CHADEMA na Udikteta Makao Makuu

hapa ni hoja kwa vielelezo hakuna cha majeshi wala nini hapa ni data zinatumika tuu kwani huyu mzee anajua tuu ile propaganda nyeusi sasa atakoma na najua kuwa humu hawezi kuja kama mpo naye muwe mnampelekea japo yaliyojiri humu ili aweze kujua jinsi watu wanavyojua alichopewa ....
 
Nimemkuta huyu mzee leo akiwa Sinza anafanya biashara ya kuuza kalenda kwani jamani huwa hammpi chochote?
 
Nimerejea jamani

Kwa kadiri ninavyofahamu mimi ni kuwa Mzee Halimoja si kada wa CHADEMA. Alitoka CCM, akaenda CHADEMA akateuliwa kuwa afisa wa kawaida wa mafunzo. Akawa anaandika makala nyingi mtanzania za kueleza kuwa CHADEMA ni chama bora cha kidemokrasia. Wakati wa uchaguzi wa makamu mwenyekiti akatumiwa na Chacha Wangwe katika kampeni. Ni yeye aliyeandika waraka na kuusambaza kwamba CHADEMA kuna ubaguzi, vijana wasomi wanapendelewa na kwamba mwenyekiti Mbowe ana makundi- anawaweka mbele zaidi wakina Zitto, Kitila na Mnyika na kuwaacha wazee. Mtakumbuka katika ile habari ya Dr Slaa na Zitto kunataka kujiuzulu kutokana na uzushi huu, ilisemwa kwamba huyu Mzee alipewa fursa na Mbowe akaalikwa kwenye Kamati Kuu pamoja na kuwa yeye si mjumbe aeleze tuhuma zake. Akashindwa kuzieleza badala yake akawaomba wajumbe waliomtuma ambao ni wa kamati kuu ndio waseme, wajumbe wale wakakaa kimya. Mzee akaonekana mzushi na mzandiki. Akapewa onyo lakini akaendelea na hatimaye sekretariati ikasitisha uteuzi wake kama afisa wa chama. Haya yaliwahi kuelezwa na mzee huyu hakukanusha. Mwanzoni wakati anaanza alikuwa kwenye pay roll ya Malecela na Kinana ambao ni marafiki zake. Baada ya uchaguzi wa CCM na baada ya tuhuma za ufisadi Rostam amemnunua na anamtumia kuandika makala za kuichafua CHADEMA. Mtakumbuka kwamba Rostam aliapa kwamba ataivunja CHADEMA kwa kupandikiza migogoro ya ndani. Na kwa ukaribu wake na Chacha anazua mambo ya uwongo ambayo anayavika sura ya ukweli ili kuweza kutimiza azma yake.

Lakini ukweli ni kuwa-

1. Matumizi ya ruzuku ya milioni 56 ya CHADEMA yanapangwa na Kamati Kuu na Baraza Kuu na ripoti za matumizi(audited) zinapitishwa kila mwaka; na kwa kila kikao kinapokaa huwa mahesabu ya kawaida yanatolewa. Hebu MODS watume link ya lile tamko la CHADEMA la Kamati Kuu na Baraza Kuu walipopitisha matumizi na ripoti ya fedha ya hivi karibuni na kutoa pia kwenye vyombo vya habari. Sasa je, ni lini mahesabu ya milioni 2000 ya CCM au vyama vingine yamewekwa wazi kama inavyofanya CHADEMA? Hata katika uchaguzi mkuu CHADEMA iliweka wazi matumizi yake ya milioni 700+ ikiwemo helikopta milioni 200?(Mzee anasema hela zote zinatumika kwenye helikopta!); na hata ya kiteto tuliwekewa hapa.

2. Eti Chacha ananyimwa ofisi! Kwa mtu yoyote ambaye amewahi kufika pale makao makuu ya CHADEMA atakubaliana kuwa chama kimekuwa na ofisi ndogo tu. Hakukuwa na ofisi hata ya Mwenyekiti taifa. Katibu Mkuu, Naibu Katibu Mkuu, Mwenyekiti nk wote walikuwa wanatumia ofisi moja. Sasa naona wamepanua na wameweka ofisi ya Mwenyekiti na kurugenzi mbalimbali. Sasa Chacha kama Makamu mwenyekiti ni sehemu ya Mwenyekiti na wanaofisi yao, sasa amenyimwa vipi? Ukisoma Katiba ya CHADEMA utakuta maana ya mwenyekiti ni pamoja na Makamu wake, hata Mpango Mkakati wao chama unasema hilo, soma hapa: http://www.chadema.net/mikakati/makao.php

Mzee halimoja naamini anayajua yote haya, ila kwa kuwa ndio kibarua ambacho Rostam amempa tutaona mengi mwaka huu.

3. Kuhusu ruzuku kwenda mikoani na wilayani mbona kabla hata ya CHACHA kugombea tayari suala hili lilishapangwa na ilisemwa kama sehemu ya yale maazimio ya mkutano mkuu wa chama wa 2006? Na kama mujibu wa Dr Slaa tayari ruzuku ilikuwa ikipelekwa? Na hata fedha taslimu zimekuwa zikipelekwa kwa wilaya ambazo zimetimiza masharti? Mimi kwetu Zanzibar tumeshaanza kupata ruzuku toka mwaka jana, tulishatimiza masharti ya kuwa na kamati ya utendaji kamili, kufungua benki akaunti na kurejesha taarifa za fedha. Nilikuwa likizo hivi karibuni na viongozi wetu wamenieleza haya. Sasa nimerejea tena Dar es salaam na najua kule wanaendelea na taribu zingine.

Hebu nipeni basi hoja ya Halimoja ya Kweli ni ipi hasa, ama sivyo tutegemee mengine zaidi ya kizushi toka Habari Corruption, na nasikia Mzee Halimoja karibuni atafanywa mwandishi wa kudumu wa makala kwenye Rostam Aziz International(RAI).

Sasa Mzee kama huyu aliyeandika vitabu vya siasa hapa nchini miaka hiyo ya fort kweusi mnataka kusema hana ya kuundika kuhusu ufisadi wa kina Rostam na Lowassa? But he can not bite the hands that feed him

Asha

huyo aliyeandika hii habari ametumia akili yake kureflect yale yanayotokea ndani ya chadema ! Mbaya zaidi mnamuongelea aliyeandika hii habari badala ya habari yenyewe ! ama kweli kichwa cha mbuzi ni kichwa cha mbuzi tu siku zote !
 
Dada Asha, kumtetea Mh. Mbowe kwa kunukuu gazeti lake mwenyewe haimsadii mwenyekiti wenu wala Chadema kama chama. Ni bora ungejenga hoja zako mwenyewe au vinginevyo mwachie Mh. Lunyungu ndie anaweza spinning za aina hii.

huyo asha anatakiwa aangalie context na sio aliyetoa hoja, hadi hivi sasa hajakubali wala kukataa kama ni kweli. huyu lunyungu amezidi nae kupotosha na wakati wake wa kutolewa uvivu upo njiani ! you can quote me on that one !
 
Taifa linazama; Kama kweli mpaka leo 2008; Chama chetu kitakatifu cha Upinzani bado kinahitaji kujisafisha chenyewe; bado ndani hawajiamini kwa kweli Taifa lina safari ndefu sana ya maendeleo!!!

Kwa vyovyote vile hizo hoja zinatoka ndani ya CHADEMA yenyewe... hii ni hatari kwa Taifa letu... lini litakuwa na Upinzani ule aliousifia/alioutabiri Kambarage?

Tutajidanganya kujibizana hapa kishaghala baghala lakini tatizo halijatatuliwa... na kwa kweli rasilimali za CHADEMA hazijaonekana vijijini bado... muda unaenda waheshimiwa wapenda maendeleo
 
Dada Asha, kumtetea Mh. Mbowe kwa kunukuu gazeti lake mwenyewe haimsadii mwenyekiti wenu wala Chadema kama chama. Ni bora ungejenga hoja zako mwenyewe au vinginevyo mwachie Mh. Lunyungu ndie anaweza spinning za aina hii.

Kakalende unapaswa kuniomba msamaha sana kwa kuniita spinner .Ila nakushangaa sana kusema gazeti la mbowe linajibu mapigo kwani Mbowe ndiye kaandika ? Katika historia ya wafanya biashara Tanzania na hasa media Mbowe hata Balile anaweza kumtetea huwa haulizi leo mmeandika nini ili abadilishe yeye kesha achana na haya .Karugendo anakaa Mwanza tena si Mwanza tu anakaa kijijini na akitaka kuandika nan kutuma anakuja Mwanza mjini .Au u nataka kusema anatumiwa kuandika kumsifu Mbowe ? Ama kweli ni mufilisi soon utaishiwa hata uwezo wa kufikiri.
 
Kada Mpinzani,
Hizo content ni zipi haswa?..Huyu mwandishi anasifia sana kuwepo kwa makundi ndani ya chama na haelewi kwa nini CCM wanapinga akieleza mazuri ya uwakilishi wa mbinu tofauti ktk chama ili kufikia malengo yaliyotarajiwa.. Huyu huyu tena anaiponda Chadema inayojitokeza kuwa na makundi ya watu wanaotaofautiana mbinu ndani ya chama akivuta Uadui kati ya viongozi wa ndani. Hoja iliyotangulia kuwa objective kaiweka madongo upande wa pili hali mtu huyu Chacha Wangwe anayezungumziwa anatumikia wadhifa wake kama mwenyekiti msaidizi wa chama ana anatambuliwa na hao watu wa Makao makuu..

Bila kupoteza muda sio lazima chama kizima kiunge mkono mbinu za kiongozi mmoja anapochukua jukumu lake binafsi kutangaza ama kusema maoni yake kama alivyofanya ktk swala la mgogoro wa Kenya..Na ikiwa kuna kiongozi ama viongozi toka maakao makuu wanatofautiana na wale wa mikoani ningependa sana kuelewa kitu kimoja... Makao makuu ni wapi na mikoani ni wapi?..
Pengine haya matatizo yanatokana na ushindani wa madaraka ndani ya chama toka mkoa mmoja au mtu mmoja!..Nina hakika kwamba tatizo kubwa la mwafrioka ni ile TITLE, siku zote tunagombea kiti kwa sababu tunataka kuitwa Mheshimiwa, Mwenyekiti, katibu na kadhalika hali sii lazima uwe ktk nafasi hizo kuweza kupanda ngazi.. Tumewaona kina Obama, Mama Clinton na wengine wote ambao wamefikia hatua za mwisho za kuchaguliwa kuwa marais bila kushika nafasi za juu ndani ya chama.
Mkuu haya ni mawazo finyu sana kukitazama chama na uendeshaji wake wa ndani kama kielelezo cha Taifa zima. Huyu mzee hana tofauti kabisa na wale wazee wa Kariakoo wanaotazama nyumba za jirani wanakula nini? ama kama kwao wamekula sembe la mlenda basi matusi yote yatapelekwa mtaani kuwa ni mateso ya wazazi..Yeye kaleta kitu gani ndani ya chama!.. hakuna zaidi ya majungu..
 
Taifa linazama; Kama kweli mpaka leo 2008; Chama chetu kitakatifu cha Upinzani bado kinahitaji kujisafisha chenyewe; bado ndani hawajiamini kwa kweli Taifa lina safari ndefu sana ya maendeleo!!!

Kwa vyovyote vile hizo hoja zinatoka ndani ya CHADEMA yenyewe... hii ni hatari kwa Taifa letu... lini litakuwa na Upinzani ule aliousifia/alioutabiri Kambarage?

Tutajidanganya kujibizana hapa kishaghala baghala lakini tatizo halijatatuliwa... na kwa kweli rasilimali za CHADEMA hazijaonekana vijijini bado... muda unaenda waheshimiwa wapenda maendeleo

Kasheshe it is only CCM will tae ages kujibu tuhuma za Kichama ama mtu mmoja mmoja kulingana na uozo walio nao .Muda wote CCM hawajibu hoja na sasa wanatumia media kufanya damaging .Spinning yangu iko wapi ?Kama sina data siwezi kuandika that is me .Nikijua na nikapata ushahidi naandika na ndiyo mimi.Siandiki kama Kanda ama wengine kwa kutimiza neno la mkono wa mjinga huandika kokote no .Siandiki kwa kuwa nina access na net no .Naandika nikiwa najua cha kuandika na si kupoteza muda .Mada kibao huwa nikiwa sina cha kusema napita na huwezi kukuta nimeandika kila mada hapana .Ila nyie ambao haya kuweka hoja hamuweki ila ushabiki mnaumia.Leo Chadema wanakuja na nondo mnasema majeshi .What a shame ? Mlitegemea nini ? Kwamba mlete umbeya na uzandik watu wakae kimya ? Endeleeni kupambana na hali halisi .Mzee Chama alifukuzwa , kama Balile yuko kwenye payroll .Kada una akili mbovu kaka .baada ya maelezo yote haya bado unasema wakubali ama wakatae ? Utatia akili mwenyewe rudi usome uelewe .The writer anakuwa attacked ili aje in public domain atetee maandiko yake.Najua anapita hapa kila siku anaweza kusema ama akupe desa uje nalo hapa .Wacha habari za Ukarume kenge hapa .
 
LUNYUNGU, you are now officially crowned as a spinner and a whinner (sp.)!! Good to have you here, now take your crown !
 
LUNYUNGU, you are now officially crowned as a spinner and a whinner (sp.)!! Good to have you here, now take your crown !

Nilidhani umechangia hoja kumbe unaendeleza yale yale ambayo wamekuzoea wengi wetu hapa ? Lini utakuja na hoja bila ushabiki na hoja ya faida ua jamii na Nchi yangu Tanzania ?
 
nusura niijibu hii hoja lakini wakati mwingine mtoto usimcheke mzee wako akikaa uchi; ningeifumua hiyo hoja ya huyo mzee na kuiacha iwe na matundu kama nguo ya kaniki.. but then ningeitwa Chadema!
 
Nilidhani umechangia hoja kumbe unaendeleza yale yale ambayo wamekuzoea wengi wetu hapa ? Lini utakuja na hoja bila ushabiki na hoja ya faida ua jamii na Nchi yangu Tanzania ?

you can take the crown home spinner!
picture me tomorrow and the thread that will be brought by Kada !
 
Mimi nilifikiri kuna madai mapya ? Haya ya ukabila mbona yamesha ongelewa sana hapa .Matumizi ya mchine kila siku yanasemwa .Kwa ni ni wabunge wametoka upande mmoja ni sababu ya wazi kabisa na zimesha semwa .Labda kw auchache kama pesa kutofika mikaoni hili laweza kuwa jambo lakini mengine mwandishi yuko katika kampeni ambazo zilisha feli kabla ya kuanza .Ukabila Chadema wala mie siuoni labda kwa kuwa mimi si mwenzao .

Mkuu Lun,
Ingawa hii article inaelekea kwenye kumpamba Lungwi, bila kuonyesha mapungufu yake, lakini nafikiri inafunua maswali muhimu ambayo wote, CHADEMA na nonCHADEMA, wanahitaji kujibiwa.
  1. Suala la ruzuku kutofika mikoani ni rahisi sana kwa CHADEMA kuliondolea kelele kwa kuchapisha mahesabu yao. Hii sio tu kuwa itaondoa kusingiziana, bali pia itawatofautisha na vyama vingine, hasa CCM, kwa kuonyesha kuwa sera ya uwazi na ukweli ni CHADMA kiukwelikwli na sio Mkapa.
  2. Ukabila nao ni kati ya mambo mengi yanayowafanya watu wengi hasa wasomi wasijiunge na CHADEMA. Hii iko wazi tokea enzi za mzee Mtei. Kwa mfano, kama 50% ya wabunge wake wote wanatokea Kilimanjaro, mmoja tu akiwa amechaguliwa, karibu 70% ya wa kuteuliwa ni wa Kilimanjaro, 25% ya wanaSecretariati ni wa Kilimajaro. Hii sidhani ni coincedence. Hawa ni kati tu ya wale waliowekwa wazi kwenye www.chadema.net. Sio ajabu kuna zaidi lakini hatuwezi kufahamu. Kwa hiyo ni muhimu kwa WanaCHADEMA wote, na wasio, kuyaongelea haya yote kwa uwazi na CHADEMA kuyatafutia ufumbuzi, bila kuficha, maana ni chama pekee hivi sasa kinachotegemewa siku moja kuchukua nafasi ya CCM.
Kwa hiyo ni kuwa hata kama Freeman au mtu mwingine yeyote atakuwa anachangia kwa kiasi kikubwa chamani kuliko wengine, hapatakuwa na Demokrasia kama atajaza watu wake na chama kukosa sura ya kitaifa.
 
Kwa argument yako hii, naona tunarudi palepale kwenye ile thread nilianzisha hapa kuwa CCM ni chama cha kiislam kwa vile 75% ya viongozi wa juu wa ccm, wajumbe wa CC na NEC ni waslam?

Hii formula yako hapa inaweza kutumiwa vyovyote vile na kutafsiri CCM na kuigeuza kuwa CCK (Chama Cha Kiislam) maana inaonekana unasahau kuwa halmashauri ya Tarime inaongozwa na Chadema (labda watu wa Tarime nao ni wachaga)!
 
Bw. Mgaya,
Nafikiri ni vema kutoifanya hii hoja kuwa ni ya CCM vs CHADEMA, bali iwe a fair analysis ya yasiyopendeza ndani ya CHADEMA kwani huenda kikawa chama chenye mguso kwa taifa zima kama hayo yasemwayo yakirekebishwa.

CCM ni grand party ambayo kwa wakati fulani kila mtu alikuwa mwanachama by default, kwa hiyo ni vigumu kuishutumu kuwa ina misingi ya udini n.k., hata kama takwimu ulizoweka ni sahihi, bado ni rahisi kwa CCM kujitetea kwa sababu ya historia yake. Hii ni tofauti kwa CHADEMA. Pia, hata kama CCM ina 75% ya viongozi wa juu wakiwa wa dini moja, hii haihalalishi CHADEMA nao kuwa na mfumo wenye sura ya kikabila.
 
Mkuu Lun,
Ingawa hii article inaelekea kwenye kumpamba Lungwi, bila kuonyesha mapungufu yake, lakini nafikiri inafunua maswali muhimu ambayo wote, CHADEMA na nonCHADEMA, wanahitaji kujibiwa.
  1. Suala la ruzuku kutofika mikoani ni rahisi sana kwa CHADEMA kuliondolea kelele kwa kuchapisha mahesabu yao. Hii sio tu kuwa itaondoa kusingiziana, bali pia itawatofautisha na vyama vingine, hasa CCM, kwa kuonyesha kuwa sera ya uwazi na ukweli ni CHADMA kiukwelikwli na sio Mkapa.
  2. Ukabila nao ni kati ya mambo mengi yanayowafanya watu wengi hasa wasomi wasijiunge na CHADEMA. Hii iko wazi tokea enzi za mzee Mtei. Kwa mfano, kama 50% ya wabunge wake wote wanatokea Kilimanjaro, mmoja tu akiwa amechaguliwa, karibu 70% ya wa kuteuliwa ni wa Kilimanjaro, 25% ya wanaSecretariati ni wa Kilimajaro. Hii sidhani ni coincedence. Hawa ni kati tu ya wale waliowekwa wazi kwenye www.chadema.net. Sio ajabu kuna zaidi lakini hatuwezi kufahamu. Kwa hiyo ni muhimu kwa WanaCHADEMA wote, na wasio, kuyaongelea haya yote kwa uwazi na CHADEMA kuyatafutia ufumbuzi, bila kuficha, maana ni chama pekee hivi sasa kinachotegemewa siku moja kuchukua nafasi ya CCM.
Kwa hiyo ni kuwa hata kama Freeman au mtu mwingine yeyote atakuwa anachangia kwa kiasi kikubwa chamani kuliko wengine, hapatakuwa na Demokrasia kama atajaza watu wake na chama kukosa sura ya kitaifa.

Kubwajinga

1. Matangazo ya gazetini pekee ya mwaka mmoja hayatoshi kuweka sura ya ruzuku kusambazwa kwa kuwa hayawezi kutaja orodha ya wilaya zote zilizopokea ruzuku. Si unajua kwamba huwa zinachapwa audited statements ambazo ni summary? Sheria ya vyama vya siasa inasema msajili anawajibu wa kuchapa mahesabu ya vyama. Sasa kamuulize msajili kwa nini hachapi wakati CHADEMA inampelekea kila wakati? CHADEMA wakati wote inaweka wazi matumizi yake kwa wanachama kupitia vikao ikiwemo kiasi kilichosambazwa na jina la eneo. Mimi ya kwetu niliyapata Zanzibar. Lakini baada ya baraza kuu unakumbuka Tamko la CHADEMA lilionyesha kwamba wajumbe walijadili na kupitisha ripoti ya fedha ikiwemo mgawanyo wa ruzuku?

2. Hilo la Uchagga wa sekretariati acha kuwasingizia. Mbona iliwahi kusemwa hapa kwamba Wasukuma ni wengi kuliko wachagga? Kama wasukuma ni zaidi ya 30% katika makao makuu ya CHADEMA kwanini unawataja wachagga tu wakati mwenyewe umesema ni 25&, au unafanya spinning? Na ni kiongozi gani wa sekretariati au mbunge ambaye amechaguliwa kwa shinikizo la Freeman kutokana na mchango wake ambao amechangia chama yeye kama Freeman?

Hebu Mods tuleteeni tena hapa tamko la CHADEMA walilolitoa kujibu suala la Uchagga, au tupe link ambapo suala hili lilishajadiliwa na kujibiwa na Zitto, Mnyika, Kitila na wengineo.

Wallah napata uchungu haya mambo kurudiwa rudiwa ili hali yalishajibiwa mpaka makada wa CCM wakasalimu amri wakati huo

Asha
 
Bw. Mgaya,
Nafikiri ni vema kutoifanya hii hoja kuwa ni ya CCM vs CHADEMA, bali iwe a fair analysis ya yasiyopendeza ndani ya CHADEMA kwani huenda kikawa chama chenye mguso kwa taifa zima kama hayo yasemwayo yakirekebishwa.

CCM ni grand party ambayo kwa wakati fulani kila mtu alikuwa mwanachama by default, kwa hiyo ni vigumu kuishutumu kuwa ina misingi ya udini n.k., hata kama takwimu ulizoweka ni sahihi, bado ni rahisi kwa CCM kujitetea kwa sababu ya historia yake. Hii ni tofauti kwa CHADEMA. Pia, hata kama CCM ina 75% ya viongozi wa juu wakiwa wa dini moja, hii haihalalishi CHADEMA nao kuwa na mfumo wenye sura ya kikabila.

Historia ipi hiyo ya CHADEMA inaonyesha kuwa ni chama chama cha wachagga? Hebu soma historia ya CHADEMA kwenye tovuti uone jinsi toka wakati chama kinaanzishwa Mzee Mtei pamoja na kuwa alikuwa mchagga lakini alijenga misingi ya chama chenye sura ya kitaifa.

Ama utakumbuka mchangiaji mmoja humu Paparazi Muwazi aliweka hii habari hapa. Ambayo hakika nimeihifadhi katika kumbukumbu zangu- hii nadhani itakupa majibu kwa maswali yao:

MNYIKA: CHADEMA SI CHAMA CHA WACHAGA
• Asema wachaga wako mpaka serikalini
• Atoa rai kwa watanzania kuwakanya wanachochea ukabila

Na Mwandishi wetu

Mkurugenzi wa Vijana wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA), John Mnyika ameibuka na kuzungumzia tuhuma kwamba chama hicho ni cha wachaga. Mnyika ambaye katika uchaguzi uliopita alikuwa mgombea wa Ubunge katika jimbo la Ubungo mkoani Dar es salaam amezungumzia suala hili kutokana na hivi karibuni kujitokeza kwa wanachama wanaojitoa katika kambi ya upinzani na kuingia Chama cha Mapinduzi(CCM) ambao pamoja na mambo mengine kutoa shutuma kwamba CHADEMA ni chama cha wachaga.

Hivi karibuni, magazeti kadhaa ya kila siku(si gazeti hili) yamemnukuu aliyekuwa kiongozi wa chama cha wananchi CUF akiwa amezunguka vyama vya UMD, UDP, NCCR-Mageuzi, CHADEMA , na kuanzisha chama cha ULIMO bila mafanikio,Aman Nzugile Jidulamabambasi( maarufu kama Jidula ama Jidu), alirejea CCM, akitokea chama cha wananchi CUF ambapo alikuwa mgombea ubunge huku akitoa shutuma za hali ya juu kuhusu Chama Cha Demokrasia na Maendeleo-CHADEMA wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa idara ya habari(MAELEZO).

Itakumbukwa kuwa baada ya kurejea CCM, Jidulamabambasi alidai na kunukuliwa na vyombo mbalimbali vya habari kuwa vyama vya upinzani havina mwelekeo na kwamba vinaubaguzi , huku akisisitiza kuwa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), ni chama cha kikabila na kwamba kimejaa wachagga na kuongeza kuwa CHADEMA kilianzishwa kabla ya uhuru kwa maslahi ya wachagga ambapo kilikuwa na jina la Chagga Development Manifesto(CHADEMA).

"Kwa hulka na tabia ya Jidula tunayemfahamu, tunaamini kuwa maneno haya hata yeye mwenyewe anaamini si ya kweli na pengine alishinikizwa na CCM aseme hivyo kwani propaganda za namna hii zimekuwa zikitumiwa na CCM kwa muda mrefu dhidi ya CHADEMA, amesema Mnyika.

Aidha Mnyika alisisitiza, "Na kwa mtu kama Jidula mwenye hulka ya kutafuta uongozi kwa udi na uvumba, sio ajabu kutamka maneno ambayo hata mwenyewe ama hayaamini au hayajui. Kwa hiyo namtaka Jidula athibitishe kauli yake kuwa CHADEMA ni chama cha wachagga kilichikuwepo kabla ya uhuru wa Tanganyika, kwa upande mmoja. Lakini pia kupinga kauli hiyo ya upotoshaji ya Jidula kwa upande wa pili".

Akizumgumzia shutuma kwamba CHADEMA ni chama si siasa kilichoanzishwa kabla ya uhuru kikiitwa Chaga Development Manifesto Mnyika alisema " kwa mtanzania yeyote mwenye ufahamu wa historia walau ya kiwango cha shule ya msingi, atakubaliana nasi kuwa katika orodha ya vyama vya siasa vilivyokuwepo kabla ya uhuru, hakuna chama kilichoitwa CHADEMA"

Kwa msomi wa kiwango cha Jidula kushindwa kung'amua vitu vidogo kama hivi, kunazua maswali mengi kuliko majibu hasa kuhusu uhalali na usahihi wa elimu yake kwa upande mmoja kama ni kweli amepotosha kwa kutojua. Lakini pia kunazua maswali kuhusu kiwango cha uzalendo wa Jidula anapokuwa anatafuta nafasi ya uongozi kama kweli alikuwa anajua lakini ameamua kuupotosha umma wa watanzania kwa malengo yake ya kisiasa katika chama hicho.

Kwa upande mwingine akijibu shutuma ya kwamba CHADEMA imejaa wa wachaga, Mnyika, "Pengine hatuna hakika na uwezo wa Jidula wa lugha ya kiswahili, labda pengine anatumia maneno asiyoyajua maana yake. Kwa mfano Jidulla anaposema CHADEMA imejaa wachagga maana yake nini?. Kwa akili za kawaida, maana yake ni kwamba CHADEMA ina viongozi na wanachama wengi wachagga kuliko kabila lolote hapa Tanzania. Kama Jidula alikuwa na ujumbe huo!, Je ni kwa kiasi gani kauli hiyo ina ukweli?"

Akitoa takwimu kuhusu idadi ya wachaga katika CHADEMA Mnyika ameweka wazi kuwa, "Katika safu ya juu ya uongozi wa kitaifa wa CHADEMA yenye viongozi sita: wenyeviti na makatibu mchaga ni mmoja tu-Mwenyekiti wa chama Taifa, Freeman Mbowe. Wazanzibari ni wengi zaidi kati ya hao viongozi sita. Kwa nini Jidula hakusema kwamba CHADEMA ni chama ambacho kimejaa wazanzibari?

Aidha katika sekretariati ya chama taifa ambacho ndio chombo kinachosimamia utekelezaji wa kila siku wa shughuli za chama kikiwa na kurugenzi 9, kati ya wakurugenzi wake mchaga ni mmoja tu. Na wasukuma kabila la Jidula ni watatu?. Kwa nini Jidula hakusema kwamba CHADEMA ni chama cha wasukuma?

Kadhalika mpaka sasa Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe ameteua wajumbe wanne wa kamati kuu, kati yao hakuna na mchaga hata mmoja na kati yao wawili ni wahaya, Profesa Mwesiga Baregu na Balozi Ngaiza. Kwa nini hakusema kwamba CHADEMA ni chama cha wahaya?

Kwa upande mwingine kwa mujibu wa matokeo ya uchaguzi uliopita, jimbo ambalo CHADEMA iliongoza kwa uwingi mkubwa zaidi wa kura ni Tarime ikiwa asilimia zaidi ya 64. Kama CHADEMA ni chama cha wachaga kwa nini jimbo la kwanza lisingekuwa la mkoa wa Kilimanjaro? Kati ya majimbo kumi ambayo CHADEMA ilifanya vizuri zaidi, jimbo la Kilimanjaro ni moja tu la Moshi mjini huku mikoa kama Kigoma, Rukwa ikiwa na majimbo mawili ambayo CHADEMA imefanya vizuri zaidi. Kama CHADEMA ingekuwa chama cha wachaga si ingefanya vizuri zaidi katika majimbo ya Kilimanjaro? Je, Jidula anataka kutuambia kuwa Mara, Kigoma, Rukwa na mikoa mingine ambayo CHADEMA imefanya vizuri kote kumejaa wachaga?

Kwa mantiki hiyo basi, si kweli kwamba CHADEMA ni chama kilichojaa wachaga. CHADEMA ni chama cha kitaifa. Kinachojumuisha wanachama na wapenzi wa asili na hali mbalimbali.

Zaidi ya hayo namshangaa Jidula akitoa hoja kwamba CHADEMA imejaa wachaga. Lakini namshangaa zaidi Jidula kwa kuwa hatukumsikia akisema chochote pale Rais Kikwete alipoteua wachaga wengi zaidi katika baraza la mawaziri. Je, kwa mantiki ya Jidula serikali ya Kikwete ni ya wachaga? Je, kwa kuwa wachaga ndio kabila lenye wabunge wengi zaidi kati ya wabunge wa viti maalumu wa CCM na CHADEMA, Je kwa kigezo hiki tu tuseme kwamba CCM na CHADEMA ni vyama vya wachaga? Je, kwa CCM kuwa na wabunge wa viti maalum wachaga hata katika mikoa mingine ya nchi yetu zaidi ya Kilimanjaro wanapotoka wachaga je, kwa uchambuzi wa mtu kama Jidula anaweza kusema kwamba CCM ni chama cha wachaga?

Nimeamua kujibu shutuma hizo kwa sababu suala la ukabila ni nyeti sana kwa mustakabali wa nchi yetu. Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere aliwahi kuasa kwamba kufanya dhambi ya ubaguzi ni kama kula nyama ya mtu, ukianza huwezi kuacha. Naamini kauli za watu kama Jidula zinapandikiza mbegu ya ubaguzi miongoni mwa watanzania na kuwashawishi watu kutazamana kwa misingi ya makabila yao. Tukiwaruhusu watu kama hawa tutaweka mashakani mshikamano na amani yetu hapa nchini.

Mwalimu Nyerere aliwahi tena kusema kwamba katika kutafuta uongozi kuna watu wanaweza kutumia vigezo vya kijinga kama udini na ukabila kujihalalisha ili kufikia malengo yao na ndivyo wanavyofanya watu jamii ya Jidula.
 
Bw. Mgaya,
Nafikiri ni vema kutoifanya hii hoja kuwa ni ya CCM vs CHADEMA, bali iwe a fair analysis ya yasiyopendeza ndani ya CHADEMA kwani huenda kikawa chama chenye mguso kwa taifa zima kama hayo yasemwayo yakirekebishwa.

CCM ni grand party ambayo kwa wakati fulani kila mtu alikuwa mwanachama by default, kwa hiyo ni vigumu kuishutumu kuwa ina misingi ya udini n.k., hata kama takwimu ulizoweka ni sahihi, bado ni rahisi kwa CCM kujitetea kwa sababu ya historia yake. Hii ni tofauti kwa CHADEMA. Pia, hata kama CCM ina 75% ya viongozi wa juu wakiwa wa dini moja, hii haihalalishi CHADEMA nao kuwa na mfumo wenye sura ya kikabila.

Jamani kuna mtu mwenye ile makala ya Mzee Mtei aliyoandika "CHADEMA ni nini, CHADEMA ni nani?" ambapo aliweka wazi historia ya kuanzishwa kwa CHADEMA na wakina nani alianzisha nao na katika maeneo gani? Iliwahi kuwekwa hapa JF na kati ya Zitto au Mnyika; hebu toeni link basi

Asha
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom