CHADEMA imewasaliti Watanzania

CHADEMA imewasaliti Watanzania

Mkuu Mshana

Wazo zima la kufanya mazungumzo na CCM/Serikali linaonekana kuwa na kasoro tangu mwanzo. Je, CHADEMA wanaanzaje kufanya mazungumzo na wale waliokataa kufanya mazungumzo nao kabla ya tarehe 29 Oktoba?

Wewe unashauri wafanye kitu gani? Bila kua na Mazungumzo Upande wa pili utajuaje madai yeenu?
 
Hizo mikakati hazieleweki. Tunachokiona ni matokeo ya mikakati hiyo. CHADEMA wametoa taarifa rasmi kwa umma kwamba Lissu yuko tayari kufanya mazungumzo endapo ataachiwa huru.

Kwenye mazungumzo kila mtu anakuja na hoja na madai yake, Ili mpate maridhiano ji lazima kila upande uridhie hoja za upande wa pili.

Sasa, Mfano kwenye mazungumzo tukapata
1. Tume mpya na muundo mpya wa tume ya uchaguzi
2.Katiba mpya.
3.Kubadirishwa kwa muundo wa jeshi la polisi.
4.Kuwajibishwa kwa waliohusika na mo29(Japo hi najua labda aje Mungu mwenyewe)

Hapo bado hatujasogea kama Nchi?
 
Kabisa
kuna wafuasi wengine wa CHADEMA wanamnyooshea TAL kidole juu ya hili .

Ilhali
-hawakuwahi kuhudhuria walau tu kesi yake au kusogelea majengo ya mahakama,
-Octer 29 walikua wamejifungia ndani.

Behind the keyboard na kuongea kwa maneno ni rahisi… TAL anapambana sana mkuu ..kule ngome pasikie tu.. ata akifanya hayo mazungumzo wakati bado yupo ngome kamwe sitamnyooshea kidole.

The guy amepambana sana na Watanzania bado hatujampa support inayotakiwa. Ata akisema anaishia hapa ana nawa mikono sintomlaumu
Jamaa amepambana lkn support kakoswa wabongo bado tumelala
 
Kwenye mazungumzo kila mtu anakuja na hoja na madai yake, Ili mpate maridhiano ji lazima kila upande uridhie hoja za upande wa pili.

Sasa, Mfano kwenye mazungumzo tukapata
1. Tume mpya na muundo mpya wa tume ya uchaguzi
2.Katiba mpya.
3.Kubadirishwa kwa muundo wa jeshi la polisi.
4.Kuwajibishwa kwa waliohusika na mo29(Japo hi najua labda aje Mungu mwenyewe)

Hapo bado hatujasogea kama Nchi?
Mazungumzo na wahalifu!?

Hao watu walikataa kufanya mazungumzo kabla ya Uchaguzi.

Kwanini sasa!?
 
Unajuaje Lissu ana nia ya kufanya mazungumzo kweli na hii habari si strategy ya kutoka jela tu?
Kwani utaratibu wa kutoka jela upoje!?

Una masharti ya kisiasa!? Kwanini yatumike masharti ya kisiasa kutoka jela!?
 
Sasa hapo hujaona kukataa mazungumzo ambayo hujui content yake ni nini ni ujinga?
Unawezaje kufanya mazungumzo na watu waliokataa kufanya mazungumzo nawe kabla ya uchaguzi? Kwa nini sasa? Je, ina maana mazungumzo yanafanyika tu pale wanapohitaji wao kufanya nawe, kama si unafiki?
 
Kwa sababu hakuna kesi, kesi nzima ni siasa.

Huelewi wapi?
Basi zitumike taratibu za kimahakama kufuta kesi hiyo. Kwa nini zitumike masharti ya kisiasa kumaliza kesi? Lissu ni mjuzi wa sheria; kwa nini akubali kesi zake zifutwe kinyume na taratibu za kimahakama kwa masharti ya kisiasa?
 
Mnataka Lissu aendelee kuwekwa ndani mpaka lini ? Hao watanzania wenyewe wamemsaliti Lissu, baadala ya kumpambania atolewe wengi wao wapo kwenye keyboard..Bado hatujajua tunataka nini
 
Unawezaje kufanya mazungumzo na watu waliokataa kufanya mazungumzo nawe kabla ya uchaguzi? Kwa nini sasa? Je, ina maana mazungumzo yanafanyika tu pale wanapohitaji wao kufanya nawe, kama si unafiki?
Unajua content ya hayo mazungumzo?

Nani alikataa mazungumzo kabla ya uchaguzi?

Ukiambiwa kuwa moja ya points za hayo mazungumzo ni kulazimisha serikali kurudia huo uchaguzi na hilo linahalalisha kufanya mazungumzo ama kulazimisha serikali iwe kwenye checkmate utasemaje?

Kama Lissu ndiye analazimisha masharti yake, utasemaje mazungumzo yanafanyika wanapotaka wao tu, kwani CHADEMA hawajakataa mazungumzo kabla ya uchaguzi? Hili hulijui?
 
Basi zitumike taratibu za kimahakama kufuta kesi hiyo. Kwa nini zitumike masharti ya kisiasa kumaliza kesi? Lissu ni mjuzi wa sheria; kwa nini akubali kesi zake zifutwe kinyume na taratibu za kimahakama kwa masharti ya kisiasa?
Taratibu za kimahakama ni zipi?

Kesi ikipigwa Nolle Prosequi na DPP huo ni taratibu ya kimahakama au si taratibu ya kimahakama?

Kwa nini unalazimisha sana kesi iende kisheria wakati kesi yenyewe ni ya kisiasa?
 
Unajua content ya hayo mazungumzo?

Nani alikataa mazungumzo kabla ya uchaguzi?

Ukiambiwa kuwa moja ya points za hayo mazungumzo ni kukazimisha serikaki kurudia huo uchaguzi na hilo linahalalisha kufanya mazungumzo ama kulazimisha serikali iwe kwenye checkmate utasemaje?

Kama Lissu ndiye analazimisha masharti yake, itasemaje mazungumzo yanafanyika wanapotaka wao tu, kwani CHADEMA hawajakataa mazungumzo kabla ya uchaguzi? Hili hulijui?
CHADEMA walikataa mazungumzo kwasababu yalikiuka masharti na misimamo yake.
 
Hatutaki aendelee kuwekwa ndani lakin yasitumike masharti ya kisiasa yeye kutoka gerezani.
Yeye ndio ameweka masharti aachiwe huru ili aweze kuingia katika mazungumzo, hapo usaliti upo wapi ? Kwenye mazungumzo kuna kukubaliana na kukataliana pia
 
Back
Top Bottom