CHADEMA Special Thread

CHADEMA Special Thread

1787248267108.jpg
 
Kada wa zamani wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ambaye kwa sasa ni Kada wa Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA), Henry Kilewo, amewataka wanaojiita watawala kuachana na madalali wa kisiasa wanaowadanganya kuwa wanaweza kukigawa chama hicho.

Kupitia chapisho aliloliweka katika mtandao wake wa X (zamani Twitter) jana Agosti 31, 2026, Kilewo amebainisha kuwa mfumo na uongozi wa sasa wa CHADEMA ni tofauti na ule wa zamani, kwani umerithi uzoefu wa nyuma na kujifunza kutokana na makosa yaliyopita ili kuepuka gharama kubwa za kisiasa

“Version ya CHADEMA ya leo sio ile iliyopita, hii imekulia kwenye ile version na ikaona makosa yake na haiwezi kuishi yale makosa kwakuwa inajua makosa yale yatawagharimu kuliko gharama wanazolipa leo,” ameeleza Kilewo.

Amesisitiza kuwa CHADEMA ni taasisi imara mno ambayo haiwezi kugawanywa hata kwa kutumia medali za juu za kivita, huku akiongeza kuwa njia iliyochaguliwa na chama hicho ndiyo sahihi katika kuondoa utawala kandamizi.

Kilewo amehitimisha kwa kutoa rai ya kimaadili akisema ni heri kuishi miaka michache duniani kwa wema na haki kuliko kuishi miaka mingi kwa uongo na unafiki ambao mwisho wake ni mbaya zaidi.

#SasaLive #HenryKilewo #CHADEMA #CHAUMMA #SiasaZaTanzania TanzaniaNews
1788277863905.jpg
 
Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Mara, Mwalimu Chacha Heche, amewataka wanachama wa chama hicho kutozungumzia suala la maridhiano na watawala endapo halipo kwenye ajenda rasmi ya chama.

Kauli hiyo imetolewa leo Septemba 1, 2026, siku chache baada ya Katibu wa CHADEMA Mkoa wa Mara, Donald Felix Mwembe, kuwataka viongozi wa chama hicho, akiwemo Makamu Mwenyekiti John Heche, kukaa mezani na watawala kwa ajili ya maridhiano yanayoweza kusaidia kuachiliwa kwa Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu.

Akizungumza leo, Chacha Heche amewataka wanachama wa CHADEMA kutoitisha mikutano au kuzungumza na waandishi wa habari kuhusu masuala ambayo hayalingani na msimamo rasmi wa chama.

Amesisitiza kuwa suala la maridhiano na Chama Cha Mapinduzi (CCM) si sehemu ya msimamo wa sasa wa CHADEMA, hivyo wanachama wanapaswa kuzingatia ajenda na maamuzi rasmi ya chama.

Kauli hiyo imeibua mjadala ndani ya chama hicho, hasa kutokana na wito uliotolewa awali na baadhi ya viongozi wa CHADEMA kuhusu umuhimu wa mazungumzo ya kisiasa katika kutafuta suluhu ya changamoto zinazokikabili chama, ikiwemo suala la kesi inayomkabili Tundu Lissu.

Hata hivyo, kwa mujibu wa kauli ya Chacha Heche, wanachama wanatakiwa kufuata msimamo rasmi wa chama na kuepuka kutoa kauli zinazoweza kutafsiriwa kuwa ni msimamo wa CHADEMA bila kuwa na mamlaka ya kufanya hivyo.
 
Back
Top Bottom