Chadema ndani ya mji mdogo wa Katoro/Buseresere

HAYUPO WAKUZUIA MABADILIKO TANZANIA niwakati wa mnyonge kupata uhuru wakweli kutoka kwa wakoloni CCM..!!..Usually
when people are sad they don't do anything they just CRY over their
condition but when they gel Angry they bring about a change" (MALCOLM X)
.
 
Mama .

Nyie wabunge mkiwa Bungeni mnalipwa posha kila siku. Je huko anawalipa nani Posho? na vipi hao wnaowahamasisha wanalipwa na nani? au ndio kuwadanganya watu wakati nyie mpo kazini?

Ndio ujue kuwa chema chajiuza kibaya chajitembeza. CCM mpaka wabebe watu kwenye malori, wawape na hela kabisa wanapopanda, wagawe fulana na Tshirts, na waandae burudani kama The comedy na bongo flava ndio watu wahudhurie lakini CHADEMA wananchi wanahamasishana wenyewe na wanakichangia. Kwa wewe uliyezoea posho nenda CHAMA CHA MAFISADI (CCM) ingawa unakaribishwa pia CHADEMA ila hakuna posho.
 
CCM wapeleke hoja Bungeni ya kufuta ruzuku ya vyama vya siasa hata kama na wao wataathirika. Inaelekea CDM hawafanyi kosa na ruzuku yao; ruzuku inatumika kuibomoa CCM kisawasawa. Dawa ya kukomesha haya maandamano na mikutano ya CDM isiyosha ni kuwaondolea uwezo wa mapato. CCM wao si wana vyanzo vingine vya mapato kama viwanja vya mipira na majengo!!!!

Kumbuka viwanja na majengo hayo wanayo kinyume cha sheria kwa vile yalijengwa kwa nguvu za watanzania wote wakati wa chama kimoja. Tutakapoanza utekelezaji wa ripoti ya tume ya Nyalali, basi CCM watabaki hawana hata ofisi.
 
Mama .

Nyie wabunge mkiwa Bungeni mnalipwa posha kila siku. Je huko anawalipa nani Posho? na vipi hao wnaowahamasisha wanalipwa na nani? au ndio kuwadanganya watu wakati nyie mpo kazini?
kama kawaida yako kijana wa vapour tupu.
 
CCM wapeleke hoja Bungeni ya kufuta ruzuku ya vyama vya siasa hata kama na wao wataathirika. Inaelekea CDM hawafanyi kosa na ruzuku yao; ruzuku inatumika kuibomoa CCM kisawasawa. Dawa ya kukomesha haya maandamano na mikutano ya CDM isiyosha ni kuwaondolea uwezo wa mapato. CCM wao si wana vyanzo vingine vya mapato kama viwanja vya mipira na majengo!!!!

Ujumbe mzito lakini unajua wabunge wengi wa CCM ni waganga njaa ukimwambia hakuna ruzuku ataacha ubunge mara moja. Nakumbuka mwaka 2002 niliandaa semina ya wabunge kuhusiana na umuhimu wa kutungwa kwa sheria ya mazingira. Mwenyekiti wa Kamati ya Mazingira wa wakati huo, ambaye sasa ni Spika, aliambia kuwa wabunge hawawezi kuhudhuria bila posho ya 60,000/-. Hiyo ni juu ya posho ya 60,000/- waliyokuwa wanapokea kwa siku. Hatukuwa na ujanja licha ya kuwafuata Dodoma ilibidi tuwape posho hiyo. Nashukuru miaka miwili baadae sheria hiyo ilipita. Nilichoelewa ni kuwa taasisi yoyote ile ya serikali, kijamii na binafsi inayoandaa semina kwa wabunge ni lazima iwalipe posho ya mahudhurio. Nadhani wabunge wa Chadema watapinga ulipwaji wa posho hizi kwa vikao vinavyofanyika Dodoma kwani huku ni sawa na kupokea posho mara mbili.

Kitu kingine kama mtu una semina ambayo umewaalika wabunge hiyo ni balaa kwani wengi wao huja na risiti za kununulia mafuta na usafiri ambazo ni za ajabu kweli kweli. Ni lazima suala hili nalo lithibitiwe.
 
Peoplessssssss powerrrrr,hakunaaaaaaaaa kulalaaaaaaaa mpakaaaaa kielewekeeeeee kikieleweka Ikuluuuuuu kwa maendeleo ya Watanzania
 
Mama .

Nyie wabunge mkiwa Bungeni mnalipwa posha kila siku. Je huko anawalipa nani Posho? na vipi hao wnaowahamasisha wanalipwa na nani? au ndio kuwadanganya watu wakati nyie mpo kazini?

Hata wakilipwa ni haki yao. unafikiri wanakula nini? wanalala wapi? kinacholipwa sio kwa ajili ya ufujaji wa fedha ila chakula na malazi unapokuwa nje ya kituo chako cha kazi kitaalam inaitwa night out allowance/ per diem
 
Unajua haya maandamano yametusaidia kuweka sawa mambo mengi sana:

1. Baada ya CCM & Co. Ltd (yaani muungano waa CCM-A, B &C, Spika, etc.) kuiadhibu CHADEMA bungeni kwa njia mbalimbali, huku wakifurahia super-majority yao, CHADEMA ime-demonstrate power yake katika supreme authority wa nchi hii: Wananchi. penda usipende, piga ua garagaza, wananchi wanaipenda CHADEMA.

2. CHADEMA wame-demonstrate kwamba shutuma wanazorushiwa kwamba wana udini na ukabila, hazina ukweli wowote. katika maandamano yao kuna watu wa dini mbalimbali: waislamu kwa wakristo na pia dini ya asili. kwa nini? kwa sababu CHADEMA hawahubiri dini majukwaani, bali wanaongea maslahi ya wananchi walio wengi. Hawaongei maslahi ya kabila fulani, bali maslahi ya taifa. mikutano yao na maandamano yana sura za kitaifa.

3. CHADEMA wamesaidia kutuonesha wapinzani wa kweli, hata ndani ya CHADEMA yenyewe, na katika vyama vya upinzani. na kwa maoni kama haya unayotoa, inaonekana wewe una matatizo na CHADEMA kwa vile tu Dr. Slaa ni padri. kama angebadili dini leo na kutwa Dr. Abdul Slaa, ungekuwa huna tatizo naye, hata kama angeendelea kufanya hayo afanyayo. ungekuwa tayari kutamka, hata kama si kweli, kwamba pesa wanazotumia zinatoka Oman. CHADEMA wametusaidia kukuelewa zaidi. cha kufanya fungua macho, achana na upofu huo. hapo hauhitajiki muujiza!

Nakufagilia mkuu kwa kutoa maelezo na uchambuzi wa kina; mwenye akili kakuelewa-asiyeelewa hawezi kueleweshwa na yeyote.
 
Naamini kuna mijitu humu jamvini inalipwa kwa kuandika upupu..haingii akilini CDM inaendeleza uzushi..hivi ni mTZ gani haguswi na ugumu huu wa maisha ulisababishwa na hawa wadhalimu CCM?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom