CHADEMA, Ludovick Rwezahula anaangamia mahabusu, utu uko wapi?

Status
Not open for further replies.
Mkuu, unataka kusema muda wote huo bado tu hajajua kuwa kijana yuko mahabusu, tena amekongoroka vibaya! CHADEMA imuangalie jamani, kiubinadamu tu.

Mwenye uchungu sana azae!!kama kweli unamuonea huruma kamuwekee dhamana wewe!!hatuwezi kulea wasaliti na wanafiki kwa kulipwa vipande vya fedha 50000 na mwigulu chemba aka savimbi...laana yake itamtafuna hapahapa duniani.
 
sisi vjana wala hatujakata tamaa kuwa wafuasi wa cdm.nyie wa uvwxyz ndo mmkata tamaa.Ludo anazidi kutufundsha usaliti wa harakat za mageuz usivo na faida.sisi vjana wa cdm tuna morali na hali nzuri kuendelea kukitumikia chama.HATUTUMIWI TUNAJITUMA .
 
hapa naona udhaifu mkubwa sana kufanywa na kiongozi wa juu wa taasisi.
hivi katika 'mpango nyeti' kama huu aliwezaje kumtumia mtekelezaji pesa kwa simu yake bila kushtuka kuwa itajulikana kirahisi na kurahisisha ushahidi!?

Sio uzembe ni Mungu ndo aliamua kumuumbua kwa kumziba ufahamu! Kama alivowagonganisha lugha wajenzi wa mnara wa Babeli
 
Mkuu, unataka kusema muda wote huo bado tu hajajua kuwa kijana yuko mahabusu, tena amekongoroka vibaya! CHADEMA imuangalie jamani, kiubinadamu tu.

Kwa ile 50 elfu aongezee kidogo atapata dhamana!
 
HAMY-D

Nadhani huelewi unachokisema la sivyo usingeandika PUMBA hizi. Au na wewe ni gaidi?

Ludovick ndiye haswa aliyetumwa kufanya kazi ya kijasusi na hao waliomtuma. Alikuwa pandikizi la usaliti. Lengo lake lilikuwa kujiweka karibu na watendaji wakuu wa CHADEMA na kisha kuweka ushahidi bandia ambao ungeonesha kwamba viongozi hao walikuwa watu hatari. Alijaribu kwa Zitto na Dr. Slaa. Wakamshtukia. Waliomtuma walipoona hali haiendi wakaamua kutengeneza ushahidi wa kukurupuka ambao walimtumia huyo huyo Ludovick. Aliifanya kazi hiyo huku akijua kwamba mambo yakienda Kusini, hakuna yeyote kati ya wale ambao walimtuma wangekuja kumwokoa. Hili alilijua tangu mwanzo tangu alipoingia kwenye mkataba huu wa kifisadi wa kuipaka matope CHADEMA. Mashirika YOTE ya kijasusi duniani - YOTE - huwaambia waajiriwa wao kwamba wakikamatwa wakiwa kazini hakuna ambaye angekuja kuwaokoa. Ludovick aliijua tahadhari ambayo alipaswa kuichukua.

Leo analia ndugu zake hawafuatilii dhamana yake. Ameitia doa familia yake. Hata kama angekuwa ndugu yangu wa kiachiana ziwa, singemdhamini na ningewakataza ndugu zangu wengine kufanya hivyo.

Na hao waliomtuma hawawezi kujitokeza hadharani kumuokoa kwani kufanya hivyo KUTATHIBITISHA hoja ambayo imekuwa ikitajwa na CHADEMA kwamba wamekuwa wakipakwa matope kupitia viongozi wake kubambikizwa kesi badia za ugaidi.

Hao waliomtuma (nachelea kuwataja nisijeulizwa mahakamani iwapo nina ushahidi) KAMWE hawawezi kumdhamini.

Ndio, tunajua kwamba kila anayekosa anastahili huruma na msamaha, lakini hili la kumsababishia mtu asiye na hata chembe ya hatia awekwe ndani kwa kosa kubwa kama hilo la ugaidi, tena akiwa mgonjwa (Lwakatare ni mgonjwa wa kisukari) ni sawa na UHAINI. Siwezi kumsemea mwokozi wetu Yesu Kristo, lakini kwenye kosa hili, kama Kristo angerudi leo, Ludovick angejikuta akifunguliwa milango ya Jehanam, akiwa amefungwa minyororo mwili mzima, akilakiwa na Lusifer huku akichekelea meno yote nje.

Ludovick, umevuna ulichopanda!
 
Last edited by a moderator:
WanaJF!

Leo ni siku ya kesi ya bwana Lwakatare kusikilizwa kwenye mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, lakini kesi imehairishwa mpaka July 22, 2013.

Pamoja na hayo, mshitakiwa na.2 bwana Ludovick Rwezahula ameshindwa kupata dhamana kwa sababu ya kutokamilika kwa nyaraka za dhamana, ingawa dhamana yake iko wazi kabisa.

Bwana Ludovick akiwa nje ya mahakama, ameonekana akiwa mnyonge na alikuwa akilia sana kwa uchungu huku akilalamika ndugu zake (ambao hawakufika mahakamani) hawafatilii dhamana yake.

Kwa hali kama hiyo, kijana Ludovick anaendelea kusota gerezani na kuzidi kuangamia, kwani wote sisi ni wanaadamu na tunajua makali ya maisha ya gerezani.

Rai yangu kwa CHADEMA; haijarishi kijana Ludovick kama alikuwa mwajiriwa wa CHADEMA kimkataba ama alikuwa volunteer, jambo la msingi ni kwamba alikuwa ana kitumikia CHADEMA kwa moyo wake wote na nguvu zake zote. Ludovick alijitoa kwa CHADEMA kwa namna ya pekee, ni kijana ambae alikuwa bega kwa bega na Dr Slaa kiutendaji na vile vile alikuwa kama mtoto kwa Dr Slaa.

Katika hali kama hiyo sikutarajia kama CHADEMA kinaweza kumtema na kumkataa kabisa bwana Ludovick Rwezaura. Kwani wote tunafahamu kuwa, kosa aliadhibiwi kwa ubaya, bali kosa dawa yake kukosolewa. Sasa kwanini CHADEMA wana muadhibu kijana Ludovick kwa ubaya? kwanini wasimsaidie hata kwa dhamana ili aweze kutoka kwenye 'jehanamu' ya duniani?

Maamuzi haya ya kumtupa mkono kijana Ludovick katika hali hii mbaya inayo mkabili, inajenga wasiwasi mkubwa kwa vijana wengi walio CHADEMA juu ya hatma yao endapo wakikosea jambo. Je, chama kitawasaidia kwa lolote? Ni wakati vijana wakawa makini sana na namna ambavyo CHADEMA na viongozi wake wana shughulikia nidhamu na makosa ya wanachama wao, hiki anacho fanyiwa Ludovick, hakina tofauti sana na walicho fanyiwa Juliana Shonza na Mtela Mwampamba.

View attachment 101283Kijana Ludovick akionekana amenyong'onyea leo mahakamani, pembeni yake ni bwana Lwakatare wakiwa na askari magereza.

Wazo zuri lakini nafikiri aliyetakiwa kulalamikiwa ni Mwigulu kwa sababu kama alimpa fedha kugharamia matengenezo ya picha hiyo kwa nini asimwonee huruma? Lakini vilevile kama yeye aliona Rwakatare ana makosa ya kutaka kudhuru kwa nini asimshauri aache mipango hiyo, akakimbilia kumrekodi na kuedit kwa matakwa ya Nchemba? Hii iwe ni fundisho kwa vijana wengine kukubali sh. 50,000/= ili kumfunga mtu kifungo kisichoendana na thamani hiyo. Hivi alikosa kazi nyingine mpaka akaona kazi pekee ni kutengeneza mikanda kama ile. Wacha asote rupango MUNGU anataka kumfundisha kupitia huko, akirudi atakuwa mzalendo wa kweli.
 
Mbona kila kitu chadema??? Kwanini msimtaje Mjengwa na wakati kila siku alikuwa anamwekea habari kwenye blog yake??
 
nashangaa sana, huo mtoa mada si ni mwanac.c.m? aende akamtolee dhamana. dhamana inatolewa kwa mtu ambaye ni mwaminifu. huyo si mwaminifu. ni muuaji. na kwa bahati mbaya mchemba aliapa mbinguni na duniani. dhambi hii ya kuwapakazia watu kesi itawaghalimu tu. ele wake mwanac.c.m mpenda mungu kama anashabikia udhalimu huu. siasa ni majukwaani sio vita au fitina za chafu. wakamtolee dhamana kina nape, mchemba, kikwete, na maafisa wa usalama wa taifa si alikubali kutumika kwa senti ndogo za muda tu?
 
mnafiki mkubwa wewe kwanini hukwenda kumwambia nwigulu huu ujinga wako akili za kuku hizo
 
WanaJF!

Leo ni siku ya kesi ya bwana Lwakatare kusikilizwa kwenye mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, lakini kesi imehairishwa mpaka July 22, 2013.

Pamoja na hayo, mshitakiwa na.2 bwana Ludovick Rwezahula ameshindwa kupata dhamana kwa sababu ya kutokamilika kwa nyaraka za dhamana, ingawa dhamana yake iko wazi kabisa.

Bwana Ludovick akiwa nje ya mahakama, ameonekana akiwa mnyonge na alikuwa akilia sana kwa uchungu huku akilalamika ndugu zake (ambao hawakufika mahakamani) hawafatilii dhamana yake.

Kwa hali kama hiyo, kijana Ludovick anaendelea kusota gerezani na kuzidi kuangamia, kwani wote sisi ni wanaadamu na tunajua makali ya maisha ya gerezani.

Rai yangu kwa CHADEMA; haijarishi kijana Ludovick kama alikuwa mwajiriwa wa CHADEMA kimkataba ama alikuwa volunteer, jambo la msingi ni kwamba alikuwa ana kitumikia CHADEMA kwa moyo wake wote na nguvu zake zote. Ludovick alijitoa kwa CHADEMA kwa namna ya pekee, ni kijana ambae alikuwa bega kwa bega na Dr Slaa kiutendaji na vile vile alikuwa kama mtoto kwa Dr Slaa.

Katika hali kama hiyo sikutarajia kama CHADEMA kinaweza kumtema na kumkataa kabisa bwana Ludovick Rwezaura. Kwani wote tunafahamu kuwa, kosa aliadhibiwi kwa ubaya, bali kosa dawa yake kukosolewa. Sasa kwanini CHADEMA wana muadhibu kijana Ludovick kwa ubaya? kwanini wasimsaidie hata kwa dhamana ili aweze kutoka kwenye 'jehanamu' ya duniani?

Maamuzi haya ya kumtupa mkono kijana Ludovick katika hali hii mbaya inayo mkabili, inajenga wasiwasi mkubwa kwa vijana wengi walio CHADEMA juu ya hatma yao endapo wakikosea jambo. Je, chama kitawasaidia kwa lolote? Ni wakati vijana wakawa makini sana na namna ambavyo CHADEMA na viongozi wake wana shughulikia nidhamu na makosa ya wanachama wao, hiki anacho fanyiwa Ludovick, hakina tofauti sana na walicho fanyiwa Juliana Shonza na Mtela Mwampamba.

View attachment 101283Kijana Ludovick akionekana amenyong'onyea leo mahakamani, pembeni yake ni bwana Lwakatare wakiwa na askari magereza.

Jaribu kuwasiliana na mhesimiwa Mwigulu akamdhamini kijana wake.. usaliti unamtafuna... alidhani watamjali baada ya kumtumia!? hawajui chama twawala, poor thing
 
Mwenye uchungu sana azae!!kama kweli unamuonea huruma kamuwekee dhamana wewe!!hatuwezi kulea wasaliti na wanafiki kwa kulipwa vipande vya fedha 50000 na mwigulu chemba aka savimbi...laana yake itamtafuna hapahapa duniani.

Hili jina na usaliti si kila siku anaitwa Zitto hivyo? mbona mnamlea?
 
Wazo zuri lakini nafikiri aliyetakiwa kulalamikiwa ni Mwigulu kwa sababu kama alimpa fedha kugharamia matengenezo ya picha hiyo kwa nini asimwonee huruma? Lakini vilevile kama yeye aliona Rwakatare ana makosa ya kutaka kudhuru kwa nini asimshauri aache mipango hiyo, akakimbilia kumrekodi na kuedit kwa matakwa ya Nchemba? Hii iwe ni fundisho kwa vijana wengine kukubali sh. 50,000/= ili kumfunga mtu kifungo kisichoendana na thamani hiyo. Hivi alikosa kazi nyingine mpaka akaona kazi pekee ni kutengeneza mikanda kama ile. Wacha asote rupango MUNGU anataka kumfundisha kupitia huko, akirudi atakuwa mzalendo wa kweli.

Mkuu, unashauri amkanye mtu mwenye mipango haramu? nikisema watu wa aina ya Lwakatare wapo wengi ndani ya CDM, je ulitaka awakanye wangapi?

Jambo la busara ilikuwa kuwafanya watanzania wote wajue mipango harama ya Lwakatare dhidi ya raia (kama ni kweli mipango ilipangwa ya kuteka na kudhuru).
 
HAMY-D

Nadhani huelewi unachokisema la sivyo usingeandika PUMBA hizi. Au na wewe ni gaidi?

Ludovick ndiye haswa aliyetumwa kufanya kazi ya kijasusi na hao waliomtuma. Alikuwa pandikizi la usaliti. Lengo lake lilikuwa kujiweka karibu na watendaji wakuu wa CHADEMA na kisha kuweka ushahidi bandia ambao ungeonesha kwamba viongozi hao walikuwa watu hatari. Alijaribu kwa Zitto na Dr. Slaa. Wakamshtukia. Waliomtuma walipoona hali haiendi wakaamua kutengeneza ushahidi wa kukurupuka ambao walimtumia huyo huyo Ludovick. Aliifanya kazi hiyo huku akijua kwamba mambo yakienda Kusini, hakuna yeyote kati ya wale ambao walimtuma wangekuja kumwokoa. Hili alilijua tangu mwanzo tangu alipoingia kwenye mkataba huu wa kifisadi wa kuipaka matope CHADEMA. Mashirika YOTE ya kijasusi duniani - YOTE - huwaambia waajiriwa wao kwamba wakikamatwa wakiwa kazini hakuna ambaye angekuja kuwaokoa. Ludovick aliijua tahadhari ambayo alipaswa kuichukua.

Leo analia ndugu zake hawafuatilii dhamana yake. Ameitia doa familia yake. Hata kama angekuwa ndugu yangu wa kiachiana ziwa, singemdhamini na ningewakataza ndugu zangu wengine kufanya hivyo.

Na hao waliomtuma hawawezi kujitokeza hadharani kumuokoa kwani kufanya hivyo KUTATHIBITISHA hoja ambayo imekuwa ikitajwa na CHADEMA kwamba wamekuwa wakipakwa matope kupitia viongozi wake kubambikizwa kesi badia za ugaidi.

Hao waliomtuma (nachelea kuwataja nisijeulizwa mahakamani iwapo nina ushahidi) KAMWE hawawezi kumdhamini.

Ndio, tunajua kwamba kila anayekosa anastahili huruma na msamaha, lakini hili la kumsababishia mtu asiye na hata chembe ya hatia awekwe ndani kwa kosa kubwa kama hilo la ugaidi, tena akiwa mgonjwa (Lwakatare ni mgonjwa wa kisukari) ni sawa na UHAINI. Siwezi kumsemea mwokozi wetu Yesu Kristo, lakini kwenye kosa hili, kama Kristo angerudi leo, Ludovick angejikuta akifunguliwa milango ya Jehanam, akiwa amefungwa minyororo mwili mzima, akilakiwa na Lusifer huku akichekelea meno yote nje.

Ludovick, umevuna ulichopanda!

MwanaHaki,

Kweli CHADEMA chama cha makamanda. Watu mmetokwa na utu hivyo?

Mbona mtu kama Zitto ambae anasemekana kuwa na utitiri wa matukio ya kiusaliti mnaendelea kumkumbatia?

Angalau CDM ingemsaidia kwenye dhamana halafu ndio hayo mengine yafuate, ila kumuacha kijana ambae alikuwa msaada mkubwa kwa chama hasa Dr Slaa aozee mahabusu si vyema. Mimi sina uwezo ila ni imani yangu CDM kama oganaizesheni haishindwi.
 
Last edited by a moderator:
Kijana mdogo na ndo kwanza alikua kamaliza ka degree kake tamaa za haraka haraka zinammaliza wacha akome kwanza mpaka aregret upinda wake. 50000 inatenda miujiza hapahapa duniani na wengine tujifunze betray is not a good thing when it comes to national matters.
 
Mkuu, ndugu zake hawana uwezo halafu ukizingatia wengi wao wako Bukoba, katika hali kama hiyo, ni ngumu kuweza kumtolea kijana Ludo dhamana hata kuja tu mahakamani inashindikana.

Dr Slaa alikuwa kama baba kwa Ludo, kwanini asilifanye hili suala kama lake na akamsaidia kijana anaengamia mahabusu. Dr Slaa awe na roho ya utu na akumbuke fadhira zote za kijana huyu katika kumtumikia. Jamani, ni utu tu.

Fadhila gani alizomfanyia dr. mpaka ukadhan kwamba dr. ana nafasi ya kumsaidia inreturn?

Inaonekana unaelewa vizuri sana mahusiano yalokuwepo kt ya dr na Ludo. Ebu tujuze interest yako ktk hilo. Je ulikuwa mtu wa karibu kati ya hao ndugu? Ni nani kati yao alekueleza juu ya ukaribu walonao?

NINA MASHAKA SANA NA AINA YA UTETEZI WAKO KWA LUDO. KUNA KITU NYUMA YA PAZIA.
 
Kijana wa Bavicha katelekezwa, Chadema mna jopo la wanasheria msaidieni huyu kijana.
CCm mna huruma na Ludovick! hivi kweli Lowasa, Rostam na JK wanashindwa kuchota kidogo tu zile pesa za DOWANS? mbona kanisani na misikitini wanatoa? japo mkakati wenu umeshindwa, muoneeni huruma mtekelezaji wa mkakati.
 
MwanaHaki,

Kweli CHADEMA chama cha makamanda. Watu mmetokwa na utu hivyo?

Mbona mtu kama Zitto ambae anasemekana kuwa na utitiri wa matukio ya kiusaliti mnaendelea kumkumbatia?

Angalau CDM ingemsaidia kwenye dhamana halafu ndio hayo mengine yafuate, ila kumuacha kijana ambae alikuwa msaada mkubwa kwa chama hasa Dr Slaa aozee mahabusu si vyema. Mimi sina uwezo ila ni imani yangu CDM kama oganaizesheni haishindwi.

Unamtumia zito kufanya justification ya usaliti? CHADEMA HAIPO IVO KIONGOZI.
 
Last edited by a moderator:
Yap kwa kweli alikitumikia kwa moyo wake wote huku wakiwasiliana na Madelu kutengeneza video mnayoiita ya ugaidi, nafikiri hata wewe mkuu au madelu mnaweza fanya utu mumtoe kwa dhamana
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom