CHADEMA anzisheni kituo cha television kabla ya uchaguzi wa 2025

Magufuli 05

JF-Expert Member
May 7, 2023
942
1,988
Kwa kuwa kumekuwa na kilio cha muda mrefu kwamba CHADEMA imekuwa ikihujumiwa na media nyakati zote hasa katika mikutano ya hadhara. Kwamba mikutano huwa haionyeshwi kwasababu ya maelekezo kutoka juu.

Mimi nawakumbusha tu kwa vile najua hata nyinyi mwalijua hili kwamba kuwa na channel yenu ya television kilio hiki kitapungua makali yake.

Ukweli ni kwamba UCHAGUZI ujao wananchi wanahamu Sana na nyinyi na njia mojawapo ya kuwafikia kwa urahisi ni kuhakikisha mnaonekana katika mikutano yenu ya hadhara.

Nawaomba muda ni sasa na si kesho kwani kesho mtakuwa mmechelewa. Hakuna ubishi UCHAGUZI ujao utakuwa na ushindani mkali na Wa tija kulingana na Hali inayopitia nchi kwasasa.

Nimewaandikia Chadema Uzi huu kwasababu katika vyama shindani vilivyopo nawaona nyinyi ndiyo chama pekee chenye mwelekeo na nia njema kwa Taifa.

Nimewaangalia katika maeneo yafuatayo:
1. Coverage. Mpo vizuri
2. Leadership structure. Mpo vizuri.
3. Propaganda. Mpo vizuri.
4. Party cohesiveness.mpo vizuri
5. Inspiration. Mpo vizuri
6. Direction. Mpo vizuri
7. Agenda setting. Mpo vizuri.
8. Political man ouvre .mpo vizuri.

Fanyieni kazi mambo haya.
1. Kabla ya kumpa mtu mic hakikisheni anatembea kwenye content zenu za chama.

2. Kama kuna tofauti kati yenu na makundi mengine kama sauti ya Watanzania msiweke hadharani tofauti hizo. Mnawapa nguvu washindani wenu Sana. Kama kuna wakati Chadema mnahitaji umoja basi ni wakati huu.

3. Kuna wakati Watanzania Wana waamini Sana lakini mnajichanganya wenyewe kwa kumshambulia Magufuli. Chadema hapa mnafeli. Magufuli yupo kwenye mioyo ya Watanzania kama Rais mzalendo. Magufuli hayupo Tena Duniani, acheni kumzungumza kwa mabaya yake kwani hamtashindana naye Tena popote.

Tumieni fursa yake ya kupendwa kutengeneza chama. Hapa msibwatuke tafadhali ni lazima mjue hasa politics is the game of Dynamics. 2025 mkitumia vizuri fursa ya Magufuli nawaona white house.
Over.

Tanzania kwanza, chama baadae
 
,"Nimewaangalia katika maeneo yafuatayo:
1. Coverage. Mpo vizuri
2.leadership structure. Mpo vizuri.
3. Propaganda. Mpo vizuri.
4. Party cohesiveness.mpo vizuri
5. Inspiration. Mpo vizuri
6. Direction. Mpo vizuri
7. Agenda setting. Mpo vizuri.
8. Political man ouvre .mpo vizuri" - Nukuu

Kwa kuwa kumekuwa na kilio cha muda mrefu kwamba Chadema imekuwa ikihujumiwa na media nyakati zote hasa katika mikutano ya hadhara. Kwamba mikutano huwa haionyeshwi kwasababu ya maelekezo kutoka juu.

Absolutely right.
 
Hawatapewa kibali cha kuanzisha hiyo TV wala redio.Ijue Tanzania,mkuu.
 
Wanalifahamu Ila wamekuwa wakilipuuza kwa muda mrefu, sa sijui Kama wameamka usingizini.
 
Not bad idea nzuri, but kama uonavyo chama hiki hakina wazo la kuanzisha kitu cha kudumu hata ofisi ni kizingumkuti
 
Watu msijitoe ufahamu.

Tatizo siyo CHADEMA kutokuwa na Tv au redio Bali Tanzania hatuna vyombo huru vya habari na wamiliki wake ni waoga kupindukia.

Vyombo vya habari Tanzania vimejawa watu aina ya kina Pascal Mayalla ambao wakiitwa Dodoma kesho yake wanageuka CHAWA.
 
Not bad idea nzuri, but kama uonavyo chama hiki hakina wazo la kuanzisha kitu cha kudumu hata ofisi ni kizingumkuti
Ile ofisi ya Mikocheni ni yako??

Hao CCM wenye ofisi Kila Kona wanafanya nini kuboresha maisha yetu watanzania!!??
 
Ile ofisi ya Mikocheni ni yako??

Hao CCM wenye ofisi Kila Kona wanafanya nini kuboresha maisha yetu watanzania!!??
Don’t take it personal mkuu, ile haina hadhi ya ofc ya chama tunachotegemea kushika hatamu ukiachilia pesa zote za msajili ziliendaga ama zinaenda wp??
Hizo ni public funds mkuu tunataka tuone vitu
 
Ile ofisi ya Mikocheni ni yako??

Hao CCM wenye ofisi Kila Kona wanafanya nini kuboresha maisha yetu watanzania!!??
Chama cha Mapinduzi kimefanyia mengi nchi hii ikiwemo kuweka mazingira mazuri ya biashara yako ya “grains, pulses and oilseeds” usingekuwa hapa ulipo mkuu
 
Chama cha Mapinduzi kimefanyia mengi nchi hii ikiwemo kuweka mazingira mazuri ya biashara yako ya “grains, pulses and oilseeds” usingekuwa hapa ulipo mkuu
Viingereza vya nini Sasa. Au Kuna kitu unaficha kwa sie maamuma wa hiyo Lugha??
 
Kwa kuwa kumekuwa na kilio cha muda mrefu kwamba Chadema imekuwa ikihujumiwa na media nyakati zote hasa katika mikutano ya hadhara. Kwamba mikutano huwa haionyeshwi kwasababu ya maelekezo kutoka juu.
Good idea, tatizo la Chadema Bado ni Chama Cha watu kutafuta maisha aka kunjunga. Ni muda mrefu wangekuwa na Ofisi kubwa hata ghorofa 5, na TV yao ingekuwa pale pale. Wanatakiwa kubadilika na kujitathimini sana. Otherwise wako vizuri wakibadilika kwa maana ya kukijenga Chama kama Taasisi siyo Cha mtu au kikundi fulani. CCM imerudi kwenye Chama çha watu fulani, anguko linakuja kubwa......
 
Safi, hii aione Allen Kilewella
 
Back
Top Bottom