CHADEMA imewasaliti Watanzania

CHADEMA imewasaliti Watanzania

Kwanza kabisa usaliti ni nini?

Tundu Lissu akisema kafanya siasa vya kutosha, afya yake si nzuri, anataka kustaafu siasa leo, wengine waendelee na kazi, atakuwa msaliti au si msaliti?
Nimewauliza hao walioweka hoja ya usaliti wakiamini Lissu kuingia katika kiitwacho maridhiano kausilit msimamo wake hivyo kawaangusha na wao kwa kuwasaliti na kuamua kukaa mezani na Samuya.
 
Katika hiyo taarifa ukiisoma hapo unaona kabisa kuna mwelekeo wa "usaliti"?
Point namba moja ina harufu ya usaliti.

Lakini mkuu.

Kwanini ukaribishe mazungumzo na watu ambao walikataa kufanya mazungumzo na wewe kabla ya Uchaguzi wa 29 October!?
 
Nimewauliza hao walioweka hoja ya usaliti wakiamini Lissu kuingia katika kiitwacho maridhiano kausilit msimamo wake hivyo kawaangusha na wao kwa kuwasaliti na kuamua kukaa mezani na Samuya.
Lissu kasema ataingia kwenye naridhiano au mazungumzo? Unaelewa kuna tofauti?

Kama kweli Lissu kasema hivyo, unajuaje kuwa ana nia kweli ya hata kufanya mazungumzo, na hii si njia ya kutoka gerezani, njia ya ku deal na magaidi ili atoke halafu akitoka atajua cha kufanya kwa imani yake?

Yani mnamuona mtu kashikwa na magaidi, kaambiwa aseme maneno fulani ama magaidi yatamuua, anayasema maneno hayo ili asiuawe, halafu mnamwambia asikubali kusema maneno hayo akubali kuuawa?

How fair is that?

Hao wanaosema Lissu abaki gerezani mbona wao hawako gerezani?
 
Linatia wasiwasi kwa nini?

Unafahamu strategy za chama nanza Lissu ni zipi?
Hizo mikakati hazieleweki. Tunachokiona ni matokeo ya mikakati hiyo. CHADEMA wametoa taarifa rasmi kwa umma kwamba Lissu yuko tayari kufanya mazungumzo endapo ataachiwa huru.
 
Hizo mikakati hazieleweki. Tunachokiona ni matokeo ya mikakati hiyo. CHADEMA wametoa taarifa rasmi kwa umma kwamba Lissu yuko tayari kufanya mazungumzo endapo ataachiwa huru.
Kwani kufanya mazungumzo ni usaliti?

Usaliti kwa nani?

Unajuaje Lissu ana nia ya kufanya mazungumzo kweli na hii habari si strategy ya kutoka jela tu?

Unajua hayo mazungumzo yatakuwa na content gani?

Umeyaona hayo masharti yote ya Lissu kwa pamoja au unashikilia hili moja tu?
 
Lissu kasema ataingia kwenye naridhiano au mazungumzo? Unaelewa kuna tofauti?

Kama kweli Lissu kasema hivyo, unajuaje kuwa ana nia kweli ya hata kufanya mazungumzo, na hii si njia ya kutoka gerezani, njia ya ku deal na magaidi ili atoke halafu akitoka atajua cha kufanya kwa imani yake?

Yani mnamuona mtu kashikwa na magaidi, kaambiwa aseme maneno fulani ama magaidi yatamuua, anayasema maneno hayo ili asiuawe, halafu mnamwambia asikubali kusema maneno hayo akubali kuuawa?

How fair is that?

Hao wanaosema Lissu abaki gerezani mbona wao hawako gerezani?
Uko sawa kabisa na ndio maana nikasema sina shaka na TAL kama aliongea hivyo mtu akapindisha akitoka ataeleza maana sio mtu wa konakona.

Na ndio maana nikasema kuna watu wamekuja na mkakati kutaka kubeba neno mazungumzo kwenda maridhiano kwenye vichwa vyao vya habari kwanini hawakusema TAL atoa masharti 7 baada ya kutembelewa gerezani?
 
Uko sawa kabisa na ndio maana nikasema sina shaka na TAL kama aliongea hivyo mtu akapindisha akitoka ataeleza maana sio mtu wa konakona.
Watu ambao hawapo gerezani hawana haki ya kulazimisha Lissu asitoke gerezani.

Kwenye suala la Lissu aendelee kukaa gerezani au akubali kutoka kufanya mazungumzo, mtu wa kwanza ninayetaka kumsikiliza ni mtu aliye gerezani, Tundu Lissu.

Kama kuna CHADEMA wengine wanataka kukaa gerezani ngangali, waende wao gerezani halafu wakatae kutoka gerezani wao tujue wanasimamia msimamo wao kwa vitendo.

Siyo mtu yupo nje, halafu analazimisha Lissu akae gerezani.
 
Hivi we una akili timamu? Amepambana kuliko waliofumuliwa vichwa october 29? Kuna sapoti kubwa kama ile ya october 29?, chadema haikushiriki maandamano lakini vijana waliingia mitaani kwa kupambania ajenda zilizopambaniwa na chadema, hivyo hata lissu ana deni, akitoka huko anatakiwa kuendeleza mapambano, watu wamemwagwa utumbo huku nje , yeye yuko jela lakini shavu dodo, TUNAWADAI

Kwamba TAL lisasi 16 alizo kula zilikua ni Maji yale sio? TAL hatuna tunachomdai, mm na wewe ambao tuko hai ndo marehemu wa mo29 wanatudai kwa sababu kama kutakua na mabadiriko yeyote yameletwa na hili zaga zaga ndo tunakua wanufaika
 
Lissu asijaribu kupata uhuru wake wa kisiasa kwa kutumia damu ya Watanzania. Taratibu za kesi zinajulikana: akipatikana na hatia, apewe adhabu kulingana na sheria; na asipopatikana na hatia, aachiwe huru. Hata hivyo, asitumie damu ya Watanzania kununua uhuru wake.

Unaelewa maana ya kuachiwa bila masharti?

HECHE amesema hili, sio mara moja kua, Mismamo wa chama ni kua TAL hana makosa hivyo serikali inapaswa kumuachia bila masharti yeyote.

Sasa kama hana makosa, atanunuaje uhuru kwa vifo vvya mo29?

Yeye mwenyewe alishaiambia mahakama haombi huruma yeyote kwa mtu yeyote, yeye anachotaka ni haki itendeke, kama ana makosa ahukumiwe anyonge ndo itakua sadaka yake kwa Taifa, mtu kama huyu wewe unamdai nn?

Au unasikiliza spinning za TISS na UVCCM zinazo fanyika kwenye media?
 
Imesalliti vipi?Utaingiaje kwenye mazungumzo usipokuwa huru?

Ety watu wamekula mboga saba huku uraiani, wanataka wazungumze na wewe unae kula mlo wa foleni Ukonga?

Ni kichaa tu anae weza fanya hivo.

Watu wanao mbeza TAL, ni wale ambao hawajawai hata kuhudhuria kesi mahakamani, hawajawai kutoa michango, wala hawakuandamana mo29
 
Kwa hyo wewe ulitaka afungwe miaka yote huku wewe ukiwa uraiani unaenjoy TU

Sion atakacho tusaliti njia nzur n yeye kuwa huru na KISHA kufanya majadiliano

NIMEGUNDUA KUNA WATU WANANUFAIKA NA LISU KUKAA JELA

Mkuu watu ni Wangese sana, Yako uraiani kila siku yanakula mbususu, ila Wanataka TAL afie Ukonga waje waandike RIP vita umevipiga vyema.

Yeye afanye lile lilosawa kulingana na Option zilizopo mezani kwake, CHADEMA imevipiga vita vilivyo.

Imagine leo HECHE ana uhuru wa kufanya mikutano watu wakajaa, kuliko Samuya?
 
Simfurahii wala simchukii Lissu, na ningependa atoke gerezani haraka. Hata hivyo, tukitafakari kwa utulivu bila hisia, suala la maridhiano lilipaswa kufanyika kabla ya uchaguzi wa Oktoba 29; huo ndio uliokuwa msimamo wa CHADEMA na baadhi ya Watanzania.

Badala yake, kuliripotiwa matukio mabaya yaliyosababisha vifo na madhara makubwa, huku serikali ikiendelea kubaki madarakani.

Baada ya matukio hayo, kuanzisha mazungumzo kunaibua maswali, je, wale waliokataa mazungumzo kabla ya uchaguzi sasa watayakubali baada ya hali kubadilika?

Ninasisitiza kuwa naheshimu Lissu, lakini siweki imani yangu yote kwa wanasiasa.

Maswali yako ni kama mgeni hapa TZ, kwani anae hitaji mazungumzo ni TAL, CHADEMA au CCM ?
 
Back
Top Bottom