lutemi
JF-Expert Member
- Dec 24, 2013
- 1,743
- 1,379
Una mpango gani na hivyo vyombo au unataka vifutwe kwenye ramani ya Dunia?.Popote mlipo, huu Ni ushauri wangu kwenu, mikutano yenu haiwezi kutegemea matangazo ya gari za matangazo na social media, katika pesa mliyonayo, ongeeni na ITV/ AZAM wawe wanarusha matangazo na ratiba za kampeni zenu. Ikishindikana kwa hizo media, basi boresheni CHADEMA TV iwe active LIVE 24 HRS. Iwe inatoa ratiba za kampeni zenu na kutangaza ilani 24hrs.
Sasa hivi mpo field, mjue Kuna kundi la watanzania huhitaji muda mwindi kushawishika na sera za chama. Lakini pia, CHADEMA inazihitaji media kuliko media zinavyowahitaji, ongeeni na TBC, kaeni meza moja kwani tayari Kuna bajeti kutoka tume ya uchaguzi kwenda TBC kurusha matangazo ya kampeni za UCHAGUZI mwaka huu.
Najua baada ya kuelewana, hawatarudia kukatakata matangazo, lakini pia Ni UKWELI TBC wanaogopa maneno ya kejeli kwa mwajiri wao, just be humble, waambieni mmeanza kueleza ilani yenu, wote tumeisikia wale tunaotumia bando lakini nyumbani kwetu Msalala hawajui hata Jana mlikuwa wapi
Ushauri wa mwisho: Huu si muda wa kutembea wote na mgombea mwenza, sambaeni kila Kona kila mtu kivyake, HERICOPTER ZENU zizunguke maana ndiyo mbadala wa wasanii kwenu. Mageuzi Ni Kazi ngumu, nyie Ni mashihidi. Unamweleza mtu mkiingia madalakani mtawalipa madeni waliotumbuliwa bila kujali stahiki zao, lakini huyo unayemtetea anakuhoji, utatoa wapi hela? Hawa watu wanaitaji ushawishi na elimu ya kila siku ndani ya hii miezi 2.
Nawatakia asubuhi njema, ngoja nikatafute buku ya kula na wanangu. Saivi Hakuna weekend kwa watanzania, maisha Ni magumu
Haya ndio anayosema MHESHIMIWA TUNDU ANDIPAS LISSU
Uhuru
Haki
Kazi
Nadhani tukiacha ushabiki tutaikomboa hii nchi.
Kumbuka mpaka viongozi wa dini wameufyata hasa wale wakuu.