CHADEMA/UKAWA: Uwekezaji usiotabirika

Nguruvi3

Platinum Member
Joined
Jun 21, 2010
Messages
13,491
Points
2,000

Nguruvi3

Platinum Member
Joined Jun 21, 2010
13,491 2,000
Nimekupata Mkuu.
Nikijibia swali lako kama tuna instructors na kama wanajua wajibu wao na kuuwajibikia. Ni wazi nafasi yao ipo, na wenyewe waliojivika kofia hizo wapo, lakini wanachofanya ni Ubatili. Hivyo tunaweza sema ni Watu Hewa.

Swali, ni je huo ndio ukomo wa ndoto za wananchi wetu? Je, Hatima ya umma wetu inabebwa na hilo tu, kiasi hatuwezi kufanikiwa katika lolote pasipo wao?

Nafikiri huo ndio msingi wa hoja ya Mwalimu, IPI I NAFASI YETU KAMA RAIA KATIKA KUONDOA UNYONGE WETU? Nafikiri huo ndio mwanzo wa UTAMBUZI wa kweli.
Nafasi yetu kama Raia ni kubwa sana, tunachotofuatiana ni jinsi gani wananchi watumie nafasi hiyo

Kama ulinisoma mwanzo niliporudisha bandiko hili la miaka mingi, nilisema ni makosa makubwa wananchi kulaumu CCM na Serikali yao wakiwa hawafanyi tofauti au lolote

Nilirudia kuonyesha udhaifu ulioifikisha CUF ilipo, nikaenda kwa Chadema

Udhaifu unao onekana unafumbiwa macho na wanachama wa vyama hivyo

Hoja ikawa huwezi kulaumu CCM kwa uzembe uliotufikisha hapa ukatamani kuiondoa kwa kutumia taasisi dhaifu ulizoshindwa kujirekebisha, zilizoshindwa kuongoza umma

Hilo ni kukwepa jukumu ''kutafuta mchawi katika paa ukiacha majoka uvunguni''

Nafasi ya wananchi inaanzia katika vyama.
Midhali kuna 'watu hewa' kabla ya kushambulia wa CCM, fanya jambo na hewa ulio nao.

Wajibu wetu kama wananchi ni kuhakikisha tunajenga taasisi imara ili ziongoze kwa wakati, kutuheshimu na kujenga kuheshimiana

Ni kwa msingi huo nikasema Chadema kama chama kikuu cha upinzani kianze kujisafisha Wanachama wachukue hatua za dharura na za lazima dhidi ya viongozi wanaozembea

Hiyo ni sehemu ya nafasi ya majukumu ya wananchi yasohitaji subra wala ruhusua

Hatuishii hapo, ACT wazalendo,TPP n.k nao wajisafishe kama kuna matatizo ili tuwe na taasisi tofauti zikiwa na something in common, usafi na kuwajibika.

Tujenge utamaduni wa kuwajibisha wazembe

Tuliobaki tutimize wajibu kwa kushea tulicho nacho kidogo sana, hiyo ndiyo nafasi yetu

Katika kutimiza wajibu tusione haya, tusistahamiliane kinafiki, tusionee au kuonewa

Tuite kole kwa jina lake na si kijiko kikubwa.

Ninawanasihi wengine kusimama katika kujitambua, si siku ya uchaguzi, si kunyooshea kidole CCM bali kujitakasa huko CUF, Chadema, ACT na kwingineko kwanza

Nipo katika rekodi nikiudhi watu kwa ukweli kuwa kazi tuliyo nayo wananchi ni ngumu

Yaliyotokea Chadema wiki iliyokwisha, sisiti kusema siioni kesho ya matumaini

Ndio msingi wa kusema, ni wakati uongozi ukae pembeni kutoa fursa ya fikra mpya

Tusemezane
 

Mwalimu

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2008
Messages
1,533
Points
1,500

Mwalimu

JF-Expert Member
Joined Aug 21, 2008
1,533 1,500
Mkuu Nguruvi3

Ni kweli vyama vya upinzani havijafanikiwa kusimama vyema kwenye nafasi yao kama "instructors" kutoa mwongozo kwa wananchi hilo halina mjadala. Ndio maana nimesema kwamba hawa waliopo sasa kesho hawatakuwepo, kesho mbowe, chadema na ukawa hawatakuwepo na tutakuwa na wapinzani wengine. Lakini suala langu la msingi ni kwamba ni muhimu tuangalie kwa makini nafasi ya mwananchi katika kuamua hatima yake. Labda nitoe mfano kidogo; Mafanikio ya mwanafunzi shuleni yanachangiwa na mambo mengi ikiwemo "mwalimu/instructor" pamoja na "jitihada" kutoka kwa mwanafunzi kwenye kujisomea na kujifunza kwa bidii alichofundishwa. Sasa inawezekana somo la mwalimu likawa halieleweki au somo likaeleweka lakini mwanfunzi akawa mzembe hajibidiishi kwenye kusoma!

Sasa tukirudi kwenye mada yetu ningependa tufanye tathmini juu ya nafasi yetu sisi wananchi kama wadau kwenye kubadili mustakabali wa nchi. Naangalia dhana ya kujitambua kwa mapana zaidi kwamba sio tu kutambua kuwa kuna tatizo bali kuwa na uelewa juu ya solution ya kutatua tatizo lakini pia uthubutu wa kuchukua hatua stahiki katika kutatua tatizo.... pia kujitambua nguvu na uwezo alio nao kwenye kuleta mabadiliko. Hapo ndipo ninaposema kwamba kwenye kujitambua bado hatujafikia kiwango kinachotakiwa, ndio tunajua kwamba kuna tatizo lakini bado tunakosa uelewa wa njia ya kujikwamua pamoja na uthubutu/ujasiri. Nguvu ya mwananchi kwenye kuleta mabadiliko ni kubwa sana lakini kwa upande wetu bado hatujafanikiwa kuichimbua ndani yetu. Ndio maana kwenye chaguzi zetu turnout huwa ni ndogo sana kulinganisha na walioandikishwa, wengine hadi wanauza kadi zao za kupigia kura! Shida ya kujitambua ni kubwa sana...

Nizungumzie kidogo kuhusu "ajenda" na ningependa turudi nyuma kwenye uchaguzi wa mwaka 2010 ambapo ajenda ya upinzani ilikuwa "ufisadi".... unadhani ajenda hii ilieleweka vyema kwa wananchi au haikuwa na mvuto kwao? Hawakuwa tayari kufanya mabadiliko? Hawakuwaamini wapinzani kiasi cha kuwapa nafasi ya kuongoza hivyo wakaona bora kubaki na CCM? Ajenda yao wananchi ilikuwa nini? Ilikuwa inaendana na ajenda ya vyama vya upinzani? Vipi kuhusu utayari na uthubutu wao? Tuangalie pia uchaguzi wa mwana 2015 ajenda ya upinzani ilikuwa ni ipi na ilipokelewa vipi na wananchi? Mwitikio wa wananchi ulikuwaje kiujumla kulinganisha na mwaka 2010?

Nikirudi kwenye suala la nafasi vyama vya siasa vina nafasi yao muhimu sana katika ku-advocate mabadiliko lakini pia wananchi wana sehemu yao ya kuchochea mabadiliko. Lakini tuangalie pia nafasi ya taasisi nyingine kwenye kuleta chachu ya mabadiliko. Mfano mzuri juzi juzi hapa DC wa Arumeru kawasweka ndani waandishi wa habari, vyama vya waandishi wa habari wamechukua hatua gani kupinga uonevu ule? Au wanasubiria mpaka ukawa waje kutoa tamko? Tumeshuhudia pia Mheshimiwa Magufuli akitoa matamko mara kadhaa kuwatishia wanasheria kwa kutetea watuhumiwa, wanasheria wamechukua hatua gani? Au nao wanasubiri mpaka Lisu akagombee TLS?
 

Freeland

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2012
Messages
14,504
Points
2,000

Freeland

JF-Expert Member
Joined Jan 24, 2012
14,504 2,000
Wakuu Nguruvi3 Mwalimu ukweli uliopo ni kuwa;

 • CHADEMA ya sasa imesinyaa na kushindwa kujua ifanye siasa kwa namna gani
 • CHADEMA ya sasa imeshindwa kurudi nyuma na kufanya tafakari ya ilipojikwaa na ifanye nini?
 • Kundi la lowasa linalotoka CCM aidha kwa kufukuzwa au kwa kumfuata yeye halitakuwa na jipya ndani ya CHADEMA...Ni kundi litakaloleta ile CCM ambayo ni ya mtandao na iliyojaa Rushwa..wakati CCM ya sasa ikijitahidi kujisafisha (Nakubali hili linaweza kukosolewa pia)
 • CHADEMA ya sasa haishauriki na haina demokrasia thabiti ya kuhoji mambo ndani ya chama.
Kinachopaswa kufanywa;

 • Mbowe akubali kukaa pembeni aache chama kwa akili nyingine inayoweza kufikiri vinginevyo.Mbowe atimize ahadi yake aliyotoa mwaka 2015 .Kwamba CHADEMA isipoingia IKULU mwaka 2015 atajiondoa Uenyekiti.Kukaa pembeni kwa mbowe kuna faida nyingi zaidi ya hasara.
 • Vyama Vya upinzani visivunje ushirikiano wao wa UKAWA..Ikiwezekana viutanue zaidi na kuuimarisha
 • Vyama vya upinzani sasa visimamie ajenda ya mabadiliko ya sheria ya Uchaguzi na muundo wa tume ya Uchaguzi
 • Mwaka 2020 na 2025 utakuwa ni mwaka wenye asilimia zaidi 60% ya wapigakura ambao wamezaliwa mwaka 1990 kwenda juu.Hiki ni kizazi cha Dot Com..Kizazi cha vijana...Vyama vya Upinzani vimsimamishe Zitto Kabwe kwa umoja wao.Wakubali kuweka tofauti zao Pembeni kwa maslahi ya Umma.
 • Lowasa na kundi lake wasiruhusiwe kuunda mtandao kama walivyokuwa wanafanya wakiwa huko CCM..Lowasa hapaswi kugombea mwaka 2020 kwa sababu hatakuwa na jipya katika kupambana na Magufuli.
 • Vyama vya Upinzani vikae chini vifanye utafiti kwa kupitia proffesional firms ili wawashauri namna ya kuwafikia wapiga kura wa mwaka 2020 na 2025...Kampeni maalum za ku target wapiga kura hao zianze sasa kwa mara moja.
 • Vyama vya Upinzani hasa CHADEMA watumie walau sh Mil 500 Kujenga ofisi ya makao makuu yenye hadhi yake...Kuwepo kwa ofisi hiyo kunatuma hata meseji ya wao kuaminika na wapiga kura.Waome saiolojia ya wapiga kura..hasa wanawake.
 

Nguruvi3

Platinum Member
Joined
Jun 21, 2010
Messages
13,491
Points
2,000

Nguruvi3

Platinum Member
Joined Jun 21, 2010
13,491 2,000
"Freeland, post: 20124561, member: 67846"]CHADEMA ya sasa imesinyaa na kushindwa kujua ifanye siasa kwa namna gani
A call for the recall of incumbent and incompetent leaders
CHADEMA ya sasa imeshindwa kurudi nyuma na kufanya tafakari ya ilipojikwaa na ifanye nini?
Ndiko kushindwa kwa uongozi uliopo
Kundi la lowasa linalotoka CCM aidha kwa kufukuzwa au kwa kumfuata yeye halitakuwa na jipya ndani ya CHADEMA...Ni kundi litakaloleta ile CCM ambayo ni ya mtandao na iliyojaa Rushwa..wakati CCM ya sasa ikijitahidi kujisafisha (Nakubali hili linaweza kukosolewa pia)
Sina uhakika CCM inajisafisha. Kinachoendelea ni visasi vya kisiasa. CCM ingetaka kujisafisha ingeenza na wahusika wa makando kando mengi

Kundi linalokuja ni asset au liability that remains to be seen, so far the impact is impalpable. Given the second chance they need to prove beyond any shadow of doubt that they're real a force to be reckon with. Again, I don't see any substantive evidence
CHADEMA ya sasa haishauriki na haina demokrasia thabiti ya kuhoji mambo ndani ya chama.
Nahisi watakusikia walipo and do the needful
Mbowe akubali kukaa pembeni aache chama kwa akili nyingine inayoweza kufikiri vinginevyo.Kukaa pembeni kwa mbowe kuna faida nyingi zaidi ya hasara.
Ameongoza mafanikio mengi sana na failures nyingi, it's time to pack and go
Haionekani kama ana jipya, ni wakati wa fikra mpya kama wanataka kubadilika
Vyama Vya upinzani visivunje ushirikiano wao wa UKAWA..Ikiwezekana viutanue zaidi na kuuimarisha
Ni wakati waalike vyama vingine, wasikubali CUF ikauuawa kwasababu baada ya hapo watafuata kingine. Ni dhambi kama ya kula nyama ya mtu. Wasimame kidete kuhakikisha njama na taasisi zinazotumiwa kuua CUF hazifanikiwi
Vyama vya upinzani sasa visimamie ajenda ya mabadiliko ya sheria ya Uchaguzi na muundo wa tume ya Uchaguzi
Bila hili, wasiingize timu uwanjani
Mwaka 2020 na 2025 utakuwa ni mwaka wenye asilimia zaidi 60% ya wapigakura ambao wamezaliwa mwaka 1990 kwenda juu.Hiki ni kizazi cha Dot Com..Kizazi cha vijana...Vyama vya Upinzani vimsimamishe Zitto Kabwe kwa umoja wao.Wakubali kuweka tofauti zao Pembeni kwa maslahi ya Umma.
Nadhani kuna potential nyingi tu. Wanachotakiwa kufanya ni kuacha ushindani bila kujali vyama na mshindi aungwe mkono. Age and gender ni vitu visivyoaminika katika kupata mgombea sahihi
Lowasa na kundi lake wasiruhusiwe kuunda mtandao kama walivyokuwa wanafanya wakiwa huko CCM..Lowasa hapaswi kugombea mwaka 2020 kwa sababu hatakuwa na jipya katika kupambana na Magufuli.
Kinachoshangaza bado EL anawatesa sana CCM, kila siku lazima aongelewe kama si mtandaoni ni mikutanoni.

Juzi kaongelewa tena Dodoma. Hivyo nani anaweza kukabaliana nao, uoga wa CCM unaeleza jambo. Je, ni mgombea mzuri wakati unaeleza jambo.
Ni wakati wa kutafuta mbadala kuzingatia nyakati na mazingira! ni open for discussions
Hapa ndipo wapinzani walitakiwa kuelekeza nguvu zao, kutafuta majibu
Vyama vya Upinzani vikae chini vifanye utafiti kwa kupitia proffesional firms ili wawashauri namna ya kuwafikia wapiga kura wa mwaka 2020 na 2025...Kampeni maalum za ku target wapiga kura hao zianze sasa kwa mara moja.
Walisema kuwa walitumia professional firm kupata mgombea 2010!
Vyama vya Upinzani hasa CHADEMA watumie walau sh Mil 500 Kujenga ofisi ya makao makuu yenye hadhi yake...Kuwepo kwa ofisi hiyo kunatuma hata meseji ya wao kuaminika na wapiga kura.Waome saiolojia ya wapiga kura..hasa wanawake.
Ni katika failures za Mbowe, ndio maana wakati haumpi nafasi tena.
 

Mag3

JF-Expert Member
Joined
May 31, 2008
Messages
10,852
Points
2,000

Mag3

JF-Expert Member
Joined May 31, 2008
10,852 2,000
Nimeupitia huu uzi nikajiuliza sana!
Ha ha haa Mkuu Nguruvi3, nimepitia uzi huu, duh! Nyakati hizo wana JF walikuwa wana JF kweli kweli na nguvu za hoja zilitamalaki tofauti na sasa ambapo hoja za nguvu ndizo zimekuwa fasheni katika mijadala. Asante kwa kutukumbusha wengine wetu tulikotoka...kwa kweli inafikirisha. Hivi Mzee Mkandara alikuwa na ugomvi gani nawe nyakati hizo?
 

TUJITEGEMEE

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2010
Messages
14,996
Points
2,000

TUJITEGEMEE

JF-Expert Member
Joined Nov 6, 2010
14,996 2,000
Udhaifu huo si wa wananchama, ni udhaifu wa viongozi.
Mchango wa wanachama ni pale wanapoachia udhaifu huo kuendelea kushamiri

Ni pale wanachama wanapoamini katika mizimu badala ya siasa ya sayansi

Hivi kweli 'Bongofleva' ni sehemu ya agenda za Upinzani? Ni sehemu ya political prowess!
Kuna mangapi yanayohitaji opposition party kusimama na kuyasemea! Bongofleva! Real!

Hili linahitaji mjadala mrefu na endelevu na kwakweli tutapiga kambi kulizungumzia

Kukaa kimya hakutakuwa na tofauti na wanaoamini katika mizimu na tunguli
Haonewi mtu hapendelewi mtu, ukweli utamalaki na ndio dawa mujarabu

Kwa kuanzia tu Mwenyekiti wa Chadema akae pembeni, kama hawezi asaidiwe kukaa pembeni. Hakuna mchawi hakuna west countries.

Tusemezane
Naam bado mwenyekiti hajakusikiliza...na sasa anasema kwa wakati huu Chadema itaimarika zaidi.
 

Mag3

JF-Expert Member
Joined
May 31, 2008
Messages
10,852
Points
2,000

Mag3

JF-Expert Member
Joined May 31, 2008
10,852 2,000
Ha ha haaa...!
===
Ndiyo maana ninawashangaa wanaowaza kuifungia JF ama kuibugudhi isifanye kazi zake sawa sawa. Asante kwa kutukumbusha Mwalimu Mkuu wangu wa JF!
Nawaomba wana JF wote waliojiunga baada ya uchaguzi wa mwaka 2010 waupitie uzi huu, kuna mengi ya kujifunza...asante JF kwa kutunza kumbukumbu!
 

Nguruvi3

Platinum Member
Joined
Jun 21, 2010
Messages
13,491
Points
2,000

Nguruvi3

Platinum Member
Joined Jun 21, 2010
13,491 2,000
Ha ha haa Mkuu Nguruvi3, nimepitia uzi huu, duh! Nyakati hizo wana JF walikuwa wana JF kweli kweli na nguvu za hoja zilitamalaki tofauti na sasa ambapo hoja za nguvu ndizo zimekuwa fasheni katika mijadala. Asante kwa kutukumbusha wengine wetu tulikotoka...kwa kweli inafikirisha. Hivi Mzee Mkandara alikuwa na ugomvi gani nawe nyakati hizo?
Mkubwa hata hizo hoja za nguvu zimekuwa hazina miguu wala kichwa.
Kwa mfano, uzi unaanzishwa '' Kwanini tusiwe na chama kimoja'' . Ukiingia kuusoma hakuna hoja yoyote, mada ina mstari mmoja '' ili tuwe kama China''. Ni ngumu sana kuchangia.
Kabla ya hapo kichwa hicho hicho cha habari kingetetewa au kupingwa kwa hoja na mantiki

Viongozi wengi sana ''wamekulia jamvini'' na wakubwa wakiingia ofisini kitu cha kwanza JF kuna trend nini. Jambo hili lilileta ustawi wa jamii, hoja zilifanyiwa kazi vyovyote iwavyo

Mwana wa Nnauye na mradi wa LB7 walifanikiwa kupoteza quality ya mada JF

Hili lina uhakika na mabaki ya LB7 ndiyo tunayosoma kila siku hapa na mada za hovyo sana
Wanakaa na kutafuta 'talk point' kisha kuileta bila kuwa na utetezi wa mantiki

Mfano, hivi kuna elimu ipi bure ikiwa watu wanalipa kodi?
Hilo lilikuwa kwa hasara ya Taifa na Mwana wa Nnauye anapaswa kuomba radhi

Mzee Kinana ni mtu makini sana. Alisoma madhaifu ya CCM hapa akafanyia kazi.
Ni kupitia hilo aliinusuru sana CCM akisaidiana na Mwana wa Nnauye

Ndiyo maana hata siku moja Kinana hakuwahi kupiga dongo JF, unajua alikuwa 'mwenzetu'

Mkuu unakumbuka mawazo kama ya ''treni ya Mwakyembe'', wazo la ring road Dodoma, mjadala wa Katiba, Diaspora, Kibaha-Dar lane 6, shule , afya n.k. ni zao la michango JF!

Hapo hujagusa vita ya ufisadi na rushwa kama UDA ambao eti leo ni vita mpya kabisa!! haha

Mkuu zama zile, leo watu wangedadavua uhusiano wa EL kurejea Lumumba, siku ya msafara wa Ruge! Waliompokea n.k.

Kudhani kuwa JF ikifa ni heri ni ujinga uliopitiliza. Watu makini wangeiacha huru ili wajue jamii inasema nini. Utafiti wa juzi umeonyesha hilo. Wangejifunza kupitia mawazo n.k

Katika makosa CCM inayofanya ni jitihada za kuiua JF. Hata wnaJF wa CCM wanaliona hilo ni wazo bovu sana na chanzo cha Chama kuchukiwa sana, kinaendeshwa na dola

Kwa bahati mbaya hakuna anayeweza kusema tena! CCM ya kupingana bila kupigana haipo

Imebaki CCM ya watu 3! Mwenye, katibu na Mwenezi. Hao ndio CC ndiyo NEC n.k

Kuhusu 'ugomvi' na Mkandara , hatukuwa na ugomvi kama wanadamu. Tuna ugomvi kuhusu Zanzibar na masuala ya kijamii ambayo Mkandara aliyawekea lens ya udini, hilo tu!
Yeye anaweza kuita red kama pink, yellow kama Orange ndiyo maana hucheza na grey area
Mimi ni color blind, ninaona white or black
 

Nguruvi3

Platinum Member
Joined
Jun 21, 2010
Messages
13,491
Points
2,000

Nguruvi3

Platinum Member
Joined Jun 21, 2010
13,491 2,000
OPEN BOOK EXAMINATION

Huu ni mtihani anaopewa mtahiniwa akiruhusiwa kufungua vitabu kufanya rejea za uchambuzi

Kupitia mtihani huo, mtahiniwa anaweza kujibu swali hasa yanayohitaji uchambuzi na tathmini

Wengi hudanganyika na kuamini ni mtihani rahisi sana, la hasha, pengine ni mgumu kuliko
Mtahiniwa anapaswa kuwa na weledi ili kupanga hoja, kujibu hoja na hata kupendekeza hoja

Tatizo kubwa linalowakabili wanasiasa wa wapinzani ni kushindwa kufungua vitabu wakati wa open book exam, hata wanapofungua hujikuta wakisoma 'chapter' isiyohusiana na mtihani.

Swali linalosumbua, mtihani wa kawaida ni tatizo, open book ni tatizo,mtihani gani watafaulu?

Nayasema haya kufuatia kauli ya M/kiti wa CDM (na nadhani ni kweli) akitoa salam zake kutoka magereza kwa kuwausia wanachama wake kwa kauli mbiu 'safari ya Kigoma inaendelea''

Kilichonishtua ni pale anaposema , Chama chake kitafanya tathmini ya wahamaji kutoka CCM

Mbowe ameshindwa open book exam! Mbona haya yapo katika uzi huu kwa kina kabisa!

Miaka 5 au zaidi tulieleza analoeleza leo kuhusu wahamaji kutoka CCM.
Tulimpa mifano ya akina Mrema, Lamwai, Ngaiwaya, Ahmad Rashid na wengine wengi tu

Nakumbuka tulimpa mfano kuwa wale Wanakijiji waliotoa ardhi ya kujenga ofisi ya CDM Iringa iliyopelekea kifo cha Mwangosi, ndio wanachama hai, wakweli na wanaoamini katika itikadi

Tukamuonya, hawa wanaokatwa majina na kuhama si wanachama ni 'wanahama'

Wakati tunampa rejea za 'open book exam' tulimpa na chapter Muhimu yenye majibu ya EL

Tulimsomea mistari , kwamba, Lowassa hakufuata itikadi ya CDM, alifuata uteuzi wa Urais.

Laiti angefuata itikadi angelifanya hivyo siku nyingi na wala asingetamani kuteuliwa

Aya ya mwisho ya chapter tuliyompa ilieleza wazi, Lowassa pamoja na mafurushi ya mizigo anayokuja nayo, tunamfahamu alivyopiga vita Upinzani kupitia katiba pengine kuliko JK

Na muhimu zaidi tulimwambia mizigo aliyobeba hailingani na itikadi ya chama chake

Majibu yakawa mepesi, kanyaga twende! EL anakuja na vigogo 20.
Ujio wake utarahisha kukamata dola kama lengo la upinzani!

Majibu hayo yakazaa kosa jingine. Kwamba, lengo la chama cha siasa ni kushika dola bila kuwa na mkakati wa kufikia lengo. Ilikuwa kana kwamba EL alikuwa Mwarobaini wa tatizo la tume huru ya uchaguzi, usimamizi wa uchaguzi, Policm, matokeo n.k.

Nguvu kubwa zikaelekezwa kumzungusha mitaani kwa lundo la mashabiki na kusahau kuwa lengo la kushika dola lina njia kadhaa, kupitia Urais au kushika Bunge au kuzuia 2/3 majority

Wapinzani wakaamini njia rahisi ya kufika 'paradiso au Akhera' ili kuupata ufalme wa mbinguni au ''kiama swahihi'' ni kukata shingo next few hours unazungumza na Maulana katika kiti cha enzi

Hawakuamini ili kufika akhera au paradiso kunahitaji kumenyeka, 'kuitangaza Injili au kufanya Daawa' kutoa zaka au sadaka na kujipekwesha kwa mola ili siku ya hesabu wawe pema peponi

Mbowe na CDM wakasahau Ubunge na matatizo ya chaguzi za nchi kwa kutokuwa na 'uwanja sawa wa ushindani' . Wakaamini EL ni tume ya uchaguzi, ni Polisi, ni Usalama n.k.

Leo EL karejea nyumbani kutoka matembezini watu wanapigwa na butwaa!

Hivi kuna kosa mtu kurejea kwao? Leo Mbowe anataka tathmini ya wahamaji akitafuta vitabu vya mwongozo wakati JF ina chapter zote za open book examination tena zikiwa ''highlighted'

Tusemezane
 

Rev. Kishoka

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2006
Messages
4,536
Points
2,000

Rev. Kishoka

JF-Expert Member
Joined Mar 7, 2006
4,536 2,000
OPEN BOOK EXAMINATION

Huu ni mtihani anaopewa mtahiniwa akiruhusiwa kufungua vitabu kufanya rejea za uchambuzi

Kupitia mtihani huo, mtahiniwa anaweza kujibu swali hasa yanayohitaji uchambuzi na tathmini

Wengi hudanganyika na kuamini ni mtihani rahisi sana, la hasha, pengine ni mgumu kuliko
Mtahiniwa anapaswa kuwa na weledi ili kupanga hoja, kujibu hoja na hata kupendekeza hoja

Tatizo kubwa linalowakabili wanasiasa wa wapinzani ni kushindwa kufungua vitabu wakati wa open book exam, hata wanapofungua hujikuta wakisoma 'chapter' isiyohusiana na mtihani.

Swali linalosumbua, mtihani wa kawaida ni tatizo, open book ni tatizo,mtihani gani watafaulu?


Mbowe na CDM wakasahau Ubunge na matatizo ya chaguzi za nchi kwa kutokuwa na 'uwanja sawa wa ushindani' . Wakaamini EL ni tume ya uchaguzi, ni Polisi, ni Usalama n.k.

Leo EL karejea nyumbani kutoka matembezini watu wanapigwa na butwaa!

Hivi kuna kosa mtu kurejea kwao? Leo Mbowe anataka tathmini ya wahamaji akitafuta vitabu vya mwongozo wakati JF ina chapter zote za open book examination tena zikiwa ''highlighted'

Tusemezane
Nguruvi3,

Marehemu Marijani Rajabu aliimba... "mimi naogopa, kuusema ukweli, ingawa ninayo haki nikisema ukweli wazee wangu "huyu mtoto siku hizi hana adabu" "

Nimetafakari sana kauli ya Lowassa "Nimerudi nyumbani" kisha vifijo hasa vya uongozi mzima wa CCM bara uliokuwapo pale Lumumba... kisha ile picha ya kikao cha faragha cha Lowassa, Rostam, Magufuli na Bashiru... Najiuliza Watanzania wanafikiria nini? Watanzania wanapaswa waitazameje CCM?

Lakini napata jibu kuwa ikiwa 2015 Watanzania milioni 6 walimpa kura ambazo Chadema waliona ni mtaji mkubwa sana baada ya jitihada za kumtakasa... je leo hii ni agenda gani Upinzani unaweza kujenga dhidi ya CCM na wananchi wakasikiliza na kufanya mapinduzi ya kweli siku ya uchaguzi?

Hii ndio Open book kwa Chadema na sisi sote...

"Mimi naogopa kusema ukweli ingawa ninayo haki...."

 

Nguruvi3

Platinum Member
Joined
Jun 21, 2010
Messages
13,491
Points
2,000

Nguruvi3

Platinum Member
Joined Jun 21, 2010
13,491 2,000
SUPER MATIMILA NA Dr REMMY (R.I.P)
MZEE ALIYEREJEA NYUMBANI ASHAURIWE

Mkuu Kishoka ameweka wimbo wa Marijani ulionikumbusha wimbo wa super Matimila
Matimila wanaimba wakisema 'Narudi nyumbani, narudi matimila, nyumbani kuzuri n.k.'

Mheshimiwa kasikika akisema amerudi nyumbani baada ya kukaa ugenini kwa miaka kadhaa

Kurudi kwake kumewaacha ''wenyeji wakiwa wamaetunduwaa' pasi kuamini kilichotokea

Wenyeji hawapaswi kumlaumu, wajilaumu kwanza, si kumlaumu mgeni
Mh ametumia haki yake ya kikatiba kwenda na kurudi,haki aliyo nayo kila mmoja wetu

Mh alipopiga hodi hakuwa na mzigo wa sera, itikadi au mkakati. Aliahidi wapambe 20 tu
Leo kaondoka bila kuchukua mzigo, sera, itikadi au mkakati, alaumiwe kwa lipi?

Wenyeji watulie , wakae kimya ,wamwache mgeni aondoke kwa amani kama alivyokuja

Lakini pia Mh anawajibu katika hili. Kuhama na kurejea ni haki yake isiyo na shaka

Kinachoshtua ni kusikia amepanga kuongea na vyombo vya habari kueleza 'sababu za kurudi'

Kama wapo watu wanaomshauri Mheshimiwa, tungewashauri wamshauri akae kimya

Mh hana cha kuongea, na wala hana cha kupoteza tena! Chapter inayomhusu imefungwa

Endapo ataamua kuongea Mh atakarabisha habari na maswali yanayoweza kumwacha pabaya na pagumu kuliko alipo sasa. Ninaamini bado ana kaheshima,ni vema alinde kidogo alichonacho

Kwanza, Mh alirudi kwa kujificha nyuma ya msiba uliokuwa unaendelea.
Ni vema akaendelea kujificha kwasababu zile zile za kujificha umma ukiwa katika majonzi

Pili, kurudi nyumbani si tukio tena. Kuondoka ilikuwa tukio! Mwiba hutoka ulipoingilia

Tatu, Mh akizungumza atueleze kilichomkimbiza nyumbani ni kipi? Na huko ughaibuni alikwenda akitaraji nini? Na alifanya nini kwa mtu wa hadhi na nafasi yake zama hizo?

Hoja ya kwamba alikatwa jina 'Idodomya'hataisema,hoja ya kutoridhika na sera hataisema wala hoja kwamba alivutiwa na sera za 'ughaibuni' haitakuwa na mashiko na hataisema

Hoja kwamba, ugenini hakufai haitakuwa na mashiko. Hakufai vipi wakati alipewa usukani?
Hoja kwamba nyumbani sasa ni kwema haina mashiko. Hii itamlipukia mikononi kwa aibu

Kwa mtu aliyefikia hadhi yake katika 'sirikali na mjengoni', kwamba, hakujua nini kifanyike itaondoa mashaka na kutia wasi wasi huenda nchi iliendeshwa kwa solar energy nyakati zake

Na hoja kwamba aliyotaka sasa yanasimamiwa haina mashiko.

Ataulizwa, kwanini asitupe mikadi ya vyama akabaki kuwa raia huru mwenye furaha badala ya kusimamishwa katika parade akitukumbusha minada ya mbuzi na kondoo!

Hoja aliyo nayo ni kusema kwa sauti akitetema ktik kuwapamba, mambo ya 'familia' yakae sawa

Hii ina mashiko kwani itamsaidia katika family level, hata hivyo itathibitisha hitimisho la kitabu chenye chapter ya Urais na karatasi zake kufungia vitumbua kama si makaimati

Tusemezane
 

Forum statistics

Threads 1,390,254
Members 528,131
Posts 34,047,287
Top