CHADEMA/UKAWA: Uwekezaji usiotabirika

Alinda na Jokakuu;

Posti zenu zilinifanya nisome sifa za Dr. Slaa na kumkubali. Ghafla bin vuu, naona mmemwacha mzee wa watu na kumbeba Lowassa. Hakika siasa hazina marafiki na maadui wa kudumu.

Zakumi sisi au mimi sikumuacha Dr. Slaa ila yenye ndo katuacha tangu tarehe 28.7 yeye si mwanasiasa tena.. Sasa tumfuate fuate kwanini?

Ila Dr. Slaa atabaki kuwa "my hero" katika siasa za Tanzania, ametutoa mbali amepitia mengi lakini ndivyo hivyo ilivyotokea, na maisha ni lazima yaendele hayatusubiri...
 
Sijakuelewa unakata sek ya nini wakati unatakiwa kumuelewa msemaji! Hii hapa rudia kusikiliza

Nimekuuliza ni wapi amesema ni "zamu ya walutheri" Huwa sipendi mijadala ya dini maana ni mijadala ambayo inabomoa badala ya kujenga, tuko hapa kujenga si kubomoa lakini pale mtu mzima kama wewe unapotoa tafisiri ya jambo kama hili kwa "mahaba yako mwenyewe ili pate kaupenyo ka kunanga dini nyingine kwa kweli ninakuwa na wasi wasi na mapenzi kwa mama yetu Tanzania.

Kumbuka sitetei maneno yake, ambayo hakupaswa kuyatoa na kwa bahati mbaya au nzuri ameona kosa lake na kuomba msamaha hivyo basi sioni mimi na wewe kukuza ili swala tunalikuza kwa faida ya nani? au ili iweje?
 
NasDaz Si kweli kuwa ninatetea mgombea wangu, kwa kweli nitasema uongo kama nitasema nina mahaba na Lowassa..rejea maandishi yangu ya nyuma. Lakini nashindwa kuelewa mtu anapomwanga petrol kwenye nyumba inayowaka moto unategemea nini..

Sipendi kujadili mambo ya dini, kwenye mjadala ya dini huwa ninakuwa na kigugumizi gafla lakini hapo hapo sipendi kuona mtu anamtia maneno binadamu mwenzake ili akidhi haja zake.. Alichokifanya Lowassa ni kosa na ameona hilo na kuomba msamaha...

Bado ninafahamu kuwa nina deni la kujibu hoja zako..
 
Last edited by a moderator:
Mwalimu,

Katika mazungumzo au majadiliano kuna kitu kinaitwa context. Ni muhimu sana katika kufikia muafaka.

FACT: Richmond ilifanyika chini ya serikali ya CCM, na kwa jinsi serikali ya CCM inavyoendeshwa hakukuwa na hatua za kisheria zilizochukuliwa.

CDM kwa kujua hiyo fact hapo juu, wakaenda kushitaki kwa wananchi. Ndio maana leo unaona yanayoitwa mafuriko kwenye mikutano ya CDM kuelekea uchaguzi mkuu. Ambaye alishtakiwa kwa wananchi na CMD akitaka kujibu mashtaka yake (kwa kipindi hiki ambacho bado CCM inaongoza), inabidi akajibu hayo mashitaka kwa wananchi ambako alishtakiwa. Sasa ukisema kuwa jukwaani sio sehemu ya kujisafisha bali ni kwenye vyombo vya sheria (which is true) katika muktadha huu tunaouongelea unakuwa out of context. Ni kama vile hujui hili suala lilianzia wapi na lipo katika mazingira gani. Hizo kauli za mwenye ushahidi aende mahakamani ni kauli za ki CCM CCM tu. Wewe unazisema kwa kebehi kelele za mitaani juu ya ufisadi kwa miaka 8 lakini najua unajua kuwa umaarufu wa kisiasa ambao upinzani unafaidi sasa hivi umetokana na hizo unazo ziita kelele za mitaani. Na sitaki kuamini kuwa katika all seriousness unahoji vyombo vya dola vinafanya kazi gani katika zama hizi za CCM katika kujenga hoja zako.

Na ili tusiende nje ya maada kidogo, naomba niseme nukta tunaizungumzia hapa, ni hoja yangu hapa ni kuwa Lowasa alipaswa sio kujieleza kwa kamati kuu peke yake, bali ilipaswa aidha akajieleza kwa wananchi ambao kwa miaka 8 waliambiwa taarifa ya uvundo wa Lowasa au kamati kuu ieleze Lowasa alitoa vielezo gani vilivyo fanya ushahidi waliotangaza kwa miaka 8 kuwa wanao juu yake uwe hauna msingi tena.

Na ili kuondoa kujirudia rudia kwa maswali na hoja zile zile, mimi ukinipa mjadala unaosema kwa nini CCM haiwezi kufanya mabadiliko yanayotangazwa na Magufuli katika kampeni zake, nitazungumza na kuzungumza kila ufisadi uliowahi kutokea katika serikali za CCM zilizopita kujenga hoja zangu. Katika mjadala huo sitakaa hata sehemu moja kwenye hoja zangu nikamtaja Lowasa eti alihusika na Richmondi. Kwa sababu hicho kitu japo ni kweli, kitakuwa kiko nje ya mada husika.

Mahala tunapotofautiana ni padogo sana ndug yangu;

Wewe unaona kujieleza mbele ya kamati kuu pekee haitoshi wakati mimi nalitazama suala hili kwa mapana zaidi. Waliokuwa na maamuzi ya kumkaribisha Lowasa na kumpitisha kuwa mgombea ni kamati kuu ya chadema pamoja na washirika wenzao wa UKAWA. Ndio maana kamati kuu walimwita kikaoni kumhoji juu ya tuhuma zake na awawapa majibu yaliowaridhisha.

Sina tatizo na yeye kusimama jukwaani kujisafisha tuhuma dhidi yake lakini mwisho wa siku tujiulize hiyo pekee inatosha? Kashfa ya Richmond imekuwapo kwa miaka 8 sasa lakini tumefanya nini zaidi ya kuongea tu majukwaani? Nini kitabadilika sasa hata kama Lowasa akisimama jukwaani "kujisafisha"? Mwaka 2010 wakati bado Richmond ni mbichi hakujisafisha jukwaani na akashinda kwa kishindo jimboni kwake huku akipigiwa debe na mwenyekiti wake, nini kimebadilika sasa hivi? Kwani JK aliposema kuwa ile ilikuwa ni "ajali ya kisiasa" hakumsafisha wakati ule?

Mwakyembe aliropoka bungeni kwamba kuna mengine waliyamezea kuinusuru serikali isianguke... alikuwa anamlinda nani wakati Lowasa alikuwa ameishajiuzulu? Halafu leo anaibuka tena na kudai ufanyike mdahalo kati yake, Lowasa na Slaa... halafu baada ya mdahalo then what?

Ndio maana nikasema shida kubwa tumekuwa ni watu wa kupiga kelele majukwaani miaka nenda miaka rudi. Richmond imekuwapo miaka 8 sasa lakini mpaka leo tunataka kuendelea kulumbana majukwaani tu! Unafikiri Lowasa akishaongea jukwaani ndio itaishia hapo?
 
Alinda na Jokakuu;

Posti zenu zilinifanya nisome sifa za Dr. Slaa na kumkubali. Ghafla bin vuu, naona mmemwacha mzee wa watu na kumbeba Lowassa. Hakika siasa hazina marafiki na maadui wa kudumu.

..hata mimi aliyenivutia kuipenda CDM ni Dr.Slaa.

..pamoja na mapungufu yake ya kibinadamu naamini CDM isingefika hapo ilipo bila mchango wa Dr.Slaa.

..binafsi I wish CDM na Dr.Slaa wangemaliza tofauti zao ktk namna tofauti na ya kistaarabu kuliko hivi walivyofanya.

..pamoja na kumpenda Dr.Slaa, wako wana-CDM wengine ambao wamenivutia; watu kama Tundu Lissu, John Mnyika, Halima Mdee, Benson Kigaila, Godbless Lema, Mohamed Mtoi, Tumaini Makene, etc etc. Hatuwezi kuwatupa mkono wote hao kwasababu tu Dr.Slaa ameamua kubwaga manyanga.

..kama wanavyosema ktk siasa hakuna maadui wa kudumu, I hope and pray kwamba Dr.Slaa atarudishwa kundini wakati CDM na UKAWA wameingia madarakani.



NB:

..Particularly nachukizwa sana na mashambulizi yanayoelekezwa kwa mke wa Dr.Slaa. Mimi naamini kumshambulia mke wa mtu, au watoto wake, ni kuvuka mpaka wa siasa za kistaarabu.
 
..hata mimi aliyenivutia kuipenda CDM ni Dr.Slaa.

..pamoja na mapungufu yake ya kibinadamu naamini CDM isingefika hapo ilipo bila mchango wa Dr.Slaa.

..binafsi I wish CDM na Dr.Slaa wangemaliza tofauti zao ktk namna tofauti na ya kistaarabu kuliko hivi walivyofanya.

..pamoja na kumpenda Dr.Slaa, wako wana-CDM wengine ambao wamenivutia; watu kama Tundu Lissu, John Mnyika, Halima Mdee, Benson Kigaila, Godbless Lema, Mohamed Mtoi, Tumaini Makene, etc etc. Hatuwezi kuwatupa mkono wote hao kwasababu tu Dr.Slaa ameamua kubwaga manyanga.

..kama wanavyosema ktk siasa hakuna maadui wa kudumu, I hope and pray kwamba Dr.Slaa atarudishwa kundini wakati CDM na UKAWA wameingia madarakani.



NB:

..Particularly nachukizwa sana na mashambulizi yanayoelekezwa kwa mke wa Dr.Slaa. Mimi naamini kumshambulia mke wa mtu, au watoto wake, ni kuvuka mpaka wa siasa za kistaarabu.
Kuhusu mchango wa Dr katika upinzani hasa CDM , hakuna shaka na hilo. Kazi yake kama katibu mkuu ilikuwa nzuri , fair to say.

Amekuwa model kwa vijana wengi. Yanayotokea yameondoa sehemu kubwa sana ya sifa zake na wengi wanamwangalia kwa jicho la shaka kuliko matumaini kama walivyoamini

Tatizo lipo pande zote mbili. Kwa upande wa CDM , walijitahidi sana ku-handle hili jambo kwa ustaraabu.
Walichokosea ni kwenda mbali katika kauli zao. Kwa mfano, ilitosha tu kusema kuwa hawakukubaliana na wengi wameamu kwenda njia wanayoona inafaa, na kwamba Slaa ameacha nafasi hiyo kutokana na tofauti zilizojitokeza za kimitazamo.

Mbowe hakutakiwa kusema, agenda si ufisadi tu lazima waongelee mambo mengine ya maendeleo.

Kauli nyingine zikatoka kwa viongozi kuwa tatizo ni Urais na mama. Hizi hazikuwa na sababu yoyote

Hapa tunaweza kusema hakukuwa na watu wa PR kumshauri mwenyekiti wao nini asema.
Hakukuwa na fikra za repercussion inayoweza kutokea na jinsi itakavyopokelewa

Kwa upande wa Dr Slaa, yeye alijipambanua kama mpiganaji dhidi ya maouvu.
Msimamo wake hauhitaji maelezo zaidi wala kuungwa mkono. Angetulia ingemjengea heshima sana.

Kutokana na hasira na pengine sababu nyingine, akaenda kwenye vyombo vya habari kuzungumza akijua linaathari si kwa chama chake cha zamani tu bali pia yeye binafsi na familia.

Hakupata muda wa kuangalia kwa upana madhara yataokanayo

Baada ya kufungua hilo 'pandora box' kila kitu kinaangaliwa kwa kina.
Tunasikia ushiriki wake hadi dakika za mwisho katika kumleta Lwassa

Swali likazuka ikiwa ameshiriki hatua nyingi hadi tarehe 26 kama ilivyosemwa, ilikuwaje akakata kona ghafla?
Again zikachimbuliwa hoja na ndipo familia yake ikajikuta imeingia

Hivyo alipaswa atambue in the end, mambo hayo yatarudi katika family level.

Na kanuni za asili zinasema mtu anapokuwa public figure maisha yake yanakuwa ni public pia.

Kama ambavyo wengi wangehoji endapo angepata jambo lenye utata hata katika maisha binafasi, ndivyo pia familia inapoingia katika suala la siasa. Ndivyo ilivyo

Na kwa sehemu kubwa, wanaomwaga mchele mbele ya kuku ni wanafamilia kama tunavyoona

Yes,ni kweli kabisa si jambo zuri kuingia hadi maisha yake, lakini pia alipaswa kuelewa jambo hili lina mzingo mkubwa na kwamba lingerudi tu katika ngazi zote za kisiasa , kijamii n.k.

Endapo lengo lilikuwa 'timing' ili kuwavuruga wenzake, yanayotokea ni collateral damage

Kwamba, busara ingetawala pande zote haya yasingetokea
 
Mwalimu hapo juu , tulisema turudi kwenye mada, hata hivyo tunatoka nje kidogo kuweka hoja inayotuondoa katika mada , sawa .

Tunaomba jamvi radhi kuchepuka

Hili la Richmond tuliongelee kwa upana wake tukijua ima ni mbinu za kuwaondoa Watanzania katika hoja, au mbinu za kutafuta ushindi kwa njia za udanganyifu

Richmond imeibuka baada ya ukimya wa miaka 8. Wengine tumepiga kelele sana hadi kuonekana wendawazimu

Tulisema , ni lazima chimbuko la tatizo na wahusika wawekewe bayana ili kulinusuru taifa siku za mbeleni

CCM hawakukubali kwa kutumia wingi na madaraka kama yale ya Spika.

Wanaishi na watuhumiwa kwa miaka 8 bila kusemana si ndani ya kamati , vikao au mikutano.

CCM wana nyaraka zote kama wanavyodai akina Mwakyembe na Sitta

CCM wameshindwa kufikisha nyaraka katika vyombo husika, hatua zichukuliwe kwa miaka 8

Kwa kutambua watanzania ni watu wa matukio na si hoja, bila aibu wanasema hilo ndilo tatizo la umeme na chanzo cha bei kubwa

Wanaotoa madai ni hao wanaoomba ridhaa ya kuongoza. Wamo katika mfumo uliolea matatizo. wanadhani tatizo ni baadhi ya watu.

Richmond haikuanguka kama comet kutoka space. Ilitengenezwa. Inakuwaje mafundi wameachwa kwa miaka 8?

Tunafahamu mgao wa umeme ni tatizo. Serikali iliyopo imengia kukiwa na tatizo hilo, na hadi sasa lipo.

Matatizo yapo katika maeneo mawiili. Kwanza rushwa, kama tulivyowahi kusikia mgao wa kutengeneza ili watu waagize mafuta, na majuzi tulikuwa na escrow ambayo haisemwi kwasababu tu inagusa maeneo kadhaa nyeti

Juzi tumesikia mgao wa umeme kwasababu ya kuunganisha gridi ya taifa. Unganisho hilo linahusu baadhi ya siku.
Mfano, zipo siku nchi nzima inapata umeme, kuna siku umeme unakosekana kwa masaa kadhaa. Hakuna sababu za msingi

Kama Richmond ni tatizo, kwanini wananchi wasijiulize, wale wazazi wanaolala sakafuni na vichanga nao ni sababu ya Richmond?

Wale wanafunzi wanaosoma chini ya mibuyu nao ni tatizo la Richmond? Wale walimu wanaotembea siku nzima kufuata haki zao za mishahara ni Richmond? Akina mama wanaotembea KM 2 na vichanga vyao migongoni kutafta maji nao ni sababu ya Richmond?

Wizi wa taarifa za CAG nao ni Richmond? Misamaha ya Trilioni za kodi inahusiana vipi na Richmond?

Utegemezi wa bajeti nao ni sehemu ya Richmond? Ajali zinazomaliza ndugu zetu nao ni Richmond?
Rushwa hadi kura za maoni, nalo ni tatizo la Richmond?

Escrow na mgao wa vigogo nalo ni tatizo la Richmond? Kukosekana kwa dawa muhimbili kwa kiasi nalo ni tatizo la Richmond?

Wagomjwa kualala mzungu wa nne Amana , Liwale na kwingineko nalo ni Richmond?

Orodha ni ndefu ya matatizo mazito tuliyo nayo. Hili la Richmond ni sehemu tu ya matatizo mazito tuliyo nayo.



Inaendelea..
 
Hao walioshindwa kuondoa Richmond, leo wanaliona tatizo na kuataka wananchi waliondoe kwa kura na si mahakamani.

Yes, Richmond ni tatizo na wengine tupo katika rekodi zaidi ya 100 tukilikemea.
Leo waliokuwa kimya wanataka kufundisha watu kusema kile walichokiacha kikamea wao wakiwa na nyaraka mifukoni.

Huu ni unafiki na uzandiki wa hali ya juu. Hoja kubwa ni kutaka kuwaondoa watu katika real issue.

Samwel Sitta ataongelea Richmond kwa maadili gani ikiwa tulimwambia aache lizungumzwe hadi mwisho akakataa?

Mwakyembe ataongea kwa maadili gani ikiwa ana yale aliyosema hatayasema?

Leo wanataka tufanye nini sisi tusio na kipande cha nyaraka hata nusu kurasa?

Hatuwezi kusamehe Richmond, kama vile tusivyoweza kusamehe ujinga, maradhi na umasikini uliolkumba taifa hili

Hatuwezi kusamehe kama vile tusivyoweza kusamehe misamaha ya kodi, Escrow, nyumba za serikali, matumizi ya fedha za wizara.

Leo wanapiga kelele kana kwamba Richmond ni jambo jipya na pekee katika taifa lililovia kimaendeleo na kutopea katika lindi la umasikini wao wakiwa wameshika usukani

Kama CCM hawakuweza kulishughulikia miaka 8, nani anaweza kutoka miongoni mwetu wananchi?

Kama wana nyaralka majumbani na hawafikishi mahali husika, sisi tufanyaje ikiwa hatuna hata kipande?

Kama walizuia Richmond isizuzungumzw bungeni, leo wanataka tuzungumze ya nini ikiwa wao hawakuta hilo?

Huu ndio unafiki mkubwa wa CCM. Kuwafanya wananchi mazezeta na kuwapa 'pipi za gum' mwisho wa siku, akina Sitta, Mwakyembe, Magufuli walioko katika serikali iliyoshindwa kushughulikia Richmond wanataka wapewe ridhaa ili washughulikie wakiwa na nyaraka mifukoni.

Wanataka mijadala na midahalo juu ya uhalifu na si mahakamani

Kuna issuezinazotakiwa kuongelewa. Hili la Richmond waachiwe CCM na hawana maadili ya kulizungumzia kwasababu wamelifuga.

Tunataka tuwasikie kuhusu umasikini wa nchi hii tajiri. Wajibu hoja kwanini baada ya miaka 50 sisi ni omba omba, watu wetu ni dhalili

Kama Richmond ndilo tatizo basi watueleze jinsi linavyosababisha akina mama kwenda kujifungua ndani ya matenga juu ya basikeli.

Aina mama wamebeba nyembe za kukatia vitovu na kufikia hospitali sakafuni wakisubiri kuzaa vichanga na kuvifunga katika marapu rapu ya kipande cha kaniki kutokana na umasikini na kukosekana huduma bora

Ndio amaana tunasema, wale wanaodhani Richmond ni tatizo au liability ya Lowassa kwa upinzani wajiangalie kwanza.

Labda wajiulize, liability iliwezaje kuishi miaka 8 nao leo waione ni tatizo?

Si hawa CCM ndio walikuwa na Lowassa, leo wanalionaje tatizo waliloishi nalo mustarehe miaka 8

Hatutetei uhalaifu wa aina yoyote kama tusivyotetea uzembe wa Richmond unaogeuzwa kuwa tatizo la miaka 50 ya ujinga, maradhi na umasikini na wale wale waliolielea miaka 8 tena wakimruhusu Lowassa agombee Urais. Hawa ndio tatizo

Tusemazane
 
Kwamba ikiwa EL ni fisadi mbona serikali haikumchukulia hatua ni hoja ya ajabu kwa kweli na ni hoja ambayo hivi sasa imepata mashiko ile mbaya! Kimsingi hoja ya kwamba mbona serikali haikumchukulia hatua ni hoja isiyo na mashiko unless kama unataka kusema nchi haina mafisadi! Ni nani miongoni mwa wengi waliotuhumiwa ufisadi wamechukuliwa hatua? Itoshe tu kusema kwamba hoja ya kwamba mbona hakuchukuliwa hatua wala haiwezi kumfanya mtuhumiwa wa ufisadi kuwa hana hatia unless kama tunataka kusema wale wote wanaotuhumiwa ufisadi nao ni wasafi!!!

Swali langu kwako ni rahisi sana nalo ni kama Serikali inafahamu kuwa Lowassa ni fisadi ni kwanini hamuchukulii hatua? tatizo liko wapi?

Richmond ni Mkataba wa kifisadi, na Richmond ndio ilizaa Dowans, ambayo serikali wanatuhaminisha kuwa ni Lowassa, na mpaka leo hii serikali hii inayolia na ufisadi wa Lowassa inaendelea kuilipa Dowans. (ambayo ni ya Lowassa fisadi). Kwa akili zetu za kawaida kwanini tusiamini maneno ya Lowassa kuwa Richmond ni kampuni ya mkubwa?

Na tatu Serikali wanatulilia kuhusu ufisadi wa Lowassa wanataka sisi tufanye nini?

Wananchi hawana shida ya ufisadi... anyway, am speechless! Binafsi mara zote nimekuwa nikisimamia jambo moja kwamba jamii yetu ni ya hovyo, imeoza kila mahali! Hata hivyo sikutarajia kama hali ni mbaya kiasi hiki cha kufikia kusema wananchi hawana shida ya ufisadi! Are you serious? Au ili mradi tu tunayemtaka ashinde urais! Lakini kwa upande mwingine unashangaza unaposema wananchi hawana shida ya ufisadi na wanachotaka ni ajira na huduma bora za kijamii!! Hizo ajira na huduma bora za kijamii zitatoka wapi ikiwa no body cares about corruptions?

Hivi vijana kukosa ajira ni kwa vile ni ufisadi wa Lowassa? Viongozi kutibiwa nje hali hospitali zetu hazina dawa nao ni ufisadi wa Lowassa?, nimeuliza swali moja kuwa hivi Tanzania kama taifa uchumi wetu unategemea nini? au nalo ni tatizo la Lowassa? mashule kukosa chaki, madawati, walimu kutolipwa mishahara inayokidhi mahitaji yao hali viongozi wakijilipa mamilioni na rais akipokea mshahara wa mil.192 nao ni ufisadi wa Lowassa?, Vifo wa watoto, wazazi kujifungulia chini, wajawazito kulazimishwa kupelekeka ndoo za maji wakati wa kujifungua hali wake wa viongozi wakienda kujifungulia Marekani nao ni ufisadi wa Lowassa? Tanzania tuna ardhi ya kutosha tena nyenye rutuba, tuna vijana hivi kama taifa tunashindwa kuwekeza kwenye kilimo hali soko lipo kuanzia hapa Afrika mpaka Ulaya and US au huo nao ni ufisadi wa Lowassa? Wakati vijana wetu wakitafuta ajira serikali inaorder samani za maofisi ya serikali kutoka China nao ni ufisadi wa Lowassa?

Mwaka 2010 hoja ya ufisadi ilikuwa moto moto lakini pamoja ya hayo watuhumiwa wote wa ufisadi akiwemo Kikwete walishinda kwa kishindo sasa labda nikuulize wewe je unafikiri ni kwanini hawa watu walishinda pamoja na tuhuma za ufisadi?

Kwamba ukiniuliza nitajibu nini kuhusu uchumi wa Tanzania unategemea nini zaidi ya madini na gesi; labda nikuulize wewe hiyo gesi ni gesi ipi unayoisema wewe? Tangu lini Tanzania imeanza kutegemea uchumi wa gesi? Hiyo gesi inauzwa nchi zipi? Na hata hayo madini unayosema wewe mapato yake hayafikii ya mapato kutoka sekta ya utalii

Nimekuuliza kama Taifa uchumi wetu unategemea nini?



Wakati wewe hutegemei chochote kutoka kwa Magufuri, mimi sitegemei chochote kutoka kwa yeyote kati ya hao mafahari wawili! Na kama umenisoma vizuri tangu mwanzo, ingawaje wengi wenu huwa mnajishitukia sana; mara zote hoja yangu imejikita kwenye suala la EL na kauli mbio ya mabadiliko! Mimi si leo wala si jana; mara zote msimamo wangu haujabadilika kwamba CCM na upinzani wote ni wale wale tu...!! Na sio CCM na upinzani tu, bali sehemu kubwa ya jamii ya Kitanzania ni corrupt community na ndio maana hata wakati wa mchakato wa katiba maoni yangu ilikuwa ni kuachana na what's the so called good governance... ingawaje lengo na misingi ya mfumo wa utawala bora ni mzuri lakini huwezi ku-practice good governance kwenye corrupt community! Na viongozi wetu wamekua wakiupigia chapuo sana huu mfumo coz' unasaidia kuficha uovu wao... ni sawa tu na ulivyosema wewe; kama EL ni fisadi mbona hajafikishwa mahakamani...

Kama utegemei chochote kutoka kwa mtu yeyote je unashauri au unawashauri watanzania wenzako wafanye nini?
 
NasDaz Si kweli kuwa ninatetea mgombea wangu, kwa kweli nitasema uongo kama nitasema nina mahaba na Lowassa..rejea maandishi yangu ya nyuma. Lakini nashindwa kuelewa mtu anapomwanga petrol kwenye nyumba inayowaka moto unategemea nini..

Sipendi kujadili mambo ya dini, kwenye mjadala ya dini huwa ninakuwa na kigugumizi gafla lakini hapo hapo sipendi kuona mtu anamtia maneno binadamu mwenzake ili akidhi haja zake.. Alichokifanya Lowassa ni kosa na ameona hilo na kuomba msamaha...

Bado ninafahamu kuwa nina deni la kujibu hoja zako..
Hivi wewe kweli unataka kusema kila mtu humu ataandika neno kwa neno la mtu alosema au unaandika ulichoelewa? Watu wote wamemuelewa hivyo, na hata viongozi wa dini wamekemea kwa hilo iweje wewe ulielewa tofauti?
Mwenyekiti wa Baraza la Makanisa ya Kipentekoste nchini, Askofu David Batenzi, akizungumzia suala hilo pamoja na kuipongeza NEC, alisema kitendo cha Lowassa kuwaomba Walutheri kumchagua si sahihi, kwa vile kiutaratibu kama taifa, hakuna zamu za dini katika urais.

Sasa kama Lowassa ameomba msamaha, kaomba msamaha kasema nini? kwamba aombewe imekuwa kosa la kuomba msamaha!? au kuna zaidi ya kuombewa! Wewe umeelewaje ile hotuba ya Lowassa pale kanisani kufikia kaomba msamaha alisema nini maana kuombewa kila mtu anasema na hakuna mahala unapozitaka dua za watu kama kanisa lako!

Zaidi ya hayo mbona humu mnaandika maneno mengi ambayo hata Dr.Slaa hakusema hivyo, lakini tumeelewa kuwa yanaendana na maana ile ile ya msemaji, iweje utake mimi niandike kila neno sawa na matamshi ya Lowassa. Kama haya sio mahaba ni nini tena dadangu!

Swala la Richmond huwezi kulifuta kirahisi hivyo kwa sbaabu wewe unaona hakuna sababu. Sababu zipo na tunataka kujua yote toka kuuzwa kwa nyumba za serikali, ubinafsishaji wa mashirika, uporaji wa nyumba za serikali na mashamba, EPA, Rada, IPTL, Meremeta, Kagoda na mengineyo mengi ambayo ndio sababu kubwa ya wananchi kuichoka CCM. Mimi binafsi nitamfagilia kiongozi yeyote ambaye atakuwa tayari kurudisha maswala yote haya mezani kwa sababu hatuwezi kuzungumzia Uadilifu na uwajibikaji wakati tunaacha Kuhujumu Uchumi kuwa ni mambo yalopita, wakati sheria zipo zimekiukwa na hawa Untouchables!.

Tumefika hapa leo kwa sababu yao,na hatuwezi kuendelea kuwafuga tukitegemea mabadiliko, wana kesi kubwa ya kujibu kwa wananchi kwa sababu sisi ndio waajiri wao. What next? Tutawahukumu kwa kuujua ukweli kuliko kuendelea kuwashutumu watu pengine hawahusiki kabisa. Ukweli utawaacha huru! Leo unamsema Mwakyembe kwa dhana tu ya kuinusuru serikali wakati msimamizi wa shughuli za serikali ni Waziri mkuu. Tunachomkana Lowassa ni Ufisadi wake, hakuwa muadilifu katika kusimamia majukumu alopewa kiasi kwamba alihujumu Uchumi wetu, hii ni Kashfa kubwa kwa mgombea urais! Na kama itawezekana ukweli ukitolewa tutaandika kwa uhakika kabisa na hatutabisha..
 
FJM,

..I agree with u kwa mambo ambayo umependekeza CDM wawaombe radhi wa-Tz.

..Je, kwa upande wa CCM unadhani wanatakiwa kuwaomba radhi wa-Tz kwa masuala gani?

cc GalaxyS3, Nguruvi3, Alinda
Mkuu samahani kuingilia hoja yako.. kama tunautaka ukweli haswaa, Chadema lazima wakubali kupotosha watu ama wameteleza kisiasa wataeleweka lakini CCM kwangu mimi sidhani kama kuna kuomba radhi kwa sababu wao ndio walokuwa madarakani, hawakuteleza bali walikusudia.

Wanachotakiwa ni kuzindua hizi KASHFA moja baada ya nyingine kwa maelezo mbele ya Kamati ya maadili tena LIVE on TV kila mtuhumiwa na mashahidi wakiitwa kutoa ushahidi wao, mashirika husika wa Release transcripts za mikataba yote na wahusika wake...

Nawaomba tu mtambue kwamba siwapendi kabisa CCM kwa yale walotufanyia na sidhani kaa naweza kuwasamehe kirahisi isipokuwa siwezi kukubali kumuona mmoja wa watu walotufikisha hapa awe rais wa nchi hii - HAPANA. What if (dhana) ikiwa CCM wenyewe wamepanga kuhakikisha wana wagonmbea Urais pande zote mbili? je kesho Lowassa akiwamwaga Chadema kuna sheria gani itakayo mnyonga chini ya katiba ya mwaka 1977.

Hivi kweli mnaamini Lowassa atakubali kupitisha Katiba ya Warioba ambayo inamuondolea madaraka makubwa na kubakia kama kiongozi jina (Ceremonial President) na serikali ambayo haina mamlaka wala vyanzo vya kukusanya fedha? yaani serikali yake asubiri mchango wa serikali za Bara na visiwani huku akiitwa head of State!.. Jamani tusidanganyane, sio Lowassa huyu tumjuaye!
 
Kitu kingine ambacho UKAWA wamebugi ni kwamba there is no way katika serikali yao iwapo watashinda wanaweza Kuiweka nje ya madaraka CCM moja kwa moja.

Ukawa walifanya Mistake ya Kugawana majimbo kwa misingi ya Vyama, Matokeo yake hakuna chama cha Ukawa chenye guarantee ya Kupata Majority ya Wabunge ili Kiweze Kutoa Waziri Mkuu kama katiba inavyosema.

Chadema wameachiwa na UKAWA Majimbo 139,
Wanahitaji kushinda majimbo hayo kwa zaidi ya Asilimia 90 ili waweze kuwa na Majority bungeni, Kitu ambacho ni ndoto!

Matokeo yake ni dhahiri Kuna Chance Kubwa kwa CCM iliyosimamisha Wagombea wengi kupata Wabunge wengi zaidi na Hivyo kutoa Waziri Mkuu.
Matokeo yake Ni kuundwa kwa Serikali ya Pamoja ya Ukawa na CCM, na hivyo lengo la Kuing'oa CCM madarakani lisifanikiwe moja kwa moja.

Je Iwapo, Ukawa watashindwa kupata Jumla ya Theluthi mbili ya Wabunge wa Bara na Visiwani, Hiyo Katiba ya Warioba watairudishaje?, Tusidanganyane, Muungano w Sasa wa Ukawa is a big Joke, na Watajikuta wanaumia Zaidi baada ya Uchaguzi huu kwa sababu muungano wao ni very Fragile!
 
Wait a minute!

Nimesoma fastafasta na hapa watu wanadai wamevutiwa na kina Slaa, Lissu na wenginewe mpaka wakaiaminia Chadema/Ukawa.

Je mlivutiwa na nini?

List of Shame? KUshikilia bango Ufisadi? kupiga kelele za Richmond? Kutaka katiba mpya ya Serikali tatu?

Nafikiri jamii yetu imejikita sana kwenye siasa za vipaza sauti kuliko matendo ya kimaendeleo ambayo yanaleta matokeo.

We are accustomed to efforts and not results and hence our Ushabiki ni wa maneno tena ya juu juu , partial details, context and contents!

Suala la kupiga vita ufisadi, sikuwahi kusikia hata siku moja Chadema, CuF au wapambanaji wa CCM wakileta muswaada bungeni wa kurekebisha sheria bubu au kuweka mamlaka yenye nguvu kikatiba kushughulikia Rushwa!

Kila mmoja wa wanasiasa wanaopiga kelele za ufisadi ni kuuza magazeti, kupayuka kwenye vipaza sauti, lakini hakuna hata mmoja mwenye uthubutu wa kuandika sheria, ikawakilishwa bungeni na ipigiwe kura (ikizimwa kwa kura za hapana, kuna ushahidi kuwa sheria ilipelekwa na kutungwa ipigiwe kura).

Nakataa kukubaliana na wanaosema walishawishiwa na Dr. Slaa, Mbowe au Seif Sharif Hamad.

Mlichoshawishiwa ni kauli za majukwani. Wameongea kile mlichotaka kukisikia, mnachoamini kinawakera na mnaweza kununua gazeti na kutumia siku na miezi kukijadili!

Uongo huu wa umaarufu wa majukwaani, ndio umetufanya leo hii bado tunaongelea Richmond na kutoleana vitisho na mikwara ya "ntasema mengine, heri kaa kimya nisikuumbue"

Dr. Slaa kayasema haya, Mwakyembe, Sitta, Lissu, Msigwa, Lipumba, Kinana, MNauye na wengine wengi tuu!

Kama ni ushabiki wa watu kutoa kauli kali kali, hapo nitakubali.

Lakini turudi kwa hawahawa "tunaowaaminia", nenda muulize Slaa tangu 1995-2010 jimbo lake Karatu likoje, nenda kwa Lissu, njoo kwa Magufuli, mbeep Lowassa, muulize Ana Kilango, mkumbushe Sitta au hata vuka mpaka kumuuliza Nkurunzinza wa Kyela!

TUna wataalamu wa kuunda maneno matamu ambao katika kazi zao, ni mashujaa wa vijembe, misamiati na kuhamasisha hisia kuwa kweli wako mstari wa mbele kwa manufaa ya Taifa letu.

Kazi ya Mbunge ni kutunga sheria, si kuwa mhuri wa Serikali kuu. Hili limeandikwa kwenye katiba.

Je kwanini Wabunge wetu hawa mashuhuri kupiga vita "Ufisadi" hawajawahi kufungua mchakato wa kuipata ripoti ya Warioba na kuifanyia kazi? Je ripoti ya Kisanga na Amina Chifupa? kama hizo ni siri sana, mbona ripoti ya CAg hawajaifanyia kazi na kuwaonyesha Watanzania jitihada/juhudi walizofanya na kama walishindwa kutokana na Serikali au CCM kuwa na kura nyingi wakazima hoja wakaishitaki CCM an Serikali yake kwa wananchi?

HIvyo ni hadaa hata tunapotathmini hoja kuu hapa na kuangalia viashiria vingi vya madhaifu ya wanasiasa.

Sisi tumefanya kazi kubwa kuliko hawa vipaza sauti.

Leo nimeonelea niliseme hili la mahaba ya mtu au watu kwa maneno mengi na hata tabasamu na uzuri wa sura, lakini ukweli unabakia wa too much efforts with zero results!

Je mbwembwe zote hizo ni kujipatia ujiko na kijiko cha kukomba kodi na ruzuku?

Take a step back and think about it
 
Mkuu Rev.Kishoka

Ahsante kwa bandiko lako, wanajamvi watakuwepo kuchangia kwa mitazamo mbali mbali

Kuhusu Dr Slaa , wengine tumesema tunamheshimu kwasababu ya jitihada zake katika kujenga upinzani

Kwa mfano, majimbo ya Karatu na Tarime yalikuwa ni role model ya wapinzani. Kwamba, kuna uwekano halmashauri ya mji au jiji ikaongozwa na wapinzani bila tofauti . Hii ilikuwa Ice breaker iliyoondoa hofu ya wananchi dhidi ya CCM mbadala

Ni kubwa kiasi gani, hilo linabaki kama mtazamo wa kila mmoja

Pili, Slaa alikuwa mbunge mwenye uhakika wa kurejea bungeni kwa jinsi alivyokubalika Karatu

Aliombwa aache ubunge ili apate full time ya ukatibu mkuu wa chama chao akiimarishe

Ukiangalia hawa waliofuata utagundua kuwa ilikuwa ni kujitoa, and we can't take anything from that!

Fikiria , leo mwenyekiti wa Bavicha yupo bize na ubunge na si shughuli za chama.

Viongozi wote wapo bize including acting sec general.

Hakuna aliyebaki kusimamia shughuli za UKAWA. Ukiwalinganisha na Slaa, tofauti ipo

Haya yanayotokea yanatupa the other side ya Dr Slaa as a person and a leader

Tunaweza kusema kwa uhakika, at the moment his demerits outweigh merits. Na sifa ya mtu hujidhihiri wakati wa crisis

Tatu, kuhusu suala la kupeleka mswada kuhusu mambo kama ufisadi, tutawahukumu kama hatutaangalia facts.

Unakumbuka Kafulila alivyonyanyaswa na Mwanasheria mkuu, Spika na waziri mkuu wakati wanaongelea Escrow

Spika alikaa kimya kijana akiitwa tumbili akitishiwa makonde n.k.

Wabunge wa CCM walikuwa wanapiga makofi wakati wapinzani wakihoji. Ilikuwa al-manusura Escrow igunikwe tu

Mswada wa mbadiliko ya katiba ulipitishwa kwa akidi chini ya wabunge 100 isiyokidhi haja ya kupitisha mswada.

Spika alijua hilo , waziri mkuu alikuwepo na mawaziri wote walikuwepo including hawa waliohama

Hakuna mwanaCCM aliyesimama kusema haikuwa sahihi. Walitumia wingi na Spika

Unakumbuka mjadala wa Escrow, Spika alizungusha zungusha hadi akina Zitto na Mbowe wakakubali suala lirudishwe serikalini!

Orodha ni ndefu hayo ni mifano tu. Sheria kama za takwimu, mitandao n.. zimeletwa makusudi kwa kutumia wingi wa CCM/Spika

Sioni namna ambavyo wapinzani kwa uchache wao wangeweza kuvunja ukatili uliokuwepo bungeni.

Kwa msingi huo, apinzani wakiwezeshwa kwa idadi wataweza kuzia uhuni wa wingi kwa kiasi kikubwa.

Hivyo, wananchi watambue, kuwapa CCM wabunge ambao wamekuwa hawasaidii hochote katika taifa ni kujiumiza.

Njia ya haraka sana na ya kwanza kama first aid ni kuzuia 2/3 ya CCM

Nne, kuhusu ripoti za watu kama Warioba, hilo nakubaliana nalo kuwa wapinzani wamezembea.

Suala si kupeleka bungeni tu bali kuweka wazi ili wananchi waone nini kinaendelea

Tano, kuhusu kuuliza wabunge na majimbo yao, ah kwa hili tutaenda mbali zaidi na kuwaambia wananchi, wajiulize tofauti iliyokuwepo miaka 20 na leo!

Tofauti ya maisha katikatangu Mkapa alipoingia ofisini hadi leo.
Na je, wananchi wapo tayari kufanya jambo lile lile lisilo na matokeo tofauti?

Na hapa tunasema huu ni uwekezaji usiotabairika maana waliokaa kimya leo wanapinga huo udhalimu.
Wengine tunapata tatizo la kuelewa!
 
Kitu kingine ambacho UKAWA wamebugi ni kwamba there is no way katika serikali yao iwapo watashinda wanaweza Kuiweka nje ya madaraka CCM moja kwa moja.

Ukawa walifanya Mistake ya Kugawana majimbo kwa misingi ya Vyama, Matokeo yake hakuna chama cha Ukawa chenye guarantee ya Kupata Majority ya Wabunge ili Kiweze Kutoa Waziri Mkuu kama katiba inavyosema.

Chadema wameachiwa na UKAWA Majimbo 139,
Wanahitaji kushinda majimbo hayo kwa zaidi ya Asilimia 90 ili waweze kuwa na Majority bungeni, Kitu ambacho ni ndoto!

Matokeo yake ni dhahiri Kuna Chance Kubwa kwa CCM iliyosimamisha Wagombea wengi kupata Wabunge wengi zaidi na Hivyo kutoa Waziri Mkuu.
Matokeo yake Ni kuundwa kwa Serikali ya Pamoja ya Ukawa na CCM, na hivyo lengo la Kuing'oa CCM madarakani lisifanikiwe moja kwa moja.

Je Iwapo, Ukawa watashindwa kupata Jumla ya Theluthi mbili ya Wabunge wa Bara na Visiwani, Hiyo Katiba ya Warioba watairudishaje?, Tusidanganyane, Muungano w Sasa wa Ukawa is a big Joke, na Watajikuta wanaumia Zaidi baada ya Uchaguzi huu kwa sababu muungano wao ni very Fragile!

..hoja yako ni ya msingi.

..nadhani ukawa walikuwa wanajaribu kujibu kiu na kilio cha muda mrefu cha wananchi kutaka vyama vya siasa viungane.

..kwa mtizamo wangu ukawa wamefanya kile kinachowezekana kwa kuzingatia matakwa ya sheria zilizopo.

..wakati wote wa majadiliano haya viongozi walikuwa wakisisitiza suala la MARIDHIANO. kwa maana nyingine walijaribu kuangalia maslahi ya kila chama kilichoko ktk ukawa.

..YES, kuna uwezekano mkubwa kwamba CDM wanaweza wasipate majority itakayowawezesha kuteua Waziri Mkuu.

..ikiwa hilo litatokea basi upinzani utakuwa na wakati mgumu. Kimbilio la mwisho katika mazingira hayo ni CCM ikose 2/3 ya wabunge na hivyo kutokuwa na uwezo wa kupitisha bajeti wao wenyewe.

..CCM wakikosa hiyo 2/3 basi watalazimika kuteua wabunge toka ukawa kuingia ktk baraza la mawaziri. Katika mazingira hayo EVERY BODY WINS na tutakuwa tumefungua ukurasa mpya ktk demokrasia ya nchi yetu.

NB:

..wakati mwingine tusiangalie tu kwamba wameshinda CCM, au wameshinda UKAWA. How about a situation where these two sides have to meet somewhere in the middle? Wouldn't that be better for the country/wananchi?


cc Rev. Kishoka, NasDaz, Mkandara, Alinda, GalaxyS3, Mchambuzi
 
JokaKuu nadhani umemfahamisha ZeMarcopolo kwa ufasaha kabisa

Ili serikali za nchi ziwe effective ni muhimu kuwa na 'majority' ya bunge

Kwa miaka mingi CCM wametumia mwanya huo si kuleta hali nzuri kwa wananchi bali ku-abuse

Wamefikia mahali serikali haina ushawishi isipokuwa kutumia bunge kutunga sheria kama zile za mtandao

Ili kuzuia kiburi na ujinga huo, matokeo yoyote yatakayobadilisha 'nguvu' za upande mmoja, na hapa ni CCM,yanatakiwa

Hilo litawarudisha katika mstari wa kukaa meza moja na wapinzani kujadili masuala kwa weledi na manufaa kwa ujumla

Hapa napo lipo tatizo. Ukiangalia kwa darubini wapinzani wameelekeza nguvu zao katika Urais bila kuliona hilo

Kuvunja mgongo wa ngamia, kutasaidia sana hili taifa. Kuendelea kuwapa CCM majority kutawafanya Watanzania kuongelea maendeleo ya majirani zetu. Hali ndivyo ilivyo sasa
 
JokaKuu nadhani umemfahamisha ZeMarcopolo kwa ufasaha kabisa

Ili serikali za nchi ziwe effective ni muhimu kuwa na 'majority' ya bunge

Kwa miaka mingi CCM wametumia mwanya huo si kuleta hali nzuri kwa wananchi bali ku-abuse

Wamefikia mahali serikali haina ushawishi isipokuwa kutumia bunge kutunga sheria kama zile za mtandao

Ili kuzuia kiburi na ujinga huo, matokeo yoyote yatakayobadilisha 'nguvu' za upande mmoja, na hapa ni CCM,yanatakiwa

Hilo litawarudisha katika mstari wa kukaa meza moja na wapinzani kujadili masuala kwa weledi na manufaa kwa ujumla

Hapa napo lipo tatizo. Ukiangalia kwa darubini wapinzani wameelekeza nguvu zao katika Urais bila kuliona hilo

Kuvunja mgongo wa ngamia, kutasaidia sana hili taifa. Kuendelea kuwapa CCM majority kutawafanya Watanzania kuongelea maendeleo ya majirani zetu. Hali ndivyo ilivyo sasa

..kuna mahali Tundu Lissu alilizungumzia suala hili.

..wachangiaji wengi walimbeza wakimtuhumu kwamba hataki ushindi.

..umesema ukweli kwamba vyama vyenye ABSOLUTE MAJORITY bungeni mara nyingi huishia kuwa ABUSIVE kwa wananchi.
 
Wanajamvi , mjadala huu utakuwa endelevu na bandiko linaendelea

Kufuatia hoja za wanajamvi kuhusu uzi pekee utakaongelea sera/ilani za wagombea na vyama, tunawataarifu uzi upo tayari na utakuwa ‘hewani' leo saa 1 usiku

Uzi utakuwa na kichwa cha habari

Duru za siasa: Uchaguzi ni sera/Ilani , si mtu au watu

Ahsanteni
 
JokaKuu nadhani umemfahamisha ZeMarcopolo kwa ufasaha kabisa

Ili serikali za nchi ziwe effective ni muhimu kuwa na 'majority' ya bunge

Kwa miaka mingi CCM wametumia mwanya huo si kuleta hali nzuri kwa wananchi bali ku-abuse

Wamefikia mahali serikali haina ushawishi isipokuwa kutumia bunge kutunga sheria kama zile za mtandao

Ili kuzuia kiburi na ujinga huo, matokeo yoyote yatakayobadilisha 'nguvu' za upande mmoja, na hapa ni CCM,yanatakiwa

Hilo litawarudisha katika mstari wa kukaa meza moja na wapinzani kujadili masuala kwa weledi na manufaa kwa ujumla

Hapa napo lipo tatizo. Ukiangalia kwa darubini wapinzani wameelekeza nguvu zao katika Urais bila kuliona hilo

Kuvunja mgongo wa ngamia, kutasaidia sana hili taifa. Kuendelea kuwapa CCM majority kutawafanya Watanzania kuongelea maendeleo ya majirani zetu. Hali ndivyo ilivyo sasa


..hoja yako ni ya msingi.

..nadhani ukawa walikuwa wanajaribu kujibu kiu na kilio cha muda mrefu cha wananchi kutaka vyama vya siasa viungane.

..kwa mtizamo wangu ukawa wamefanya kile kinachowezekana kwa kuzingatia matakwa ya sheria zilizopo.

..wakati wote wa majadiliano haya viongozi walikuwa wakisisitiza suala la MARIDHIANO. kwa maana nyingine walijaribu kuangalia maslahi ya kila chama kilichoko ktk ukawa.

..YES, kuna uwezekano mkubwa kwamba CDM wanaweza wasipate majority itakayowawezesha kuteua Waziri Mkuu.

..ikiwa hilo litatokea basi upinzani utakuwa na wakati mgumu. Kimbilio la mwisho katika mazingira hayo ni CCM ikose 2/3 ya wabunge na hivyo kutokuwa na uwezo wa kupitisha bajeti wao wenyewe.

..CCM wakikosa hiyo 2/3 basi watalazimika kuteua wabunge toka ukawa kuingia ktk baraza la mawaziri. Katika mazingira hayo EVERY BODY WINS na tutakuwa tumefungua ukurasa mpya ktk demokrasia ya nchi yetu.

NB:

..wakati mwingine tusiangalie tu kwamba wameshinda CCM, au wameshinda UKAWA. How about a situation where these two sides have to meet somewhere in the middle? Wouldn't that be better for the country/wananchi?


cc Rev. Kishoka, NasDaz, Mkandara, Alinda, GalaxyS3, Mchambuzi

Sidhani kuwa wananchi wengi watanzania walitaka vyama vya upinzani viungane. Kwenye uchaguzi wa 2005 ni watanzania wengi walitaka CCM. Na uchaguzi wa 2010, mahudhurio ya wapiga kura yalikuwa madogo katika historia ya nchi.

Ukweli wa mambo, kilio cha watanzania wengi ni kupata kiongozi au viongozi ambao ni effective kwenye utatuzi wa matatizo yao ya kijamii na kiuchumi. Kama watawapata viongozi wenye sifa hizo, wapo tayari kabisa kukumbatia chama kimoja na kuacha upinzani kuwa uliodhoofika.

Kuhusiana na mvutano unaoweza kutokea iwapo Chama vyama havitashinda ushindi wa kuunda serikali ya wengi, huu ni upungufu wa katiba ya 1977. Hii ni katiba ya chama kimoja na inatumika mpaka sasa kwa makubaliano au ujanja ujanja. Na upungufu ulikuwepo toka mwanzo na baadhi ya watu waliueleza. Lakini kwa sababu CCM ilikuwa na majority hakuna aliyejaribu kutafuta ufumbuzi wa mapungufu ya kikatiba.

Kwa maoni yangu binafsi,ningependelea waliohamia CDM kwa kufuata Lowassa, wawapigie kura wabunge wa vyama vya upinzani pia. Suala kubwa kwa taifa sio kumweka Lowassa madarakani. Swala ni kupata katiba ambayo itafanya nchi ipate viongozi effective na wenye kukubalika.
 
Zakumi,

..asante kwa maoni yako hapo juu.

..naomba nirekebishe kidogo hoja yangu ambayo umeijibu.

..kuna maeneo ambapo wapinzani "waligawana" kura, na kusababisha ccm kupenya ktk uchaguzi.

..pia kumekuwepo na matukio ya vyama vya upinzani kushambuliana wao kwa wao huku wakiwaacha ccm wakipeta.

..mambo hayo ndiyo yaliyopelekea baadhi ya watu kushauri kwamba vyama vya upinzani viungane ili kuweza kuleta ufanisi ktk kukabiliana na ccm.

..nakubaliana na maoni yako kuhusu wapenda MABADILIKO kuwa na sauti zaidi ktk BUNGE letu.
 
Back
Top Bottom