Chadema ndani ya mji mdogo wa Katoro/Buseresere

Inaonesha Mkutano utakuwa mzuri sana kwani maandalizi mazuri yamefanyika.Baadhi ya Wabunge tuko hapa Twiga Lodge tunasubiri muda ufike.Jana nako Chato mambo yalikuwa mazuri sana.

Mheshimiwa tunaomba picha tafadhali. Tuko nyuma yenu na msiyumbishwe na propaganda mfu za kina Kikwete na jeshi lake. Wana siraha lakini tutawashinda kwa sababu Mungu yuko upande wetu (sauti ya wengi ni sauti ya Mungu)
 
CCM wapeleke hoja Bungeni ya kufuta ruzuku ya vyama vya siasa hata kama na wao wataathirika. Inaelekea CDM hawafanyi kosa na ruzuku yao; ruzuku inatumika kuibomoa CCM kisawasawa. Dawa ya kukomesha haya maandamano na mikutano ya CDM isiyosha ni kuwaondolea uwezo wa mapato. CCM wao si wana vyanzo vingine vya mapato kama viwanja vya mipira na majengo!!!![/SIZE]


Ndiyo, wanavyo viwanja vyetu na majengo walivyo vipora mikononi mwa wananchi, kwani kwa hakika vilikuwa vyetu sote, si haki eti vilibaki mikononi mwa wana CCM peke yao, Na tukisha ikomboa nchi yetu, hilo litakuwa kati ya mambo ya msingi ya kurudisha mali zetu zote zilizoporwa!

GO CHADEMA...

 
ilianza operesheni sangara enzi hizo.. hii ya sasa ni funika bovu ndio maana wasira mpaka haja inambana

cdm aluta continua endeleeni kuwafungua macho watanzania tupo pamoja japo kwa sala
 
Wadau wapenda maendeleo nipo ktk mji mdogo wa katoro mpakani mwanza na kagera hali ni ya mashamsham utafikiri anakuja cjui nani maana hata rais huwa cio hivi,muda mfupi ujao kutakuwa na maandamano na mkutano wa hadhara,hii ni wakeup cal kwa cheyo,wasira, nk wanaowatia hofu wtz,kwa hali ilivyo naomba serkali ifate ushauri wa kuwakamata ili iwe rahisi kuiondoa madarakani.pipooos pr ni noma

i love it iwe mkoa kwa mkoa.... mpk kieleweke watu wote waamke
 
Hm hafifu,utajiharishia sana tu na bado na udini wenu watu wamewashtukia tayari
 
CDM endeleeni kukomaa, tuko watu wengi sana nyuma yenu msituangushe.....
Yalisemwa mengi,mmepangua ...endeleeni kuyapangua ili siku moja Mungu atusaidie tuje tuongozwe na watu wenye akili timamu kama DR Slaa!
CCM imekufa.......
 
Inaonesha Mkutano utakuwa mzuri sana kwani maandalizi mazuri yamefanyika.Baadhi ya Wabunge tuko hapa Twiga Lodge tunasubiri muda ufike.Jana nako Chato mambo yalikuwa mazuri sana.

Dada Regia inabid tukio kama hilo lije lipigwe hapa Dar,
Hilo litasaidia kuwaamsha usingizin CCM na makuwadi wao kina Cheyo, Mrema Wastaafu wa JWTZ nk wajue kuwa TZ ya leo ni tofauti na wanaoijua wao...
Hii pia itasaidia kumfanya Mkwere ajue kuwa Wa Tanzania tunaunga mkono Maandamano hayo
 
Mama .

Nyie wabunge mkiwa Bungeni mnalipwa posha kila siku. Je huko anawalipa nani Posho? na vipi hao wnaowahamasisha wanalipwa na nani? au ndio kuwadanganya watu wakati nyie mpo kazini?

Hii kauli ya POSHO inatoka kwa mtu mwenye harufu ya uCCM...how crap are you...Unafikiria kila kitu kutanguliza tumbo mbele kama chama cha mafisadi.ONDOA NJAA ZAKO HAPA ZIRUDISHE CCM.
 
poleni sana wana CCM! Chadema haiendeshwi na ruzuku...inaendeshwa na nguvu za wananchi...CCM igeni mfe!

Msafara wote ulio kanda ya ziwa unalipiwa na wananchi? Kilo ya sukari inatushinda sembuse bei ya chumba hotelini na ticket za ndege? Mimi nakataa hiyo ni kazi ya RUZUKU
 
Hapo kwenye RED, Hivyo viwanja vya mipira vilijengwa kwa nguvu za wananchi wala si vya CCM, Subiri utaona siku tunaichukua nchi vitawatokea puani!!! Kibanga ampiga mkoloni naikumbuka sana hii stori!! Sisi tutawapiga kwa sanduku la kura!!

Nani alijenga hiyo si hoja. Muhimu ni kuwa mapato yanakijenga CCM
 
Mama .

Nyie wabunge mkiwa Bungeni mnalipwa posha kila siku. Je huko anawalipa nani Posho? na vipi hao wnaowahamasisha wanalipwa na nani? au ndio kuwadanganya watu wakati nyie mpo kazini?

wewe humu unalipwa na nani?
 
Una uhakika na unacho kinena?

Muulize Padri Slaa atakuonyesha sponsor wote wanaomdhamini

Unajua haya maandamano yametusaidia kuweka sawa mambo mengi sana:

1. Baada ya CCM & Co. Ltd (yaani muungano waa CCM-A, B &C, Spika, etc.) kuiadhibu CHADEMA bungeni kwa njia mbalimbali, huku wakifurahia super-majority yao, CHADEMA ime-demonstrate power yake katika supreme authority wa nchi hii: Wananchi. penda usipende, piga ua garagaza, wananchi wanaipenda CHADEMA.

2. CHADEMA wame-demonstrate kwamba shutuma wanazorushiwa kwamba wana udini na ukabila, hazina ukweli wowote. katika maandamano yao kuna watu wa dini mbalimbali: waislamu kwa wakristo na pia dini ya asili. kwa nini? kwa sababu CHADEMA hawahubiri dini majukwaani, bali wanaongea maslahi ya wananchi walio wengi. Hawaongei maslahi ya kabila fulani, bali maslahi ya taifa. mikutano yao na maandamano yana sura za kitaifa.

3. CHADEMA wamesaidia kutuonesha wapinzani wa kweli, hata ndani ya CHADEMA yenyewe, na katika vyama vya upinzani. na kwa maoni kama haya unayotoa, inaonekana wewe una matatizo na CHADEMA kwa vile tu Dr. Slaa ni padri. kama angebadili dini leo na kutwa Dr. Abdul Slaa, ungekuwa huna tatizo naye, hata kama angeendelea kufanya hayo afanyayo. ungekuwa tayari kutamka, hata kama si kweli, kwamba pesa wanazotumia zinatoka Oman. CHADEMA wametusaidia kukuelewa zaidi. cha kufanya fungua macho, achana na upofu huo. hapo hauhitajiki muujiza!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom