CHADEMA imewasaliti Watanzania

CHADEMA imewasaliti Watanzania

Kwenye harakati Lissu alishawahi kumiminiwa risasi(assassination attempt) zaidi ya thelathini na risasi zisizo chini ya 16 zikamuingia mwilini, hao waliofariki kwa kupigwa risasi pasina shaka yoyote ni mashujaa sana katika historia ya kupambana haki na demokrasia lakini kwa kuwa tu walifariki haiwafanyi kuwa mashujaa zaidi ya mtu ambaye pia kwenye mapambano alimiminiwa risasi nyingi kwa lengo la kumuua ila akanusurika na mwili umejazwa mavyuma na una makovu lukuki ya majeraha ya risasi na ya surgeries alizofanyiwa katika kumtoa risasi nyingi mwilini mwake.
Lissu amevipigana vita vya kupigania haki na demokrasia na amehatarisha maisha yake kwa kiwango cha juu sana hivyo HADAIWI kabisa.
Nakubaliana nawe kabisa kwamba Lissu ni shujaa katika harakati za kupigania haki na demokrasia nchini Tanzania. Hata hivyo, hatua anayopanga kuchukua inaweza kuathiri sifa na heshima yake. Aidha, tukumbuke kuwa Watanzania wengi wamepoteza maisha wakipigania haki katika nchi hii; hivyo si vyema kutumia vifo vyao kwa manufaa ya kisiasa. Nina imani kwamba hatafanya hivyo
 
Iwapo jambo hili ni kweli, basi ni wazi kwamba CHADEMA imewasaliti Watanzania.
View attachment 3574549ma
Nadhani kila mmoja kafanya kwa upande wake. Itoshe tu kusema haikutosha hasa kwa upande wa wananchi cause CHADEMA walijitoa kushiriki mpaka uchaguzi mkuu,Chama kikapasuka katikati kama pazia la hekalu, mwenyekiti akakamatwa kwa kesi ya uhaini, Chama kikazuiwa mikutano na shughuli zote za siasa, waliohudhuria kesi ya uhaini walikiona cha moto. Lakini yote kwa yote et Chama hiki kipo hadi leo kana kwamba ndo kimeanzishwa. Wakati wa kielekea uchaguzi mpaka makamu mwenyekiti wa Chama walimshweka ndani. Kwa kifupi ilikuwa kama hamna Chama sabab walidhibitiwa kila kona ila kile chama cha mbogamboga kuna sehemu walijichanganya na hawatoweza kurekebisha bila kutumia nguvu. Watanzania pia kwa upande wao walifanya jambo ingawa halikutosha kulingana na nguvu waliyokutana nayo inayosemekana ilikuwa sawaswa kutumiwa.. SASA SI WAKATI WA KULAUMIANA sababu Chadema na pia TL amepambana sana kwa upende wake hata akitoka akikaa pembeni kwangu sitomdai maana anahistoria chungu sana juu ya siasa za Tanzagiza na kiukweli kawafungua wenye akili macho!!
 
Hivi we una akili timamu? Amepambana kuliko waliofumuliwa vichwa october 29? Kuna sapoti kubwa kama ile ya october 29?, chadema haikushiriki maandamano lakini vijana waliingia mitaani kwa kupambania ajenda zilizopambaniwa na chadema, hivyo hata lissu ana deni, akitoka huko anatakiwa kuendeleza mapambano, watu wamemwagwa utumbo huku nje , yeye yuko jela lakini shavu dodo, TUNAWADAI
Mkuu Lisu huyo asingekuwa bahati yake basi ni zaidi ya oct29. Jamaa bado anatembea na risasi mwilini. Tukio la oct29 Lisu lilishampata nyuma zaidi na bado karudi anapambania hadi kesi ya uhaini kapewa. Unataka afanye nini? Unamdai nini? Sidhani kma majeruhi waliopigwa risasi oct29 wanaweza kurudi kupambana tena kma TL alivyofanya. Lisu aliweza kuacha hizi mambo na shavu likawa dodo zaidi. Usimlaumu mtu alikuwa jela yeye na makamu wake ni wamesimuliwa tu kilichotokea.
 
Mlitaka afie jela?

Hao anaowafia wanafanya nini?

Mnashia kupiga kelele jf tu

Mkiambiwa changia chama hamtaki, lissu amekaa mwaka mzima gerezani

Nyie mmefanya nini?

Mwache atoke tu
Hatuna shida na Lisu, lakini asijaribu kununua uhuru wake kwa kutumia damu ya watanzania waliouawa tarehe 29 October.
 
Why usimfate aliefanya watu wafe?
Lissu asijaribu kupata uhuru wake wa kisiasa kwa kutumia damu ya Watanzania. Taratibu za kesi zinajulikana: akipatikana na hatia, apewe adhabu kulingana na sheria; na asipopatikana na hatia, aachiwe huru. Hata hivyo, asitumie damu ya Watanzania kununua uhuru wake.
 
Nadhani kila mmoja kafanya kwa upande wake. Itoshe tu kusema haikutosha hasa kwa upande wa wananchi cause CHADEMA walijitoa kushiriki mpaka uchaguzi mkuu,Chama kikapasuka katikati kama pazia la hekalu, mwenyekiti akakamatwa kwa kesi ya uhaini, Chama kikazuiwa mikutano na shughuli zote za siasa, waliohudhuria kesi ya uhaini walikiona cha moto. Lakini yote kwa yote et Chama hiki kipo hadi leo kana kwamba ndo kimeanzishwa. Wakati wa kielekea uchaguzi mpaka makamu mwenyekiti wa Chama walimshweka ndani. Kwa kifupi ilikuwa kama hamna Chama sabab walidhibitiwa kila kona ila kile chama cha mbogamboga kuna sehemu walijichanganya na hawatoweza kurekebisha bila kutumia nguvu. Watanzania pia kwa upande wao walifanya jambo ingawa halikutosha kulingana na nguvu waliyokutana nayo inayosemekana ilikuwa sawaswa kutumiwa.. SASA SI WAKATI WA KULAUMIANA sababu Chadema na pia TL amepambana sana kwa upende wake hata akitoka akikaa pembeni kwangu sitomdai maana anahistoria chungu sana juu ya siasa za Tanzagiza na kiukweli kawafungua wenye akili macho!!
Ni mada ya kichokonozi tu; haina lolote jipya..

Mtu ukitaka kupima upepo, anzisha mada ya kichokonozi kama hii.

Sasa wasomaji tukikubali kuwa "CHADEMA imewasaliti watanzania"..., halafu iweje? Tufurahi pamoja na hao wanaotukandamiza?

"CHADEMA imewasaliti watanzania"!
Kwa kufanya nini?
Wametangaza kuwa wanakubaliana na matakwa ya hao waovu waliopo madarakani kwa kutumia mabavu?

Uelewa wa kilichosemwa na hicho chama wa huyo mleta mada, ndicho kipimo sahihi cha kutuonyesha sisi wote kwamba "CHADEMA imewasaliti watanzania"?
 
Lissu asijaribu kupata uhuru wake wa kisiasa kwa kutumia damu ya Watanzania. Taratibu za kesi zinajulikana: akipatikana na hatia, apewe adhabu kulingana na sheria; na asipopatikana na hatia, aachiwe huru. Hata hivyo, asitumie damu ya Watanzania kununua uhuru wake.
Wewe ni mpuuzi, unayefaa kupuuzwa.
Useless bitch!

Lissu amekwambia anataka uhuru wake kwa kutumia damu ya waTanzania? Hivi kichwani zinakutosha kweli wewe?

Nilitaka nikuache uendelee na upumbavu wako; lakini sasa nimeamua kuwa nawe.
 
Hivi we una akili timamu? Amepambana kuliko waliofumuliwa vichwa october 29? Kuna sapoti kubwa kama ile ya october 29?, chadema haikushiriki maandamano lakini vijana waliingia mitaani kwa kupambania ajenda zilizopambaniwa na chadema, hivyo hata lissu ana deni, akitoka huko anatakiwa kuendeleza mapambano, watu wamemwagwa utumbo huku nje , yeye yuko jela lakini shavu dodo, TUNAWADAI
Wewe uliingia? Mambo huwa yanaenda kwa hatua, nadhani ni muda jamaa apumzike awe anatoa ushauri. Huenda wewe au mwingine umefika muda wako wa kwenda kufikisha hayo makwazo. Sio lazima hata uwe mwanasiasa, unaweza kufanya kwa namna yako. Andika hata vitabu, tengeneza content n.k
 
Lissu asijaribu kupata uhuru wake wa kisiasa kwa kutumia damu ya Watanzania. Taratibu za kesi zinajulikana: akipatikana na hatia, apewe adhabu kulingana na sheria; na asipopatikana na hatia, aachiwe huru. Hata hivyo, asitumie damu ya Watanzania kununua uhuru wake.

Afie jela au
 
😎 Okay,unakiri watu walikufa? Je nani aliwauwa? Kwa idhini ya nani?
 
Iwapo jambo hili ni kweli, basi ni wazi kwamba CHADEMA imewasaliti Watanzania.
View attachment 3574549ma
Hao Watanzania walio HURU wamefanyia nini hadi sasa kukabiliana na wauaji wa ndugu zetu??
Kama kweli matarajio yao ni kwa CHADEMA na LISSU ni kwanini wanahofu na UHURU wa LISSU?

CHADEMA tayari imekuwa HURU kisheria.
LISSU naye awe HURU kisheria!
Yap, sote tuwe HURU kisheria alafu mpira uletwe kati!

Hapo usaliti ni upi?
 
Back
Top Bottom