Chadema nao mafisadi, wametumia milioni 60 uchaguzi mdogo tu Uzini ~ Jussa

Jaman msameheni mpakistan wa watu, tatzo nyie mmevamia ndoa ya mtu tena sultan ccm na mwandani wake cuf, jusa umeshikwa pabaya huku hamad rashid kule chadema. Aaa! Lazma uokote makopo mwaka huu
 
jussa wewe si ulisema "cuf ilishindwa uzini kwasababu kuna watu wengi watokao bara na pia kuna wakristo wengi"

orodha ya visingizio haijaisha tu?

huyu jamaa kama alitamka hayo maneno basi hafai kabisa kuwa kiongozi.analeta sababu za kibaguzi tu! Kwa hiyo cuf ni ya wazanzibar na waislamu tu! Ashindwe na alegee!

 
Hivi mbona matamko kuhusu Uzini hayamuishi Jussa, kuna nini cha ajabu?

Kiwewe cha kushuka kwa umaarufu wa CUF kuliko walivyotegemea kwamba muafaka wa vyama viwili tu vya siasa ndio ungewabeba..kumbe wenzao CCM walishapiga hatua tano mbele..wanatakiwa waangalie wapi walijikwaa sio walipoangukia kama kweli wanataka kurudi katika siasa za ushindani...!
 
Jusa kaa chini utafakari kwanini cuf imeshindwa then tafuta mikakati ya 2015, swala la chadema wamtumia m 60 na wewe m 7 sio hoja wote hamkufanikiwa kulipata hilo jimbo. Kapange timu yako sio kumsemea mwenzako hujawa mgaguzi wa hesabu za serikali wewe
 
Kama mmegundua tangia mwanzo Jussa hajasema chochote kuhusu CCM! Hasemi kwa nini CCM wamashinda Uzini, wala CCM walitumia kiasi gani!
 
Anzia na uchaguzi wa Igunga,
Nenda maandalizi ya miaka 50 ya uhuru,
baada ya hapo njoo jimbo la uzini.
 
Watu wengine akili zao afadhali za panya! Hata ukifanya hesabu za haraka haraka kuna ufisadi gani katika milioni 60!
  1. Nauli kwa timu iliyotoka bara.
  2. Posho ya timu ya kampeni ambayo inajumuisha bara na visiwani.
  3. Gharama za kukodi kumbi za mikutano ya ndani, chakula na viburudisho wakati wa mikutano hiyo.
  4. Gharama za kukodi magari na vyombo vingine vya usafiri.
  5. Gharama za shajala (Stationary) nk.
Hivi kuna cha kushangaza hapo!
 
Hoja hii ni pumba, mil 60 kwa Chadema wewe ndiye msemaji mkuu wa matumizi ya vyama kwenye kampeni? na Chama chenu na michemko ya Chlorine mtaimaliza lini?
Mimi mzanzibara na Nipo Machui, Chadema mpaka kamasi rangi ya Bendera ya Chadema, CCM imetumia pesa ngapi kwa kura hizo Alfu 5???????????????? Kama wajua Kichaga... Nya olye
 
yeye kazi ni kuishambulia chadema tu utadhani CDM ni chama tawala!!!!atakaye iua cuf na kuizika ni huyu mmanga,...
 
Jusa ni mfa maji asieacha kutapatapa, anaona aibu ya kupigwa nyumbani kwake na mgeni. mara udini, mara wabara, mara 60m, ya nini yote ulishindwa kupinga barua ya posa sasa ushaolewa kelele za nini? tulia ulinde ndoa yako weye.
 
Chadema hawajatoa ripoti rasmi ya fedha na tathmini ya Uchaguzi wa Uzini. Hayo mengine ya Jusa ni uwongo na propaganda ya Kisiasa. Lakini yeye Kama Kiongozi wa Kisiasa simshangai sana.

Mkuu kwa bandiko lako hili naomba thread ifungwe maana umemaliza kila kitu...
 
Back
Top Bottom