CHADEMA Special Thread

CHADEMA Special Thread

JESHI LA POLISI LIMEVAMIA NYUMBANI KWA MBYELLA (ANAYEUZA NGUO NA VIFAA VYA CHADEMA NA KUONDOKA NA TSHIRT, KOFIA, NGUO NA BENDERA ZA CHADEMA.

Nimepata taarifa kwamba usiku wa kuamkia leo mida ya saa nane, Jeshi la Polisi limevamia nyumbani kwa Yoromu Mbyella, mfanyabiashaa ambae huwa anauza sare za CHADEMA wakidai wanamtafuta kwa kosa la kutengeneza Tshirt zenye maandishi “FREE TUNDU LISSU”

Kwa mujibu wa mtoa taarifa, Mbyella mwenyewe hakuwepo nyumbani so Polisi walifanya upekuzi na baada ya kumkosa waliondoka kwa muda.

Baadaye walirejea wakiwa na Gari aina ya Fuso kisha wakabeba nguo zote na vifaa vyenye nembo ya chadema ikiwemo Bendera za Chadema ambazo huwa anauza kisha wakaondoka na mali hizo bila kutoa sababu zaidi.

Kwa mujibu wa mke wa Mbyella (anayeuza nguo na vifaa vya chama) nyumbani kwao kuna duka la kuuza vifaa hivyo ambavyo Polisi wameondoka navyo vyote.

Tunafuatilia kufahamu sababu hasa ya kuvamia nyumbani hapo na kuleta taharuki kwa mtu ambaye hata kama wangemhitaji Polisi, wangempatia wito na angefika kituoni kama Polisi walikuwa na jambo na Mbyella.

Kuuza vifaa vya chama kama nguo, kofia, Bendera siyo kosa kisheria.
1780222898591.jpg
 
Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara, Mhe. John Heche, pamoja na Katibu Mkuu wa Chama, Mhe. John Mnyika, leo tarehe 4 Juni 2026 wamewasili Pemba, Zanzibar, kwa ziara ya kikazi ya siku tatu itakayofanyika kuanzia tarehe 5 hadi 7 Juni 2026.

Viongozi hao wamepokelewa na Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Zanzibar, Mhe. Said Mzee Said, Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA Zanzibar, Mhe. Ali Ibrahim Juma, pamoja na viongozi wa Kanda ya Pemba wakiongozwa na Mwenyekiti wa Kanda hiyo, Mhe. Omar Nassor.

Ziara hiyo ni sehemu ya shughuli za chama za kuimarisha uhai wa chama, kuzungumza na wanachama na viongozi, pamoja na kujadili masuala mbalimbali ya kisiasa Zanzibar.
1780600508357.jpg
 
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kanda ya Pemba kimeutaarifu umma kuwa kimemvua uanachama Ndugu Said Issa Mohammed kufuatia makosa ya kinidhamu. Uamuzi huo umefikiwa katika kikao cha dharura cha Kamati Tendaji ya Kanda kilichofanyika Juni 06, 2026 katika Ukumbi wa Pride ya Zamani, Chake Chake, Pemba, chini ya uongozi wa Mwenyekiti wa Kanda, Mheshimiwa Omar Nassor, kwa kuzingatia Katiba, Kanuni na taratibu za chama.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, kikao kilijadili suala la nidhamu dhidi ya mwanachama huyo na kufanya tathmini kabla ya kubaini kuwa amekiuka masharti ya chama, hali iliyosababisha hatua ya kumfukuza uanachama. Kutokana na uamuzi huo, chama hicho kimesema kuwa kuanzia tarehe hiyo Said Issa Mohammed hatambuliki tena kama mwanachama, kiongozi au mwakilishi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo katika ngazi yoyote.

Aidha, CHADEMA imesisitiza kuwa kauli au matendo yoyote atakayofanya baada ya kufukuzwa yatakuwa ya binafsi na hayatahusishwa na chama hicho
1780835617941.jpg
 
Leo, tarehe 07 Juni 2026, Kamati Maalum ya CHADEMA Zanzibar imeketi katika kikao chake kilichofanyika Kisiwani Pemba. Kikao hicho kimeongozwa na Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Zanzibar, Mhe. Said Mzee Said, na kuhudhuriwa na Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara, Mhe. John Heche, pamoja na Katibu Mkuu wa CHADEMA, Mhe. John Mnyika.

Kikao hicho kinajikita katika kujadili hali ya siasa ya Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa ujumla, kwa lengo la kufanya tathmini ya mwenendo wa kisiasa na kuweka mwelekeo wa hatua za chama katika kipindi kijacho.

Aidha, kikao hicho kinajadili na kupitisha Mpango Mkakati wa CHADEMA Zanzibar wa miaka mitano, utakaokuwa mwongozo wa utekelezaji wa shughuli, sera na vipaumbele vya chama kwa kipindi husika.
1780838796112.jpg
1780838793504.jpg
1780838790753.jpg
 
Baada ya kuhitimisha kikao cha Kamati Maalum ya CHADEMA Zanzibar leo Jumapili Juni 07, 2026, Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Zanzibar, Mhe. Said Mzee Said, akiongozana na Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara, Mhe. John Heche , pamoja na Katibu Mkuu, Mhe. John Mnyika wametembelea kaburi la Hayati Maalim Seif Sharif Hamad lililopo Mtambwe, Mkoa wa Kaskazini Pemba, Kisiwani Pemba.

Viongozi hao walipata fursa ya kuweka heshima zao na kuungana katika dua maalum kumuombea marehemu, wakitambua mchango wake mkubwa katika harakati za ujenzi wa demokrasia, na maendeleo ya siasa Zanzibar na Tanzania kwa ujumla.
1780855717393.jpg
1780855714408.jpg
1780855710637.jpg
1780855706987.jpg
 
HABARI PICHA

Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Pwani na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA Taifa, Boniface Jacob (Bon Yai), akizungumza na wananchi wa Kyela Mjini mkoani Mbeya wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika leo Juni 7, 2026.

Mkutano huo ni sehemu ya ziara ya viongozi wa chama hicho ya kukutana na wananchi, kusikiliza kero zao na kuwasilisha msimamo wa CHADEMA kuhusu masuala mbalimbali ya kisiasa na maendeleo ya taifa.
1780859941805.jpg
1780859938632.jpg
1780859935214.jpg
 
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom