Watu ambao hawapo jela hawana haki ya kuwaita watu walio jela wasaliti.
Labda ikiwa mtu A aliye jela akapewa nafasi ya kutoka kwa masharti, akakataa, halafu mtu B aliye jela akapewa masharti hayohayo ya kutoka, akakubali, hapo mtu A anaweza kumuita mtu B msaliti.
Lakini wewe mtu uko nje unamuita mtu aliyefungwa jela msaliti hata haya huoni?
Pia, mtu kusema yuko tayari kufanya mazungumzo kuna usaliti gani hapo wakati kukubali mazungumzo si kukubali jambo lokote zaidi ya mazungumzo?
Mnajuaje kwenye mazungumzo Lissu atasemaje?
Mnajuaje kwenye mazungumzo Lissu hawezi kuwabana vizuri?