo wao na inawezekana vikafika mahala vikaishiwa pumzi... Sisi wananchi/raia tunasimama kwenye nafasi yetu?
 

Nguruvi3

Platinum Member
Joined
Jun 21, 2010
Messages
13,417
Points
2,000

Nguruvi3

Platinum Member
Joined Jun 21, 2010
13,417 2,000
"Mwalimu, post: 19901963, member: 11689"]Watatekeleza vipi wajibu huo wa kutoa elimu ya kiraia wakati mikutano ya hadhara imepigwa marufuku?
Au katika mazingira ambayo tamko la mwanasiasa linaweza kusababisha kushitakiwa kwa uchochezi?
Mkuu na hapa ndipo hoja yangu ilipo kuanzia mwanzo, kwamba, badala ya kushughulika na mambo madogo kama tunayosikia sasa, walipaswa kusimama kidete ili marufuku na madhila mengine yaondoke na kuwawezesha kuendelea na kazi. Kukaa kimya kwasababu kuna marufuku si jawabu la tatizo.

Akina Nyerere hawakukaa kimya hadi tukapata uhuru. Walikutana na vikwazo kama hivyo

Isitegemewe kuwa fursa, uhuru n.k. vinaweza kupatikana katika sahani ya dhahabu

Nikupe mifano, kuna kesi mahakamani. Halafu kuna shauri kuhusu haki ya dhamana.
Ni mambo mawili tofauti , moja likiwa la kisheria na lingine la 'kishari' . Mbona hatukuona jitihada

Vijana wa Chadema waliweza kuibua jambo hadi serikali ikajitokeza kuhusuvifo mto Ruvu

Uongozi haukuwa na habari wala haukutilia mkazo. Vijana waliwezaje uongozi ukashindwa? Maana yake, hoja inapojengwa mbele ya umma haikwepeki.
Walifanya hivyo kwa haya mengine?
Vipi kuhusu nafasi ya wadau wengine kwenye kutoa elimu ya uraia?Au jukumu hili ni la vyama vya kisiasa pekee? ....na kwa muktadha wa mjadala huu tuseme ni jukumu la vyama vya upinzani? ...manake suala la elimu ya uraia sio kwa maslahi ya chama tawala...
Ni jukumu letu sote lakini pia ukumbuke hoja yangu ya awali kuwa kuna jitihada za kuua au kudumaza taasisi zinazoshughulika na demokrasia.

Nikuulize, sakata la mikutano na marufuku ni taasisi gani binafsi au ya umma iliyowahi kutolea ufafanuzi? Hata vyombo vyenye dhima ya kutafsiri sheria havigusia.

Kila mmoja anaujua ukweli lakini nani amfunge paka kengele?
Hakuna ! kwasababu taasisi zote ziwe binafsi au umma zimeshaingiliwa

Ni kweli kila mmoja ana jukumu, lakini kufanikisha kazi kwa urahisi na ufanisi walio na platform wanatakiwa kuongoza wakisadiwa na mmoja mmoja
Lakini najaribu kuangalia upande wa pili juu ya mazingira ya kisiasa kwa ujumla na nafasi yetu sisi kama raia kwenye ushiriki wa kikamilifu. Sisi wote ni mashahidi jinsi mchakato wa katiba mpya ulivyovurugwa kiasi kwamba hakuna matumaini kama utakuja kufufuka tena.
Ni kweli raia wana mchango wao katika hili, lakini pia umehoji uelewana pengine tujiulize hawa Raia wasio na uelewa wanawezaje kuwa na uelewa kwa hili la elimu?
Inatupaswa sote tutimize wajibu, lakini wajibuuwe n a mwongozo kwa wenye weledi
Ndio maana bado naendelea kujiuliza swali hili tena na tena; nini nafasi yetu kama raia kwenye ujenzi wa demokrasia imara? Au tunasubiri ujio wa "messiah" kutoka chama cha upinzani aje kutuokoa?
Si ndio maana tuna mjadala hapa kama sehemu ya mchango wetu? Ni kweli Raia wana nafasi lakini usisahau swali lako, uelewa ni kiwango gani? Maana unaweza kuwa na milioni 30 wenye uelewa wakawa 3,000! Pamoja na hayo 3,000 wanaweZa kusaidia milioni 30, lakiji je wana platform?
Na hakuna messiah anayesubiri, bali kuna kuzembea tu unaoendelea
Hivi vyama vya siasa vitafanya juhudi kwa kadiri ya uwezo wao na inawezekana vikafika mahala vikaishiwa pumzi... Sisi wananchi/raia tunasimama kwenye nafasi yetu?
Kuna kuishiwa pumzi na kuzembea kuvuta pumzi.

Jitihada zikionekane zinathaminika bila kujali ukubwa au udogo wake.
Hizo zina justify kuishiwa pumzi. Lakini uzembe hauwezi kuwa sababu ya kuishiwa pumzi

Kama tunakubaliana, si mara zote Chadema waliwahi kufanikiwa siku za nyuma.

Hata hivyo wananchi waliweza kuona wapi wamekwama na kwanini na ndio maana palipokuwa na ugumu walikuwa tayari kuunga mkono jitihada hizo.
CCM wanatambua, ndio maana mambo kama ukuta yaliwatisha sana

Tatizo ni ambapo 'pumzi' hakuna, mwelekeo wa kutafuta pumzi haupo na wala maono ya kupatikana hayapo.

Huwezi kuishiwa pumzi kwa mambo mazito ukatumia kidogo kwa haya tunayoyaona

Lakini pia kama viongozi wanaona wameishiwa pumzi, na kweli wameishiwa, ndipo hoja ya kuwataka wakae pembeni ili waje wengine wenye mtazamo tofauti.

Mtu akizembea kuvuta pumzi huwezi kusema watu hawavuti pumzi.
Wapo wenye uwezo na ndio wanatakiwa sasa hivi

Wapo wanaojua pumzi inapatikanaje na ndio wanaohitajika.
Hawa walioshiwa pumzi kama Mwenyekiti wa Chadema watoe nafasi.

Kuishi na walioishiwa pumzi kwa kudhani hakuna wenye mbinu tofauti ni kosa kubwa linalosubiri kuigharimu Chadema.

Mkuu katika michezo kama soka kuna substitution, aliyeishiwa pumzi anatoka
Kama hataki kutoka anatolewa na benchi la ufundi.

Ni makosa kusubiri walioshiwa pumzi wafie uwanjani, timu itakuwa inapokea magoli

Mwisho wake wasio na pumzi watazimia, timu itafungwa. Kwanini kusiwe na sub sasa hivi?

Tusemezane
 

JingalaFalsafa

JF-Expert Member
Joined
Apr 13, 2012
Messages
762
Points
250

JingalaFalsafa

JF-Expert Member
Joined Apr 13, 2012
762 250
Mkuu Mwalimu umehoji maswali mawili ya msingi sana katika mjadala huu...
A: Ni nini wapiga wengi wanazingatia katika chaguzi zetu juu ya wanasiasa. Nini kinamsukuma mtu kumpigia kura mgombea fulani?

B: Sisi kama raia wa kawaida ipi i nafasi yetu katika yote haya yanayoondelea? Na ni tumeicheza kwa kiasi gani?

Tukianza na hoja A niseme haya... Kupiga kura ni tendo la Kufanya Maamuzi, na maamuzi ya binadamu hutegemea mambo makuu mawili. Aidha ni maamuzi zao la HISIA zake au ni maamuzi zao la MANTIKI YA MAMBO kutokana na tafakari zake za kina. Kwanini uamue hivi na si vinginevyo.

Uwezo wa kuamua jambo kwa Hisia zake mtu ni wa kuzaliwa nao/wa asili, lakini ule wa kutumia Tafakari za kina ni lazima uasisiwe.

Daily experience zetu ni aidha zitakomaza Hisia zetu ama kuzidumaza na kukweza Mantiki vichwani mwetu. Jambo muhimu ni nini kinafunga nyendo zako za kila siku. Unasikia nini, Unaona nini, Unaongea nini, Unatenda nini na nini ni marufuku. Ni mvutano kati ya Vifungo vyako na Uhuru wako.

Siasa zinahubiri unafiki halikadhalika makanisa na misikiti, mitaani tunashuhudia unafiki, mashuleni na vyuoni, si redio si Tv na gazeti, si bunge, mahakama wala serikali ni unafiki kila kona. I wapi nafasi ya kutumia mantiki? Nisipoamua kwa dini yangu, basi chama changu, au kabila langu, hata sura zao pia mavazi yao, au potelea mbali kama si usela na umaarufu. Ni HISIA zetu juu ya wanasiasa wetu. Na atakayewagusa wengi ndio mshindi wetu.

Watu aina hiyo si wa kupewa WANACHOTAKA ila tu kile WANACHOPASWA KUPATA, ndio maana natamka wazi Mimi si muumini wa Demokrasia aina hii ya hapa kwetu, Si wakati wake hapa kwetu, ni KIINI MACHO CHA WAZI KABISA.

Kuna kauli za kujifariji ati hizi ni hatua za kujenga hiyo Demokrasia ya kwa wenzetu, ni Uongo, na hicho ni Kifungo cha Unyonge wetu. Dunia haiwezi kufikia huko, na kama ikifika haitomaliza Unyonge tulionao. Nafasi yetu hawezi kubadilishwa na hilo, tutabaki kuwa Wanyonge milele, labda kama kuna atakayetuthibitishia uwepo wa Afrika pasipo kufungamana na dunia ya nje.

Hoja B, ipi ni nafasi yetu kama raia inaumiza zaidi moyo...
Mkuu Nguruvi3, tutabaki kuilamu serikali na upinzani, na vizazi vitapita. Kama unakubali kuwa werevu 3000 wanaweza kuwabadili watu milioni 30, hiyo ndio Fahari kuu kabisa ijengayo tumaini jipya, kumbe INAWEZEKANA. Kukosa platform hakufanyi isiwezekane, na Werevu hapo utapimwa kwanza kwa kujitengenezea hiyo platform, na kwa kuwa u mwerevu Hautashindwa, kwani dhambi haijawahi kuwa smart.

Kamwe wajibu wetu hauwezi ishia katika kukosoa serikali na upinzani tu, nafasi yetu ni kuu na takatifu pia.

Harakati za kweli hazilengi Ikulu, tutabaki kuwa watumwa wa uchaguzi vizazi na vizazi. Harakati sahihi ni zile zilengazo Zinazotanguliza maslahi ya umma kwanza laa ni kiini macho.

Hizi si nyakati za mivutano isiyokuwa na lazima, aina ya serikali ya sasa ni mtaji bora kabisa kwa wanasiasa wetu, tatizo tu Ikulu ndio lengo letu. Hatutafika tusipobadilika.
Anaita sasa.
 

Mwalimu

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2008
Messages
1,532
Points
1,500

Mwalimu

JF-Expert Member
Joined Aug 21, 2008
1,532 1,500
Wakuu Nguruvi3 na JingalaFalsafa nawasoma vyema.

Mimi naamini mabadiliko yatakuja kwa njia mbili,

Njia ya kwanza ni njia ya kistaarabu kupitia sanduku la kura
AU
Njia ya pili ni pale wananchi wakichoka wakaamua kuanzisha mabadiliko Tunisia style bila kusubiri wanasiasa na vyama vyao vya upinzani.

Kwa upande wetu njia ipi tutatumia ni juu yetu sisi kwa namna tunavyoendenda sasa... vyama vya siasa vikishindwa basi wananchi wenyewe wakichoka wataamua basi imetosha!
 

Freeland

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2012
Messages
14,506
Points
2,000

Freeland

JF-Expert Member
Joined Jan 24, 2012
14,506 2,000
Wakuu Nguruvi3 na JingalaFalsafa nawasoma vyema.

Mimi naamini mabadiliko yatakuja kwa njia mbili,

Njia ya kwanza ni njia ya kistaarabu kupitia sanduku la kura
AU
Njia ya pili ni pale wananchi wakichoka wakaamua kuanzisha mabadiliko Tunisia style bila kusubiri wanasiasa na vyama vyao vya upinzani.

Kwa upande wetu njia ipi tutatumia ni juu yetu sisi kwa namna tunavyoendenda sasa... vyama vya siasa vikishindwa basi wananchi wenyewe wakichoka wataamua basi imetosha!

Mkuu Mwalimu Nguruvi3 JingalaFalsafa nawasoma vyema.

Kwa nchi yetu suala la mabadiliko bado ni jambo linalohitaji subira sana.

Wananchi wanajua ni mabadiliko gani wanayataka? Je wananchi wanajua kuwa mabadiliko yanatakiwa yaanzie kwa nani?

Mabadiliko ya kweli ya jamii yoyote yale yaliyofanikiwa yalitokana na watu "People centred"

Umekuwa ni utamaduni wa watanzania kutegemea fulani..lets say Mbowe atafanya wonders peke yake.Tuna mfano wa viongozi wengi ambao wamejitoa hadi kifo mfano mawazo...wengine wamefungwa mfano Lema .Hawa wote jamii haijawathamini na kuona kama walikuwa ni advocates wa mabadiliko.Wamekufa na familia zao tu ndio zimebaki kusononeka...Lema yuko jela lakini wananchi hawajaonesha walau hata mwamko wa kumwunga mkono mbunge wao.

Nguruvi3 ilihali tunakubaliana kabisa kuwa tunahitaji watu wa kutuongoza katika ajenda ya mabadiliko ,watu ambao watawaeleza wananchi na kuwaongoza katika mabadiliko ya kweli..Watu hao wamekuwa wanapoteza focus...na wamekuwa dhaifu sana katika kuwafumbua wananchi na kuwaongoza katika mabadiliko hayo.

Kitu kingine ni tabia ya unafiki ya watanzania....watanzania ni wanafiki watajifanya wanachukia kitu fulani lakini kumbe hawamaanishi wakisemacho.Mfano Ufisadi ni kwamba watanzania wanajifanya wanauchukia wakati sio kweli..Jamii ya watanzania inapenda kuongelea ufisadi kama ni tatizo lakini si kweli..Mfano sio ajabu kukuta mtu aliyepata madaraka makubwa serikalini na akaacha kuiba jamii ikamuona kama ni mjinga na kwamba hakutumia nafasi.

Hawa ndio watanzania na ndivyo tulivyo

Mimi sijui suluhisho la tabia ya unafiki "dishonesty " ni nini
 

JingalaFalsafa

JF-Expert Member
Joined
Apr 13, 2012
Messages
762
Points
250

JingalaFalsafa

JF-Expert Member
Joined Apr 13, 2012
762 250
Wakuu Nguruvi3 na JingalaFalsafa nawasoma vyema.

Mimi naamini mabadiliko yatakuja kwa njia mbili,

Njia ya kwanza ni njia ya kistaarabu kupitia sanduku la kura
AU
Njia ya pili ni pale wananchi wakichoka wakaamua kuanzisha mabadiliko Tunisia style bila kusubiri wanasiasa na vyama vyao vya upinzani.

Kwa upande wetu njia ipi tutatumia ni juu yetu sisi kwa namna tunavyoendenda sasa... vyama vya siasa vikishindwa basi wananchi wenyewe wakichoka wataamua basi imetosha!
Mkuu, Tunachotaka kubadilisha si watu, bali ni ile hali iliyoota mizizi muda mrefu, hali ya keki ya Taifa kutowafikia wapaswao kwa Usawa na kwa Wakati. Hicho ndicho cha kubadilisha.

Silaha pekee katika vita hiyo ni KUJITAMBUA, watu Wajitambue. Na kujitambua ni Kutimiza Wajibu wako ili Kuilinda Haki yako kama raia katika umma.

Boksi la Kura au kushikiana mishale mitaani pasi na Watu Kujitambua ni kazi bure na hasara tupu. Kama raia, tumeshindwa kutimiza wajibu wetu na ndio maana tunapoteza haki zetu, ni kutojitambua.

Inahitajika SADAKA katika kutimiza wajibu, watu wanapaswa kuona/kushuhudia matunda ya Kutimiza wajibu, ni lazima tupate wa kujitoa kuishi wajibu wao. Ni sadaka kwa kuwa wajibu wako leo hauwezi kuwa ulinzi wa haki yako leo, ila ni mbegu bora ya ulinzi wa haki yako kesho.

Kama kitakachotangulizwa ni maslahi ya umma, pasi na shaka hiyo ni sadaka ndogo. Tunachopaswa kuanza kujenga ni hali ya Kujitambua kwa umma, ili kesho umma uwe na nafasi ya kufanya maamuzi sahihi, iwe kwenye box la kura, barabarani, mstuni, shuleni, n.k. Ni lazima watu Wajitambue kwanza.
Anaita sasa.
 

Mwalimu

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2008
Messages
1,532
Points
1,500

Mwalimu

JF-Expert Member
Joined Aug 21, 2008
1,532 1,500
wakuu JingalaFalsafa & Freeland nimewasoma vyema,

Mabadiliko ya kweli lazima yatoke kwa WANANCHI. Wananchi wanapaswa kuwa ndio wanaotoa ajenda itakayofuatwa na wanasiasa na sio kinyume chake. Hapo ndipo suala zima la kujitambua na kuelewa haswa mabadiliyo yanayotakiwa ni yepi haswa. Vyama vya siasa vimefanya kadiri ya uwezo wao. Kina Mbowe, CHADEMA, UKAWA hawatakuwepo milele... wanaweza kufutika na wakaja wengine lakini mwisho wa siku kama sisi wananchi hatutasimama kwenye nafasi yetu tutaendelea kupiga danadana zilezile miaka nenda rudi. Tutaendelea kusubiri "masihi" wa upinzani aje lakini hatatokea...

Hivi tumewahi kutafakari ni nini kilichotokea kule Tunisia kiasi kwamba tukio la yule kijana kujichoma moto ndilo likasababisha maandamano yalioing'oa serikali? Tukio lile lingeweza kulalamikiwa kwa wiki kadhaa halafu ingesahaulika lakini hali haikuwa hivyo. Wale wananchi walikuwa na machungu yao ya miaka mingi na lilivyotokea lile tukio ikawa kama petroli imemwagwa kwenye kijinga cha moto... na walipofikia hatua ile hawakusubiri wanasiasa wakalianzisha wenyewe.

Sisi kama wananchi bado hatujafikia kiwango cha kupigika vya kutosha kiasi cha kusema "sasa imetosha" tunataka mabadiliko. Tukishafika hatua hiyo hata wanasiasa watatuheshimu na watafuata matakwa yetu sababu watakuwa wanajua fika kwamba wakienda kinyume wataondolewa kwa heri ama kwa shari! Sasa hivi wanasiasa wanaenjoy sababu wanajua kwamba hata wavurunde kiasi gani ikifika wakati wa kampeni watagawa tshirt, khanga na ubwabwa inatosha kuwabakisha madarakani.
 

Nguruvi3

Platinum Member
Joined
Jun 21, 2010
Messages
13,417
Points
2,000

Nguruvi3

Platinum Member
Joined Jun 21, 2010
13,417 2,000
Ni kweli Tunisia ilitokea hivyo.
Lakini pia kumbuka Poland ilikuwa zao la vyama vya wafanyakazi.
Iran ilikuwa zao la wanafunzi wa vyuo vikuu.
Kenya ilikuwa zao la vyama vya upinzani
Zambia ilikuwa mwamko wa wafanyakazi
Kuanguka kwa Berlin wall ilikuwa zao la kizazi kipya cha vijana
Tianmen ilikuwa zao la kupiga kwa wananchi kiuchumi na kidemokrasia

Hoja ni kuwa katika mabadiliko hakuna formula moja au 'one size fits all'

Muda wa kusubiri 'masiah'upinzani ni sawa na ule wa kusubiri watu wajitambue

Kujitambua ni tukio la asili (natural) kwamba watu wanafahamu lipo tatizo

Kujikwamua baada ya kujitambua ni tukio linalopatikana (acquired)

Bunge la kwanza la Upinzani Karimjee Marando na Lamwai waliangaliwa kama 'wahaini'.

Walipojenga hoja wananchi wakaona waongeze.
Tulipokuwa na akina Slaa msisimko ukazidi na leo si suala tena la kuwatisha wananchi

Role ya kuufanya upinzani uonekane mbadala wa serikali ilifanywa na wapinzani

Hatupo tena zama hizo, hoja ni je wapinzani wanasaidia umma kujitambua zaidi na kwenda next level?

Kwa hali ya sasa ni afadhali miaka 15 iliyopita.
Hakuna jitihada za kimkakati kusaidi watu wajikwamue hata kama wanajitambua.

Wanafunzi darasani wanajitambua wapo kubadilisha maisha kwa elimu. Wanajitambua

Haitoshi tu kujitambua, lazima wawe na instructors kuwasaidia kuweka tambuzi zao katika muktadha sahihi, kuwapa mbinu na njia mbadala za kufikia matarajio yao

Mfano huo ni sawa na huu wa Watanzania wanapkwenda kupiga kura
Tusiwalaumu kwasababu kitendo tu cha kutumia haki hiyo ni kujitambua

Tuwalaumu instructors kwa kushindwa kuwasaidia kutambua utambuzi walio nao

Ungeniuliza kama 'instructor' wao ningekwambia tatizo si kura, tatizo ni mfumo mzima

Mfumo umezinga njia zote za kidemokrasia au ziwazo.
Mahali pa kuanzia ni kurekebisha mfumo huo.

Marekebisho si ya watu ni ya taratibu tunazojiwekea ili wanasiasa watuheshimu nasi tuwaheshimu. Taratibu hizo ni katiba ambayo ni mwongozo

Wapinzani wanaposhindwa kuliona hilo, wanawezaje kuweka msukumo wa mabadiliko? Wapinzani wanapohangaika na bongofleva watawezaje kuufikia umma kwa utambuzi? Wapinzani wanapodorora nani amebeba dhima ya uamsho na uongozi?
 

JingalaFalsafa

JF-Expert Member
Joined
Apr 13, 2012
Messages
762
Points
250

JingalaFalsafa

JF-Expert Member
Joined Apr 13, 2012
762 250
Mkuu Nguruvi3 sifikiri kama nimekupata vyema katika hoja zako hapo juu...

Kwamba muda wa kusubiri watu Wajitambue, ni sawa na kusubiri muujiza wa masiah kushukia upinzani. Je, ni lipi tunaloweza kufanikisha pasipo kusubiri watu kujitambua?

Kwamba Kujitambua ni tukio la Asili, je inamaananisha kujitambua hutokea accidentaly?

Nafikiri tunaposema Kujitambua, ni kujitambua kwake mtu kama raia sehemu ya umma wa Taifa fulani, si ile hali ya kupayuka hovyo labda.

Kusimama tu peke yake kwenye mistari ya Kura au kuingia darasani, hakushuhudii Utambuzi huu tuusemao, labda tu kumtofautisha na viumbe vingine. Labda huo ndio waweza itwa wa asili. Utashi tu wa kawaida hauwezi kuwa ni Kujitambua kama raia wa umma wa Taifa fulani.

Mkuu, tuwatupie lawama ma-instructors na si raia, je huko si kusubiri mesiah wa kutuletea ukombozi?

Kama tatizo ni ma-instructors na mfumo, je ni nini kinachoweza kuleta mabadiliko hayo pasi na umma kujitambua? Je, kuna njia mbadala ya kusonga mbele licha ya kutojitambua kwetu? Taratibu ziliwekwa na zitawekwa, lakini zitavunjwa na haohao wasiojitambua, na watakenua meno.

Ninasisitiza, tunachopaswa kukibadilisha, ni ile hali ya Rasilimali za nchi kushindwa kufikia umma kwa usawa na kwa wakati. Si rangi ya chama wala bendera. Ili kufikia hilo watu hawana budi Kujitambua.

Ni SADAKA, haikwepeki.

Anaita sasa.
 

Nguruvi3

Platinum Member
Joined
Jun 21, 2010
Messages
13,417
Points
2,000

Nguruvi3

Platinum Member
Joined Jun 21, 2010
13,417 2,000
JingalaFalsafa ninaposema kujitambua nilikuwa najibu hoja ya Mwalimu kuwa Watanzania hawajitambui.

Kujitambua ni katika hali ya kuelewa kuwa hakuna kinachoweza kubadilika katika kutenda yale yake kila siku kwa mtindo ule ule na watu wale wale 'insanity'

Watu wanatambua, umasikini wetu si jambo la bahati mbaya, ni zao la tatizo
Hiyo tu inatosha kujitambua, na kujitambua ni hatua ya kwanza ya ku solve tatizo

Haitoshi kujitambua, inapaswa mwongozo wa kuondoka katika utambuzi kwenda mbele
Hapo ndipo niliposema si kila mmoja ataweza, tutahitaji wakutuongoza 'instructors'

Mwalimu anauliza, tumsubiri mesiah wa upinzani au tuache kwanza watu wajitambue?
Nina maoni, watu wanajitambua, hawahitaji mesiah wanahitaji mwongozo

Mwongozo si kuwaambia wanachague nini, wanapata nini katika sanduku la kura
Mwongozo si kumtaka nani awe kiongozi nani awe mfuasi

Mwongozo ni utaratibu utakaongoza jamii iishi kwa kuheshiminiana na kuwajibika

Hatuwezi kuwa na mwongozo wa mfukoni, bali ule tutakaojiwekea kwa jina la katiba
Ni kupitia katiba hiyo tutaweza kufumua mfumo usiotupa matokeo kwa miaka 50

Tutaweza kuwapa wananchi silaha ya kuwawajibisha wahusika na si kuwajibishwa tu. Tutawapa wananchi sauti na nguvu ya kuamua hatma yao na si kaumuliwa

Tutaweza kuwekea mizani za haki zetu na mipaka yake, na kuzilinda kwa matakwa yetu
Ni kwa njia hiyo tu, tutaweza kutumia vema utambuzi wetu katika kuamua hatma yetu

Hoja, ni je tuna instructors wa kazi hiyo? Wanajua wanatakiwa kufanya nini?
Wanatimiza wajibu wao ili nasi tutimize wetu? n.k.

Tusemezane
 

JingalaFalsafa

JF-Expert Member
Joined
Apr 13, 2012
Messages
762
Points
250

JingalaFalsafa

JF-Expert Member
Joined Apr 13, 2012
762 250
Nimekupata Mkuu.
Nikijibia swali lako kama tuna instructors na kama wanajua wajibu wao na kuuwajibikia. Ni wazi nafasi yao ipo, na wenyewe waliojivika kofia hizo wapo, lakini wanachofanya ni Ubatili. Hivyo tunaweza sema ni Watu Hewa.

Swali, ni je huo ndio ukomo wa ndoto za wananchi wetu? Je, Hatima ya umma wetu inabebwa na hilo tu, kiasi hatuwezi kufanikiwa katika lolote pasipo wao?

Nafikiri huo ndio msingi wa hoja ya Mwalimu, IPI I NAFASI YETU KAMA RAIA KATIKA KUONDOA UNYONGE WETU? Nafikiri huo ndio mwanzo wa UTAMBUZI wa kweli.

Anaita sasa.
 

Forum statistics

Threads 1,365,007
Members 521,095
Posts 33,335,608
Top