Uchaguzi 2020 CHADEMA, tafuteni television station itakayorusha kampeni zenu mubashara

Popote mlipo, huu Ni ushauri wangu kwenu, mikutano yenu haiwezi kutegemea matangazo ya gari za matangazo na social media, katika pesa mliyonayo, ongeeni na ITV/ AZAM wawe wanarusha matangazo na ratiba za kampeni zenu. Ikishindikana kwa hizo media, basi boresheni CHADEMA TV iwe active LIVE 24 HRS. Iwe inatoa ratiba za kampeni zenu na kutangaza ilani 24hrs.

Sasa hivi mpo field, mjue Kuna kundi la watanzania huhitaji muda mwindi kushawishika na sera za chama. Lakini pia, CHADEMA inazihitaji media kuliko media zinavyowahitaji, ongeeni na TBC, kaeni meza moja kwani tayari Kuna bajeti kutoka tume ya uchaguzi kwenda TBC kurusha matangazo ya kampeni za UCHAGUZI mwaka huu.

Najua baada ya kuelewana, hawatarudia kukatakata matangazo, lakini pia Ni UKWELI TBC wanaogopa maneno ya kejeli kwa mwajiri wao, just be humble, waambieni mmeanza kueleza ilani yenu, wote tumeisikia wale tunaotumia bando lakini nyumbani kwetu Msalala hawajui hata Jana mlikuwa wapi

Ushauri wa mwisho: Huu si muda wa kutembea wote na mgombea mwenza, sambaeni kila Kona kila mtu kivyake, HERICOPTER ZENU zizunguke maana ndiyo mbadala wa wasanii kwenu. Mageuzi Ni Kazi ngumu, nyie Ni mashihidi. Unamweleza mtu mkiingia madalakani mtawalipa madeni waliotumbuliwa bila kujali stahiki zao, lakini huyo unayemtetea anakuhoji, utatoa wapi hela? Hawa watu wanaitaji ushawishi na elimu ya kila siku ndani ya hii miezi 2.

Nawatakia asubuhi njema, ngoja nikatafute buku ya kula na wanangu. Saivi Hakuna weekend kwa watanzania, maisha Ni magumu
Una mpango gani na hivyo vyombo au unataka vifutwe kwenye ramani ya Dunia?.
Haya ndio anayosema MHESHIMIWA TUNDU ANDIPAS LISSU
Uhuru
Haki
Kazi

Nadhani tukiacha ushabiki tutaikomboa hii nchi.
Kumbuka mpaka viongozi wa dini wameufyata hasa wale wakuu.
 
Popote mlipo, huu Ni ushauri wangu kwenu, mikutano yenu haiwezi kutegemea matangazo ya gari za matangazo na social media, katika pesa mliyonayo, ongeeni na ITV/ AZAM wawe wanarusha matangazo na ratiba za kampeni zenu. Ikishindikana kwa hizo media, basi boresheni CHADEMA TV iwe active LIVE 24 HRS. Iwe inatoa ratiba za kampeni zenu na kutangaza ilani 24hrs.

Sasa hivi mpo field, mjue Kuna kundi la watanzania huhitaji muda mwindi kushawishika na sera za chama. Lakini pia, CHADEMA inazihitaji media kuliko media zinavyowahitaji, ongeeni na TBC, kaeni meza moja kwani tayari Kuna bajeti kutoka tume ya uchaguzi kwenda TBC kurusha matangazo ya kampeni za UCHAGUZI mwaka huu.

Najua baada ya kuelewana, hawatarudia kukatakata matangazo, lakini pia Ni UKWELI TBC wanaogopa maneno ya kejeli kwa mwajiri wao, just be humble, waambieni mmeanza kueleza ilani yenu, wote tumeisikia wale tunaotumia bando lakini nyumbani kwetu Msalala hawajui hata Jana mlikuwa wapi

Ushauri wa mwisho: Huu si muda wa kutembea wote na mgombea mwenza, sambaeni kila Kona kila mtu kivyake, HERICOPTER ZENU zizunguke maana ndiyo mbadala wa wasanii kwenu. Mageuzi Ni Kazi ngumu, nyie Ni mashihidi. Unamweleza mtu mkiingia madalakani mtawalipa madeni waliotumbuliwa bila kujali stahiki zao, lakini huyo unayemtetea anakuhoji, utatoa wapi hela? Hawa watu wanaitaji ushawishi na elimu ya kila siku ndani ya hii miezi 2.

Nawatakia asubuhi njema, ngoja nikatafute buku ya kula na wanangu. Saivi Hakuna weekend kwa watanzania, maisha Ni magumu
Mkuu uko nchi hii kweli au unaandika ukiwa China?
 
Naunga mkono hoja bila TV Ni wengi hawatowasikia kabisa na hili na bao Tena kubwa,mfano Mimi tu ilani ndo naiskia leo kwa kuwa siku mbili zote sikua na bando,Sasa Ni waTz wangapi wanna hali kama yangu
 
Chama hakina TV yake wala online TV yake ya kurusha matukio live.

Hivi mnakwama wapi?
Leo nilikuwa nafuatilia online TV kwa uzinduzi wa kampeni za segerea, yaani zimeikata speech ya Lissu nusu. Yaani jamaa anavyozidi kushuka nondo wamekata.

Nahisi kuna mkono mzito unainfluence hata hizi online TV ziwahujumu!

Lakini Sasa Chadema inakosaje plan hadi kutegemea hisani za wengine?

Aisee mna potential ya kufanya vizuri uchaguzi huu lakini kama mnasuasua hivi kwenye media mtapigwa kipigo cha mbwa mwizi!
 
Mbowe angejenga chama kwa ruzuku ya 2015-2020 ingependeza. Walipata wabunge wengi na pesa nyingi za ruzuku. Leo walitakiwa wawe na TV na ofisi nzuri angalau ya HQ. Kweli kutegemea watu ambao wametishwa na Magufuli ndio wawafikishie ujumbe ni kazi bure.
 
Wanafukuza na nakuwatukana wa Wana habari angali hawana vyanzo vyao vya habari.

Kama siyo ujuha unafikiri Nini.

Ngoja waje mkuu, kutukana kwao ndo maisha yao.
 
Huu ushauri ni mzuri sana, na laiti ungeshauri mwaka Jana au mwanzoni mwa mwaka huu ingeleta Tija zaidi. Hata angeitisha mchango wananchi wangemchangia.

Binafsi nahisi Mbowe alishaingiza upepo tangu kipindi kile alipoletewa figisu la kodi ya Billicanas na Mali zake zingine

Kwasasa anaogopa mambo mengi.

Who is CDM think tank?

Where are CDM investors?

What are their priorities?

Where are their strength?
 
Mkuu ni rahisi sana kuwalaum bila kuvaa viatu vyao...
Hapa ITV wana case ya mirath mahakamani haijalish
Hapa tbc inaonesha habar vip and
Hapa clouds imefungwa kabisa for about a week now
Hapa TCRA wanataka "maadili"
Hapa Tanzania Daima lipo banned completely
Hapa Mwananchi x boss ni mgombea ubunge Kawe kwa chadema..
Hapa Police, TRA , Immigration etc wapo kazni..
Hapa wagombea ubunge wanaenguliwa kwa makumi with no solid grounds

Na bado upo top list kwenye election potential. ..
Hakuna game tough kama hii... this is for big boys...
 
Mbowe angejenga chama kwa ruzuku ya 2015-2020 ingependeza. Walipata wabunge wengi na pesa nyingi za ruzuku. Leo walitakiwa wawe na TV na ofisi nzuri angalau ya HQ. Kweli kutegemea watu ambao wametishwa na Magufuli ndio wawafikishie ujumbe ni kazi bure.
Chadema ilikuwa inapata ruzuku kubwa kuliko vyama vyote vya upinzani; wabunge wa kuchaguliwa walikuwa 33 halafu wabunge wa viti maalumu walikuwa 37. Halafu ikawa inchukua michago ya TShs 0.52m kwa mwezi kutoka wa kila mbunge wa kuchaguliwa, na TSh 1.56m kutoka kila mbunge wa viti maalum. Hesabu hiyo ni kuwa kila mwezi CHADEMA ilikuwa inakusany TShs 17.16m kutoka wabunge wa kuchaguliwa na TShs 57.72m kutoka wabunge wa viti maalumu; kwa hiyo mfuko wa chadema ulikuwa unaingiza TSh 74.88m kwa mwezi. Sasa kwa kipindi chote cha miaka mitano ambayo takriban miezi 55 ya bunge, CHADEMA ilikusanya Tsh 4.12b kutokana na michango ya bunge.

Kutokana na idadi ya wabunge wake CHADEMA pia ilikuwa inapata ruzuku ya takriban TSh 330 m kwa mwezi; hivyo kwa uhai wa miezi 55 ya bunge, ilipokea ruzuku ya Tsh 18.15 b. Kwa hiyo ukichanganya na ile michango ya wabunge, CHADEMA iliingiza mapato ya kiasi cha TSh22.3 b katika kipindi cha bunge la 2015-2020.

Lakini CHADEMA mpaka sasa haina network nzuri huko vijijini bali ni kwenye mikoa michache tu, ile effort aliyokuwa amefanya Dr. Slaa kujenga network vijijini aliondoka nayo. Ofisi zao zote ni kama vile siyo za chama kikubwa, yaani hata Ofisi ya makao makuu haiendani kabisa na hadhi ya chama kikuu cha Upinzani Bungeni. Sasa uchaguzi umefika, wanaanza kupigisha michango ya paopo kwa papo kutoka kwa wananchi kama vile hawakuwa wanajua kuwa kuna kampeini. Yaani walipokea billioni 22 lakini kweli hawakutunza hata billion 4 tu za kuendeshea kampeini kwa wastani wa bilioni 2 kwa mwezi?

Sasa hii michango ya harambee wawe makini wasijejikuta wanavunja sheria ya matumizi ya kampeini; wakikosea kuzi-handle wanaweza kujikuta matatani halafu wakalia faulo.
 
Mkuu ni rahisi sana kuwalaum bila kuvaa viatu vyao...
Hapa ITV wana case ya mirath mahakamani haijalish
Hapa tbc inaonesha habar vip and
Hapa clouds imefungwa kabisa for about a week now
Hapa TCRA wanataka "maadili"
Hapa Tanzania Daima lipo banned completely
Hapa Mwananchi x boss ni mgombea ubunge Kawe kwa chadema..
Hapa Police, TRA , Immigration etc wapo kazni..
Hapa wagombea ubunge wanaenguliwa kwa makumi with no solid grounds

Na bado upo top list kwenye election potential. ..
Hakuna game tough kama hii... this is for big boys...
Kukalama haisaidii, tafuta solution kwenye challenge kama hizo, halafu ucjitie kwenye nothing potential.
 
Kuna vikwazo sana sema watu hawajui, kuna figisu za wazi wazi na za chini kwa chini wanazofanyiwa Chadema. Sio rahisi kama watu wanavyowaza
 
Tupa kuleeee....
Kwanini misukule ya lumumba inaogopa uchaguzi?
Wanaogopa au wamewapiga bao? Wameanza kutoa Ilani yao na sasa kila hoja yenu wana mamlaka ya kusema: Tumetekeleza na tutaendeleza utekelezaji mkitupatia
 
CHADEMA hawana lolote ni kundi kubwa la waropokaji na wapigaji! Hawana investments, hawana strategies wala hawana strategists.Kwa kifupi ni watu wa kwenda na UPEPO/ VIMBUNGA.
Watu wa kwenda kwa UPEPO au VIMBUNGA lazima wapigwe kama MAPEPO.
 
Sio tuu hali ni mbaya sana kwa Chadema, wanachama na washabiki walio wengi wameharibikiwa kiasi wamechanganyikiwa na kupoteza muelekeo. Uthibitisho wa hili ni tarehe 29th October-2020. Wanatengeneza mazingira ili waukatae uchaguzi na matokeo.
Waukatae au wasuse hamna anayejali, maana hawana nguvu ya kufanya lolote, hakuna raia anayewaelewa, na waki ingia barabarani wataishia kula virungu tu.
 
Back
Top Bottom