Uchaguzi 2020 CHADEMA, tafuteni television station itakayorusha kampeni zenu mubashara

PAZIA 3

JF-Expert Member
Jan 30, 2018
1,026
2,000
Popote mlipo, huu Ni ushauri wangu kwenu, mikutano yenu haiwezi kutegemea matangazo ya gari za matangazo na social media, katika pesa mliyonayo, ongeeni na ITV/ AZAM wawe wanarusha matangazo na ratiba za kampeni zenu. Ikishindikana kwa hizo media, basi boresheni CHADEMA TV iwe active LIVE 24 HRS. Iwe inatoa ratiba za kampeni zenu na kutangaza ilani 24hrs.

Sasa hivi mpo field, mjue Kuna kundi la watanzania huhitaji muda mwindi kushawishika na sera za chama. Lakini pia, CHADEMA inazihitaji media kuliko media zinavyowahitaji, ongeeni na TBC, kaeni meza moja kwani tayari Kuna bajeti kutoka tume ya uchaguzi kwenda TBC kurusha matangazo ya kampeni za UCHAGUZI mwaka huu.

Najua baada ya kuelewana, hawatarudia kukatakata matangazo, lakini pia Ni UKWELI TBC wanaogopa maneno ya kejeli kwa mwajiri wao, just be humble, waambieni mmeanza kueleza ilani yenu, wote tumeisikia wale tunaotumia bando lakini nyumbani kwetu Msalala hawajui hata Jana mlikuwa wapi

Ushauri wa mwisho: Huu si muda wa kutembea wote na mgombea mwenza, sambaeni kila Kona kila mtu kivyake, HERICOPTER ZENU zizunguke maana ndiyo mbadala wa wasanii kwenu. Mageuzi Ni Kazi ngumu, nyie Ni mashihidi. Unamweleza mtu mkiingia madalakani mtawalipa madeni waliotumbuliwa bila kujali stahiki zao, lakini huyo unayemtetea anakuhoji, utatoa wapi hela? Hawa watu wanaitaji ushawishi na elimu ya kila siku ndani ya hii miezi 2.

Nawatakia asubuhi njema, ngoja nikatafute buku ya kula na wanangu. Saivi Hakuna weekend kwa watanzania, maisha ni magumu.
 
Jile79

JF-Expert Member
May 28, 2009
17,495
2,000
SIKUMBUKI LINI NIMEANGALIA TBC

Na Thadei Ole Mushi.

Kama kuna chombo chenye nguvu ya kupashana habari kwa sasa ni hizi Social Media kama vile Facebook, Twitter, Instagram na nyinginezo nyingi.

Asilimia 95 ya tabaka la wasomi na wafanyabiashara wa kati na wakubwa chombo chao kikubwa kwa sasa ni hizi Social Media.

Redio, TV na Magazeti yanafuata baada ya Social media hizi nilizozitaja. Ndio maana ili magazeti yao yasomeke au vipindi vyao visokilizwe au kutazamwa wanalazimika kufanya matangazo kwenye Social Media.

Chama cha Republicans cha Marekani kilihamasisha wanachama wake kufanya kampeni na kupiga kura za Opinion Poll kwenye mitandao ya kijamii.

Rais Obama kupitia mtandao wake wa Obama Twitter Town Hall hupokea zaidi ya maswal 70,000 kwa siku toka kwa wananchi kipindi akiwa madarakani yaliyomtaka Obama kuyajibu au kutatolea ufafanuzi.

Trump Leo akitaka kufanya jambo anakimbilia account yake ya Twitter anatangaza. Hata wasaidizi wake amekuwa akiwafukuza kupitia Twitter. Wote ambao amewaondoa kazini mwaka huu amewapa tangazo huko huko twitter. Viongozi wote wa marekani wakiamka wanakimbilia Twitter ya Trump

Kenya ukurasa Wa FB wa Rais Kenyata ndio kila kitu. Wakenya wote wakiamka wanakimbilia pale na kusoma.

List ni kubwa sana ya viongozi wakubwa wanavyonufaika na kutoa habari zao kupitia Social media.

Hapa Kwetu Mange Kimambi tunaona anavyotukimbiza kupitia Social Media. Kina Maria Sarungi, Chahali, Kigogo wote Hawa TV lakini wanatukimbiza mchaka mchaka kwenye social media

NATAKA KUSEMA NINI?

Leo kwenye mkutano wa Chadema TBC wameingia kwenye mgogoro kwa kile watu wanachokilalamikia kuwa Walikuwa wakirusha matangazo Ila ikifikia Kiongozi wa Chadema kuhutubia wanakata matangazo na kuanza kuleta uchambuzi.

Siku za nyuma pia Chadema walilalamika kuwa kwamba vyombo vya habari haviwafanyii coverage. Mkurugenzi wa Tume ya taifa ya uchaguzi akawataka vyombo vyote vya habari kutenda haki kipindi hiki Cha kampeni.

Nani anawatumia TBC? Swali Hilo siwezi kulijibu kwa kuwa sijui. Kitu ambacho watu hawajui ni kuwa dunia ilishahama kukaa Mbele ya chogo la tv na kufuatilia habari.

Kwa mwezi ukiniambia Ni Mara ngapi nimeangalia Tv sijui Ila kila siku na kila saa nakamata simu yangu ya mkononi na kuperuzi nini kinaendelea duniani.

Yaani niitegemee TBC kabisa inipe habari? Hapana Kwanza nitaangalia saa ngapi? Simu nipo nayo kila Mahali naweza kufuatilia Jambo nikiwa kazini, safarini hata Chooni.

Tuna mifano.

Nendeni kafuatilieni spring Revolution iliyotokea nchi za kaskazini mwa Afrika. Napunduzi yalianzia Tunisia baada ya Abouaziz kujichoma Moto kupitia tu social media Ben Ali aliitoroka nchi. Baadaye social media ilisambaza napunduzi hayo Misri na kwingineko.

Wanaofikiri kuwa TV na magazeti yanaweza kufanya kazi Sasa anakosea sana. Kwenye kampeni hizi vyama viwekeze kwenye Social Media... Wafanye coverage ya maana kwa vifaa vya kisasa Social media inatosha. Dunia ipo kwenye social Media.... Wekezeni kwa watu smart wanaweza kupush agenda kwenye social media....

Ole Mushi
0712702602.

Ole Mushi.
0712702602
 
brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
7,658
2,000
TV za kutangaza zipo zimefanya hili fursa. Channel ten Ina wenyewe. TBC ni kama mlivyoona.

Kwa vile hawa wanajinadi kuwa ni biashara, biashara haigombi:Vigezo na masharti huzingatiwa.
 
kandamatope

JF-Expert Member
May 19, 2018
541
1,000
Ni kweli social media kwa sasa inanguvu kubwa
Na kama tunakumbuka vizuri ndio iliyowapa ukawa majiji 2015
Tukapata wenyeviti wa halmashauri na mameya katika majiji
lakini ni lazima tumurike kote kote ccm bado wakaendelea kuzoa kura vijijini
Ukienda kule kijijini kwetu kwa babu tale tale mkuyuni, kinole , kiroka , mvua, dutumi, madamu nk,
Bibi na babu zangu pamoja na baba zangu kule kijijini sim zao wanafunga na mipira,
Ukiona kanunua bando la kupiga sim basi kuna mtu kafa:)
Leo uje useme social media ina nguvu kuliko tv
Mm nasema hapana
Vijijini wanaangalia zaid tv na kusikiliza radio
Pesa za kununulia smartphone awana na pesa za kununua bando awana vile vile
Tv na radio
Sasa nani wa kuonyesha mikutano live ya wapinzani iliyojaa kejeli, chuki, uchochezi na uwarakati
Hapo ndio kila mmiliki wa chombo anakula kona Kurusha mikutano ya wapinzani
Nini kifanyike sasa……. Wapinzani wajitasmini na kuanza kufanya siasa badala ya harakati. ..
 
YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
28,113
2,000
Ni kweli social media kwa sasa inanguvu kubwa
Na kama tunakumbuka vizuri ndio iliyowapa ukawa majiji 2015
Tukapata wenyeviti wa halmashauri na mameya katika majiji
2015 Chadema hawakushinda hayo majiji sahabu ya social media sio kweli

Sababu kuu zilikuwa mbili
1.Hayo majiji ndio yenye walutheri wengi .Lowasa mgombea Uraisi Ni Mlutheri alisema Ni zamu ya walutheri ndio ukaona majiji yenye walutheri wengi ya Dar es salaam,Iringa mjini,Mbeya,Arusha,Moshi na manyara yakienda Chadema

2.Ukabila majiji ambayo Chadema ilishika Kuna wachaga wengi na wamasai wa kabila ya Lowasa .Ukabila ukitumiwa Sana
Ukienda kote Iringa mini ako wengi,dar es salaam wako wengi,Arusha wako wengi,Moshi wako wengi na Manyara
Hizi factor mbili ndizo zilikuwa kigezo kikubwa Cha 2015

Kwa Sasa hizo factor hazina nguvu Tena Baada ya Chadema kuweka mgombea Lisu mkatoliki na mnyaturu asiyetoka kabila kubwa la kaskazini ambako Chadema ndio Ina nguvu hivyo kutokubalika kwa wachaga na Masai

Slaa alikubalika na ukatoliki wake sababu mkewe Ni Mlutheri
Chadema interested win ulutheri Kama ingemsimamisha Nyalandu kugombea sababu Ni Mlutheri

Lisu hakubaliki kwenye ukatoliki pamoja na kuwa Ni mkatoliki hewa kwa sababu alibadli jina la ubatizo.Kwa kawaida mkatoliki akibatizwa hupewa jina la mtakatifu mfano Raisi magufuli alipobatizwa alipewa jina la mtakatifu John ndio maana anaitwa John

Lisu alibadili na kulikana jina la mtakatifu alilobatizwa nalo na kujiita Tundu.Kudharau jina la mtakatifu na kujipa jina la kujitungia Ni dharau kubwa kwa mtakatifu husika kuwa unaona jina lake Ni takataka

Ndio maana viongozi kanisa Katoliki wako mbali naye sababu ya hizo dharau kwa mtakatifu anayeheshimiwa na kanisa
Hivyo hakubaliki kwa wakatoliki na kwa walutheri hakubaliki na kwa wachaga na Masai hakubaliki ndio maana hata mikutano yake inadoda
 
kandamatope

JF-Expert Member
May 19, 2018
541
1,000
2015 Chadema hawakushinda hayo majiji sahabu ya social media sio kweli

Sababu kuu zilikuwa mbili
1.Hayo majiji ndio yenye walutheri wengi .Lowasa mgombea Uraisi Ni Mlutheri alisema Ni zamu ya walutheri ndio ukaona majiji yenye walutheri wengi ya Dar es salaam,Iringa mjini,Mbeya,Arusha,Moshi na manyara yakienda Chadema

2.Ukabila majiji ambayo Chadema ilishika Kuna wachaga wengi na wamasai wa kabila ya Lowasa .Ukabila ukitumiwa Sana
Ukienda kote Iringa mini ako wengi,dar es salaam wako wengi,Arusha wako wengi,Moshi wako wengi na Manyara
Hizi factor mbili ndizo zilikuwa kigezo kikubwa Cha 2015

Kwa Sasa hizo factor hazina nguvu Tena Baada ya Chadema kuweka mgombea Lisu mkatoliki na mnyaturu asiyetoka kabila kubwa la kaskazini ambako Chadema ndio Ina nguvu hivyo kutokubalika kwa wachaga na Masai

Slaa alikubalika na ukatoliki wake sababu mkewe Ni Mlutheri
Chadema interested win ulutheri Kama ingemsimamisha Nyalandu kugombea sababu Ni Mlutheri

Lisu akubaliki kwenye ukatoliki pamoja na kuwa Ni mkatoliki hewa kwa sababu alibadli jina la ubatizo.Kwa kawaida mkatoliki akibatizwa hupewa jina la mtakatifu mfano Raisi magufuli alipobatizwa alipewa jina la mtakatifu John ndio maana anaitwa John

Lisu alibadili na kulikana jina la mtakatifu alilobatizwa nalo na kujiita Tundu.Kudharau jina la mtakatifu na kujipa jina la kujitungia Ni dharau kubwa kwa mtakatifu husika kuwa unaona jina lake Ni takataka

Ndio maana viongozi kanisa Katoliki wako mbali naye sababu ya hizo dharau kwa mtakatifu anayeheshimiwa na kanisa
Hivyo hakubaliki kwa wakatoliki na kwa walutheri hakubaliki na kwa wachaga na Masai hakubaliki ndio maana hata mikutano yake inadoda
Naheshimu mchango wako,
Naufanyia kazi
 
Kifaurongo

JF-Expert Member
Jan 18, 2010
3,973
2,000
SIKUMBUKI LINI NIMEANGALIA TBC

Na Thadei Ole Mushi.

Kama kuna chombo chenye nguvu ya kupashana habari kwa sasa ni hizi Social Media kama vile Facebook, Twitter, Instagram na nyinginezo nyingi.

Asilimia 95 ya tabaka la wasomi na wafanyabiashara wa kati na wakubwa chombo chao kikubwa kwa sasa ni hizi Social Media.

Redio, TV na Magazeti yanafuata baada ya Social media hizi nilizozitaja. Ndio maana ili magazeti yao yasomeke au vipindi vyao visokilizwe au kutazamwa wanalazimika kufanya matangazo kwenye Social Media.

Chama cha Republicans cha Marekani kilihamasisha wanachama wake kufanya kampeni na kupiga kura za Opinion Poll kwenye mitandao ya kijamii.

Rais Obama kupitia mtandao wake wa Obama Twitter Town Hall hupokea zaidi ya maswal 70,000 kwa siku toka kwa wananchi kipindi akiwa madarakani yaliyomtaka Obama kuyajibu au kutatolea ufafanuzi.

Trump Leo akitaka kufanya jambo anakimbilia account yake ya Twitter anatangaza. Hata wasaidizi wake amekuwa akiwafukuza kupitia Twitter. Wote ambao amewaondoa kazini mwaka huu amewapa tangazo huko huko twitter. Viongozi wote wa marekani wakiamka wanakimbilia Twitter ya Trump

Kenya ukurasa Wa FB wa Rais Kenyata ndio kila kitu. Wakenya wote wakiamka wanakimbilia pale na kusoma.

List ni kubwa sana ya viongozi wakubwa wanavyonufaika na kutoa habari zao kupitia Social media.

Hapa Kwetu Mange Kimambi tunaona anavyotukimbiza kupitia Social Media. Kina Maria Sarungi, Chahali, Kigogo wote Hawa TV lakini wanatukimbiza mchaka mchaka kwenye social media

NATAKA KUSEMA NINI?

Leo kwenye mkutano wa Chadema TBC wameingia kwenye mgogoro kwa kile watu wanachokilalamikia kuwa Walikuwa wakirusha matangazo Ila ikifikia Kiongozi wa Chadema kuhutubia wanakata matangazo na kuanza kuleta uchambuzi.

Siku za nyuma pia Chadema walilalamika kuwa kwamba vyombo vya habari haviwafanyii coverage. Mkurugenzi wa Tume ya taifa ya uchaguzi akawataka vyombo vyote vya habari kutenda haki kipindi hiki Cha kampeni.

Nani anawatumia TBC? Swali Hilo siwezi kulijibu kwa kuwa sijui. Kitu ambacho watu hawajui ni kuwa dunia ilishahama kukaa Mbele ya chogo la tv na kufuatilia habari.

Kwa mwezi ukiniambia Ni Mara ngapi nimeangalia Tv sijui Ila kila siku na kila saa nakamata simu yangu ya mkononi na kuperuzi nini kinaendelea duniani.

Yaani niitegemee TBC kabisa inipe habari? Hapana Kwanza nitaangalia saa ngapi? Simu nipo nayo kila Mahali naweza kufuatilia Jambo nikiwa kazini, safarini hata Chooni.

Tuna mifano.

Nendeni kafuatilieni spring Revolution iliyotokea nchi za kaskazini mwa Afrika. Napunduzi yalianzia Tunisia baada ya Abouaziz kujichoma Moto kupitia tu social media Ben Ali aliitoroka nchi. Baadaye social media ilisambaza napunduzi hayo Misri na kwingineko.

Wanaofikiri kuwa TV na magazeti yanaweza kufanya kazi Sasa anakosea sana. Kwenye kampeni hizi vyama viwekeze kwenye Social Media... Wafanye coverage ya maana kwa vifaa vya kisasa Social media inatosha. Dunia ipo kwenye social Media.... Wekezeni kwa watu smart wanaweza kupush agenda kwenye social media....

Ole Mushi
0712702602.

Ole Mushi.
0712702602
Sijui tafiti zenu mnafanyiaga wapi. Tanzania ina wapiga kura 28,000,000. Wanaoshinda kwenye social media ni wangapi? Tuangalie mfano wa jana Kawe.
Screenshot_2020-08-30-08-55-04-1.png

Mitandao mingine nayo inaonyesha hali halisi pia.
Screenshot_2020-08-30-08-49-27-1.png
Huwezi linganisha na live ya CCM siku hiyo hiyo ambapo bar zote mijini, majumbani mijini na vijijini, vyombo vya usafiri watu walikua wanafuatilia uzinduzi wa Kampeni. TBC pamoja na kuwa ilikuwa inafanya sensorship, mkutano wa Chadema Mbagala ulionwa nchi nzima sababu watu walikuwa na hamu ya kumsikia Lissu anakuja na sera gani. Chadema hawakutumia nafasi hiyo ya kuwa wa kwanza kuzindua kutangaza ilani. Wangetumia leo hii kila wanachoongea CCM tungewachana kuwa wanaiga ilani ya Chadema tuliyoanza kuisikia. Kwenye mechi hakuna goli tamu kama goli la kuongoza!
 
Nazgur

JF-Expert Member
Apr 19, 2020
2,747
2,000
Tutaona kwa kupitia drone wingi mnaokuwa nao, kisha mtawafukuza.
 
brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
7,658
2,000
Watafungiwa wajinga hawa! Wanafikri li Magu linapenda ujinga?

Hiiiii bagosha. Kwanza kumradhi kushindwa kusomana kwenye yale 'mabusatu'.

Wamesema biashara, tusiwasemee. Acha wakatae wenyewe. Au tuone hiyo jitihada ya kufunga.

Mbona Pemba kimeshaeleweka?
 
ofisa

JF-Expert Member
May 15, 2011
2,776
2,000
CDM Hamjui nguvu ya TV.Nilikuwa na hamu ya kumsikia sera zenu na nilihamasika na TBC kuonyesha live lakini maamuzi tena yamefanyika kumbe hamna bajeti ya TV mbadala.kwa sisi ambao hatujalipia ving'amuzi tunaipata TBC.
Ila lile jukwaa ni dhahiri kwamba mnaukata wa fedha.
 
technically

JF-Expert Member
Jul 3, 2016
10,099
2,000
Naunga mkono hoja hata ikiwa TV ya Kenya tutachangia ili mradi iwe kwenye vingamuzi vya ndani..

Mfano Citizen, Ktn hata k24
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom