Safari_ni_Safari
JF-Expert Member
- Oct 5, 2007
- 23,268
- 17,099
Shehe wa Msikiti wa Bondeni, Shaaban Juma, alisema familia hiyo haina haja ya kuomba radhi, kwa kuwa alishirikiana nayo kwa hali na mali, lakini akashangazwa alipoambiwa na mmoja wa wanafamilia, aondoke kwenye chumba cha maiti na angempigia simu baadaye, kwa kuwa suala hilo lilikuwa likiihusu familia pekee.
Alisema kamwe hawezi kuiomba radhi familia hiyo wala kutoa msamaha yeye, kwani familia imemkosea Mwenyezi Mungu na si Waislamu, kwa kukiuka misingi na taratibu za dini hiyo na iwapo iliona inazidiwa nguvu, ilipaswa kukabidhi jukumu hilo kwa viongozi wa kiislamu ili walisimamie.
"Mbali na Qur'an na Hadithi za Mtume kukataza, lakini kitendo cha kumpeleka marehemu wa
kiislamu uwanjani pale, ambao uligubikwa mapambio ni kinyume na maamrisho ya Mwenyezi Mungu na ni moja ya sababu iliyosababisha yeye asihudhurie maziko hayo," alisema Shehe Shaaban.
Juzi Chadema iliendesha ibada maalumu ya kuaga miili ya marehemu wawili waliopoteza maisha katika mapambano baina ya wafuasi wa Chadema na Polisi kutokana na kufanya maandamano yaliyozuiwa kwa kuhofia uvunjifu wa amani ambapo watu watatu walipoteza maisha.
SOURCE: Habari Leo
Watu wanacheza na Mungu