hii hoja nayo haina mashiko; kama CCM wananunua kadi kuna namna nyingi za kuweza kucounter hili. Mara nyingi tunaambiwa CDM inawasomi wengi; ni kweli wasomi wetu walioko CDM wameshindwa kufikiria namna ya kushughulikia hili? Lakini inakuwaje kama ni kweli wapo wanaCDM wanaorudisha kadi zao kirahisi hivyo? Ni kitu gani kinawafanya watu warudishe kadi? Kama wapo mamia ya wana CCM wanahamia CDM na kuleta kadi zao kwa CDM haiwezekani kweli kuwa wapo pia wana CDM kwa mamia ambao na wanarudisha kadi zao kwa CCM? Kwanini iwe kweli kwa CCM lakini isiwe kweli kwa CDM?
Hatari ya hili ni kuwa vyama havikui idadi kwa sababu namba zao zina cancel each other each time
Hoja yangu au ya Matola haina mshiko? Kama mdau mmoja alivyowahi kuuliza haya maswali:
Kwa nini kadi hizo zisirudishwe kwa vyama husika katika matawi yao ili waweze kuhakiki wananchama wao?
Vyama vya siasa vinahakiki vipi wanachama wake?
Kwa nini mikutano mingi ya hadhara ya vyama vya siasa agenda kubwa ni kuwapokea wanachama wapya?
Kazi ya idara ya uenezi ya chama ni nini? Idara hii kichama kwa jinsi vyama vinavyofanya kazi hivi sasa ina mapungufu gani?
Viongozi ambao walikuwa na dhamana wanapohamia vyama vingine tunajifunza nini? Wanakuwa wamekosa nini? Kuhamia chama kingine ni suluhisho?
Ni vigumu kuelewa pamoja na vyama vya siasa kumiliki wataalamu wa uchambuzi wa mambo ya siasa na uchumi, bado wameshindwa kutumia taaluma yao kuwashauri vyama vyao kuweka agenda ya kuwapokea na wanachama wapya katika mikutano yao ya siasa ni matumizi mabaya ya muda na fedha.
Kubwa zaidi ni kutafuta umaarufu wa kichama tuu. Kuna uhakika gani kama wanachama hao siyo wanachama wa chama hicho hicho? Je hao wanaorudisha hizo kadi sio mamluki wa kisiasa ambao kwa upeo na uelewa wa ukuaji wa demokrasia ndani ya vyama wanasiasa wanafikiri kuwa matukio kama haya yanawaongeza wananchama kumbe wanongeza kero ndani ya vyama vyao kwa kuwapata wananchama wa msimu ambao wengi wao huishia kuwa mamluki wa kisiasa wanaohama tuko chama kimoja kwenda kingine?
Kesho wakisikia CUF wako Jangwani watarudisha hizo kadi na kuingia CUF. Keshokutwa ikirudi CDM watarudisha za CUF na CCM na kuingia CDM. Na CCM wakirudi tena kufanya mkutano watarudisha hizo kadi na kuchukua za CCM.
Vyama vya siasa hata CCM wana tatizo la kutojua idadi ya wanachama wao ambao ni hai na ambao wanaweza kukisaidia chama katika kukiletea maendeleo na kukipigia kura wakati wa uchaguzi. vyama vinapumbazwa na halaiki ya watu wakati wa mikutano yao ya wazi.
Siasa ni zaidi ya ushabiki wa mpira. Siasa safi na zenye tija ndizo zitakazowezesha taifa hili kusonga mbele.