CHADEMA na Udikteta Makao Makuu

Mzee Kifimbo

Senior Member
Mar 25, 2007
153
3
Naomba makada wa Chadema tupeni mwanga juu ya habari ya mzee Halimoja ambaye ni kada wa Chadema.

=======

Na Mzee Yusuf Halimoja - Gazeti la Mtanzania

KAMA tujuavyo, baada ya Tanzania kuingia kwenye mfumo wa vyama vingi mwaka 1992, Watanzania walikuwa huru kuanzisha vyama vya siasa. Kati ya vyama vilivyoanzishwa ni Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, alipata nafasi ya kuangalia sera za vyama mbalimbali. Hakuficha alichoona. Alisema afadhali CHADEMA ilikuwa na sera nzuri.

Baada ya kauli ile ya Baba wa Taifa, ambaye amefariki dunia akiwa bado anaendelea kuheshimiwa na umma wa Tanzania, wananchi walitarajia kuona CHADEMA ikitumia kauli ya Mwalimu kueneza mtandao wake nchi nzima. Lakini haikuwa hivyo. CHADEMA imeshindwa kutimiza matarajio ya wananchi. Kwa nini?

Hebu turudi nyuma. Tumesikia watu wakisema kuwa chama tawala, CCM, kina makundi yake. Wenyewe wameendelea kupinga vikali kauli hiyo. Wanadai kuwa hakuna makundi ndani ya CCM. Tuanzie hapo.

Sipati sababu ya CCM kukataa kuwa na makundi. Makundi ni jambo la kawaida katika sekta mbalimbali za maisha, ikiwa ni pamoja na ndani ya vyama vya siasa. Hayana ubaya. Ubaya unakuja wakati makundi hayo yanapotumiwa vibaya.

Kwa mfano, katika dini ya Kikristo kuna makundi yanayoitwa "madhehebu". Kwa mfano kuna Wakristo Wakatoliki, Waanglikana, Walutheri, Wapentekoste, na wengineo wengi tu. Makundi haya yakishirikiana katika shughuli mbalimbali hujenga. Lakini yakipoteza wakati kupambana yenyewe kwa yenyewe huharibu.

Kwa upande wa vyama vya siasa, tuna mfano hai kutoka Marekani. Ndani ya chama kimoja cha Democrat wagombea wawili, Barack Obama na Hillary Clinton, wanapambana wakiungwa mkono na makundi ndani ya chama hicho hicho kimoja.

Kwa jumla chama bila makundi si chama hai. Ni chama kilichokufa. Makundi ndani ya chama huleta ushindani unaokisaidia chama kuwa hai, kupata mawazo mapya yanayokipeleka chama mbele, na hata makundi hukisaidia chama kupata viongozi bora wanaotokana na ushindani.

Tukiiangalia CHADEMA hatuwezi kuficha ukweli kwamba nayo pia ina makundi yake. Ni mawili. Kundi la kwanza liko Makao Makuu ya chama. La pili liko mikoani.

Imedaiwa kwa haki kabisa kwamba kundi la kwanza la CHADEMA lililoko Makao Makuu ya chama ni kundi linaloundwa na viongozi wa Makao Makuu na watendaji wakuu wa chama hicho, wakiwamo wakurugenzi.

Inaonekana kuwa lengo kuu la kundi hili ni kulinda maslahi binafsi. Furaha kubwa ya kundi hili ni kuhakikisha kuwa ruzuku ya shilingi milioni 66 inayopata CHADEMA kila mwezi haifiki mikoani. Badala yake inatumiwa nao kwa mishahara na posho za safari za magari na helikopta zisizokwisha na zisizo na manufaa yoyote kwa chama.

Kuna habari kwamba baadhi ya wale walioko makao makuu wamenufaika na fedha za CHADEMA, kiasi cha kuanzisha miradi na biashara ambazo hawakuwa nazo kabla hawajajiunga na CHADEMA.

Kwa jumla kundi la kwanza la CHADEMA lililoko makao makuu linatuhumiwa kwa ubadhirifu, ufisadi, udikteta, matumizi mabaya ya fedha ikiwa ni pamoja na matumizi ya helikopta ambayo hayana tija yoyote katika ujenzi wa chama.

Juu ya yote, kundi hili linaaminiwa kuwa lina mawakala wa chama tawala ambao wamekaa pale kukomba tu fedha ya chama zinazowapeleka mikoani, huku wakiuacha Mkoa wa Dar es Salaam ukiwa hauna uhai wa chama kwa sababu safari ndani ya Dar es Salaam hazina posho. Kwa kifupi kundi la kwanza la CHADEMA lililoko makao makuu ni kundi la wababe wasio na uchungu wowote na chama na wanaoendesha chama kama vile ni kampuni yao binafsi. Kiongozi au mtendaji yeyote anayethubutu kupambana na maovu yanayoendelea kutendwa na kundi hili la kwanza anahatarisha nafasi yake. Atafukuzwa bila kupewa nafasi ya kujieleza, hata kama atakuwa ameitwa kwenye kikao hicho ili ajieleze. Hiyo ni demokrasia kwa staili ya Makao Makuu ya CHADEMA. Nani anabisha?

Kundi la pili la CHADEMA ni lile lililoko mikoani. Lengo kuu la kundi hili ni kuhakikisha kuwa lengo la chama cha upinzani la kushika madaraka ya utawala linatimia. Hili ni kundi lenye uchungu wa kweli na chama. Ni kundi linalotaka nguvu zote za chama zielekezwe kwenye kujenga chama ngazi zote.

Ni kundi linalotaka kujenga mtandao wa chama nchi nzima. Kundi hili linataka chama kiwe na ofisi mikoani kote na wilayani ili wanachama wapate mahali pa kukutana, kupata wanachama wapya, kufundishana sera za chama, na kubadilishana mawazo juu ya ujenzi wa chama utakaosaidia kuleta ushindi katika chaguzi mbalimbali. Kwa kifupi hili ni kundi linalotaka chama kiwe cha watu wote badala ya kugeuzwa kuwa kampuni ya watu binafsi.

Kundi hili la pili lililoko mikoani ambalo ndilo lenye uchungu na chama linapinga vikali matumizi ya helikopta wakati wa kampeni za uchaguzi, wakati wagombea ubunge na udiwani hawapewi hata shilingi moja ya kuwawezesha. Kundi hili pia linataka ruzuku ya chama isiishie kufujwa makao makuu, bali ifike mikoani ili kusaidia kufungua matawi na kuwafikia wananchi wa vijijini ambao hawana habari zozote za CHADEMA.

Lakini kundi hili la CHADEMA lililoko mikoani linapodai lifikishiwe ruzuku huambiwa na Katibu Mkuu wa chama kuwa mikoa na wilaya zinapata ruzuku kwa kupelekewa bendera na kadi za chama! Hapa mtu hakosi kujiuliza.

Bendera za chama zitatundikwa wapi na kadi za chama zitagawiwa wapi wakati chama hakina ofisi mikoani na wilayani? Na viongozi wa chama mikoani watakwendaje kufungua matawi kama ruzuku wanayopelekewa ni bendera na kadi tu za chama bila kupelekewa nauli na kodi za mapango?

Kwa kila hali, CHADEMA Makao Makuu imepoteza matarajio ya wanachama wake na wananchi kwa jumla. Kibaya zaidi Katibu Mkuu wa CHADEMA hajui matatizo ya mikoani. Hatembelei mikoa.

Wakati chama kikiendelea kuendeshwa vibaya makao makuu, kundi la CHADEMA lililoko mikoani lilikaa likisubiri saa ya ukombozi. Ikafika.

Ilitokea kwamba Desemba mwaka 2007, CHADEMA ilifanya uchaguzi wa makamu mwenyekiti wa chama. Kundi la kwanza la CHADEMA lililoko makao makuu likamwandaa mgombea wake. Kundi la mikoani halikukutana kumwandaa mgombea.

Wajumbe wa Baraza Kuu la CHADEMA ndio waliopewa jukumu la kumchagua makamu wa mwenyekiti kwa mujibu wa katiba ya chama. Kura zikapigwa. Mgombea aliyeandaliwa na makao makuu alipata kura 37, wakati mgombea ambaye makao makuu yalipambana naye, Zakayo Chacha Wangwe, alipata kura 56. Nguvu ya umma ilifanya kazi.

Huko nyuma viongozi wa CHADEMA walizoea kuhubiri kuwa nguvu ya umma inayotakiwa ni ya kuiondoa CCM madarakani. Hawakuona uwezekano wa kutumiwa nguvu ya umma kuleta mabadiliko na ushindani wa kweli ndani ya chama.

Lakini hapa wajumbe wa mikoani, kwa kumchagua Chacha Wangwe aliyekuwa ameandaliwa kushindwa, walikuwa wamefanya mapinduzi makubwa yaliyothibitisha kuwa nguvu ya umma, inaweza kutumika ndani ya chama kutimiza matakwa ya walio wengi.

Wajumbe wa Baraza Kuu waliomchagua Chacha Wangwe kihalali na kidemokrasia kuwa Makamu Mwenyekiti waliamini kuwa huo ulikuwa mwisho wa ushindani. Lakini sivyo ilivyotokea. Makao Makuu ya CHADEMA hawakukubali kushindwa.

Hivi leo Makao Makuu ya CHADEMA si tu kama Chacha Wangwe anatengwa na haungwi mkono katika mipango yake ya kukileta chama kwa watu. Ananyanyaswa pia. Kwa mfano aliendelea kunyimwa chumba cha ofisi makao makuu.

Akalazimika kujipatia kwa nguvu. Lakini Chacha Wangwe ambaye amedhamiria kukijenga chama si mtu wa kukata tamaa. Anaandaa mikutano na maandamano yanayofanikiwa kutokana na ushirikiano mkubwa anaopata kutoka viongozi wa mikoa na wilaya, huku watu wa makao makuu wakimwangalia kwa husuda. Katika kumharibia jina Chacha Wangwe Makao Makuu ya CHADEMA yanaeneza uzushi kwamba yeye ni wakala wa CCM. Lakini nani hajui kuwa yeye ndiye mpinzani wa kweli?

Kwa jumla kundi la CHADEMA lililoko makao makuu ni kikwazo kikubwa kwa maendeleo na uhai wa CHADEMA. Ni kundi lisiloheshimu demokrasia. Makao Makuu CHADEMA kimebaki chama kinachotaka kiendelee kuitwa cha "kidemokrasia" huku kikiendeshwa kidikteta.

Kwa mfano hatua ya makao makuu kumtenga Chacha Wangwe aliyechaguliwa kihalali kuwa Makamu Mwenyekiti siyo ya kidemokrasia. Ni ya kidikteta. Vile vile hatua ya kufukuza watendaji wenye mtazamo tofauti bila kupewa nafasi ya kujieleza pia ni udikteta. Hivi sasa kuna uhasama mkubwa kati ya makao makuu na wanachama wa CHADEMA Mkoa wa Dar es Salaam wanaoshirikiana na Chacha Wangwe kukijenga chama Dar es Salaam. Kwa mfano mwanachama mmoja wa CHADEMA mkoani Dar es Salaam ametiwa ndani na mtendaji wa makao makuu bila kufanywa juhudi yo yote ya kumaliza masuala ya chama ndani ya chama.

Na huko Makao Makuu ya CHADEMA kinachoendelea ni juhudi za kumkwamisha Chacha Wangwe ili kazi yake isionekane, kusudi asipate nafasi ya kuchaguliwa tena kuwa kiongozi. CHADEMA itafanya makosa kumpoteza kiongozi safi asiyehusishwa na ubadhirifu wala ufisadi.

Chacha Wangwe ni mpambanaji hodari asiyetetereka na kila mwananchi mwenye mapenzi ya kweli na CHADEMA, hasiti kumuunga mkono. Kwa mfano mjini Dar es Salaam aliungwa mkono alipoitisha maandamano ya kupinga hatua ya wananchi wa Tabata Dampo kuondolewa kwenye makazi yao kwa nguvu ili kumpisha mwekezaji.

Na Chacha Wangwe ni mpiganiaji mkubwa wa haki za binadamu, ameamua kuendeleza mapambano ya kutetea ardhi ya wananchi.

Lazima aungwe mkono ama sivyo tutakuwa tunawandaa watoto wetu kwa vita dhidi ya wawekezaji ambao kwa kweli watageuka kuwa walowezi.

Tukirudi CHADEMA Makao Makuu tutaona kwamba yamekaa kulaumu CCM kwa udikteta, wakati CHADEMA inaendeshwa kidikteta. Wamekaa kulaumu serikali ya CCM kwa ubadhirifu na ufisadi kana kwamba CHADEMA hakuna wabadhirifu na mafisadi.

Lakini pia CHADEMA imeendelea kulaumiwa kwa ukabila. Ni ukabila wa CHADEMA uliosababisha kati ya wabunge sita wa viti maalumu watano watoke kabila moja. Pia ni ukabila uliosababisha karibu nusu ya wakurugenzi wote wa CHADEMA watoke kabila moja. Na hivi sasa kuna tetesi kuwa vigogo wa kabila moja wanamwandaa mtu wao ili achaguliwe kuwa Rais mwaka 2010. Watanzania wasifanye makosa kumpeleka Ikulu Rais atakayejaza watu wa kabila lake.

Hivi basi, ndivyo makao makuu ya CHADEMA yalivyoshindwa kutimiza matarajio ya wananchi. Lakini CHADEMA si makao makuu. CHADEMA ni wanachama na wananchi. Kwa hivyo wanachama wa CHADEMA mikoani wana jukumu kubwa la kusafisha CHADEMA Makao Makuu ili CHADEMA itimize matarajio ya wananchi.
 
Matatizo yakitumiwa kama Stepping Stone siku zote hujenga badala ya kubomoa. Habari kwa jinsi ilivyoandikwa ina ukweli mwingi usio weza kupingwa.
Watu wenye mionyo ya ubinafsi na roho za kihayawani wapo kila mahali, watakosekana vipi Chadema?

Binafsi sioni tatizo la kutumia helkopta kusafiria lakini naona umuhimu wa ku priotize matumizi ya helkopta kulingana na safari.
Isiwe tu kwamba kila mara Mwenyekiti akitaka kwenda mikoani basi ni lazima apande hiyo machine.

Kuhusu kutumia ruzuku yote makao makuu na kuacha mikoa na wilaya na sehemu zote za nchi zikitapatapa, hilo nadhani ni kosa la kimiani mnyonya damu.
Chama siyo makao makuu, chama ni mtandao mzima wa utendaji nchini kote.
Kwa sabau Ruzuku inatolewa kufuata idadi ya wabunge ni vema kutoa fungu kubwa katika majimbo yaliyotoa wabunge na fungu jingine libaki HO na jingine liwekwe kuimarisha chama sehemu ambazo hazina wabunge.

Ukweli kwamba HO inatumia fedha karibu yote ya Ruzuku na wakati huo huo imeshindwa kabisa kutwaa hata kiti kimoja cha Ubunge katika majimbo ambayo yanaizunguka HO na lile ambalo ni la HO ni dalili moja kwamba kuna kundi la watu ambao Vision zao zinaishia kwenye mifuko yao ya kaptula na Account zao za Benki.

Njaa ni jambo la kujirudia rudia kwa kila kiumbe.
Ni vema kujenga mazingira ya kula leo kesho na siku zote kwa kila kiumbe kuliko kujenga mazingira ya kula leo na kuacha kesho ijishughulikie.

Uchunguzi uliomo ndani ya Taarifa hii nauunga mkono kwa dhati na bila kusita nawapa changamoto Chadema kuweka sawa mambo kuliko kuanza kuleta Mizengwe ya kukataa madai ambayo yana kila dalili ya ukweli.
 
yah wasiogope kutofautiana ila wawe tayari kutatua tofauti zao bila unafiki wowote wala woga.
 
Habari zenyewe za magazeti ya RA, lakini hata hivyo wanaitaji vilevile kurekebisha mambo haya mapema sana maana tusitengeneze hakina EL RA AC na wengine kwenye vyama vya upinzani maana sasa hivi Tanzania tunahitaji watu makini kwa ajiri ya kurekebisha hali ya ufisadi uliojaa kwenye nchi yetu.
 
Mimi nilifikiri kuna madai mapya ? Haya ya ukabila mbona yamesha ongelewa sana hapa .Matumizi ya mchine kila siku yanasemwa .Kwa ni ni wabunge wametoka upande mmoja ni sababu ya wazi kabisa na zimesha semwa .Labda kw auchache kama pesa kutofika mikaoni hili laweza kuwa jambo lakini mengine mwandishi yuko katika kampeni ambazo zilisha feli kabla ya kuanza .Ukabila Chadema wala mie siuoni labda kwa kuwa mimi si mwenzao .
 
Kwa jumla kundi la kwanza la CHADEMA lililoko makao makuu linatuhumiwa kwa ubadhirifu, ufisadi, udikteta, matumizi mabaya ya fedha ikiwa ni pamoja na matumizi ya helikopta ambayo hayana tija yoyote katika ujenzi wa chama.

JJ aje na spinning zake atuambie haya!!!.

Kuhusu mambo ya Udikteta Kitila alishasema CCM pia inakosa mwenyekiti ambaye ni dikteta; Alisema tatizo la CCM ina viongozi wanaofuata wanachama wanasema nini? Hivyo haitoi maamuzi mazuri.

Kwa hiyo kwa hili CHADEMA, udikteta ni moja ya "core values zao"; Kwa CHADEMA viongozi wanajua zaidi ya wanachama na wanaweza kuwasemea wanachama wao.

Nimesitushwa na uchangiaji wa lugha laini kwenye mambo mazito kwenye chama chetu hiki no. cha upinzani!!! yaani lugha laini kweli kweli as if mambo wanayofanya ni madogo sana... ati Tunapiga vita ufisadi!!!
 
CHADEMA; chama cha demokrasia kinachoendeshwa kidikteta


**hao wanachama wa CHADEMA sidhani kama watadiriki kuja hapa kwa uoga wao !**

Na Padri Privatus Karugendo,

GAZETI la Mtanzania Jumapili la Aprili 6, 2008, lilikuwa na makala iliyoandikwa na mzee Yusuf Halimoja, yenye kichwa cha habari: CHADEMA: Chama cha demokrasia kinachoendeshwa kidikteta.

Kwa jinsi ninavyomfahamu mzee huyu mwenye busara na mwandishi asiyechoka, sikuamini kama makala hiyo iliandikwa na yeye. Hata kama ni yeye aliandika, kichwa cha habari kitakuwa kimetengenezwa na mhariri kwa lengo lake mwenyewe.

Makala inaongelea mambo matatu makuu ndani ya Chama cha CHADEMA: udikteta, matatizo ya makao makuu ya chama na ukabila.

La kushangaza ni kwamba mengine mawili yamefafanuliwa vizuri lakini la udikteta, linalobeba kichwa cha habari, limeachwa kuelea tu! Huu si uandishi wa mzee Yusuf Halimoja, ninayemfahamu. Kama ni yeye, basi angeuchambua vizuri udikteta wa CHADEMA na kuutolea mifano.

Kabla ya kuendelea kutoa hoja, niunge mkono maneno haya kwenye makala tajwa: “Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, alipata nafasi ya kuangalia sera za vyama mbalimbali. Hakuficha alichoona. Alisema afadhali CHADEMA ilikuwa na sera nzuri.”

Mwalimu, hakukosea, ni kweli kabisa kwamba sera ya CHADEMA ni nzuri na imeboreshwa zaidi kuliko ile aliyoiona Mwalimu.

Ingawa mzee Yusuf Halimoja, baadaye katika makala yake, anaiponda CHADEMA, kushindwa kutekeleza sera, yake, ukweli utabaki pale pale kwamba CHADEMA ina sera safi, ni chama makini, kinasikiliza na kushirikisha. CHADEMA, ni miongoni mwa vyama bora Tanzania na Afrika kwa ujumla.

Kamusi ya Kiswahili sanifu inaeleza kwamba dikteta ni mtu anayetawala nchi kwa amri yake peke yake bila kushauriwa au mtu mwenye tabia ya kutaka lifanywe lile analosema bila ya kupingwa.

Kama CHADEMA, ingekuwa inaendeshwa kidikteta, kufuatana na maana ya neno dikteta, basi mwenyekiti angekuwa ni yuleyule tangu mwaka 1992 kilipoanzishwa.

Mwenyekiti wa kwanza, bado yu hai, ana afya na akili nzuri. Hadi sasa CHADEMA, imekuwa na wenyeviti watatu: Mzee Edwin Mtei, mzee Bob Makani na mwenyekiti wa sasa, Freeman Mbowe. Wenyeviti wote hawa walichaguliwa kidemokrasi na sote tulishuhudia.

Ukifuata mantiki ya kifalsafa, kwa vile kumekuwepo kupokezana uongozi ndani ya CHADEMA, udikteta hauna nafasi. Kwa vile mzee Halimoja (kama kweli ni yeye aliyeandika makala ile) ameshindwa kuuelezea udikteta wa CHADEMA, sintaliongelea sana hili, ila ni bora Watanzania wakafahamu kwamba hakuna udikteta ndani ya CHADEMA, chama hiki kinaongozwa na vikao vya chama. Huu ni ukweli ulio wazi na wala hatuna haja ya kuandikia mate!

Tuangalie hili la ukabila na matatizo yanayojitokeza makao makuu ya CHADEMA kama ilivyoelezwa na mwandishi wa makala tajwa.

Tukianza na hili la ukabila. Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe, anatoka Machame. Makamu wake wawili; Chacha Wangwe anatoka Tarime na makamu wa pili, Mzee Said Mzee, anatoka Zanzibar.

Katibu Mkuu wa CHADEMA Willibrod Slaa, anatoka Karatu na manaibu wake wawili mmoja Hamad Yusuf Mzee anatoka Zanzibar na mwingine ni Zitto Kabwe, kutoka Kigoma. Je, hapa kuna ukabila gani? Uongozi wa juu umetanda kutoka Zanzibar hadi Kigoma.

Wakurugenzi wanaolalamikiwa kwenye makala tajwa kwamba karibu nusu wanatoka kabila moja, kwanza ieleweke wazi kwamba kazi ya kuwachagua wakurugenzi ni ya kamati kuu.

Hata hivyo, si kweli kwamba wanatoka kabila moja: Mkurugenzi wa Fedha na Utawala, Anthony Komu, anatoka Moshi, Mkurugenzi wa Habari na Uenezi, Erasto Tumbo, anatoka Shinyanga, Mkurugenzi wa Kampeni na Uchaguzi, Msafiri Mtemelwa anatoka Rufiji, Mkurugenzi wa Vijana, John Mnyika, anatoka Iringa.

Mkurugenzi wa Wanawake, Naomi Kaihula, anatoka Mbeya, Mkurugenzi wa Rasilimali, Susan Lyimo, anatoka Moshi, Mkurugenzi wa Wazee, Victor Kimesera, anatoka Manyara, Mkurugenzi wa Organization, Benson Kigaila, anatoka Dodoma, Mkurugenzi wa Sheria na Katiba, Tundu Lisu, anatoka Singinda, Mkurugenzi wa Mambo ya Nje, ni Zitto Kabwe, anatoka Kigoma, Mkurugenzi wa Bunge na Halmashauri ni John Mrema, anatoka Moshi. Wakurugenzi wanatoka mikoa mbali mbali ya Tanzania. Hapa kuna ukabila gani?

Kwamba kuna makundi mawili ndani ya CHADEMA, kundi la makao makuu na kundi la mikoani, si kweli. Huu ni upotoshaji wa makusidi.

Vyama vyote vina uongozi wa makao makuu na uongozi wa mikoani. Haya si makundi bali ni mfumo wa ungozi ndani ya vyama. Hata CCM, ina uongozi wa makao makuu na uongozi wa mikoani na wilayani.

Hii ni tofauti na makundi kama ya wanamtandao halisi na wanamtadao masilahi. Ni tofauti na makundi ya wanachama wenye msimamo mkali ndani ya chama na wale wenye msimamo wa kati. Hivyo mwandishi wa makala ameshindwa kuyaonyesha wazi makundi ndani ya CHADEMA.

Ruzuku ya sh milioni 66 kwa mwezi, ni kidogo sana kwa shughuli za chama. CCM yenye mabilioni ya ruzuku bado ina matatizo ya fedha kuendesha shughuli zake makao makuu mpaka ipate misaada kutoka ndani na nje ya nchi, iwe CHADEMA yenye sh milioni 66?

Lakini pia si kweli kwamba ruzuku ya CHADEMA inaishia makao makuu.

Kwamba wale walio makao makuu wanajitajirisha kwa kutumia ruzuku? Mwandishi hakutoa majina ya wanaojitajirisha. Bila shaka si mwenyekiti! Si mwanasiasa mwenye njaa. Huyu ni kati ya wazelendo wachache wenye ‘vision’ ya kutoa mchango katika uongozi na maendeleo ya taifa letu.

Kama sikosei, Mbowe anawekeza zaidi kwenye CHADEMA, kuliko anavyovuna. Karibu viongozi wote wa ngazi ya juu ndani ya CHADEMA, wanawekeza zaidi ya wanavyovuna. Kusema wanavuna fedha makao makuu ni kuwakosea haki.

Pia si kweli kwamba helikopta inatumika bila maamuzi na baraka za CHADEMA. Helikopta inaendelea kutumika kufuatana na maamuzi ya mkutano mkuu maalumu wa 2006. Hivyo si kweli kwamba helikopta inatumika kidikteta.

Haya ni maongezi ya vijiweni yasiyokuwa na utafiti, ni maongezi yenye hatari kwa lengo la kuwapotosha Watanzania. Ni maongezi ya kupingwa kwa nguvu zote.

Kwamba fedha za ruzuku zinatumika makao makuu bila kusambazwa kwenye mikoa si kweli. Chaguzi ndogo zinazofanyika za ubunge na udiwani, fedha zinatoka makao makuu. Ofisi ya CHADEMA ya Mkoa wa Mwanza, imelipia pango kwa kushirikiana na makao makuu.

Kwamba Chacha Wange ananyanyaswa na kutengwa na hana ofisi, ninafikiri ni propaganda za kisiasa zenye malengo ya kuichafua CHADEMA.

Kama ningekuwa mhariri wa gazeti la Mtanzania Jumapili, makala ya mzee Yusuf Halimoja ningeipatia kichwa cha habari: Chacha Wangwe ananyanyaswa ndani ya CHADEMA, badala ya kichwa cha habari kilichokuwa kwenye makala tajwa: ‘CHADEMA: Chama cha demokrasia kinachoendeshwa kidikteta.’

Maana shutuma kwamba Chacha Wangwe anabaguliwa, zimechukua sehemu kubwa ya makala. Kabla ya kuandika makala hii nimeuliza juu ya tatizo hili, na kugundua kuwamba ni uzushi mtupu wa kutaka kumchonganisha Chacha Wangwe na viongozi wenzake na hatimaye kuleta vurugu ndani ya CHADEMA.

Tumesikia kwenye vyombo vya habari Chacha Wangwe akilalamika kwamba CCM inamhujumu. Kuvuruga vyama vya siasa vyenye mafanikio ni mbinu kongwe ya Chama Cha Mapinduzi.

Inawezekana CHADEMA ina kasoro. Hata hivyo vyama vyote vya siasa vina kasoro zake. Kama mtu anataka kuzitaja kazoro hizi, basi afanye hivyo kwa uwazi na ukweli, bila kutumia mbinu chafu za kifisadi.

CHADEMA, imesakamwa baada ya wabunge wake kusimama kidete ndani ya Bunge na kufichua ufisadi wa kutisha ulio ndani ya serikali.

Walianza na Mbowe, wakamshikia bango la deni la NSSF, sasa wamegeukia udikteta, na ukabila ndani ya CHADEMA. Haya yote ni kutapatapa, daima penye ukweli uongo hujitenga.
Toka: http://www.freemedia.co.tz/daima/2008/4/13/makala7.php
 
Naomba makada wa Chadema tupeni mwanga juu ya habari ya mzee Halimoja ambaye ni kada wa Chadema.
http://www.newhabari.com/mtanzaniajumapili/habari.php?id=432&section=jarida


Nimerejea jamani


Kwa kadiri ninavyofahamu mimi ni kuwa Mzee Halimoja si kada wa CHADEMA. Alitoka CCM, akaenda CHADEMA akateuliwa kuwa afisa wa kawaida wa mafunzo. Akawa anaandika makala nyingi mtanzania za kueleza kuwa CHADEMA ni chama bora cha kidemokrasia. Wakati wa uchaguzi wa makamu mwenyekiti akatumiwa na Chacha Wangwe katika kampeni. Ni yeye aliyeandika waraka na kuusambaza kwamba CHADEMA kuna ubaguzi, vijana wasomi wanapendelewa na kwamba mwenyekiti Mbowe ana makundi- anawaweka mbele zaidi wakina Zitto, Kitila na Mnyika na kuwaacha wazee. Mtakumbuka katika ile habari ya Dr Slaa na Zitto kunataka kujiuzulu kutokana na uzushi huu, ilisemwa kwamba huyu Mzee alipewa fursa na Mbowe akaalikwa kwenye Kamati Kuu pamoja na kuwa yeye si mjumbe aeleze tuhuma zake. Akashindwa kuzieleza badala yake akawaomba wajumbe waliomtuma ambao ni wa kamati kuu ndio waseme, wajumbe wale wakakaa kimya. Mzee akaonekana mzushi na mzandiki. Akapewa onyo lakini akaendelea na hatimaye sekretariati ikasitisha uteuzi wake kama afisa wa chama. Haya yaliwahi kuelezwa na mzee huyu hakukanusha. Mwanzoni wakati anaanza alikuwa kwenye pay roll ya Malecela na Kinana ambao ni marafiki zake. Baada ya uchaguzi wa CCM na baada ya tuhuma za ufisadi Rostam amemnunua na anamtumia kuandika makala za kuichafua CHADEMA. Mtakumbuka kwamba Rostam aliapa kwamba ataivunja CHADEMA kwa kupandikiza migogoro ya ndani. Na kwa ukaribu wake na Chacha anazua mambo ya uwongo ambayo anayavika sura ya ukweli ili kuweza kutimiza azma yake.

Lakini ukweli ni kuwa-

1. Matumizi ya ruzuku ya milioni 56 ya CHADEMA yanapangwa na Kamati Kuu na Baraza Kuu na ripoti za matumizi(audited) zinapitishwa kila mwaka; na kwa kila kikao kinapokaa huwa mahesabu ya kawaida yanatolewa. Hebu MODS watume link ya lile tamko la CHADEMA la Kamati Kuu na Baraza Kuu walipopitisha matumizi na ripoti ya fedha ya hivi karibuni na kutoa pia kwenye vyombo vya habari. Sasa je, ni lini mahesabu ya milioni 2000 ya CCM au vyama vingine yamewekwa wazi kama inavyofanya CHADEMA? Hata katika uchaguzi mkuu CHADEMA iliweka wazi matumizi yake ya milioni 700+ ikiwemo helikopta milioni 200?(Mzee anasema hela zote zinatumika kwenye helikopta!); na hata ya kiteto tuliwekewa hapa.

2. Eti Chacha ananyimwa ofisi! Kwa mtu yoyote ambaye amewahi kufika pale makao makuu ya CHADEMA atakubaliana kuwa chama kimekuwa na ofisi ndogo tu. Hakukuwa na ofisi hata ya Mwenyekiti taifa. Katibu Mkuu, Naibu Katibu Mkuu, Mwenyekiti nk wote walikuwa wanatumia ofisi moja. Sasa naona wamepanua na wameweka ofisi ya Mwenyekiti na kurugenzi mbalimbali. Sasa Chacha kama Makamu mwenyekiti ni sehemu ya Mwenyekiti na wanaofisi yao, sasa amenyimwa vipi? Ukisoma Katiba ya CHADEMA utakuta maana ya mwenyekiti ni pamoja na Makamu wake, hata Mpango Mkakati wao chama unasema hilo, soma hapa: http://www.chadema.net/mikakati/makao.php

Mzee halimoja naamini anayajua yote haya, ila kwa kuwa ndio kibarua ambacho Rostam amempa tutaona mengi mwaka huu.

3. Kuhusu ruzuku kwenda mikoani na wilayani mbona kabla hata ya CHACHA kugombea tayari suala hili lilishapangwa na ilisemwa kama sehemu ya yale maazimio ya mkutano mkuu wa chama wa 2006? Na kama mujibu wa Dr Slaa tayari ruzuku ilikuwa ikipelekwa? Na hata fedha taslimu zimekuwa zikipelekwa kwa wilaya ambazo zimetimiza masharti? Mimi kwetu Zanzibar tumeshaanza kupata ruzuku toka mwaka jana, tulishatimiza masharti ya kuwa na kamati ya utendaji kamili, kufungua benki akaunti na kurejesha taarifa za fedha. Nilikuwa likizo hivi karibuni na viongozi wetu wamenieleza haya. Sasa nimerejea tena Dar es salaam na najua kule wanaendelea na taribu zingine.

Hebu nipeni basi hoja ya Halimoja ya Kweli ni ipi hasa, ama sivyo tutegemee mengine zaidi ya kizushi toka Habari Corruption, na nasikia Mzee Halimoja karibuni atafanywa mwandishi wa kudumu wa makala kwenye Rostam Aziz International(RAI).

Sasa Mzee kama huyu aliyeandika vitabu vya siasa hapa nchini miaka hiyo ya fort kweusi mnataka kusema hana ya kuundika kuhusu ufisadi wa kina Rostam na Lowassa? But he can not bite the hands that feed him

Asha
 
Asha na Karugendo mmewakata ngebe maana nimeona watu wanaanza kuwaita watu wengine spinners .Ni mbaya sana badala ya kuongelea issue jinsi ilivyo watu wanaanza kuleta ushabiki lakini nadhani Chadema kuweni makini zaidi .Kwa kuweka a clean record na kujibu tuhuma kwa uharaka namna hii .Maana walitgemea Mnyika as he was mentioned here lakini wamekuta JF imejaa wajuaji wa mambo haya .Mtu kweli unaweza kutafuta sababu ya kuzima uozo wa Chama tawala na uharamia kwa wananchi then kasema wewe ni Mtanzania Mzalendo ?

I am shocked kwa kweli

Chadema endeleeni kujibu hoja kwa muda unaotakiwa kila uchafu ukianzishwa ndiyo dawa pekee ya kupambana na Mzee wa hali mbili .
 
Nashukuru woten waliojiutokeza kujibu hoja hizi za kizushi tena kwa vielelezo.

Mzee Halimoja kwa hali ya ajabu kabisa huyu mzee mwenzangu amejikuta akijaribu kupotosha eti kuwa nusu ya wakurugenzi ni wa kabila moja sasa naona padri Karugendo kamjibu kwa vielelezo na ukiangalia kwa umakini ni kuwa katiba ya CHADEMA inasema ni nani ambaye ana jukumu la kumteua wakurugenzi wa CHADEMA .

Sasa hapa ni kuwa hata Kamati kuu ya CHADEMA nusu wamejaa wachagga?

Mbona watu wanakosa hoja sasa wanakuja na mikakati ya kizamani kiasi hicho?

Kuhusu ruzuku kutumika makao makuu hiyo sio kweli kwani kwa mfano ninachokijua mimi ni kuwa wakati huu wa zoezi la kuboresha daftari la wapiga kura CHADEMA wamekuwa wakituma fedha pamoja na nyezo mikoa yopte ambayo zoezi hioli linaendelea.

Pia CHADEMA kimekuwa chama kinachotuma fedha tasilimu kama ruzuku kila mwezi mikoani kwa ajili ya kuendesha chama na haswa wilaya zile ambazo tayari zimetimiza masharti yaliyowekwa na kamati kuu kama vile kuwa na account,kuwa na viongozi kamili, kufanya vikao vya kikatiba, n.k.

Kumbukeni tuu kuwa huu ni mwaka wa uchaguzi ndani ya CHADEMA ,na mwezi ujao naamini ndio habari hizo zitaanza kutoka sana kwani ndio wanaingia ngazi ya tawi hivyo kuwa na mvuto.

Mzee Halimoja anaweza akawa anatumika kuhakikisha kuwa uchaguzi huu unakuwa na "mtu wake " to say that .... ila kuna kila sababu ya kuangalia kila jambo kwa umakini mkubwa na kama mjuavyo siasa za Tanzania mafisadi wamefanikiwa kuhakikisha kuwa ni za kuchafuana na sio za hoja hivyo hata huyu mzee anaweza akawa ametumbukia kwenye mtego huo.

Huyu mzee alikuwa ni afisa wa mafunzo wa CHADEMA kwa zaidi ya miezi sita na ndipo alipofuatiliwa na vyombo vya usalama vya chama akakutwa kuwa kumbe kila wakati alikuwa anaenda kutoa taarifa kwa Kinana na viongozi kadhaa wa CCM.....NISIENDELEE ZAIDI YA HAPO.

naamini kwa wale wote ambao wanataka kujua ukweli wa hili limejibiwa kwa ufasaha na kwa kina na wengine hapo juu hivyo sioni haja wala sababu za msingi kuendeleza ama kama kuna mwenye hoja ya ziada basi hana budi kujitokeza na kuuliza jambo jipya ili aweze kujibiwa hapam kwa kina na ufasaha.

RA na wenzake wanatakiwa kuhakikisha kuwa strategy yao ni ya maana na sio ile ambayo tulijifunza enzi zile ya propaganda nyeusi , nyeupe n.k. dunia ya sasa imebadilika sana sana .
 
Naomba makada wa Chadema tupeni mwanga juu ya habari ya mzee Halimoja ambaye ni kada wa Chadema.
http://www.newhabari.com/mtanzaniaju...section=jarida

Padri Privatus Karugendo

GAZETI la Mtanzania Jumapili la Aprili 6, 2008, lilikuwa na makala iliyoandikwa na mzee Yusuf Halimoja, yenye kichwa cha habari: CHADEMA: Chama cha demokrasia kinachoendeshwa kidikteta.

...

Toka: http://www.freemedia.co.tz/daima/2008/4/13/makala7.php

Dada Asha, kumtetea Mh. Mbowe kwa kunukuu gazeti lake mwenyewe haimsadii mwenyekiti wenu wala Chadema kama chama. Ni bora ungejenga hoja zako mwenyewe au vinginevyo mwachie Mh. Lunyungu ndie anaweza spinning za aina hii.
 

Dada Asha, kumtetea Mh. Mbowe kwa kunukuu gazeti lake mwenyewe haimsadii mwenyekiti wenu wala Chadema kama chama. Ni bora ungejenga hoja zako mwenyewe au vinginevyo mwachie Mh. Lunyungu ndie anaweza spinning za aina hii.

Ina maana wewe unakubali kumpondea Mbowe kwa kutumia magazeti ya Rostam Azizi? Wewe kweli ndiye umekunywa maji ya kijani!
 
GAZETI la Mtanzania Jumapili la Aprili 6, 2008, lilikuwa na makala iliyoandikwa na mzee Yusuf Halimoja, yenye kichwa cha habari: CHADEMA: Chama cha demokrasia kinachoendeshwa kidikteta.
Tukianza na hili la ukabila. Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe, anatoka Machame. Makamu wake wawili; Chacha Wangwe anatoka Tarime na makamu wa pili, Mzee Said Mzee, anatoka Zanzibar.

Katibu Mkuu wa CHADEMA Willibrod Slaa, anatoka Karatu na manaibu wake wawili mmoja Hamad Yusuf Mzee anatoka Zanzibar na mwingine ni Zitto Kabwe, kutoka Kigoma. Je, hapa kuna ukabila gani? Uongozi wa juu umetanda kutoka Zanzibar hadi Kigoma.

Hata hivyo, si kweli kwamba wanatoka kabila moja: Mkurugenzi wa Fedha na Utawala, Anthony Komu, anatoka Moshi, Mkurugenzi wa Habari na Uenezi, Erasto Tumbo, anatoka Shinyanga, Mkurugenzi wa Kampeni na Uchaguzi, Msafiri Mtemelwa anatoka Rufiji, Mkurugenzi wa Vijana, John Mnyika, anatoka Iringa.

Mkurugenzi wa Wanawake, Naomi Kaihula, anatoka Mbeya, Mkurugenzi wa Rasilimali, Susan Lyimo, anatoka Moshi, Mkurugenzi wa Wazee, Victor Kimesera, anatoka Manyara, Mkurugenzi wa Organization, Benson Kigaila, anatoka Dodoma, Mkurugenzi wa Sheria na Katiba, Tundu Lisu, anatoka Singinda, Mkurugenzi wa Mambo ya Nje, ni Zitto Kabwe, anatoka Kigoma, Mkurugenzi wa Bunge na Halmashauri ni John Mrema, anatoka Moshi. Wakurugenzi wanatoka mikoa mbali mbali ya Tanzania. Hapa kuna ukabila gani?

Kwamba kuna makundi mawili ndani ya CHADEMA, kundi la makao makuu na kundi la mikoani, si kweli. Huu ni upotoshaji wa makusidi.

Ruzuku ya sh milioni 66 kwa mwezi, ni kidogo sana kwa shughuli za chama. CCM yenye mabilioni ya ruzuku bado ina matatizo ya fedha kuendesha shughuli zake makao makuu mpaka ipate misaada kutoka ndani na nje ya nchi, iwe CHADEMA yenye sh milioni 66?

Lakini pia si kweli kwamba ruzuku ya CHADEMA inaishia makao makuu.

Kwamba wale walio makao makuu wanajitajirisha kwa kutumia ruzuku? Mwandishi hakutoa majina ya wanaojitajirisha. Bila shaka si mwenyekiti! Si mwanasiasa mwenye njaa. Huyu ni kati ya wazelendo wachache wenye ‘vision' ya kutoa mchango katika uongozi na maendeleo ya taifa letu.

Kama sikosei, Mbowe anawekeza zaidi kwenye CHADEMA, kuliko anavyovuna. Karibu viongozi wote wa ngazi ya juu ndani ya CHADEMA, wanawekeza zaidi ya wanavyovuna. Kusema wanavuna fedha makao makuu ni kuwakosea haki.

Pia si kweli kwamba helikopta inatumika bila maamuzi na baraka za CHADEMA. Helikopta inaendelea kutumika kufuatana na maamuzi ya mkutano mkuu maalumu wa 2006. Hivyo si kweli kwamba helikopta inatumika kidikteta.

Haya ni maongezi ya vijiweni yasiyokuwa na utafiti, ni maongezi yenye hatari kwa lengo la kuwapotosha Watanzania. Ni maongezi ya kupingwa kwa nguvu zote.

Kwamba fedha za ruzuku zinatumika makao makuu bila kusambazwa kwenye mikoa si kweli. Chaguzi ndogo zinazofanyika za ubunge na udiwani, fedha zinatoka makao makuu. Ofisi ya CHADEMA ya Mkoa wa Mwanza, imelipia pango kwa kushirikiana na makao makuu.

Kwamba Chacha Wange ananyanyaswa na kutengwa na hana ofisi, ninafikiri ni propaganda za kisiasa zenye malengo ya kuichafua CHADEMA.

Kama ningekuwa mhariri wa gazeti la Mtanzania Jumapili, makala ya mzee Yusuf Halimoja ningeipatia kichwa cha habari: Chacha Wangwe ananyanyaswa ndani ya CHADEMA, badala ya kichwa cha habari kilichokuwa kwenye makala tajwa: ‘CHADEMA: Chama cha demokrasia kinachoendeshwa kidikteta.'

Maana shutuma kwamba Chacha Wangwe anabaguliwa, zimechukua sehemu kubwa ya makala. Kabla ya kuandika makala hii nimeuliza juu ya tatizo hili, na kugundua kuwamba ni uzushi mtupu wa kutaka kumchonganisha Chacha Wangwe na viongozi wenzake na hatimaye kuleta vurugu ndani ya CHADEMA.

Tumesikia kwenye vyombo vya habari Chacha Wangwe akilalamika kwamba CCM inamhujumu. Kuvuruga vyama vya siasa vyenye mafanikio ni mbinu kongwe ya Chama Cha Mapinduzi.

Inawezekana CHADEMA ina kasoro. Hata hivyo vyama vyote vya siasa vina kasoro zake. Kama mtu anataka kuzitaja kazoro hizi, basi afanye hivyo kwa uwazi na ukweli, bila kutumia mbinu chafu za kifisadi.

CHADEMA, imesakamwa baada ya wabunge wake kusimama kidete ndani ya Bunge na kufichua ufisadi wa kutisha ulio ndani ya serikali.

Walianza na Mbowe, wakamshikia bango la deni la NSSF, sasa wamegeukia udikteta, na ukabila ndani ya CHADEMA. Haya yote ni kutapatapa, daima penye ukweli uongo hujitenga.

Long live Karugendo!

Umewakata ngebe makada wa ccm waliodhani kuna issue hapa kwenye story ya magazeti ya Rostam Azizi. Huyu Rostam anaiharibia ccm kwa hizi propaganda za kipuuzi kuwa Chadema ni chama cha wachaga na inaonekana anataka watu waendelee kuulizia uraia wake.
 
Ndugu wanabiodi,
Mimi sintaliongelea swala hili kwa kuitazama Chadema zaidi ya mwandishi mwenyewe kisha nitarudi ktk kutoa hitimisho langu wapi nakubalaiana na mwandishi..

Kama alivyosema Asha Abdala, huyu mwandishi kazitoa lawama nyingi ambazo binafsi ningependa kama angekuja na mifano hai ambayo imewahi kutokea..haya maneno ya kusema kama ukimpinga mtu fulani utafukuzwa kazi ni dhana ambayo ipo ktk utawala wowote ule, sheria na sera zipo lakini hazifuatwi nchi nzima hii sote tunafahamu lakini haitoshi kama hakuna mfano hai ambao unaweza kujenga ukweli wa hoja hii.

Mwandishi anapozungumzia Ukabila ni muhimu atueleze vizuri huo Ukabila unafanya kazi vipi kwani kutoa ajira kwa mtu wa kabila lako haiwezi kujenga hoja ya Ukabila ikiwa hakuna mifano inayohusu makabila mengine kutengwa...
Swala la helikopta kutumiwa na mwenyekiti ni swala lisilo kuwa na msingi kabisa kwani JK anaitumia ndege ya serikali kwa kila safari zake mbona hakuna mtu aliyewahi kuuliza matuinda yanayotokana na usafiri huo?..Swala kubwa la ndege ya rais ni Ununuzi wake kutoka mfuko wa Taifa baada ya hapo matumizi yake haiwezi kuwa hoja ya msingi hata kidogo unless ndege hiyo iwe inafanya kazi zake binafsi..

Swala la Chacha Wangwe! hata sioni kinachozungumzwa hapa ikiwa matokeo yalikuwa upande wa nguvu ya wananchi tofauti na matakwa ya hao wanaoitwa nguvu ya makao makuu kushindwa, hawakumtoa nje kama alivyofanyiwa Malecela ama Salim kutopewa nafasi kabisa ya kugombea.. Mfano wa Upinzani wa Wangwe unatakiwa kuigwa na Chadmea walipokubali matokeo ni mfano mzuri sana wa kuigwa na vyama vingine.

Kisha mwandishi anatumia lugha nyepesi sana anapoweka madai yanayohusu Chadema kuilaumu CCM kama vile Chadema hakuna Mafisadi!...Kwa msomaji mwenye hekima ataelewa wazi kuwa malengo ya huyu mwandishi yametokana ama yamejengwa na chama kimoja CCM!...Lawama zote alizoziweka hapa zinatendeka CCM, hivyo kwa nini yeye kama mwandishi anayeweza kuiona ufinyu wa madai ya Chadema ktk swala la Ufisadi imekuwaje tena yeye anatumia mifano ya Udikteta kwa Chadema ktk maswala ambayo yanafanyika ndani ya CCM kila siku?..

Kitu kimoja tu ambacho naweza kukisema hapa ni kwamba Vyama vyetu Tanzania vina tatizo moja kubwa na ndio maana demokrasia haiwezi kusimama hata siku moja....

Ninakubaliana sana na mwandishi huyu alipotumia mifano ya dini na madhehebu yake, vyama kama vya Amerika ambavyo vinaweka upinzani ndani ya vyama na Kitaifa kuwa ni mfano bora wa Upinzani ktk fikra endelevu...

Tatizo la Tanzania na sio CCM peke yake ni kwamba kuna Uadui mkubwa kati ya vyama vya Kisiasa.. Uadui ambao umejenga mizizi ndani ya vyama vyenyewe kiasi kwamba ukiwa unapingana na JK, Seif hamad, Freeman Mbowe nje ya sera za chama basi wewe ni mkorofi na hutapewa nafasi...Hii tabia ipo Afrika nzima kiasi kwamba Upinzani una maana ya kujenga chuki baina ya watu iwe ktk vyama ama kitaifa. Tofauti za watu ndizo zinatukuzwa kuliko sera za chama, anayempinga Freeman Mbowe basi Chadema nzima haifai. Mpinzani wa Freeman lazima ajenge chuki kuonyesha udhaifu wa Freeman na pengine chama kizima badala ya kutumia nafasi hiyo kurekebisha mapungufu ya mgombea...

Nimeshangaa sana kuona Chacha Wangwe alipewa nafasi ya Makamu Mwenyekiti dhidi ya matakwa ya vigogo wa Chadema, kwani kila chama kina vigogo wake hata huko Amerika wana vigogo wao. Hutoa mapendekezoi yao isipokuwa kura za wananchi pekee ndizo huwabana.

Kuwa na mapendekezo haikataliwi hata huko Marekani kwenye hao super delegates wana mapendekezo yao ambayo hayajengi Uadui kati ya mgombea na makao makuu kwani mwamuzi wa yote haya sio Makao makuu isipokuwa wananchi wenyewe.

Mwisho nasema mwalimu Nyerere siku zote alikuwa mbele ktk fikra.. aliweza kuona ubora wa sera za Chadema akiwa mwanachama wa CCM.. na hakuona ubaya kutoa maneno hayo!..

Leo hii thubutu kama kuna kiongozi yeyote ndani ya CCM anaweza kusema hayo kama hata pote kesho yake!
 
Majeshi yamekuja kwa kasi kujibu mapigo!

Ulitegemea nini uliposema hiki?

Natumai Mwanakijiji naye atachangia mada hii

Wewe kweli umeishiwa. Unategemea habari shallow kama hii kila mtua aache kufanya kile anachofanya aje kukujibu? na baadhi ya watu wakikujibu unawaita majeshi?

Rudini chuo cha propaganda pale kivukoni mkasomee propaganda au muwaulize wana ccm wengine wazoefu hapa wawafundishe namna ya kuspin. Wewe hujiulizi kwa nini wana ccm vigogo hapa JF wamekaa pembeni kwenye hii mada?

Ukijaribu kuwagawa watanzania kwa ukabila kama unavyojaribu hapa hutafanikiwa. Mlijaribu kwa kukiita CUF chama cha kiislam kumbe ndio mkakipa umaarufu zaidi huko Zanzibar maana huko waislam ni wengi.
 
Back
Top Bottom