CHADEMA kina wanachama wangapi?

Siasa ni zaidi ya ushabiki wa mpira. Siasa safi na zenye tija ndizo zitakazowezesha taifa hili kusonga mbele.

EMT umewahi kusikia CCM inachofanya pale penye uchaguzi? huwa wanatuma watu hasa viongozi wake wa mashinda kuanza kukagua wanachama wake. Hivi CDM wamewahi kujiuliza ni kwanini CCM hufanya hivyo? Wengi wanafikiria ni kwa sababu "wanataka kununua shahada za kupigia kura"... I beg to differ...
 
nadhani viongozi wa chadema kwanza wangeuelimisha umma juu umuhimu wa kupiga kura ili mpiga kura ajue dhamani ya kura yake
 
Viongoz wa CDM HAWASHAURIKI WANAJIONA MALAIKA NA KUANGALIANA SURA NDIO MAANA BAWACHA IMEKUFA NA HAWATAKI KUIVUNJA.KUNA TATIZO KUBWA CDM HATA MIKOAN HAMNA VIONGOZ WA KUFANYA KAZ ZA CHAMA BALI MATAPELI WA KUPEANA RUZUKU VIONGOZ WE2 NI DHAIFU WAWAJIBIKE WANAKIUA CHAMA HUKU 2KIENDELEA KUCHEKA NAO
 
Mzee Mwanakijiji kama una jambo lingine la maana kujadili au kuwashauri ni bora ungefanya hivyo, Dr Exavery Lwaitama ni kada wa CCM na hata mimi Matola ni kada wa CCM, wacha kujishughurisha na takwimu za uwongo zisizo na takwimu za waliohama chama na waliofariki.

Takwimu unayotueleza wewe hapa ni tangu kuanzishwa kwa CCM, natowa Offer ya $ 100 aje hata katibu tu wa tawi la CCM atuthibitishie ni lini aliwahi ku update reja yake ya wanachama kwa kuwaondowa walioamia vyama vingine na waliokufa, nina uhakika wa 100% hakuna wa kuichukuwa $ 100 yangu. Si kweli hata kidogo kwamba eti CCM ina wanachama millioni 5.

Hi thread ni useless kwangu kwa sababu mimi binafsi si mwanachama wa Chadema lakini ni zaidi ya Mwanachama. ni kwa nini tusiwaige Wasouth Afrika ambao wao itikadi iko moyoni? sijawahi kuona bendera za vyama vya siasa mitaani South Afrika zaidi ya Head qouters. Wewe Mwanakijiji unaishi Marekani unataka kuniambia Obama anatalajia kushinda kwa sababu Democratic ina wanachama zaidi?
its tru matola, na ifike mahali tuwe tunafanya vitu kadiri ya uwezo wetu na kulingana na ruzuku tulionayo na sio tupeleke mambo kishabikishabiki
 
Chadema hawapendi ushauri,wanajifanya wanaijua siasa..kuna sehemu hadi leo hawajafika wanakimbilia ulaya na usa..ili walipane per diem nene.

Kusini uko kuna maeneo walisikia tu cdm walipita kisingizio msiba wa Makani au bajeti haitoshi, ila bajeti ya kufanya mikutano Arusha haikosekani.

Matokeo ya udiwani ni ujumbe mzuri kwa ukaidi wao.
wakianza kutaka kufika waambie makamanda wasianze kusingizia intelejensia
 
Wanachama wa Chadema ukitaka kuwaona subiri mikutano ya Chadema Chopa akitua utawaona, Chopa ikiondoka na wao wanaondoka.
 
Hadi mwaka 2010 Chama cha Mapinduzi kilikuwa na wanachama takribani milioni tano kwa mujibu wa alkiyejuwa katibu mkuu wakati ule Bw Yusuph Makamba. Idadi hii ni ongezeko kutoka wanachama milioni tatu hivi waliokuwepo mwaka 2000. Ili kuweza kuelewa mwelekeo wa chama kikuu cha upinzani nchini na hasa kukubalika kwa ajenda yake ni vizuri kujiuliza CDM sasa hivi sasa wanachama wangapi wente kuveba kadi? Na wanachama hawa wametawanyika vipi katika nchi yetu?

Idadi ya wanachama wa chama cha siasa (siyo mashabiki) inaweza kujulikana to almost exact figures.

a. Mwanachama anapojiunga analipia kadi kwenye tawi lake
b. Kila tawi lina orodha ya wanacham wake
c. Mwanachama akihama tawi kuna utaratibu kuwa kule anakoenda atajiunga na tawi jipya na rekodi zitaonesha hivyo
d. Kila tawi linatuma idadi ya wanachama wake makao makuu
e. Kuna utaratibu wa kuupdate idadi ya wanachama (wanaoingia na kutoka)
f. Kwa kuangalia idadi hizo unaweza kuona movement ya wanachama na kupata demographia ya wanachama wako (vijana, wazee, kina mama, mijini, vijijini n.k).
g. Kulipa ada za kila mwezi za chama. Mfumo mbaya ni kulipa kwa mwaka! Ni vizuri kuweka quarterly fees ili kila baada ya miezi mitatu walio wanachama (loyal party members) wanaenda kulipa ada zao. Hii inakupa mwanga.
h. censored.

Sasa kujua hili la wanachama ni kuijua base yako. Huwezi kujenga chama kwa kutegemea independents au undecided voters. Ni kwa kutegemea your core supporters ndio chama kinaweza kusimama.
I think ni muhimu kwa chama chochote ku keep track ya wanachama wake....be it a political party or any organization/social party....that said....nadhani ni muhimu pia kwa CDM kama chama kuwa na data base ya members wake....kwa maana ya kujua pia locations zao na idadi yao.....on the other side though...kujua/kuwa na idadi kubwa ya wanachama si determinant factor ya kushinda chaguzi za kisiasa....kwa maana ya kwamba wale wanaoenda kupiga kura(haswa ktk nchi kama tz)wengi wao si wanachama wa vyama vya siasa.....mifano ni mingi na mfano mkubwa ni chaguzi za rais tz.....rejea uchaguzi wa 2010.....I think pia kigezo cha raia kuwa mwanachama wa chama fulani hakitumiki wakati wa chaguzi tz.......Labda kama ungetaka kuwasaidia CDM ungewashauri wazidi kutoa elimu ya uraia ili kila mtanzania ajue haki na umuhimu wa yeye kupiga kura wakati wa chaguzi.....na pia kila raia anayepaswa kujiandisha ktk daftari la wapiga kura.....Hili ndilo jambo litakaloleta mabadiliko ktk jamii ya mtanzania kwasasa...otherwise..you can be a member of a party(like CDM)and still not vote during elections.......
 
kama mtu (mwanachama)anaweza kua na kadi mbili (ccm na cdm) ni unafki kisiasa na anaweza kusaliti chama chochote ili mradimkuwe na maslah!,ni upuuz!
 
Hadi mwaka 2010 Chama cha Mapinduzi kilikuwa na wanachama takribani milioni tano kwa mujibu wa alkiyejuwa katibu mkuu wakati ule Bw Yusuph Makamba. Idadi hii ni ongezeko kutoka wanachama milioni tatu hivi waliokuwepo mwaka 2000. Ili kuweza kuelewa mwelekeo wa chama kikuu cha upinzani nchini na hasa kukubalika kwa ajenda yake ni vizuri kujiuliza CDM sasa hivi sasa wanachama wangapi wente kuveba kadi? Na wanachama hawa wametawanyika vipi katika nchi yetu?

Idadi ya wanachama wa chama cha siasa (siyo mashabiki) inaweza kujulikana to almost exact figures.

a. Mwanachama anapojiunga analipia kadi kwenye tawi lake
b. Kila tawi lina orodha ya wanacham wake
c. Mwanachama akihama tawi kuna utaratibu kuwa kule anakoenda atajiunga na tawi jipya na rekodi zitaonesha hivyo
d. Kila tawi linatuma idadi ya wanachama wake makao makuu
e. Kuna utaratibu wa kuupdate idadi ya wanachama (wanaoingia na kutoka)
f. Kwa kuangalia idadi hizo unaweza kuona movement ya wanachama na kupata demographia ya wanachama wako (vijana, wazee, kina mama, mijini, vijijini n.k).
g. Kulipa ada za kila mwezi za chama. Mfumo mbaya ni kulipa kwa mwaka! Ni vizuri kuweka quarterly fees ili kila baada ya miezi mitatu walio wanachama (loyal party members) wanaenda kulipa ada zao. Hii inakupa mwanga.
h. censored.

Sasa kujua hili la wanachama ni kuijua base yako. Huwezi kujenga chama kwa kutegemea independents au undecided voters. Ni kwa kutegemea your core supporters ndio chama kinaweza kusimama.

Mzee Mwanakijiji,

Ushauri wako ni mzuri. Ila katika utangulizi wako umetoa data za wanachama wa CCM ambazo mimi siziamini. Hizi za CCM zilipatikanaje? Hata CCM kuna wanachama wengi waliacha kulipia kadi zao mwanzoni mwa miaka ya 80. Wengi waliingia CCM wakati wa chama kimoja ili wapate scholarships au kazi. Wengine waliingia wakiwa JKT na walipotoka ikawa nitolee.
 
Mzee Mwanakijiji wanachama wa CDM wanapatikana kwenye mikutano ya hadhara na maandamano na sidhani kama majina yao huorodheshwa zaidi ya kupewa kadi
 
Last edited by a moderator:

Njaare miezi michache kabla ya kifo cha Horace Kolimba alizungukia mashirika yote ya umma kugawa kadi za CCM; kama hesabu ya CCM ni pamoja na hao hiyo idadi siyo sahihi
 
Last edited by a moderator:
Kitu kimoja nilicho na uhakika nacho ni kwamba Chadema inafahamu idadi ya wanachama wake. Kiutaratibu kila robo mwaka makatibu wa majimbo/ wilaya huwasilisha ripoti za maendeleo ya chama makao makuu na mojawapo ya taarifa ambazo hupelekwa ni pamoja na idadi ya wanachama toka kila kata na matawi. Na kwa umuhimu wa pekee kila mwisho wa mwaka ripoti muhimu kuliko zote inayotiliwa mkazo na kuwasilishwa ofisini kwa katibu mkuu toka majimboni na wilayani ni idadi ya wanachama, nakumbuka ripoti hiyo kwetu Ukonga iliandaliwa na kutumwa makao makuu mwezi December mwaka jana, kwahiyo lazima idadi ya wanachama inafahamika. Sasa suala la kutaja hadharani kwamba so far tuna wanachama wangapi hilo nawaachia wenyewe wa makao makuu waseme.

Binafis sitarajii sana kwamba tunahitaji kuishinda ccm kwa kuwategemea wanachama wetu tu, kwakuwa kuna watu wengi sana ambao hawahitaji kuwa wanachama wa chama chochote cha siasa lakini wanatambua haki zao za kiraia na huzitumia kwa kupiga kura kila mara uchaguzi unapokuwepo. Cha msingi ni kujielekeza kwa wananchi waweze kuelewa dhamira yetu, malengo yetu na dira yetu katika kutaka kuwatumikia ili wawe na imani kwetu na hatimaye kutuchagua na kukataa hila zote za ccm na serikali yake pamoja na vyombo vya dola.

Assuming ccm ina wanachama milioni tano, Chadema ina wanachama milioni tano, cuf ina wanachama milioni tano, hadi hapo jumla ni watu milioni 15, na watanzania tuko zaidi ya takribani milioni 45 kwahiyo kuna watanzania zaidi ya milioni 30 wasio wanachama wa vyama vya siasa lakini hao nao ni wapiga kura. Kwahiyo hoja yangu ya msingi hapa si kujikita sana kuingiza wanachama wengi bali tunachopaswa kuanza nacho ni kuwa na viongozi walio committed toka ngazi za misingi, matawi, kata hadi taifa ili waweze kuratibu kazi za chama kwa urahsi na ukaribu na wananchi, maeneo ambayo hatuna viongozi katika ngazi za chini kabisa hasa misingi na matawi ndipo tunapata shida kuwafikia watu.
 
EMT umewahi kusikia CCM inachofanya pale penye uchaguzi? huwa wanatuma watu hasa viongozi wake wa mashinda kuanza kukagua wanachama wake. Hivi CDM wamewahi kujiuliza ni kwanini CCM hufanya hivyo? Wengi wanafikiria ni kwa sababu "wanataka kununua shahada za kupigia kura"... I beg to differ...

MMKJ,

Nadhani kuwa na wapiga kura ni muhimu zaidi kuliko kuwa mwanachama kwa sasa. Kampeni zielekezwe watu wajiandikishe katika daftari la kupiga kura na wapigwe kampeni wapige kura. What use kuwa na wanachama wengi wasio piga kura. Hao milioni 5 wa Makamba wapo mpaka akina marehemu.

Hata marekani sidhani Obama alipata kura za memeber wa Democrats tu
 
Chadema hawapendi ushauri,wanajifanya wanaijua siasa..kuna sehemu hadi leo hawajafika wanakimbilia ulaya na usa..ili walipane per diem nene.

Kusini uko kuna maeneo walisikia tu cdm walipita kisingizio msiba wa Makani au bajeti haitoshi, ila bajeti ya kufanya mikutano Arusha haikosekani.

Matokeo ya udiwani ni ujumbe mzuri kwa ukaidi wao.

Nakupa 99%
 
Mzee Mwanakijiji wanachama wa CDM wanapatikana kwenye mikutano ya hadhara na maandamano na sidhani kama majina yao huorodheshwa zaidi ya kupewa kadi

Hakuna mtu anayegawiwa/kununua kadi kwenye mikutano ya hadhara bila kuandikwa jina lake na namba yake ya simu na mahali anapoishi. Mimi binafsi nimefanya mikutano ya hadhara mitatu ambayo tuliingiza wanachama zaidi ya 170. Mkutano mmoja tulipata wanachama 103, mkutano mwingine wanachama 25 na mwingine wanachama 46 na wote waliandikishwa majina yao, makazi yao na namba zao za simu. Na baada ya mikutano tulifanya mawasiliano na viongozi wa matawi husika kuwajulisha wanachama waliopatikana katika mikutano ambao wanaoishi maeneo yao ili wawafuatilie na kuwaingiza kwenye ledge zao.
 
Kitu kimoja nilicho na uhakika nacho ni kwamba Chadema inafahamu idadi ya wanachama wake. Kiutaratibu kila robo mwaka makatibu wa majimbo/ wilaya huwasilisha ripoti za maendeleo ya chama makao makuu na mojawapo ya taarifa ambazo hupelekwa ni pamoja na idadi ya wanachama toka kila kata na matawi. Na kwa umuhimu wa pekee kila mwisho wa mwaka ripoti muhimu kuliko zote inayotiliwa mkazo na kuwasilishwa ofisini kwa katibu mkuu toka majimboni na wilayani ni idadi ya wanachama, nakumbuka ripoti hiyo kwetu Ukonga iliandaliwa na kutumwa makao makuu mwezi December mwaka jana, kwahiyo lazima idadi ya wanachama inafahamika. Sasa suala la kutaja hadharani kwamba so far tuna wanachama wangapi hilo nawaachia wenyewe wa makao makuu waseme.

Binafis sitarajii sana kwamba tunahitaji kuishinda ccm kwa kuwategemea wanachama wetu tu, kwakuwa kuna watu wengi sana ambao hawahitaji kuwa wanachama wa chama chochote cha siasa lakini wanatambua haki zao za kiraia na huzitumia kwa kupiga kura kila mara uchaguzi unapokuwepo. Cha msingi ni kujielekeza kwa wananchi waweze kuelewa dhamira yetu, malengo yetu na dira yetu katika kutaka kuwatumikia ili wawe na imani kwetu na hatimaye kutuchagua na kukataa hila zote za ccm na serikali yake pamoja na vyombo vya dola.

Assuming ccm ina wanachama milioni tano, Chadema ina wanachama milioni tano, cuf ina wanachama milioni tano, hadi hapo jumla ni watu milioni 15, na watanzania tuko zaidi ya takribani milioni 45 kwahiyo kuna watanzania zaidi ya milioni 30 wasio wanachama wa vyama vya siasa lakini hao nao ni wapiga kura. Kwahiyo hoja yangu ya msingi hapa si kujikita sana kuingiza wanachama wengi bali tunachopaswa kuanza nacho ni kuwa na viongozi walio committed toka ngazi za misingi, matawi, kata hadi taifa ili waweze kuratibu kazi za chama kwa urahsi na ukaribu na wananchi, maeneo ambayo hatuna viongozi katika ngazi za chini kabisa hasa misingi na matawi ndipo tunapata shida kuwafikia watu.
Mwita Maranya nadhani uhai wa chama ni wanachama. Lakini je ni wanachama wa aina gani wanaoshikilia uhai wa chama. Mimi naona tatizo labda Chama kimefocus zaidi kupata numbers zaidi kumbe labda unaweza kuwa na wanachama 2 mbili tu nchi nzima katika key strategic areas ambao wana tija kuliko kuwa na milioni kumi ambao ni namba tu.
 
Nakubaliana na wewe Elizabeth Dominic. Katika mazingira yetu ya siasa za kitanzania ni muhimu sana kuwa na wanachama ambao wako committed kuliko kuangalia wingi wa wanachama, ambao wanakuwa hawana msaada sana na chama.

Ukishakuwa na wanachama ambao wako committed, wakipewa majukumu wanatekeleza kwa ukamilifu wake. Lakini kwa hali yetu ambayo tuna siasa za mlipuko inakuwa ni vigumu kuwakwepa wanachama maslahi binafsi wanaokimbia kutoka vyama mbalimbali wakitoa sababu mbalimbali lakini kumbe genuinely wanahama kwa sababu ya maslahi yao binafsi.

Na ndio maana nikasema kilichokuwa cha msingi zaidi pamoja na kuongeza wanachama, kuhakikisha kuna viongozi kuanzia ngazi za chini kabisa ili kuhakikisha kwamba kupitia wao sera za chama zinaweza kuwafikia watu kwa urahisi na uzuri zaidi.
 
Last edited by a moderator:
Hakuna mtu anayegawiwa/kununua kadi kwenye mikutano ya hadhara bila kuandikwa jina lake na namba yake ya simu na mahali anapoishi. Mimi binafsi nimefanya mikutano ya hadhara mitatu ambayo tuliingiza wanachama zaidi ya 170. Mkutano mmoja tulipata wanachama 103, mkutano mwingine wanachama 25 na mwingine wanachama 46 na wote waliandikishwa majina yao, makazi yao na namba zao za simu. Na baada ya mikutano tulifanya mawasiliano na viongozi wa matawi husika kuwajulisha wanachama waliopatikana katika mikutano ambao wanaoishi maeneo yao ili wawafuatilie na kuwaingiza kwenye ledge zao.
Mwita Maranya ahsante kwa ufafanuzi lakini idadi ya wanachama wapya 170 ambao hupewa kadi mwishoni mwa mkutano anayewaandikisha majina na mtu mmoja au wanaandikwa na zaidi ya mtu mmoja; chukulia unatumia dakika moja kuandikisha mwanacha mmoja, 170 ni sawa na masaa matatu (170/60); na labda kazi mnaanza nusu saa kabla ya muda mnaoruhusiwa kisheria kuendelea na mkutano
 
Last edited by a moderator:
g. Kulipa ada za kila mwezi za chama. Mfumo mbaya ni kulipa kwa mwaka! Ni vizuri kuweka quarterly fees ili kila baada ya miezi mitatu walio wanachama (loyal party members) wanaenda kulipa ada zao. Hii inakupa mwanga.

hilo lina walakini. mimi nilichukuwa kadi yangu 2010, immedietely baada ya uchaguzi mkuu. lakini huwezi kuamini hadi leo sijawahi kulipa ada, si kama sitaki au ni kuishi kwa mazoea, hasha! mimi nimechangia mikakati mingi tu ya chama changu, japo si kivile, lakini nimeshiriki kuchangia mikakati mbalimbali kwa ajili ya ustawi wa chama changu, sasa sioni sababu kwa nini nishindwe kulipia ada ya kadi. viongozi wa matawi wanasema hawana stika. zinapatikana wapi? wanasema makao makuu. hivi kweli mtu kulipia kadi ya chama mpaka aende makao makuu? haiingii akilini. kujiunga nilijiunga makao makuu, na kulipia ada nikalipie makao makuu!?

viongozi wa matawi wanapashwa kumulikwa.

siyo kila kitu Mbowe, Slaa, Zitto.
 
Back
Top Bottom