CHADEMA Special Thread

CHADEMA Special Thread

Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara, John Heche, amehoji sababu za kuahirishwa kwa kesi inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Tundu Lissu, akitaka uwazi zaidi kuhusu mwenendo wa shauri hilo.

Akihutubia mamia ya wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika Viwanja vya Mwembetogwa June 13, 2026mkoani Iringa, Heche amesema kuna maswali ambayo yanahitaji majibu kuhusu hatua za kuahirishwa kwa kesi hiyo.

"Mnaficha nini?" amehoji Heche mbele ya umati wa wananchi waliohudhuria mkutano huo.

Kiongozi huyo wa CHADEMA pia amezungumzia suala la amani na usalama nchini, akisisitiza kuwa jukumu la kulinda amani ni la wananchi wote na si la vyombo vya usalama pekee.

"Polisi hawawezi kulinda amani peke yao, amani inalindwa na raia," amesema.

Heche ameeleza kuwa baadhi ya viongozi na wanachama wa chama hicho wameamua kuendelea kusimamia wanachokiamini kuwa ni haki zao za kikatiba bila kuongozwa na hofu.

"Sisi wengine tumekataa kuogopa, hatutakubali," amesema huku akishangiliwa na wananchi waliohudhuria mkutano huo.

Kauli hizo zimetolewa wakati CHADEMA ikiendelea na kampeni zake za kisiasa na mikutano ya hadhara katika maeneo mbalimbali nchini, ambapo viongozi wake wamekuwa wakizungumzia masuala ya demokrasia, haki za kiraia na utawala wa sheria.
 
WEZESHA Maandalizi ya Mikutano ya Kanda ya Kusini.
Sasa ni Zamu ya #NguvuYaKusini
1781541624951.jpg
 
WITO WA JESHI LA POLISI KWA MWENYEKITI WA CHADEMA KANDA YA PWANI, MH. BONIFACE JACOB

CHADEMA Kanda ya Pwani inapenda kuujulisha umma kuwa Mwenyekiti wa Kanda ya Pwani, Mh. Boniface Jacob amepokea wito wa Kufika ofisi za RCO, Mkoa wa Kipolisi Kinondoni siku ya Kesho Jumanne Juni 16,2025.

Kwa mujibu wa taarifa tulizopokea kutoka kwa Mwenyekiti wa Kanda akiwa safarini kuelekea Ifakara Morogoro kwa ajili ya kushiriki mialiko ya mikutano ya hadhara ya CHADEMA Kanda ya Kati (Mkoa wa Morogoro) ameeleza kuwa amepokea simu kutoka Jeshi la Polisi Kimara (W).

Katika mazungumzo hayo, amearifiwa kuwa Polisi Wilaya ya Kimara wamepokea maelekezo rasmi yanayomtaka kufika katika Ofisi za RCO, Mkoa wa Kipolisi Kinondoni ,Dar es Salaam siku ya kesho Jumanne, tarehe 16 Juni 2026.

Jeshi la Polisi limemtaka kuwa anapofika katika ofisi hizo, aongozane na Mawakili wake au watu wake wa karibu.

Kufuatia wito huo, ninatoa rai na kuwaomba Mawakili wetu, Viongozi wote wa Chama (CHADEMA), Wanachama na Wapenda Haki wote kuungana pamoja na Mwenyekiti wa Kanda kuelekea Polisi Siku ya Kesho Jumanne Juni 16 , 2026 Kuanzia Saa 3:00 Asubuhi katika Ofisi za RCO, Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Dar es Salaam.

Imetolewa na:

Ntele Benjamin
Katibu, CHADEMA Kanda ya Pwani
Juni 15, 2026.
1781581870845.jpg
 
Mwenyekiti wa Baraza la Wazee la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (BAZECHA) Mkoa wa Mbeya, David Mwambigija, ametoa wito mzito kwa askari wa jeshi la polisi nchini kutojihusisha na matukio ya utekaji wa raia, akisisitiza kuwa wanapaswa kulinda haki badala ya kutekeleza maagizo haramu.

Mwambigija ametoa kauli hiyo jana, Juni 13, 2026, alipokuwa akihutubia mkutano mkubwa wa hadhara wa CHADEMA uliofanyika katika Viwanja vya Mwembetogwa mkoani Iringa, uliolenga pia kumkaribisha aliyekuwa Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa, kurejea kikamilifu kwenye mapambano ya chama hicho.

Mwanasiasa huyo amewaasa askari hao ambao amewataja kama watoto wa wakulima, kuwa na hofu ya Mungu wanapoamriwa kutekeleza matukio yanayohatarisha usalama wa raia, akitolea mfano matukio ya utekaji yanayoripotiwa nchini.

"Ndugu zangu maaskari sikiliza, nyie watoto wa wakulima wadogo zetu, hivi mnapoambiwa maelezo ya juu kwani lazima ufanikishe dili? Ukimpigia simu kwamba nakuja, sogea mbele kidogo... kwani ukisema hili nimefeli shida iko wapi? Kazi kujipendekeza tu," amesema Mwambigija.

Akizungumzia kuhama na kurejea kwa viongozi ndani ya chama hicho, Mwambigija amesema kuwa CHADEMA ni taasisi imara ambayo haitikiswi na kuhama kwa mtu mmoja, akitolea mfano wanasiasa wakubwa waliowahi kuondoka na kurudi kama Edward Lowassa na Frederick Sumaye, huku akibainisha kuwa kuondoka kwa Msigwa huko nyuma kuliisaidia CHADEMA kujenga safu mpya imara.

Kuhusu afya na hali ya kisiasa ya Makamu Mwenyekiti Tundu Lissu, mzee huyo amewashangaza wanasheria wa Serikali na CCM wanaohangaika kumgandamiza kisheria, akieleza kuwa Lissu alinusurika kifo kwa miujiza mikubwa baada ya kupigwa risasi zaidi ya 16 mkoani Dodoma na kwamba amebaki kuwa nguzo imara ya chama hicho inayowaumiza kichwa watawala.

View: https://www.facebook.com/share/v/1MgHcfLcsp/
 
Kanda ya Kusini, katika Jimbo la Nachingwea katika viwanja vya Mahuridi Majengo C. Wananchi na chadema huwezi kuwatenganisha.
1781807055163.jpg
1781807051842.jpg
 
Ofisi Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kanda ya Nyasa zilizopo Kadege mkoani Mbeya zimevamiwa na kuvunjwa na watu wasiojulikana, huku kiasi kikubwa cha mali, vifaa vya kielektroniki, nyaraka za siri, na kadi za wanachama zikiwa zimeibiwa.
Matukio hayo yamebainishwa leo, Juni 18, 2026, na Katibu wa CHADEMA Mkoa wa Mbeya, Hamad Mbeyale, ambaye ameeleza kuwa taarifa za uvamizi huo zilibainika majira ya saa saba mchana wakati viongozi wa vijana walipofika ofisini hapo kwa ajili ya maandalizi ya mkutano wa hadhara uliopangwa kufanyika Juni 23.

Mbeyale amefafanua kuwa wahalifu hao walikuwa na vifaa maalum vilivyowafanya wavunje makomeo na vitasa vya milango ya ndani, ikiwemo ofisi ya Katibu wa Kanda na ofisi za mabaraza ya chama (BAWACHA na BAVICHA), ambapo wameiba 'printer' aina ya Epson inayotumika kuzalisha kadi, kompyuta ya kanda, nyaraka muhimu, bendera za chama, pamoja na kadi za wanachama (zilizochapishwa na ghafi).

"Wavamizi wamechukua nyaraka na kadi zetu za chama. Tunatoa taarifa hii mapema kwa umma na Msajili wa Vyama vya Siasa ili kadi hizi zikitumika mitaani au kugeuzwa kuwa kuna wanachama wamerudisha kadi, ijulikane ni njama zilizopangwa na watu wenye nia ovu ya kukidhoofisha chama kuelekea mkutano wetu mkuu," amesema Mbeyale.

Uongozi wa CHADEMA tayari umetoa taarifa rasmi kwa Jeshi la Polisi mkoani Mbeya, ambapo Kamanda wa Polisi wa Mkoa (RPC), Benjamin Kuzaga, pamoja na Mkuu wa Upelelezi wa Wilaya (OCD) wamefika eneo la tukio na kuanza uchunguzi wa kina wa kiuhalifu ili kuwakamata waliohusika na tukio hilo lililofanyika kwa kukata nguzo ya chuma ya bendera ya chama hapo nje.
#Sasalive #CHADEMA #HamadMbeyale #KandaYaNyasa #Mbeya #BenjaminKuzaga #JeshiLaPolisi #UhalifuWaKisiasa #HabariTanzania #SiasaZaTanzania
 
 
Katibu wa CHAUMMA Mkoa wa Mbeya, Protas Mgimbila, leo tarehe 23 Juni 2026 ametangaza kukihama chama hicho na kurejea Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Mgimbila alikuwa mwanachama wa CHADEMA kabla ya kuhama mwaka 2015. Amepokelewa rasmi kurejea CHADEMA katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Stendi ya Kabwe, mjini Mbeya, ambapo viongozi na wanachama walimkaribisha.
1782300164594.jpg
1782300161950.jpg
1782300159099.jpg
1782300156703.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom