Chadema hawajakiuka maadili?

Chadema hawajakiuka maadili?

Wakuu hebu someni hiyo habari hapo chini kutoka huko huko habari leo utaona jinsi walivyokuwa wanataka ku-invent kitu ambacho hata hakikuwepo. Yaani ni ushabiki mtupu.

Cha ajabu hata polisi wenyewe hawajamshtaki Dr. Slaa kwa makosa ambayo habari leo walitaka wananchi wayaamini!


ARUSHA KWALIPUKA

Imeandikwa na John Mhala, Arusha; Tarehe: 5th January 2011

Source: Hapa

WABUNGE wanne wa Chadema wamesekwa rumande katika kituo kikuu cha Polisi mjini hapa baada ya kukaidi amri ya Polisi ya kuacha maandamano.

Mbali ya wabunge hao kutiwa ndani pia mke wa Katibu Mkuu wa Chadema Willibrod Slaa, Josephine Mushumbusi, naye amekamatwa na kutiwa ndani huku akiwa na majeraha ya kupigwa na polisi.

Pia wafuasi watatu wa chama hicho walijeruhiwa kwa risasi za moto na polisi waliokuwa wakidhibiti maandamano ya wafuasi hao.

Kabla ya matukio hayo, tangu jana asubuhi hadi mchana ulinzi wa polisi uliimarishwa karibu kila kona za Jiji, lakini wafuasi wa Chadema walikaidi amri ya Mkuu wa Polisi, IGP Said Mwema ya kutofanya maandamano.

Badala yake, wafuasi hao walitii mwito wa Dk. Slaa aliyetangaza kupitia vyombo vya habari kuwa wataandamana licha ya amri halali ya Jeshi la Polisi ya kutoandamana.

Wafuasi hao ambao wote walikuwa na vitambaa vyeupe kichwani na vingine vikubwa vilivyoandikwa ujumbe, mabango na wengine wakiimba nyimbo za kumtukuza Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, waliandamana wakielekea uwanja wa NMC.

Katika hoteli ya kitalii ya Mount Meru ambako ndiko viongozi wa juu wa Chadema walikofikia, polisi walilazimika kutumia maji ya kuwasha kutawanya wafuasi hao.

Mbali ya hilo katika Kata ya Sombetini, wafuasi hao waliokuwa na vitambaa vilivyosomeka ‘Meya wa Jiji la Arusha wa CCM ni wa kuchongwa’, mengine yakisomeka: 'Tunataka uchaguzi wa Meya urudiwe’, walitawanywa kwa nguvu.

Hata hivyo polisi, mgambo na askari wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) walidhibiti kwa asilimia kubwa maandamano hayo licha ya kwamba wengine waliandamana kwa magari yenye bendera za chama hicho ili kuchelea kibano.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Thobis Andengenye, alipoulizwa kwa njia ya simu kama ana taarifa juu ya matukio hayo, alijibu kwa kifupi kuwa yuko kwenye kikao hivyo hawezi kutoa maelezo hadi baadaye.

Hata hivyo, katika mkutano wa hadhara ambao Slaa alianza kuhutubia saa 6 mchana, aliwataja kwa majina wabunge waliokamatwa, kuwa ni pamoja na wa Hai, Freeman Mbowe ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama hicho na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni.

Dk. Slaa aliwataja wengine kuwa ni Joseph Selasini wa Rombo, Lucy Owenya wa Viti Maalumu na wa Arusha Mjini Godblles Lema ambao wote wako ndani katika kituo kikuu cha Polisi.

Katibu huyo alisema pia kuwa vijana watatu wa chama hicho walijeruhiwa kwa risasi na waliswekwa rumande walipokwenda kituoni hapo kutaka kuchukua fomu namba tatu ya matibabu - PF3.

Dk. Slaa aliwahamasisha wananchi waliofurika katika mkutano huo kuwa iwapo polisi watagoma kuwaachia huru wabunge, mkewe na vijana waliojeruhiwa, atawaachia wafuasi wa chama hicho mjini hapa, kuamua cha kufanya kwani yeye hatahusika kwa lolote.

“Ninawapa muda polisi kuwaachia viongozi wote wa Chadema walioko ndani na ikishindikana umma wa wakazi wa Arusha utaamua la kufanya na mimi sitahusika na lolote,’’ alisema.

Baadaye amri hiyo ilitolewa na wafuasi hao kuelekea kituo cha Polisi ambako walikumbana na mabomu ya kutoa machozi.

Dk. Slaa alifikia hatua hiyo baada ya kuona hakuna uwezekano wa kuwaachia viongozi hao bila masharti ili warudi kuhutubia wananchi juu ya mustakabali wa kwa nini Jiji la Arusha lina Meya wa CCM.

Baada ya kauli hiyo umati ulielekea katika kituo cha Polisi wakitii amri ya kiongozi wao, lakini ghafla Polisi ilionesha ubavu wake na kumimina mabomu huku mamia ya wafuasi hao wakionesha hofu na kutawanyika hovyo mitaani.

Hali hiyo pia iliwakuta pia waandishi wa habari. Hata hivyo habari zilisema waandishi wanne wanashikiliwa na Polisi kwa kilichoelezwa na Jeshi hilo kuwa ni kushabikia Chadema.

Baadhi ya wachambuzi wa masuala ya kisiasa wamesema hatua ya Dk. Slaa kuruhusu wafuasi wake kuvamia kituo cha Polisi ili kuwatoa watuhumiwa ni uchochezi usiovumilika, ambao unaweza kuhatarisha maisha ya watu na amani ya nchi kwa jumla.

Hata hivyo, wengine wameomba suluhu ya kudumu ipatikane ili kuepusha umwagaji damu mkoani humo ambao unachochewa na tofauti za itikadi za kisiasa lakini na uchochezi wa wanasiasa.

Wakati huohuo, katika hali isiyotarajiwa, Diwani wa Sombetini kwa tiketi ya CCM, Alphonce Mawazo, alimkana Rais Jakaya Kikwete mbele ya umati mkubwa wa watu kuwa hakumpigia kura bali alimpigia Dk. Slaa.

Mawazo ambaye aliibuka ghafla kwenye mkutano huo na kulazimishwa kupanda jukwaani, alisema yeye ni mwanamageuzi wa kweli na anaikubali Chadema kwa asilimia kubwa na ndiyo maana katika kura ya urais aliipigia Chadema.

Diwani huyo alisema hayo jukwaani alipokaribishwa na Dk. Slaa na kupewa kipaza sauti na kutamka kuwa yeye ni Chadema ‘damu damu’ ndiyo maana alikuwa hapo kusikiliza mkutano huo na kushukuru kupewa nafasi na kueleza azma yake.

Chadema imekuwa ikidai kupitia kwa Dk. Slaa, kwamba halmashauri za majiji ya Mwanza na Arusha; Hai na Kigoma Ujiji, uchaguzi wa mameya ulivurugwa katika mazingira yanayoashiria kuwapo maelekezo kutoka ngazi za juu.

Hivyo chama hicho kutoa masharti kwamba usifanyike uchaguzi wowote wa mameya au wenyeviti wa halmashauri Mwanza, Kigoma/Ujiji, Arusha na Hai.

Pia Mkurugenzi wa Manispaa ya Arusha ajiuzulu kwa madai ya kukiuka kanuni za halmashauri na kusimamia uchaguzi kinyume na taratibu, vilevile kinalalamika kwamba uongozi wa TAMISEMI uliingilia uchaguzi hasa Kigoma/Ujiji, hivyo wahusika wote wachukuliwe hatua.

Chama hicho pia kinaitaka Serikali imchukulie hatua Ofisa Upelelezi wa Arusha kwa madai ya kuingia na kumkamata mbunge ndani ya kikao halali kinyume na kanuni za uendeshaji wa halmashauri, hivyo kinataka ofisa huyo ajiuzulu au aondolewe.

Chadema pia inadai kuwa polisi ni watuhumiwa katika matukio ya Arusha, hivyo kama hakutakuwa na maridhiano Serikali itakuwa imewalazimisha kuchukua hatua.

Hii ni mara ya pili katika kipindi cha chini ya mwezi, kwa wafuasi wa Chadema kukabiliana na Polisi, mara ya kwanza ikiwa ni Desemba 18 Polisi ilipokabiliana na vurugu zilizoongozwa na Mbunge wa Arusha, Godbless Lema.

Katika ghasia hizo, Lema alipigwa na kulazwa katika Hospitali ya Mkoa ya Mount Meru kwa matibabu, kabla ya hapo Polisi ilishatumia maji ya kuwasha na mabomu ya kutoa machozi kutawanya wafuasi hao waliokuwa wamezingira Ofisi ya Manispaa ya Arusha.

Vurugu hizo zilitokana na Chadema kususia uchaguzi wa meya na hivyo CCM na TLP kuendelea nao na kumchagua Diwani wa Olorien, Gaudence Lyimo akisaidiwa na Michael Kivuyo wa TLP, ambaye ni Diwani wa Sokoni.
 
FAMILIA ya marehemu Ismail Omari (25) aliyeuawa katika vurugu za kisiasa zilizotokea Januari 5 mwaka huu mkoani hapa, imedai kushinikizwa na Chadema kumpeleka marehemu wao katika uwanja wa NMC kuagwa kinyume na maamrisho ya dini yao.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, baba mzazi wa marehemu huyo Omar Juma,
alisema shinikizo lililowafanya kukubali kitendo hicho lilitolewa juzi usiku baada ya msemaji wa familia yake, Nyerere Kamili, kupokea simu kutoka kwa mmoja wa viongozi wa Chadema; Diwani wa Elerai, John Bayo, kuwa iwapo hawatakubali kupeleka mwili wa ndugu yao kwenye uwanja huo, chama chake kitajitoa kushughulikia mazishi.

Alidai mbali na shinikizo hilo, pia juzi wakiwa chumba cha maiti, katika hospitali ya mkoa ya Mount Meru, kuchukua mwili huo, walikuta mazingira yasiyo mazuri kwao kugomea kupeleka mwili huo wakihofia kudhuriwa na wafuasi wa Chadema, ambao walikuwa wamefurika eneo hilo wakitaka miili yote ipelekwe uwanjani kuagwa.

Alisema kutokana na sababu hizo, pia alilazimika kuwapigia simu viongozi hao wa Chadema na alikutana nao siku hiyo, wakakubaliana kuupeleka mwili huo uwanjani hapo, ili kupata msaada wa chama hicho wa mazishi kwa kuwa hawana uwezo wa kuendesha mazishi hayo.

“Sasa baada ya sisi kupokea simu hiyo, tulilazimika kuwapigia simu ili kupata msaada, maana vifo vimetokana na mkutano wao, sasa uwezo hatuna na hali ilivyokuwa pale, tungeweza kupigwa hata mawe na wafuasi wao kwa hiyo ilikuwa hivyo,” alisema Omar.

Pia alisema kutokana na shinikizo hilo, liliipa wakati mgumu familia yake baada ya Waislamu kuchukizwa na kitendo hicho hadi kufikia kunyimwa jeneza la kubebea maiti hali iliyowalazimu kuhangaika katika zaidi ya misikiti mitatu bila mafanikio.

Aliongeza kuwa baada ya hali hiyo, alikwenda kuchukua jeneza kwenye msikiti wa hospitali ya Mount Meru akikodi kwa Sh 5,000 ambayo hadi jana walikuwa wakidaiwa kutokana na kushindwa kulipa.

Kwa hali hiyo na kutambua kuukosea Uislamu na Waislamu kwa jumla, aliwaomba viongozi kuisamehe familia yake kwa kuwa haikuwa dhamira yao kufanya hivyo, bali kwa shinikizo la Chadema.

Mwenyekiti wa Wenyeviti wa Baraza la Wazee wa Chadema wa Mkoa wa Arusha, Haruna Fundikira, alipoulizwa kuhusu suala hilo alikiri na kusema hata yeye aliungana na familia ya marehemu, kuwa suala la kupeleka maiti katika uwanja huo halikuwa sahihi kulingana na maamrisho ya dini.

Alisema walichokubaliana ni kupata japo picha ya marehemu Ismail ili ioneshwe uwanjani hapo, lakini maiti achukuliwe na kupelekwa kwa maziko Usa River, lakini alishangazwa na taarifa kuwa mwili huo ulipelekwa uwanjani hapo.

Alisema siku moja kabla ya maziko, alikwenda kwa familia ya marehemu kupanga mipango ya maziko hayo na walipokubaliana juu ya taratibu hizo, aliahidi kutoa sanda, lakini alilazimika kuahirisha kuitoa, baada ya kuona utaratibu tofauti na aliokubaliana na familia hiyo.

"Mimi jana sikwenda uwanjani hapo, nilikuwa na mgeni nyumbani, lakini nilichosikia ni kwamba walipeleka mwili huo uwanjani tofauti na nilivyokubaliana nao na sikutoa tena sanda, maana walikuwa na uamuzi wao kama familia,” alisema Fundikira.

Aliongeza kuwa, baada ya kuahirisha kutoa sanda, alipokea simu kutoka kwa Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, akisema ameshakubaliana na familia kuhusu taratibu zote za maziko na asihangaike kutoa sanda, kwani chama kitatoa.

Shehe wa Msikiti wa Bondeni, Shaaban Juma, alisema familia hiyo haina haja ya kuomba radhi, kwa kuwa alishirikiana nayo kwa hali na mali, lakini akashangazwa alipoambiwa na
mmoja wa wanafamilia, aondoke kwenye chumba cha maiti na angempigia simu baadaye, kwa kuwa suala hilo lilikuwa likiihusu familia pekee.

Alisema kamwe hawezi kuiomba radhi familia hiyo wala kutoa msamaha yeye, kwani familia imemkosea Mwenyezi Mungu na si Waislamu, kwa kukiuka misingi na taratibu za dini hiyo na iwapo iliona inazidiwa nguvu, ilipaswa kukabidhi jukumu hilo kwa viongozi wa kiislamu ili walisimamie.

“Mbali na Qur’an na Hadithi za Mtume kukataza, lakini kitendo cha kumpeleka marehemu wa
kiislamu uwanjani pale, ambao uligubikwa mapambio ni kinyume na maamrisho ya Mwenyezi Mungu na ni moja ya sababu iliyosababisha yeye asihudhurie maziko hayo,” alisema Shehe Shaaban.

Juzi Chadema iliendesha ibada maalumu ya kuaga miili ya marehemu wawili waliopoteza maisha katika mapambano baina ya wafuasi wa Chadema na Polisi kutokana na kufanya maandamano yaliyozuiwa kwa kuhofia uvunjifu wa amani ambapo watu watatu walipoteza maisha.

Katika hatua nyingine mwili wa marehemu Denis Shirima, nao ulihamishwa kutoka sanduku ambalo lilionekana kuwa duni na kuingizwa katika sanduku la kifahari, ambalo lilinunuliwa na Chadema.

Awali marehemu alikuwa kwenye sanduku la kawaida la rangi nyeupe wakati mwili ukiwa hospitalini tayari kupelekwa kwenye uwanja wa NMC kuuagwa, lakini baadaye ukabadilishiwa kwenye sanduku hilo jipya na la zamani haikujulikana lilikopelekwa.



SOURCE: Habari Leo
 
Tulishajibu kwamba ni AHERI UWE NA KASHFA YA CHADEMA KUOKOTA NA KUZIKA MWILI WA BINADAMU ULIOCHINJA KIKATILI NA KUTELEKEZWA PEMBENI MWA BARABARA KWENYE MTARO WA MAJI MACHAFU ARUSHA KULIKO kujibidisha uonekane MALAIKA kama CCM mbele ya Mabalozi kwenye sherehe ya kukata na shoka ikulu muda mfupi tu baada ya kutoka kuua raia wako mwenyewe katika nchi yako.
 
Kumbe nacho hicho ki-gazeti ka-serikali nako sikuhizi kanaandika HABARI ZA KIINTELIJENSIA YA UDAKU sawa tu na 'Sani' na 'Ijumaa'?
 
Nawashangaa hawa habari leo yaani tangia mauwaji yametokea Arusha yaani ndiyo habari yao ya kwanza waliyoipata


hahaha


Tunataka KATIBA mpya jamani
 
Ishu sio mwili ulizikwaje au ulizikwa na nani, ishu ni kwanini polisi waliua raia wasio na hatia?
Polisi wana maslahi gani na CCM kiasi kwamba hadi wapo tayari kuua ili kukiweka ccm madarakani?
Mhariri wa Habari leo awafafanulie wasomaji wake swala hilo.
 
Hawa ni waongo na wapuuzi,ni polisi waliotishia familia ya marehemu na kuwashawishi kutokupeleka maiti uwanjani,hali iliyofanya cdm wajitoe,dakika za mwisho hiyo familia mida ya saa mbili asubuh wakaja kuomba wasamehewe na cdm wakakubali,sasa tatizo hapa ni nini?ila hii familia pia haina msimamo maana walikuwa kama wanatukomoa kwa kutoa masharti eti cdm watoe kg 400 za mchele ndipo wakubali,cdm wakakataa kutoa ila walipewa ubani wa 500000,
 
Serikali haijawandendea haki wafiwa, inaonekana kama kwamba wailokufa si Watanzania, CCM na Vyama vingine vya Siasa kama CUF hawajatoa hata Salaam za rambi rambi kwa Wafiwa au Kwa Cdm. Siasa zetu zinaonekana kama chuki ya aina yake(Mauaji) na siyo chuki ya kuendeleze jamii, hasa kuwatoa Masikini hapo walipo kufikia sehemu ambayo watazeza kupata hata mlo mmoja wa uhakika.
 
Strangely habari hii imeandikwa kwenye Uhuru na Habari Leo pekee!
 
hiyo ni mipango ya kujisafisha tu,lakini hakuna jipya kwani tumeshawazoea hao
wanatumia kodi za wananchi kujisafisha
 
hata mimi nilisema haya, nikaambiwa mzushi na muongo. lkn sasa ni valid kabisa
 
Upuuzi mtupu, kwani pale ilipelekwa kwa minajilili ya dini au kuonyesha mshikamano na kupinga udhalili wa polisi na serikali.

Lakini mara ngapi maiti za kiislam zinawekwa kwenye hadhara kwa ajili ya heshima za mwisho. Kikubwa hairuhusiwi kufunua!. Maiti ya Kawawa ilipelekwa Karimjee, Dr. Omary Juma, Mzee Natepe na hata Prof. Haroub Othman au hawakuwa waislam (makafir)
 
Huu ni mwanzo tu bado yatakuja mengi.
Swala lenyewe tayari lishahusishwa na dini, mara mashehe wapingana na maaskofu juu ya umeya Arusha, hivyo mgongano wa mawazo lazima uwepo, ukute huyo msemaji wa familia kashinikizwa pia kusema maneno hayo aliyoyasema.

Na hapo wazee wa kijani wakishaingilia ndipo tutasikia mengi. Siasa za nchi balaa
 
This is one side of story, what about another side? we cant conclude anything from Habari leo!

All in all, the new religion of deceased (RIP) was neither christian nor muslim... he had new religion "Mtanzania" that sound better than these 'imported' religions of muslim and christian
 
Walikua na uhuru wa kukataa kumpeleka. kwanini hawakukataa, wasituzuge! au sisiemu wameshatia sumu yao katika hiyo familia?
 
Hiv habari leo mechoka vya kuandika ss upuzii gani mnatuambia kama mechoka acheni mcwe kama sani,ijumaa,na tabasamu upuuziiiiiiiiiiiiiiiiiii mtupu
 
i smell something fish here..... these people they never seize to find something to implicate others... sasa hapo wanataka kutuambia nini... ok dini yaho hairuhusu so?... typical crap...... hao wanafamilia wanatumiwa kwa kigezo cha udini.... hakuna mtu anayelazimishwa kwa maswala ya msiba eti kisa hawana uwezo angekuwa amekufa kwa ajali aisngezikwa huyo kwasababu hamna uwezo au?... acheni mambo yenu ya ajabu .....
 

Shehe wa Msikiti wa Bondeni, Shaaban Juma, alisema familia hiyo haina haja ya kuomba radhi, kwa kuwa alishirikiana nayo kwa hali na mali, lakini akashangazwa alipoambiwa na mmoja wa wanafamilia, aondoke kwenye chumba cha maiti na angempigia simu baadaye, kwa kuwa suala hilo lilikuwa likiihusu familia pekee.
HabariLeo | Chadema kwenye kashfa ya maiti
Inaelekea familia hiyo imegawanyika!
 
Hawa habari leo wamekosa cha kuandika, mwisho wao unakaribia.
 
Back
Top Bottom