CHADEMA: Ufafanuzi juu ya Taarifa ya Ndugu Ali Omari Chitanda

CHADEMA: Ufafanuzi juu ya Taarifa ya Ndugu Ali Omari Chitanda

Umbali kwako ni mwisho wa pua yako. Udini haukuanza na tamko la Mtei, uliasisiwa na Chama fulani kwenye ilani yake ya mwaka 2005 na kukuzwa sana kwenye kampeni za 2010

Kwahiyo Mtei aliendelleza tu?
 
Mkuu Makene tunashukuru kwa kazi nzuri ya kujibu kwa wakati mwafaka, hii imekuwa ndani ya masaa yasiyopungua sita

Huu ndio uwajibikaji wa chama kinachojiandaa kushika dola

Utagombea Ubunge jimbo la Kalenga au Butiama ??!
 
Kama Chitanda alifikiri kujitoa uongozi Chadema ni kumsaidia Zitto aonekane ameonewa mbele ya Jamii, amejidanganya sana. Sasa hivi naimarika katika hisia zangu kwamba wale wanaotuhumu maamuzi ya CC-Chadema ni wale watanzania walio na uvivu wa fikira, wenye kuangalia sura, udini na ukanda wa mtoa hoja kuliko hoja yenyewe.
 
Nadhani ifike mahali wana CDM kuzipima hoja zote... Kuanzia ile ya Zitto, Kitila, Nyakarungu kwny blog ya bongoafrica na hii ya M/kiti wa Lindi... Sitaki kuamini kuwa hoja hizi hazina mashiko... Kwa mf hivi ni kweli tukizingatia gender balance hakuna wanawake wenye uwezo wa kushika nyadhifa za kurugenzi na hii tuhuma ya viongozi wa juu kuchukuliwa kikanda ambayo ni ya muda mrefu... Je, hakuna wanachama wenye uwezo wa kushika nyadhifa hizo... Tuache kuyafumbia macho haya na kujipa matumaini kuwa CDM ina nguvu... Tusisahau kuwa ngoma ikivuma sana yaweza pasuka... Inaonekana tunasahau sana enzi za NCCR!!?? Iko wapi leo... Ushauri: Zitto na Kitila warudishiwe nyadhifa zao haraka iwezekanavyo kabla ya kuchafua hali ya hewa hawa watu wana siri kubwa za chama ambazo zitakuwa mtaji kwa vyama pinzani...
 
Makene umefanya vizuri sana,,,kujibu tuhuma hizi,,,mtu mwenye kuleta hoja za udini, ukabila na ukanda ni wa kuogopwa kama ukoma,,,ila pamoja na hayo,,,tunaingiwa na shaka ni kwanini hamkujibu ule upotoshaji juu ya ripoti ya siri kwa haraka kama hivi,,,,na hili ndio tatizo letu ndani ya chadema, na tatizo hili ndio linalopelekea tuonekane wabaguzi, wadini na wa kanda ingawa si kweli. Chama kijirekebishe, kilitakiwa kujibu ule upotoshaji kwa haraka kama ilivyofanya sasa hivi.
 
Tunaishukuru Kurugenzi ya Habari kwa Taarifa za uhakika na kwa wakati muafaka. Wapotoshaji na Wanafiki ni wengi lakini kwa msaada wa Mungu CHADEMA itashinda na itazidi kuwa imara.
 
Nnachokiona hapa ni propaganda tu.....!!! bado hujajibu hoja Ndg Makene, kama amepotosha wewe umepotosha zaidi coz hujataja kiasi wanachopokea, pili suala la ubaguzi me nahisi lazima lifanyiwe kazi, mf sitaki kuamini kuwa ndani ya CDM hakuna wanawake wenye sifa za kuwa katika nafasi tajwa, huu ni ubaguzi katika suala hili la udini msilichukulie kiurahisi ni suala ambalo limeongelewa muda mrefu pia na usituaminishe kuwa hakuna waislamu wenye sifa na vigezo vya kuwa katika nafasi hizo kuanzia kwa M/kiti, Katibu, na waurugenzi!!!!!..... laikini pia sitaki kuamini kuwa hoja zilizotolewa na kuwa ni za uongo kwa watu wote. Rejea maelezo ya Nyakarungu kwny blog ya bongoafrica, Zitto, Dr. Kitila nk...... nadhani kuna haja ya kuacha propaganda na kujipanga upya... msisahau historia ya kuvunjika kwa vyama mbalimbali duniani. nionavyo mimi bado hujajibu hoja...
 
Najua ni vigumu kwa baba ndani ya nyumba akikosea watoto kukiri kuwa amekosea hizi ndo mila zetu za kiafrika.... inawezekana Viongozi wa juu wakaona wako sahihi lakini wasisahau kuwa uchaguzi wa aina yeyote iwe ndani ya Chama na nje ya chama unahitaji maandalizi.... kujiandaa kwa wapambe wa Zitto ama yeye mwenyewe binafsi siyo kosa..... hili liangaliwe kwa macho yote na fikra pevu kwa kuacha hisia mbaya walizonazo watu.... Nilichojifunza kwetu Afrika siasa inachukuliwa kama uadui baadala ya kuichukulia siasa kama hoja.... Ushindi wa siasa ni hoja siyo chuki. Kumchukia mtu kisa ni mpinzani wako hili ni tatizo..... Nadhani njia rahisi ya kumjua mpinzani wako anawaza nini ana hoja gani ni kuwa karibu nae..... kitu kingine tunasahau kuwa hawa watu wamelelewa pamoja wamekuwa pamoja tofauti za siasa ndiyo ziwatenganishe???? Huu ni ushamba......!!!! tuache haya maisha ya kuwachukulia wapinzani wetu kuwa maadui huu ni utumwa wa akili..... jaribu kurudi nyuma kwa Obama na Mama Clinton, Kikwete na Mbatia nk. Mtu kama anaweza mpeni heshima yake.... Zitto ni moja ya wanasiasa mashuhuri na Nguri ndani na nje ya nchi..... hivi sasa ni moja ya wanasiasa aikoni vijana ndani Africa na hata nje.... Mh. Kafurila alifukuzwa bado anaendelea vema, Je, hili si fundisho kwa CDM. Tuache uzembe wa kufikiri........
 
BW. Makene kuna suala la udini [CCM watalitumia sana kama walivyofanya kwa CUF] kuna MuIslam mwenye wadhifa mkubwa CDM? Fafanua sasa kwani huko mbele litawagharimu
 
Nadhani ifike mahali wana CDM kuzipima hoja zote... Kuanzia ile ya Zitto, Kitila, Nyakarungu kwny blog ya bongoafrica na hii ya M/kiti wa Lindi... Sitaki kuamini kuwa hoja hizi hazina mashiko... Kwa mf hivi ni kweli tukizingatia gender balance hakuna wanawake wenye uwezo wa kushika nyadhifa za kurugenzi na hii tuhuma ya viongozi wa juu kuchukuliwa kikanda ambayo ni ya muda mrefu... Je, hakuna wanachama wenye uwezo wa kushika nyadhifa hizo... Tuache kuyafumbia macho haya na kujipa matumaini kuwa CDM ina nguvu... Tusisahau kuwa ngoma ikivuma sana yaweza pasuka... Inaonekana tunasahau sana enzi za NCCR!!?? Iko wapi leo... Ushauri: Zitto na Kitila warudishiwe nyadhifa zao haraka iwezekanavyo kabla ya kuchafua hali ya hewa hawa watu wana siri kubwa za chama ambazo zitakuwa mtaji kwa vyama pinzani...

Ndugu Nzilo,warudishwe kwa kigezo gani,cha kuwa na siri kubwa za Chama....???
Yaani kwa kuwa mtu ana siri kubwa za chama hata kama ni msaliti arudishwe....???
Sioni kama huo ni ushauri mzuri kwa Chama na kama unadhani kufukuzwa uanachama kwa hao wasaliti CHADEMA itakuwa kama NCCR nakuhakikishia hicho kitu hakitatokea na badala yake CHADEMA itazidi kuweka heshima na kuaminiwa na wanachama na wapenzi wake kuliko unavyofikiri.

Watanzania wa leo si wajinga wa masuala ya Demokrasia tena kama mwanzo vyama vya upinzani vilipo anzishwa.Naamini hata leo hii wasaliti wakijitokeza ndani ya vyama vingine vya upinzani kama NCCR hawatafanikiwa katika uzandiki wao labda kama wameisha mpandikiza mtu wao katika nafasi ya UWENYEKITI WA CHAMA kama anavyotaka kumpandikiza Zitto Kabwe awe mwenyekiti wa CHADEMA.
Na kwa UNAFIKI wao huu wasitegemee asilani ZZK kuwa M/Kiti wa Chadema,labda akitaka aunde chama kingine cha siasa lakini sio Chadema.
Kila la kheri CHADEMA ITADUMU MILELE ASILANI.
 
..
Kupitia taarifa yake, anasema alikuwa mtu aliyeaminiwa hadi kuwa katika vikao muhimu, lakini wakati huo huo anasema kuna ubaguzi! ...

He he hee! Kuna ubaguzi, wakati huo huo anaaminiwa hadi kuhudhuria vikao muhimu! Hakujipanga!
 
Nnachokiona hapa ni propaganda tu.....!!! bado hujajibu hoja Ndg Makene, kama amepotosha wewe umepotosha zaidi coz hujataja kiasi wanachopokea, pili suala la ubaguzi me nahisi lazima lifanyiwe kazi, mf sitaki kuamini kuwa ndani ya CDM hakuna wanawake wenye sifa za kuwa katika nafasi tajwa, huu ni ubaguzi katika suala hili la udini msilichukulie kiurahisi ni suala ambalo limeongelewa muda mrefu pia na usituaminishe kuwa hakuna waislamu wenye sifa na vigezo vya kuwa katika nafasi hizo kuanzia kwa M/kiti, Katibu, na waurugenzi!!!!!..... laikini pia sitaki kuamini kuwa hoja zilizotolewa na kuwa ni za uongo kwa watu wote. Rejea maelezo ya Nyakarungu kwny blog ya bongoafrica, Zitto, Dr. Kitila nk...... nadhani kuna haja ya kuacha propaganda na kujipanga upya... msisahau historia ya kuvunjika kwa vyama mbalimbali duniani. nionavyo mimi bado hujajibu hoja...

Nzilo

Hatutakulazimisha kuamini. Waweza kuamini unakopenda kuamini. Wakati mwingine, mbali ya ushawishi wa hoja, kuamini au kutokuamini huambatana na kupenda au kutopenda.

Labda hujasoma kwa uzuri, mathalani taarifa iliposema;

Hadi sasa uteuzi wa kurugenzi za Makao Makuu ya CHADEMA haujakamilika. Bado kuna nafasi zinazotakiwa kujazwa kwa kufuata taratibu za chama."

Nafasi kama ya uenyekiti ni ya kuchaguliwa. Halikadhalika Makamu wake, bara na Zanzibar. Hiyo ndiyo demokrasia. Kama ulitaka wachaguliwe wanawake wote au '50/50'mnayoimba, kura hazikufanikiwa katika hilo.

Lakini mnaotaka kuifanya dini ya mtu kuwa moja ya vigezo vya uongozi, mbona hamtaki kusema ukweli kuwa CHADEMA imeongozwa na watu wa dini zote, kutoka makabila na maeneo ya nchi. Tena viongozi wakuu kabisa. Mbona hamuhoji safu ya uongozi wa CCM ilivyo sasa.

Hatuwezi kuzungumzia hoja za watu kama Nyakarungu...ni nani! Bila shaka walijibiwa na vijana wa CHASO kwa usahihi kabisa. Mtu mmoja akasema ''hawa kweli ndiyo vijana wa CHADEMA...si wale wengine waliokuwa wamevaa suti na jua lote hili la Dar es Salaam." Vijana wa CHASO walionekana kwenye picha wakiwa na kombati. Alama ya mapambano dhidi ya status quo. Hakuna kulala...

Watu wa namna hiyo (ya Nyakarungu) wanaweza ku-exist na kupata nafasi wasizostahili kuwa sehemu ya nukuu za vyombo vya habari kwa sababu tu tuna uzembe fulani katika baadhi ya vyombo vyetu vya habari.
 
Dr. Slaa alisema watajibu pale patakapokuwa na upotoshaji mkubwa. Pamoja na uongo mwingi aliosema huyu Chitanda, vile vile alipotosha mahali wanapotoka wakurugenzi ndio maana Makene akamsahihisha.....Kwenye suala la udini, viongozi hawachaguliwi kwa udini wao, bali kwa uwezo wao, na huyu jamaa hajapotosha aliposema wote ni wakristo bali ameonyesha tu kwamba yeye ni mdini (anaangalia watu kwa jicho la udini bila kujali uwezo). Ulitaka Makene ajibu upotoshaji gani hapo? Sasa kama wote ni wakristo ulitaka Makene asema mmoja ni muislam ?
Mkuu vipio kuhusu maneno ya huyu mwasisi wa Chadema hapa chini. Yeye anazingatia nini katika kuchagua viongozi?


Kwa mfano ni jambo la kichekesho kwamba Tanzania Bara ambayo ina Watu takriban 42 milioni iwakilishe na wajumbe sawa na Tanzania Zanzibar ambayo ina watu wasiozidi 1.5 milioni. Mfano wa pili ni kwamba, licha ya kwamba Tanzania siyo nchi inayozingatia dini katika maamuzi yake ya kisiasa, ni lazima tukubali kuwa madhehebu ya dini yana influence katika mchakato na hatimaye maamuzi. Nikihesabu Waislamu katika hii Tume kwa kuzingatia majina naona zaidi ya theluthi mbili ni Wao. Wengine ni Wakristo au watu wasiokuwa na dini yoyote.

Hata kama ni lazima tujali Muungano wa Jamhuri yetu, hatuwezi kupuuza ukweli kuwa sasa kuna matatizo ya umilikaji wa raslimali maliasili (e.g. gas), na kuna wananchi wamediriki hata kwenda Umoja wa Mataifa kudai Zanzibar ijiondoe.

Haya ni mambo mazito na nimeona ni vema niyataje sasa, siyo tu yajadiliwe na Tume, bali ikiwa ni lazima, basi mjadala uendelee hata baada ya Tume kutoa taarifa na Bunge Maalum kupitisha Katiba Mpya.
 
Umejibu nini sasa mbona haujasema wakurugenzi wanalipwa kiasi gani, halafu kulikuwa na haja gani kutaja mikoa wanaotoka wakati hoja ilikuwa mbona wote ni Wakirsto, rudi ujibu.

Kwan dini si kitu chenye kubadilika leo akiwa mkristo na kesho akisilimu je aondolewe kwny wadhifa wake?Pendekeza katiba ifanyiwe mabadiliko ili kila nafasi iwekewe kigezo cha dini
 
BW. Makene kuna suala la udini [CCM watalitumia sana kama walivyofanya kwa CUF] kuna MuIslam mwenye wadhifa mkubwa CDM? Fafanua sasa kwani huko mbele litawagharimu

Kivava

Kitu pekee kinaweza kuigharimu CHADEMA ni endapo itaacha kusimama katika haki na ukweli. Kusimama katika misingi yake; katiba, taratinu, kanuni, maadili, itifaki na miongozo. Ni pale itakapoacha kusimamia haki na matumaini ya Watanzania wanyonge wasiokuwa na sauti, bila kujali wanakotokea, wanaswali au kusali wapi wala rangi zao.

Kwa sababu tu hujawahi kujisumbua kutafuta majibu ya swali lako kwa sababu yako wazi mno, nalazimika kufanya 'udini' kwa kutaja fulani na fulani katika nafasi fulani ni dini fulani. Shame kbs.

Kabla ya maamuzi ya karibuni ya Kamati Kuu na hatua ya Mzee Arfi, katika uongozi wa juu kabisa, kulikuwa na waislamu wanne, Makamu Mwenyekiti Bara, Makamu Mkiti Zanzibar, Naibu Katibu Bara, Naibu Katibu Zanzibar.

Kwa mujibu wa katiba, Naibu Zanzibar ndiye pia Chief of Staff, mkuu wa itifaki ndani ya chama.

Hofu yako haina sababu wala hoja yoyote yenye mashiko. Propaganda za CCM ambazo wenyewe ndiyo wanaziishi. Angalia safu ya sekretarieti yao Makao Makuu na Uongozi wa juu wa chama hicho!

Mbona Mzee Mtei alipostaafu na nafasi yake ya uenyekiti kuchukuliwa wa CHADEMA kuchukuliwa Mohamed Ali Nyaga Makani "Bob", na wasaidizi wake akiwemo Dkt. Amani Walid Kabourou na wengine mnaowajua, hamkulalamika hofu ya udini?

Uadilifu, uwezo na utayari wa mtu kuwatumikia watu, ndiyo masuala ya msingi ndani ya CHADEMA! Mtu mwenye sifa hizo hawezi kuangalia rangi, kabila, kanda wala dini atakapokuwa katika nafasi ya uongozi au utendaji.

Makamu Mkiti Zanzibar, Said Issa Mohamed huwa ana kauli yake moja hupenda kuisema katika mikutano ya hadhara, husema hivi;

"Mnasema udini eti kwa sababu Dkt. Slaa alikuwa padri...alikuwa...alikuwa hiyo ni historia. Mimi hapa leo...hadi leo hii unavyoniona hapa ni imamu wa msikiti huko kwetu Pemba...naswalisha..."

 
Jenifa hivi huna boy friend wa kukuscrew muda huu? Maana nana unajambajamba tu hapa kwa kusumbuliwa na stress.

Tangu lini mtoto akachukuwa kabila la mama yake?

out of topic vp mkuu ule mchezo wa kutongoza wanaume umeacha au?
 
kweli nimeamini 2015 tunachukua nchi tukiwa wasafi maana naona chui waliokuwa zizini mwa kondoo wanaanza kujitoa taratibu kwa kuhofia kugundulika mlobaki mlango upo wazi
 
Back
Top Bottom