CHADEMA Special Thread

CHADEMA Special Thread

‼️MPANGO WA JESHI LA POLISI DHIDI YA CHADEMA‼️

Kama mtakumbuka siku kadhaa zilizopita ilisambaa taarifa kuhusu Jeshi la Polisi kuvamia nyumbani kwa Yoramu Mbyela (Huyu kwenye picha) ambae ni mfanyabiashara anaeuza vifaa vya CHADEMA ikiwemo matisheti, bendera, madera, kombati, n.k

Siku kadhaa zilizopita Polisi wakiwa na gari aina ya FUSO walivamia nyumbani kwa Mbyela, wakamlazimisha mke wa Mbyela afungue mlango wa duka, kisha wakaingia dukani, wakabeba na kuondoka na mzigo wote wa vifaa vya CHADEMA ambao waliukuta dukani kwake.

Mke wa Mbyela pamoja na Wakili wake wamefuatilia huo mzigo wa sare za CHADEMA, Polisi wakarudisha baadhi ya vitu lakin mzigo mkubwa wakakataa kurudisha mpaka leo bado wamebaki nao.

Sasa nimejulishwa kwamba Jeshi la Polisi wamebaki na huo mzigo wa sare za CHADEMA kwasababu wanampango wa kuutumia kufanikisha mpango wao OVU dhidi ya CHADEMA, hii ni kutokana na hofu waliyonayo kuhusu Maandamano ya 7/7 yani Julai 7, 2026.

Wamepanga kuwapeleka porini watu wao ambao ni Green guard (UVCCM) na baadhi ya mgambo kisha watawavalisha nguo za CHADEMA badae Polisi watasema kwamba wamevamia eneo hilo la pori baada ya kupata taarifa kiintelijensia, Polisi watautangazia umma kwamba Vijana wa CHADEMA wamekamatwa huko porini wakiwa wanapewa mafunzo ya kijeshi kwa ajili ya kujiandaa na Maandamano ya Julai 7, 2026 lengo la kufanya ivo ni kutisha watu ili waogope.

Lakin pia Jeshi hilo limepanga kwamba litakuwa linawavalisha UVCCM izo nguo za CHADEMA kisha wanawatuma kwenye mikutano ya hadhara ya CHADEMA kufanya fujo ili ionekane CHADEMA wanagombana wao kwa wao.

Sasa ni muhimu sana Wanachama wenzangu mnapoenda kwenda Mikutano, hakikisha unamtambua mtu ambae umekaaa nae jirani ukiona kuna mtu/watu huwaelewi toa taarifa kwa Viongozi wa CHAMA, hawa wahuni wakivamia mikutano yetu inatakiwa muwape HAKI YAO YA KIKATIBA.
1781067468034.jpg
 
Mweka Hazina wa CHADEMA Jimbo la Iringa Mjini, Rose Chumi, amewataka wanachama na wapenzi wa chama hicho kuchangia kwa hiari ili kufanikisha maandalizi ya mkutano mkubwa wa chama unaotarajiwa kufanyika Mwembetogwa mkoani Iringa.

Akizungumza katika kipindi cha Nyambizi, Chumi amesema chama kinahitaji shilingi milioni 8.7 kwa ajili ya kugharamia shughuli mbalimbali za maandalizi, ikiwemo matangazo, muziki na jukwaa litakalotumika siku ya mkutano.

Amesema CHADEMA haitumii usafiri wa kulazimisha watu kuhudhuria mikutano, bali hutegemea wananchi kujitokeza kwa hiari baada ya kupata taarifa kupitia kampeni za uhamasishaji zitakazofanyika katika kata zote 18 za Jimbo la Iringa Mjini.

Aidha, amewahimiza wanachama na wadau wa CHADEMA kuchangia kiasi chochote walicho nacho kupitia namba 0745 477 788 jina CHADEMA Jimbo la Iringa mjini, ambapo fedha hizo zitaelekezwa katika kufanikisha maandalizi ya mkutano huo.

Cc: @dadtwinny @azoryorema5

📽️💻@crgenius_tz

#nurufm
#nurufmhabari
#nurudigital
1781069274707.jpg
 
Mungu ibariki CHADEMA
Mungu mbariki Tundu Lissu
Mungu ibariki Tanganyika


#MuunganoNaZanzibarUvunjiketuNiMizigoKwaTanganyikaYetu
 
Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimekanusha vikali madai ya Jeshi la Polisi kuwa kimeandaa vikundi vya kufanya vurugu, kikitaja hatua hiyo kama propaganda iliyopikwa ili kuhalalisha matumizi ya nguvu za kijeshi dhidi ya raia.

Kupitia tamko rasmi lililotolewa leo Juni 10, 2026 na Mkurugenzi wake wa Mawasiliano na Uenezi, Brenda Rupia, chama hicho kimesema kina taarifa za kiintelijensia kuwa polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam wamepewa amri ya kumiminika kwa wingi Mahakama ya Rufaa wakiwa na silaha nzito.

Hatua hiyo inakuja saa chache kabla ya kuanza kunguruma kwa kesi ya Mwenyekiti wa chama hicho, Tundu Lissu, inayotarajiwa kusikilizwa kesho Alhamisi, Juni 11, 2026, kuanzia saa tatu asubuhi.

"Chama kinapenda kuchukua fursa hii kukanusha taarifa hizo za uongo zilizopikwa ili kuwatisha wanachama na Watanzania wanaokusudia kuja mahakamani, wapate hofu ya kujitokeza," amesema Rupia katika tamko hilo.

Chadema kimeonya kuwa polisi wasitengeneze visingizio vya kutimiza nia ovu, huku kikikumbushia tukio la Aprili 2025 katika Mahakama ya Kisutu, ambapo kilidai kuwa viongozi na wafuasi wake walipigwa, kuteswa na kutupwa msituni na askari wakati wa usikilizwaji wa kesi ya uhaini ya Lissu.

Pamoja na tishio hilo la kiusalama, chama hicho kimeshikilia msimamo wake wa amani na kuwasihi wafuasi wote kujitokeza kwa wingi na kwa utulivu mkubwa kushuhudia shauri hilo la kihistoria.
1781088935398.jpg
 
Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam, imetoa wito wa kisheria kwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) pamoja na Wadhamini Waliosajiliwa wa chama hicho, kuwataka kuwasilisha utetezi wao wa maandishi kufuatia kesi ya madai namba 13832 ya mwaka 2026 iliyofunguliwa dhidi yao.

Kesi hiyo imefunguliwa na walalamikaji wawili, Said Issa Mohammed na Ahmed Rashid Khamis kwa madai ya chama kusimamishwa kuendesha shughuli za kisiasa au kufutwa kabisa. Kupitia hati hiyo iliyotolewa rasmi tarehe 9 Juni 2026, upande wa utetezi (CHADEMA) unapewa muda wa siku ishirini na moja (21) tangu kupokelewa kwa wito huo kuwasilisha maelezo ya utetezi wao, ambapo isipofanya hivyo, mahakama inaweza kutoa uamuzi dhidi yao.

Mbali na agizo hilo la utetezi, mahakama imepanga shauri hilo kutajwa kwa mara ya kwanza mbele ya Mheshimiwa Jaji A. Mbagwa mnamo tarehe 15 Juni 2026, saa tatu kamili asubuhi (9:00\text{ AM}). Nyaraka hizo zinaonyesha tayari zimepokelewa na Ofisi ya Katibu Mkuu wa CHADEMA Makao Makuu jijini Dar es Salaam.
1781224541646.jpg
 
Kuelekea Mkutano wa Hadhara wa kesho, tarehe 13 Juni 2026, utakaofanyika Iringa Mjini katika Uwanja wa Mwembetogwa, ambapo Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara, Mhe. John Heche , atakuwa Mgeni Rasmi, leo tarehe 12 Juni 2026 amewasili mkoani Iringa na kuanza ziara yake ya kazi.

Mara baada ya kuwasili, Mhe. Heche alishiriki zoezi la kupandisha bendera za Chama katika Kata ya Kihesa, ikiwa ni sehemu ya kuendelea kuimarisha uhai na shughuli za chama ngazi za msingi.

Aidha, katika Kata ya Kihesa, amezindua Jiwe la Msingi la Tawi la Semutema A na amechangia kiasi cha shilingi 1,000,000 kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa Ofisi ya Kata ya Kihesa, akionesha dhamira ya kuimarisha miundombinu ya chama.

Wanachama, wapenzi, wafuasi na wananchi wote mnakaribishwa kujitokeza kwa wingi katika Mkutano wa Hadhara utakaofanyika kesho, tarehe 13 Juni 2026, katika Uwanja wa Mwembetogwa, Iringa Mjini.
1781310851115.jpg
1781310855114.jpg
1781310860238.jpg
1781310866335.jpg
 
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA bara , John Heche amewasili Mkoani Iringa leo 12 Juni 2026 Kwa ajili ya kufanya ziara na kuhutubia wanachama na wakazi wa Iringa.

Heche amewasili na kupokelewa na wanachama wa Chadema Jimbo la Iringa Mjini ambapo Leo atazindua matawi mawili ya Chadema katika Eneo la Semtema na Mafifi huku akitarajiwa kufanya Mkutano wa hadhara kesho kuanzia saa 6 mchana katika Uwanja wa Mwembetogwa.

#KatibaMpya #FreeTunduLissu #TUTAKUWEPO
1781312906875.jpg
1781312911281.jpg
1781312914766.jpg
1781312918137.jpg
 
Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara, John Heche , ameagwa kwa shangwe na mamia ya wananchi, wanachama na wafuasi wa chama hicho mjini Iringa baada ya kukamilisha ziara yake ya kisiasa iliyohusisha mkutano mkubwa wa hadhara katika Viwanja vya Mwembetogwa.

Wananchi waliojitokeza katika shughuli za kumuaga walionekana wakiwa na furaha, wakimshangilia kwa Peoples Power wakionesha kuunga mkono ujumbe alioutoa wakati wa mkutano huo.

Ziara ya Heche mkoani Iringa ilivutia idadi kubwa ya wananchi na viongozi wa CHADEMA kutoka maeneo mbalimbali ya mkoa huo, ambapo masuala ya demokrasia, maendeleo na mustakabali wa taifa yalikuwa sehemu ya ajenda zilizojadiliwa.

Miongoni mwa matukio yaliyovutia wengi katika ziara hiyo ni ushiriki wa aliyekuwa Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa, ambaye hivi karibuni alirejea rasmi ndani ya CHADEMA.

Wanachama wa chama hicho walisema ujio wa Heche pamoja na kurejea kwa Msigwa umeongeza hamasa mpya ndani ya chama mkoani Iringa.
 
Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara, John Heche , ameagwa kwa shangwe na mamia ya wananchi, wanachama na wafuasi wa chama hicho mjini Iringa baada ya kukamilisha ziara yake ya kisiasa iliyohusisha mkutano mkubwa wa hadhara katika Viwanja vya Mwembetogwa.

Wananchi waliojitokeza katika shughuli za kumuaga walionekana wakiwa na furaha, wakimshangilia kwa Peoples Power wakionesha kuunga mkono ujumbe alioutoa wakati wa mkutano huo.

Ziara ya Heche mkoani Iringa ilivutia idadi kubwa ya wananchi na viongozi wa CHADEMA kutoka maeneo mbalimbali ya mkoa huo, ambapo masuala ya demokrasia, maendeleo na mustakabali wa taifa yalikuwa sehemu ya ajenda zilizojadiliwa.

Miongoni mwa matukio yaliyovutia wengi katika ziara hiyo ni ushiriki wa aliyekuwa Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa, ambaye hivi karibuni alirejea rasmi ndani ya CHADEMA.

Wanachama wa chama hicho walisema ujio wa Heche pamoja na kurejea kwa Msigwa umeongeza hamasa mpya ndani ya chama mkoani Iringa.


View: https://www.facebook.com/share/v/1ECPS6f6KC/
 
John Mnyika aisimamisha kibaha Leo,13/6/26
Ahsanteni Kwa Kuja wangu, Niliona na Kusikia Shauku yenu, i love you my People, here we are✌🏽💪🏽🙏🏽🔥
#FreeTunduLissu #KatibaMpy
1781374439122.jpg
a
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom