Kampeni za CHADEMA/UKAWA Arusha au Mwanza au Mbeya ziwe live kwenye TVs na Radio!

The Palm Tree

JF-Expert Member
Apr 13, 2013
7,951
12,535
Habari zenu wanabadiliko wote nje ya CCM!!

Wote tunakumbuka vizuri kwamba uzinduzi wa kampeni za uchaguzi mkuu wa Urais, wabunge na madiwani za Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), NCCR Mageuzi, CUF na NLD chini ya mwavuli wa muungano usio rasmi (kwa sababu haujasajiliwa) wa "UKAWA" ulifanyika tarehe 29/8/2015 katika viwanja vya Jangwani - Dar es Salaam.

Macho na masikio ya watanzania wapenda Mabadiliko na wenye hamu ya kuitokomeza kabisa CCM iliyotawala nchi hii kwa takribani miaka 50+ yalielekezwa huko.

Mimi pia ilikuwa hivyo. Na kwa kuwa Mungu amenijalia kuwa na TV nyumbani kwangu nilihakikisha siku hiyo sipitwi na tukio lolote. Japo umeme ulikatwa siku hiyo lakini bahati tena nina umeme wa nguvu ya jua. Kwa hiyo mimi na jirani tulibanana kwenye kasebure kangu kuangalia TV.

Tulikuwa very ovewhelmed na umati wa watu uliohudhuria ktk uzinduzi huo pamoja na hamasa ya mabadiliko waliyokuwa nayo watu hao. Hii inadhihirisha wazi kuwa, watu wameichoka CCM, wanaichukia na wako tayari kwa mabadiliko ya kuindoa ktk uongozi wa nchi hii hata kama mabadiliko hayo yataletwa na jiwe, basi watu hao wako tayari kulipigia jiwe hilo kura na si CCM!!

Hata hivyo sherehe hizo ziligubikwa na dosari kadhaa ambazo zilitia doa uzinduzi huo, zilitia doa hamasa ya wengi waliojitokeza kwenye sherehe za uzinduzi huo hapo uwanjani na sisi huku majumbani tuliokuwa tunafuatilia tukio hilo moja kwa moja kupitia vyombo vya habari kama TV, Redio pamoja na mitandao ya kijamii kama huu.


Dosari hizo ni pamoja na;


1. Kuchelewa kuanza kurushwa matangazo ya moja kwa moja kwenye baadhi ya TV na Radio. Tuliambiwa matangazo yangekuwa live kuanzia saa 9:00 alasiri lakini TV kama ITV, TBC na Channel 10 walichelewa kuanza kurusha. Star TV hawakurusha kabisa.

Sina hakika na TV zingine kama Azam, Clouds kwa sbb sina access nazo. Mimi nina king'amuzi cha Dstv.

Hili lilitukera baadhi yetu kwa sbb tuliona kama ni muendelezo wa culture ya kutojali muda na ahadi za kitanzania zilezile tunazozokataa za uongo uongo!!


2. Wageni na hususani mgeni rasmi kuchelewa kufika uwanjani wakati ratiba ya shughuli na tukio zima ilikuwa inaanza SAA 9:00 alasiri. Hii ilipelekea hata mgombea wa Urais ambaye tukio na sherehe hizo zilikuwa zinamuhusu yeye zaidi kuliko mtu mwingine yeyote kutokupata muda wa kutosha wa kuueleza na kutoa ufafanuzi wa kina wa ilani ya uchaguzi na vipaumbele vyake atakavyovisimamia kama Rais wa nchi kwa umma uliokuwa mbele yake na uliokuwa unafuatilia kupitia vyombo vya habari.

Hii ilipelekea kupata muda ambao haukuzidi dakika 15 kitu ambacho ni kasoro kubwa!!


3. Kuwapa watu ambao hawakuwa na umuhimu wowote muda mwingi wa kuzungumza mambo ambayo hata hayahusiani na ilani. Mfano Richard Tambwe Hizza, alitumia muda mrefu wa bure tu kwa sababu tunamfahamu vyema tu tangu akiwa kitengo cha propaganda cha CCM.

Hata hivyo hakuna anayepinga kwamba, hoja za upotoshaji za CCM hazihitaji kujibiwa, la hasha!..

Ni lazima zijibiwe lakini lililo muhimu zaidi ni kupanga muda na wazungumzaji kwa umakini na ufasaha huku "main issues" ambayo ni Ilani ya uchaguzi na vipaumbele vya mgombea wetu wa Urais vikipewa muda wa kutosha na kufafanuliwa kwa ufasaha na mgombea mwenyewe.

Tukumbuke kuwa uchaguzi ni kushawishi wapiga kura kwa nini wakuchague Wewe na si yule!!

Ziko kasoro nyingine nyingi lakini kubwa Na muhimu kwa mtazamo wangu ni hizo. Kwa maana hiyo Mwenyekiti wa Taifa CHADEMA na Katibu mkuu wake na strategists na pundits wa timu nzima ya kampeni ya mgombea Urais, lazima wajipange na kusimama ktk nafasi zao.

NINI KIFANYIKE KUREKEBISHA KASORO HIZO?

kwanz nianze kwa kuwaambia kuwa CCM na mgombea wao Bw Magufuli ni wepesi mno, hawana jipya na hawawezi tena kuwadanganya watanzania kwa uongo na ulaghai wao wa miaka yote;

Kwa sababu asilimia kubwa ya watanzania wamewachoka, hawawataki na wana kumbu kumbu ya kudanganywa kwa miaka 50+;

Na Pili, watanzania wako tayari kwa mabadiliko nje ya CCM kwa gharama yoyote hata kama wakiambiwa wabebe mtutu wa bunduki!!....

Lakini si wa kufikia huko, bali kwa sanduku la kura tu inatosha kuwakaanga hawa. Wataiba kura mpaka hata za kuiba hazitatosha, mwisho wake wataachia tu!!

Sasa nawashauri CHADEMA/UKAWA kufanya yafuatayo ili kurekebisha kasoro zilizojitokeza siku hiyo na kujionesha dhahiri shahiri siku ambayo ilikuwa ya muhimu sana kwao kuliko siku zingine zote zilizo mbele yao za kampeni!!


1. Katika mikutano ya kampeni katika moja ya miji mikubwa ya aidha Arusha au Mbeya au Mwanza, wafanye tena kilichopaswa kufanyika kwa ufasaha na usahihi wake ktk viwanja vya jangwani Dsm. Na hapa makosa yaliyofanyika siku ya ufunguzi yaepukwe!!

2. Mkutano huo urushwe moja kwa moja na vituo vyote vya runinga na radio. Mkutano uchukue masaa manne sharp kuanzia saa 8:00 mchana hadi 12:00 jioni. Kila mtu atakayepata kuzungumza azungumze yote. Awepo mtu maalumu wa kujibu hoja za CCM za kizushi (nadhani Sumaye anafaa sana). Kina Taslima, Makaidi, Tambwe Hizza, Mnyika, Msigwa, Tundu Lissu, Jussa Ismail, Mbatia, Maalim Shariff Hamad wapewe nafasi ya kutosha wamwage Sera na wazungumze yote!.

Mgombea Urais Bwana Edward Lowassa apate muda usiopungua dkk 60 au saa nzima kufafanua ilani na vipaumbele vyake akiingia ikulu.


3. Katika hili,wiki moja kabla, mkutano huo utangazwe kwa nguvu zote kupitia vyombo vyote vya habari na social medias ili Ku build awareness ya watu kujiandaa kwenda uwanjani na sisi ambao hatutapata nafasi kuwa huko, tuhamasishe watu kumtazama na kumsikiliza kupitia vyombo vya habari.

4. Kwenye vipaumbele vya mgombea ni lazima kwa mfano kama anaposema Elimu bure kuanzia chekechea hadi chuo kikuu, isiwe ni kusema tu kama wanavyojisemea CCM, bali ni sharti aseme how? Vyanzo vya fedha kugharamia elimu hiyo? kwanini CCM imeshindwa na kwa vipi yeye na chama chake wataweza?

Lazima pia atoe hata mifano hai ya nchi zinazofanana na sisi kiraslimali na uchumi zilitekeleza Sera hiyo na ikawezekana!!...

Isiwe ni kuorodhesha ahadi tu kama wanavyofanya CCM ambacho ndicho chanzo cha udanganyifu na uongo wao hata kushindwa kutekeleza kwa walichoahidi wao wenyewe.

Ni kwa njia hii tu wapiga kura watampima mgombea na kuamua kwa kuwianisha anachokiongea na sura yake (kama anamaanisha akisemacho au usanii tu) pamoja na hali halisi ya iwapo hayo anayoyasema yanatekelezeka!!....

Hiki ndicho watu tunachokihitaji katika mabadiliko haya tunayoyataka!!


5. Tunajua kuwa baada ya fyongo ya jangwani siku ya ufunguzi wa kampeni, mligundua kuwa mmefanya makosa ya kiufundi na ndiyo maana haraka haraka mkatafuta namna ya kurekebisha damage ambayo mmekwisha kuifanya kwa kununua airtime ITV ili mgombea wenu asome/atoe hotuba yake.

Hata hivyo hiyo haikuwa na msaada mkubwa sana kurekebisha kasoro na damage hiyo kwa sbb mrikurupuka na watu wengi hawakuwa aware na hilo.

Aisha, summary ya ilani kwa mtindo wa hotuba aliyoitoa mgombea EL haikuleta difference na impact yoyote na hizi tunazozisikia kwa maCCM kwa sbb iko kwa mtindo ule ule wa kiCCM, ya kuorodhesha tu mambo pasipo kutoa ufafanuzi wa namna gani yatatekelezwa (nimefafanua halo juu).

Hii inawezekana iliababishwa na vitu vingi.

Mosi, Inawekana mgombea mwenyewe aliamua kujiandikia au;

Timu yake iliamua kumpotosha na kumharibia.

Hata hivyo ni kwa nini hii haikupitia kwa wenyeviti wenza wa UKAWA ili wajiridhishe kuwa kinachokwenda kutoka kwenye public kimebeba matamanio yao, malengo yao na kitakidhi haja ya hadhira inayotaka mabadiliko?

Na tunajiuliza tu, kwamba, ina maana Ukawa mmekosa watu wa kuwasaidia kumwandalia mgombea wetu hotuba inayo address matatizo ya nchi na kwa namna gani ninyi ndiyo mnaamini ni suluhisho la matatizo hayo?

Katika hili mimi napendekeza hili lifuatalo lifanyike haraka sana:

Kwamba, waliohusika kumwandalia mgombea hotuba ya ovyo ya kiCCM ambayo haikuwa na substance waondolewe mara moja katika nafasi zao hawafai wawekwe watu wenye uwezo.

Inakuwaje hotuba ya mtu anayetarajiwa kuleta mabadiliko anatoa hotuba isiyokuwa na tofauti yoyote na ya mgombea wa CCM?


6. Katika vipaumbele vya mgombea wa CHADEMA/UKAWA ni sharti kiongezwe kipengele kwa uwazi na upekee cha Kufuta mchakato wa ulioleta Katiba Pendekezwa ya Sitta na Chenge na kwamba mara tutakapomchagua, aseme waziwazi kuwa, mchakato wa katiba mpya utaanzia kwa kuunda bunge jipya la katiba ili kujadili Rasimu ya Pili ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliyoongozwa na Jaji Joseph Warioba ambayo ilitokana na maoni ya sisi wananchi!!

Mimi naliona hili kama vile halisemwi kwa uwazi na tunajiuliza ni kwa nini? Pia tukumbuke hili ndilo msingi wa kuanzishwa kwa UKAWA!!

Mwisho katika Edward Lowassa kama anataka kupata hizo kura milioni 10, ni lazima na yeye mwenyewe na watu wake aliokuja nao wabadilike. Wakae kimabadiliko kweli nje ya CCM, na sisi tilione hilo pasipo shaka!!

Amekaribishwa na ni vyema akaheshimu nyumba ya watu na kuheshimu hiyo heshima aliyopewa kwa kuitumikia ipasavyo nyumba hiyo!!

Binafsi namuunga mkono, lakini anaanza kutukatisha tamaa kwa kufanya makosa madogo madogo kama haya!

Muda bado upo na unatosha kurekebisha makosa. CCM wao jua lilisha chwea, hawana muda wa kurekebisha makosa yao. Wamekaa mkao wa kupigwa tu, hawana jinsi lakini ni pale tu mtakaeupeka makosa kama gaya!!
 
Hata mkifanya ziwe live mpaka kwenye maji mtapigwa mapema sana huyo fisadi wenu hana jinsi kwisha habari yake.
 
Mnaweka mgombe fisadi halafu mnataka watanzania tuwachekee komeni kabisa mafisadi yenu pelekeni huko kwenu siyo watanzania.
 
Iko vuzuri kama mwandiko wa saa8, ila kumbuka Castro alikuwa abahutubua zaidi ya saa 4 hadi inaboa so mimi nadhani awe anafafanua japo kufupi tu...
 
sitaki tena upuuzi wa hotuba ndefu huo ni mfumo mchafu tuliozoeshwa na ccm mpaka muongeaji akimaliza mnasahau alipo anzia na ndomana wanatoa ahadi nyingi za uongo.
mie nataka asizidishe dk 20 tu.
Kura yangu ni kwa LOWASA tu nilizompigia kikwete zinatosha. Hata lowasa aongee dk 0 .
kura yangu anayo
 
habari kwa wanabadiliko wote nje ya ccm!!

Wote tunakumbuka vizuri kwamba uzinduzi wa kampeni za uchaguzi mkuu wa urais, wabunge na madiwani kwa kwa chama cha demokrasia na maendeleo (chadema) na nccr mageuzi, cuf na nld chini ya mwavuli usio rasmi (kwa sababu haujasajiliwa) wa muungano wa vyama hivi almaarufu "ukawa" ulifanyika tarehe 29/8/2015 katika viwanja vya jangwani - dar es salaam.

Macho na masikio ya watanzania wapenda mabadiliko na wenye hamu ya kuitokomeza kabisa ccm iliyotawala nchi hii kwa takribani miaka 50+ yalielekezwa huko. Mimi pia ilikuwa hivyo. Na kwa kuwa mungu amenijalia kuwa na ka tv nyumbani kwangu nilihakikisha siku hiyo sipitwi na tukio lolote. Umeme ulikatwa siku hiyo lakini nina umeme wa nguvu ya jua. Kwa hiyo mimi na jirani zangu hatukubanduka kwaenye tv.

Tulikuwa very ovewhelmed na umati wa watu uliohudhuria ktk uzinduzi huo pamoja na hamasa ya mabadiliko waliyokuwa nayo watu hao kwa kuwatazama tu. Hii inadhihirisha wazi kuwa, watu wameichoka ccm na wanaichukia na wako tayari kwa mabadiliko ya kuindoa ccm na uoza wake wote hata kama mabadiliko hayo yataletwa na jiwe, wako tayari kulipigia jiwe hill kura!!

Hata hivyo kulukuwa na dosari kadhaa ambazo zilitia doa uzinduzi huo, zilitia doa hamasa ya wengi au baadhi wana wa nchi waliojitokeza kwenye sherehe za uzinduzi huo hapo uwanjani na sisi tuliokuwa tunafuatilia moja kwa moja kupitia vyombo vya habari kama tvs, redio na mitandao ya kijamii kama huu. Dosari hizo ni pamoja na;

1. Kuchelewa kuanza kurushwa kwa matangazo ya moja kwa moja kwenye baadhi ya tvs na radio. Tuliambiwa matangazo yangekuwa live kuanzia saa 9:00 alasiri lakini tv kama itv, tbc na channel 10 walichelewa kuanza kurusha.star tv hawakurusha kabisa. Sina hakika na tv zingine kama azam, clouds kwa sbb sina access nazo. Mimi nina king'amuzi cha dstv. Hili lilitukera baadhi yetu kwa sbb tunaendeleza ahadi za kitanzania za uongo uongo!!

2. Wageni na hususani mgeni rasmi kuchelewa kufika uwanjani wakati ratiba ya shughuli na tukio zima ilikuwa inaanza saa 9:00 alasiri. Hoi ilipelekea hata mgombea wa urais ambaye tukio na sherehe hizo zilikuwa ni zake kuliko mtu mwingine yeyote kutokupata muda wa kutosha wa kuueleza na kutoa ufafanuzi wa kina wa ilani ya uchaguzi na vipaumbele vyake atakavyovisimamia kama rais wa nchi kwa umma uliokuwa mbele yake na uliokuwa unafuatilia kupitia vyombo vya habari. Hii ilipelekea kupata muda ambao haukuzidi dakika 15 kitu ambacho ni kasoro kubwa!!

3. Kuwapa watu ambao hawakuwa na umuhimu wowote muda mwingi wa kuzungumza mambo ambayo hata hayahusiani na ilani. Mfano richard tambwe hizza, alitumia muda wa bure tu. Hakuna anayepinga kwamba, hoja za upotoshaji za ccm hazihitaji kujibiwa, la hasha!..ni lazima zijibiwe lakini lililo muhimu zaidi ni kupanga muda na wazungumzaji kwa umakini na ufasaha huku main issues ambayo ni ilani ya uchaguzi na vipaumbele vya mgombea wetu wa urais vikipewa muda wa kutosha na kufafanuliwa kwa ufasaha na mgombea mwenyewe. Tukumbuke kuwa uchaguzi ni kushawishi wapiga kura kwa nini wakuchague wewe na si yule!!

Ziko kasoro nyingine nyingi lakini kubwa na muhimu kwa mtazamo wangu ni hizo. Kwa maana hiyo mwenyekiti wa taifa chadema na katibu mkuu wake na timu nzima ya kampeni ya mgombea urais, fanyieni kazi kasoro hizo na ikibidi mrekebishe time ya kampeni!!

Nini kifanyike kurekebisha kasoro hizo?

Kwanza nianze kwa kuwapa na kuwatia moyo kuwa ccm na mgombea wao bw magufuli ni wepesi mno, hawana jipya na hawawezi tena kuwadanganya watanzania kwa uongo na ulaghai wao kwanza; kwa sababu asilimia kubwa ya watanzania wamewachoka, hawawataki na wana kumbu kumbu ya kudanganywa kwa miaka 50+; na pili kwa sababu hiyo watanzania hawa wako tayari kwa mabadiliko nje ya ccm kwa gharama yoyote hata kama wakiambiwa wabebe mtutu wa bunduki!!....lakini hawa si wa kufikia huko, bali sanduku la kura tu linatosha, wataiba kura mpaka hata za kuiba hazitatosha, mwisho wake wataachia tu!!

Sasa nawashauri chadema/ukawa kufanya yafuatayo ili kurekebisha kasoro zilizojitokeza na kujionesha dhahiri shahiri siku ya ufunguzi kwa sbb muda upo unatosha!!

1. Katika mikutano ya kampeni katika moja ya maeneo haya arusha au mbeya au mwanza kilichopaswa kufanyika kwa ufasaha na usahihi wake ktk viwanja vya jangwani dsm kifanyike. Na hapa makosa yaliyofanyika siku ya ufunguzi yaepukwe!!

2. Mkutano huo urushwe moja kwa moja ktk vituo vyote vya runinga na radio. Mkutano uchukue masaa manne sharp kuanzia saa 8:00 mchana hadi 12:00 jioni. Kila mtu atakayepata kuzungumza azungumze yote. Awepo mtu maalumu wa kujibu hoja za ccm za kizushi na wengine na mengine kwa kadiri mtakavyojipanga. Sumaye, tambwe hizza, mnyika, msigwa, tungu lissu, jussa ismail, mbatia, maalif shariff hamad wazungumze!!. Mgombea urais bwana edward lowassa apate muda usiopungua dkk 60 au saa zima kufafanua ilani na vipaumbele vyake akiingia ikulu.


3. Katika hili, mkutano huo utangazwe kwa nguvu zote kupitia vyombo vyote vya habari na social medias ili ku build awareness ya watu kujiandaa kwenda uwanjani na sisi ambao hatutapata nafasi kumtazama na kumsikiliza kupitia vyombo vya habari.

4. Kwenye vipa umbele vya mgombea ni lazima kwa mfano kama anasema elimu bure kuanzia chekechea hadi chuo kikuu, isiwe ni kusema tu kama wanavyojisemea ccm, bali ni sharti aseme how? Vyanzo vya fedha kugharamia elimu hiyo? Kwanini ccm imeshindwa na kwa vipi yeye na chama chake wataweza?. Lazima pia atoe hata mifano hai ya nchi zilizotekeleza sera hiyo na ikawezekana!!... Isiwe ni kuorodhesha ahadi tu kama wanavyofanya ccm ambacho ndicho chanzo cha udanganyifu na kushindwa kutekelezwa kwa walichoahidi wao wenyewe. Ni kwa njia hii tu wapiga kura watampima mgombea na kuamua kwa kuwianisha anachokiongea na sura yake (kama anamaanisha na si usanii tu) pamoja na hali halisi iwapo hayo anayoyasema yanatekelezeka!!....hiki ndicho watu tunachokihitaji katika mabadiliko haya tunayoyataka!!

5. Tunajua kuwa baada ya fyongo ya jangwani siku ya ufunguzi wa kampeni, mligundua kuwa mmefanya makosa ya kiufundi na ndiyo maana haraka haraka mkatafuta namna ya kurekebisha damage ambayo mmekwisha kuifanya kwa kununua airtime itv ili mgombea wenu asome/atoe hotuba yake. Hata hivyo hiyo haikuwa na msaada mkubwa sana kurekebisha kasoro na damage hiyo kwa sbb mrikurupuka na watu wengi hawakuwa aware na hilo. Hata hivyo pia summary ya ilani kwa mtindo wa hotuba haikuleta difference yoyote na hizi tunazozisikia kwa maccm kwa sbb iko kwa mtindo ule ule wa kiccm, ya kuorodhesha tu mambo pasipo kutoa ufafanuzi wa namna gani yatatekelezwa (nimefafanua halo juu).

Hii inawezekana kusababishwa na vitu vingi. Inawekana mgombea mwenyewe aliamua kujiandikia au timu yake iliamua kumpotosha na kumharibia. Hata hivyo ni kwa nini hii haikupitia kwa wenyeviti wenza wa ukawa ili wajiridhishe kuwa kinachokwenda kutoka kwenye public kimebeba matamanio yao, malengo yao? Na tunajiuliza tu, kwamba, ina maana ukawa mmekosa watu wa kuwasaidia kumwandalia mgombea wetu hotuba inayo address matatizo ya nchi na kwa namna gani ninyi ndiyo suluhisho la matatizo hayo? Katika hili mimi napendekeza hili lifanyike haraka sana: Kwamba, waliohusika waondolewe mara moja katika nafasi zao hawafai wawekwe watu wenye uwezo. Inakuwaje hotuba ya mtu anayetarajiwa kuleta mabadiliko anatoa hotuba isiyokuwa na tofauti yoyote na ya mgombea wa ccm?

6. Katika vipaumbele vya mgombea wa chadema/ukawa ni sharti kiongezwe kipengele kwa uwazi na upekee cha kufuta mchakato wa ulioleta katiba pendekezwa ya sitta na chenge na kwamba mara tutakapomchagua, mchakato wa katiba mpya utaanzia kwa kuunda bunge jipya la katiba ili kujadili rasimu ya pili ya tume ya mabadiliko ya katiba iliyoongozwa na jaji joseph warioba ambayo ilitokana na maoni ya sisi wananchi. Mimi naliona hili kama vile halisemwi kwa uwazi na tunajiuliza ni kwa nini. Pia ndiyo msingi wa kuanzishwa kwa ukawa, wasisahau!!

Mwisho katika edward lowassa anataka kupata hizo kura milioni 10, ni lazima na yeye mwenyewe na watu wake aliokuja nao abadilike na tumwone amebadilika. Amekaribishwa na ni vyema akaheshimu nyumba ya watu na kuheshimu hiyo heshima aliyopewa.

Binafsi namuunga mkono, lakini anaanza kutukatisha tamaa kwa kufanya makosa madogo madogo kama haya!

kama harufu ya msaliti flani hivi..anyway
 
Hata lowassa aongee dk 2 na nusu tu, kwa mtz mwenye nia ya dhati ya mabadiliko atamchagua lowassa!!! Tz ya sasa hatutaki kuendelea kuongozwa na kikwete nyuma ya mwamvuli wa makofuli!!! Mungu atuepushie hayo yasitupate!!!!!!!!! Ccm out by any means, it must go!!!!!!!!!!!!!

Sera ya ccm ni kilimo kwanza kwa watanzania maskini lakini kwa watoto wao ni "elimu kwanza"!!!!!!!!!!!

Ewe mtanzania mwenye uelewa atagundua ni kwanini kila mwaka ccm wanatuaminisha watz eti sera ni kilimo kwanza huku wao na wana wao wakiishi katika sera ya elimu kwanza na ndo'maana huwezi ona mtoto yeyote wa kiongozi wa ccm katika shule za serikali/kata!!!! Wanataka wao na vizazi vyao waendelee kuwa watawala wetu nasi tuendelee kuwa watumwa wao, very very bad indeed!!!!!

Ndiyo maana walivyomsikia lowassa anasema elimu kwanza wote walishtuka na kuponda sana kwani walijua sasa watz wanaenda kujielewa vizuri na itakuwa vigumu mno kwao kuwadanganya kirahisi watz!!!!

We need "elimu kwanza" then kilimo baadaye, hapa namaanisha, mtu akishapata elimu ya kutosha anaweza jua namna gani alime, zao gani linalipa, je kuna soko la uhakika? Na mambo kadha wa kadha muhimu kabla ya kulima na atenda mwenyewe tena kwa raha bila kushawishiwa na mtu!!!!!!

Chagua chadema/ukawa, chagua edward n. Lowassa!!!!
 
Mimi napendekeza wawe wanaongea wengine tu alafu Lowassa anatupungia mkono tu,inatosha kabisa.Jamani mbona watu wengine ni wagumu sana kuelewa!mmeshaambiwa mwaka huu hatafutwi Lowassa,Yanatafutwa mabadiliko lakini watu wapi!!

#mabadiliko
 
sitaki tena upuuzi wa hotuba ndefu huo ni mfumo mchafu tuliozoeshwa na ccm mpaka muongeaji akimaliza mnasahau alipo anzia na ndomana wanatoa ahadi nyingi za uongo.
mie nataka asizidishe dk 20 tu.
Kura yangu ni kwa LOWASA tu nilizompigia kikwete zinatosha. Hata lowasa aongee dk 0 .
kura yangu anayo
Mikutano mingine yote ya kampeni ni okay, DKK 15 au 20 zinatosha

Ila kwa pale Jangwani siku ya ufunguzi wa kampeni na kuzindua ilani ya uchaguzi kilitakiwa kufanyika kitu cha ziada mkuu

Na hicho kitu ilikuwa ni hiki na rahisi tu, kuichambua ilani na vipaumbele in details!!

Mathalani katika kipaumbele No. 1, 2 na 3 ambacho ni Elimu bure kuanzia chekechea hadi chuo kikuu, ilipaswa tuambiwe how? Pesa toka wapi? Atabana wapi? Kwa nini hawa CCM wameshindwa for 50+ na wao Chadema wataweza nk

Si lazima atumie 4hrs, lakini at least angetengewa 45 - 60mins angeweza!!

Katika hoja yangu sijasema masaa 4 ayatumie mgombea yeye peke yake bali huo ni muda wa shughuli yote!!
 
Mimi napendekeza wawe wanaongea wengine tu alafu Lowassa anatupungia mkono tu,inatosha kabisa.Jamani mbona watu wengine ni wagumu sana kuelewa!mmeshaambiwa mwaka huu hatafutwi Lowassa,Yanatafutwa mabadiliko lakini watu wapi!!

#mabadiliko

It is impossible mkuu!

Lazima yeye mwenyewe azungumze ktk maeneo muhimu yote ili awe ktk record!

Utakuja kumbanaje sasa iwapo hatasema kwa mdomo wake kuwa serikali itasimamia au kutekeleza hili na like kama atasemewa na watu wengine?

Nadhani lililo muhimu ni kusema mambo key machache na muhimu kulingana na resources ulizonazo utakayoyasimamia na kuyatekeleza kweli si kama JK ambaye leo anamaliza muda wake, 50% ya mambo aliyoahidi ameshindwa kutekeleza na leo Mdogo wake (Magufuli) naye anaahidi mengine mepya tena!
 
Teamlowassa.
friends of lowassa.
team ukawa.
Malofa. Huu ujumbe ni mzuri Sana ufanyieni Kazi
 
Back
Top Bottom