CHADEMA Special Thread

CHADEMA Special Thread

Tazama Picha zikionyesha Msaidizi wa TUNDU LISSU akiwa ameumizwa vibaya na watekaji usiku wa kuamkia leo.

David Djumbe alitekwa siku ya Jana Maeneo ya Bunju akiwa na rafiki yake wakati wa kutekwa alipiga kelele sana bodaboda wakafukuzia GARI kwa nyuma

Walipofika umbali wa kilometa kama 3 watekaji walipoona bodaboda bado wanafuatilia GARI, watekaji walishuka na kuanza kupiga RISASI wakati huo Djumbe wakiwa wamemuacha ndani ya GARI.

Ndio David Djumbe akapata upenyo na kukimbia akiwa na Pingu mkononi na ameporwa damu kama anavyoonekana.
.
1779358102425.jpg
 
Jeshi la Polisi Oysterbay limemfungua pingu David Jumbe, ambazo zilikuwa zimembana kisiasi cha kusababisha mikono kuvimba.

Djumbe alitekwa usiku wa kuamkia leo akafanikiwa kuwakimbia watekaji.

Maumivu haya Mpaka lini, sasa Djumbe apelekewe hospitalini.
Imeandikwa na Twaha Mwaipaya
1779358778339.jpg
1779358775743.jpg
1779358772120.jpg
 
Katibu Mkuu wa CHADEMA Mhe. JOHN MNYIKA ameongoza zoezi la upandishaji wa bendera katika vizimba mbalimbali Arusha Mjini. Zoezi hilo limefanyika leo tarehe 22 Mei 2026 ambapo hapo baadae mchana Chama kinatarijia kufanya uzinduzi wa Operesheni #KatibaMpya #FreeLissu Kanda ya Kaskazini.
1779477738758.jpg
1779477735586.jpg
1779477738758.jpg
 
Wasogezeni wabunge wa mchongo haya mdo masharti ya kuondolewa vikwazo 👇🏾

“(b) UTHIBITISHO.—Marufuku chini ya kifungu kidogo cha (a) itaisha kuanzia tarehe ambayo ni siku 30 baada ya tarehe ambayo waziri wa mambo ya nje atawasilisha kwa kamati zinazofaa za Bunge uthibitisho wa maandishi kwamba Serikali ya Tanzania ime—
(1) tekeleza mabadiliko ya uchaguzi ili kuendeleza uchaguzi huru, wa haki, na wa uwazi;
(2) kusitisha kesi za jinai zenye motisha ya kisiasa au zisizo halali, kusahihisha hukumu za kimahakama zenye dosari au zisizofaa,na kuwaachilia viongozi wa upinzani na watu wengine waliokamatwa kwa misingi ya kisiasa;
(3) kuchukua hatua zinazoonekana kuwawajibisha maafisa wa serikali, wanajeshi wa usalama, na wafanyakazi wa kutekeleza sheria kwa utekaji nyara wa kisiasa, vurugu za uchaguzi, na vitendo vinavyodhoofisha taasisi za kidemokrasia; na
(4) kusitisha vitisho vya kisiasa na udhibiti wa watu mashuhuri katika vyombo vya habari, waandishi wa habari, na watendaji wa asasi za kiraia.”

Hiyo namba (4) mmeielewa? Acheni kututisha na kutuwinda! Maridhiano feki na wanasiasa njaa haitawasaidia! Mtuhehsimu na wajibikeni!
 
MAHAKAMA YA RUFAA KUSIKIKIZA KESI DHIDI YA MHE. LISSU, June 11,2026:

Mahakama ya Rufaa itasikiliza maombi ya Mkurugenzi wa mashitaka nchini dhidi ya Mwenyekiti wa Chama Taifa, Mhe Tundu Antipas Lissu Alhamisi ya tarehe 11 June, 2026.

Haya ni yale maombi ya Jamhuri ambayo waliyapeleka baada ya Mahakama kuu kukubali pingamizi la Mhe Lissu dhidi ya maombi ya Serikali kuraka kuongeza maelezo ya nyongeza ya shahidi.

Jopo la Majaji 3 wa Mahakama ya Rufaa wamepangwa ambao ni, Mhe Mwalija, Mhe Jaji Muruke na Mhe Jaji Khamisi.

Hakikisha ujumbe huu umewafikia kwa wingi marafiki wa Demokrasia na Haki.

Gaston Shundo Garubindi
Mkurungenzi wa Sheria wa CHADEMA HQ
 
ANAANDIKA MH BONIFACE MWABUKUSI RAIS TLS

HII NI HATARI.

Nimepokea taarifa asubuhi hii kwa njia ya Simu kwamba ya Jeshi la Polisi Mkoa wa Dar es Salaam kuvamia makazi ya muuzaji na msambazaji wa vifaa vya uenezi vya CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO ( CHADEMA) na kwamba baada ya kumkosa mhusika wamemkamata Mke wake na vilevile wamesomba vifaa vya uenezi na kuondoka navyo.

Je hapa Naibu Msajili anasemaje? hii ndiyo siasa safi?

BAK Mwabukusi

Ujumbe huo ni huu hapa?

Muuzaji na Msambazaji (Mzabuni) wa vifaa vya uenezi vya CHADEMA Bw.Mbyela amevamiwa na jeshi la polisi katika makazi yake Mburahati usiku wa kuamkia leo.

Pamoja na jeshi la polisi kumkosa muhusika,wamemkamata mke wa Mbyela na kuondoka na mzigo wote wa vifaa vya uenezi vya CHADEMA.

Polisi wameshuhudiwa na majirani asubuhi hii wakipakia katika lori la polisi vifaa vyote vya uenezi vya CHADEMA vikiwemo bendera zote,Tshirts,kofia,skafu,madera,Kombati,key holders,kanga,viremba,na vikoi vyenye nembo na rangi za CHADEMA.

HUJUMA:
Maana yake jeshi la polisi litakuwa limefanikiwa Kuihujumu CHADEMA hawa wakati huu wa mikutano kwa kuzuia nchi nzima wanachama na viongozi wa CHADEMA wasipate vifaa vya uenezi vya chama chao kwa kushikikia mzigo huo kwa muda usiojilikana.
1780216326559.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom