WanaJF!
Leo ni siku ya kesi ya bwana Lwakatare kusikilizwa kwenye mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, lakini kesi imehairishwa mpaka July 22, 2013.
Pamoja na hayo, mshitakiwa na.2 bwana Ludovick Rwezaura ameshindwa kupata dhamana kwa sababu ya kutokamilika kwa nyaraka za dhamana, ingawa dhamana yake iko wazi kabisa.
Bwana Ludovick akiwa nje ya mahakama, ameonekana akiwa mnyonge na alikuwa akilia sana kwa uchungu huku akilalamika ndugu zake (ambao hawakufika mahakamani) hawafatilii dhamana yake.
Kwa hali kama hiyo, kijana Ludovick anaendelea kusota gerezani na kuzidi kuangamia, kwani wote sisi ni wanaadamu na tunajua makali ya maisha ya gerezani.
Rai yangu kwa CHADEMA; haijarishi kijana Ludovick kama alikuwa mwajiriwa wa CHADEMA kimkataba ama alikuwa volunteer, jambo la msingi ni kwamba alikuwa ana kitumikia CHADEMA kwa moyo wake wote na nguvu zake zote. Ludovick alijitoa kwa CHADEMA kwa namna yake, ni kijana ambae alikuwa bega kwa bega na Dr Slaa kiutendaji na vile vile alikuwa kama mtoto kwa Dr Slaa.
Katika hali kama hiyo sikutarajia kama CHADEMA kinaweza kumtema na kumkataa kabisa bwana Ludovick Rwezaura. Kwani wote tunafahamu kuwa, kosa aliadhibiwi kwa ubaya, bali kosa dawa yake kukosolewa. Sasa kwanini CHADEMA wana muadhibu kijana Ludovick kwa ubaya? kwanini wasimsaidie hata kwa dhamana ili aweze kutoka kwenye 'jehanamu' ya duniani?
Maamuzi haya ya kumtupa mkono kijana Ludovick katika hali hii mbaya inayo mkabili, inajenga wasiwasi mkubwa kwa vijana wengi walio CHADEMA juu ya hatma yao endapo wakikosea jambo. Je, chama kitawasaidia kwa lolote? Ni wakati vijana wakawa makini sana na namna ambavyo CHADEMA na viongozi wake wana shughulikia nidhamu na makosa ya wanachama wao, hiki anacho fanyiwa Ludovick, hakina tofauti sana na walicho fanyiwa Juliana Shonza na Mtela Mwampamba.
View attachment 101283Kijana Ludovick akionekana amenyong'onyea leo mahakamani, pembeni yake ni bwana Lwakatare wakiwa na askari magereza.