Alinda
Platinum Member
- Jun 26, 2008
- 1,695
- 2,145
Hivi wewe kweli unataka kusema kila mtu humu ataandika neno kwa neno la mtu alosema au unaandika ulichoelewa? Watu wote wamemuelewa hivyo, na hata viongozi wa dini wamekemea kwa hilo iweje wewe ulielewa tofauti?
Sasa kama Lowassa ameomba msamaha, kaomba msamaha kasema nini? kwamba aombewe imekuwa kosa la kuomba msamaha!? au kuna zaidi ya kuombewa! Wewe umeelewaje ile hotuba ya Lowassa pale kanisani kufikia kaomba msamaha alisema nini maana kuombewa kila mtu anasema na hakuna mahala unapozitaka dua za watu kama kanisa lako!
Zaidi ya hayo mbona humu mnaandika maneno mengi ambayo hata Dr.Slaa hakusema hivyo, lakini tumeelewa kuwa yanaendana na maana ile ile ya msemaji, iweje utake mimi niandike kila neno sawa na matamshi ya Lowassa. Kama haya sio mahaba ni nini tena dadangu!
Nashukuru sana kwa kukiri kuwa "ulichomeka maneno ya uongo kwa manufaa yako"ni hilo nililotaka kukuonyesha..
Maadam huwa sipendi kujadili mada zinazohusu udini kwa leo nitaishia hapo.
Swala la Richmond huwezi kulifuta kirahisi hivyo kwa sbaabu wewe unaona hakuna sababu. Sababu zipo na tunataka kujua yote toka kuuzwa kwa nyumba za serikali, ubinafsishaji wa mashirika, uporaji wa nyumba za serikali na mashamba, EPA, Rada, IPTL, Meremeta, Kagoda na mengineyo mengi ambayo ndio sababu kubwa ya wananchi kuichoka CCM. Mimi binafsi nitamfagilia kiongozi yeyote ambaye atakuwa tayari kurudisha maswala yote haya mezani kwa sababu hatuwezi kuzungumzia Uadilifu na uwajibikaji wakati tunaacha Kuhujumu Uchumi kuwa ni mambo yalopita, wakati sheria zipo zimekiukwa na hawa Untouchables!.
Tumefika hapa leo kwa sababu yao,na hatuwezi kuendelea kuwafuga tukitegemea mabadiliko, wana kesi kubwa ya kujibu kwa wananchi kwa sababu sisi ndio waajiri wao. What next? Tutawahukumu kwa kuujua ukweli kuliko kuendelea kuwashutumu watu pengine hawahusiki kabisa. Ukweli utawaacha huru! Leo unamsema Mwakyembe kwa dhana tu ya kuinusuru serikali wakati msimamizi wa shughuli za serikali ni Waziri mkuu. Tunachomkana Lowassa ni Ufisadi wake, hakuwa muadilifu katika kusimamia majukumu alopewa kiasi kwamba alihujumu Uchumi wetu, hii ni Kashfa kubwa kwa mgombea urais! Na kama itawezekana ukweli ukitolewa tutaandika kwa uhakika kabisa na hatutabisha..
Mpaka hapo tuko pamoja..