Chadema nao mafisadi, wametumia milioni 60 uchaguzi mdogo tu Uzini ~ Jussa

Hivi mbona matamko kuhusu Uzini hayamuishi Jussa, kuna nini cha ajabu?
Hizo ni kelele za "MFAMAJI, HAWACHI KUTAPATAPA".
KAFU wamekuwa wakijimaliza wenyewe. Hiyo inayoitwa "ndoa na CCM" ni kama kujipigilia msumari wa mwisho tu, lakini ukweli ni kama Dk. Omar Ali Juma (R.I.P) alivyokuwa akiwmambia mtani wake Sefu kwa utani na kweli humo humo - "Balahau huna sera."

KAFU hawana sera. Katika "evolution" yao walipitia hatua hizi:
1. Walianza kama chama chama cha kiliberali, cha kuwakomboa Wazanzibari, hasahasa Wapemba.
2. Walipoona hawakufanikiwa, wakajivua magamba wakawa chama cha chuki, fitna na ugomvi na kuwafanya Wazanzibari wasusiane hata kwenye mazishi, vibaraza vya kahawa na viduka vya mafuta ya taa.
3. Walipohisi hawafanikiwi na sera hizo, wakafuata sera ambazo kama ingekuwa siku hizi tungewafananisha na "wanamgambo wa AL-Shabaab": kuripua madaraja, vinu vya umeme, kutia vinyesi katika visima vya maji na kupaka shule vinyesi, kuwalazimisha wanafunzi kugomea shule hata watoto wadogo wa darasa la kwanza; kumwagia watu tindikali, kulipua makanisa na maduka ya ulevi. Cha kushangaza, wakati wanalipua maduka haya ya ulevi, walikuwa wanaiba ulevi na kuunywa.
4. Baada ya yote hayo kutowapeleka popote, ndipo mkuu wao na kikundi kidogo cha walaji wenzake alipoungana na CCM Visiwani kuingia Ikulu kwa mlango wa nyuma na kuwaacha yatima wafuasii wao.

KAFU kama KAFU imekufa, na CCM Zanzibar kama CCM haipo. Amani ya uoga iliyopo sasa kwa mwavuli wa SUK itadumu muda mdogo kwani Wazanzibari wamedanganywa. Hapa nakusudia wamedanganywa na KAFU na CCM. Dhiki ya maisha kwa walalahoi iko pale pale na hili litawagharimu kwenye chaguzi zijazo.

Huu ni wakati muafaka kwa CDM kutumia mwanya huu. Wazanzibari kwa sasa ni mayatima, hawajui wamfuate nani. Ninachowashauri tu na kuwatahadharisha CDM waachane na siasa za kisisiemu na kikafu badala yake kiwe kweli chama cha demokrasia na maendeleo.

MAPAMBANO YANAENDELEA!
ALUTA CONTINUA!
 
Jussa sasa amefilisika kisiasa amebaki tu na siasa za maji taka na za kidini. Kuwa CUF mlitumia millioni 7 na CDM walitumia millioni 60, tatizo ni nini? Kule Igunga mlifadhiliwa na mme wenu CCM mka-kodi Helkopita, vipi safari hii hajawapa chochote?

huyu JUSA auJUISI? MAANA AKILI ZAKE ZINAMTOSHA MWENYEWE, MASIKINI WATU WAKE ANAOWAWAKILISHA NAWAHURUMIA KWA KUWA NA MTU KILAZA KAMA HUYU LOOH!
 
Chadema hawajatoa ripoti rasmi ya fedha na tathmini ya Uchaguzi wa Uzini. Hayo mengine ya Jusa ni uwongo na propaganda ya Kisiasa. Lakini yeye Kama Kiongozi wa Kisiasa simshangai sana.
Oooh...bora umewaambia wananchi waelewe!
Kumbe hii ndio maana halisi ya siasa? This is what You, Slaa, Mbowe n co. mnachokifanya!
Kumbe siasa ni uongo...na ni propaganda tu! Watu kama nyie ni wabaya sana..,na its better tuwaavoid mapema sana!
 
Jussa:Chadema wametumia milioni 60 uchaguzi mdogo tu uzini.
Na Ismail Jussa

Tumetumia milioni 7 tu wakati Chadema wamenambia wametumia milioni 60 (haidhuru mimi naamini wametumia zaidi kwa mambo tuliyoyaona kule). Sasa katika hali hiyo, kuna lipi jipya? Nani aliyepoteza? CUF inajua inachokifanya.

source: mtandao wa Mzalendo

Mmh sasa Jussa siku hizi amekuwa CAG, iweje CHADEMA watoe bajeti na matumizi yao katika uchaguzi mdogo (Uzini) kwa Jussa? I'm just curious....that's all.
 
Tangu kabla na hasa baada ya Uchaguzi wa Uzini, haipiti siku bila kusikia Jusa kasema jambo kuhusu chadema:
mara chadema imetumia udini, ukabila, ...mara chadema imetumia hela nyingi... sisi afadhali...mara.....
hivi Jusa amekosa kingine cha kuzungumza...hasa namna ya kuboresha chama chake ambacho kinaelekea kaburini...? Hivi kwanini asiwe na mikakati ya kufuta aibu ya kushika nafasi ya tatu nyuma ya Chadema katika uchaguzi husika huko Uzini?
Ama kweli sasa naamini Chadema ni chama tishio bara na visiwani..... Maana huku bara CCM hofu kubwa ni Chadema, na sasa tunatambua tangu uchaguzi wa Uzini, Jusa amedhihirisha kuwa Chadema ni kiboko ya CUF pia......
Mungu ibariki chadema. Mungu ibariki Tanzania
 
Jussa unatakiwa utambue kuwa watanzania wana uwezo binafsi wa kuchambua mambo!hawahitaji nguvu sana kujua chama chenye sera,uongozi imara na dhana halisi ya upinzani ni kipi!ni bora kama kwanza ungekubali chdm kuwa chama halisi cha upinzani,pili uache unafiki na tatu at least ujitahd kukijenga cuf ambay n dhahiri kinakufa.unavyozidi kuikashifu chdm unzidi kuonesha ni kwa jinsi gani usivyo imara na unavyoiogopa chadema
 
jussa:chadema wametumia milioni 60 uchaguzi mdogo tu uzini.
Na ismail jussa

tumetumia milioni 7 tu wakati chadema wamenambia wametumia milioni 60 (haidhuru mimi naamini wametumia zaidi kwa mambo tuliyoyaona kule). Sasa katika hali hiyo, kuna lipi jipya? Nani aliyepoteza? Cuf inajua inachokifanya.

Source: Mtandao wa mzalendo

ni wakupuuza tu.kwanza sio mtanzania wala mwafrika..analeta fujo ugenini
 
MFA MAJI HAACHI KUTAPATAPA, JUSA hana jipya wala analolijua, ni mbabaishaji tu aliyeishiwa kisiasa, CUF yao inawafia na mawazo yao duni, CUF wanaizika wantuletea porojo, kwa kauli yake hiyo inadhihirisha namna walivo ccm B, inakuja hiyo CDM kuwashika zenj na mtachonga sn akna Jusa
 
chadema kama chama hakina misingi ya ufisadi sema kuna watu wachache wasiopenda ukweli na wengi wao ni wale waliotoka vyama jirani wakaenda chadema ndiyo mafisadi wa hela pale lakini pia jussa weka wewe draft ya hiyo m7 mliyotumia ilikuwaje weka hapa mgawanyo ndiyo uanze kushutumu chadema
 
Jamani huyo Jussa ni mke wa magamba,sasa ameacha ndoa yake na Magamba anafuatilia mambo ya Chadema,aachane kabisa na chadema,hajui kuwa yeye na Maalim wanaendelea kuiua CUF aka CCM B.
 
This is hypothetical question, CCM na CUF waliingia makubaliano ambayo yanasema chama cha pili kwa wingi wa kura
kwenye uchaguzi mkuu kitafanya serikali ya MSETO na chama kilichokuwa cha kwanza. Uchaguzi wa 2010 ilikuwa CCM na CUF.
Wakaunda SUK

MIND YOU hayo yalikuwa makubaliano ya CCM na CUF. Lakini yameingizwa kwenye katiba ya Zanzibar.

Hebu tujiulize hivi mathalani 2015, CCM ikawa No. 1, CDM No. 2 na CUF No. 3 (kama ilivyotokea Uzini).
  1. Je CCM na CDM watangeneza Serikali ya MSETO ZNZ?
  2. Je, Nafasi ya CUF (Maalim) itakuwe Je SuK?
  3. Je, hili ndilo linalomuogopesha Jussa?
 
katika kurasa zake za facebook
nape nauye asema kuwa chadema wanunua kura kwa mill 60
aandika hivi
Chadema inasemekana wametumia 60 Mill. uchaguzi mdogo Uzini na kuambulia kura 281, ukigawanya karibu kila kura wameinunua kwa zaidi ya Tshs 200000(laki mbili)...Tafakari!​
 
Kwa nini Chadema hizo pesa wasingezitumia kujengea Makao Makuu ya Chama.
 
Ukiona mwanaume anajikirimu uso ujue kuna tatizo la msingi....... Sana sana ataishia kuwa msengenyaji, sikai barazani pa watu wenye mizaa, thz days mods wamekuwa wakali sana when it comes to this political morron. Am outta here!!!!!!!!
 
Back
Top Bottom