Mbunge Mwambe Awakutanisha Viongozi wa Vyama vya Msingi Vilivyo Jimbo la Ndanda

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,897
941

MBUNGE MWAMBE AWAKUTANISHA VIONGOZI WA VYAMA VYA MSINGI VILIVYO JIMBO LA NDANDA

Huu hapa ushauri wa vyama vya ushirika vya Ndanda juu ya sheria ya mabadiliko ya ushirika

Viongozi wa vyama vya msingi kutoka Jimbo la Ndanda wameshauri sheria ya ushirika ifanyiwe marekebishi ili kuongeza idadi ya watu wanaoweza kuanzisha chama cha msingi, AMCOS.

Sheria ya sasa inaruhusu watu 20 wanaweza kuanzisha AMCOS jambo ambalo wanasema linasababisha kuwanna utitiri wa vyama ambavyo vingi vinashindwa kujiendesha.

Hivyo wajumbe wameshauri kila kata kuwa na AMCOS moja bila kuathiri zilizopo.

Huu ni moja ya ushauri uliotolewa leo Januari 22, 2024 katika kikao cha Mbunge wa Ndanda Cecil Mwambe na wawakilisha wa viongozi wa vyama 23 vya msingi katika Jimbo la Ndanda juu ya mabadiliko ya sheria ya ushirika na stakabadhi za ghala.

Wawakilisha hao wa wakulima pia wameshauri uongozi wa vyama vya Msingi na vyama vikuu viwe na muda wa miaka mitano na bila ukomo kama ilivyo kwa wabunge na madiwani, kwani kipindi cha miaka mitatu ni kifupi, na endapo Mwenyekiti atakuwa amefanya makosa, basi sheria ya Ushiriki itamuondoa na kuitisha uchaguzi mwingine.

Wajumbe walishauri pia Mh. Mbunge aishauri serikali kuendelea kupunguza makato kwenye zao la korosho ili kumuongezea tija mkulima.

Viongozi wamependekeza na kushauri Serikali kutoruhusu zao la choroko kuingia kwenye mfumo Wa stakabadhi ghalani kwani zinabunguliwa sana hata zikiwa shambani na kuwa na hofu ya kusababisha hasara kwa wakulima.

Pia wameshauri sheria kuwatambua makatibu wa AMCOS kuwa ni wawakilishi au wajumbe wa nkutano mkuu wa chama kikuu kwani wao ndiyo wawajibikaji wa ofisi za AMCOS kwa kila siku, lakini sheria haiwaruhusi kuingia kwenye mkutano mkuu.

Katika kikao hicho
Mkuu wa Wilaya ya Masasi, Lauteri Kanoni amewasihi viongozi wa vyama vya msingi kuwatumikia wakulima kwa uadilifu.

Amewataka viongozi hao kuwawakilisha wakulima na kuwakumbusha kuwa huu ni mwaka wa uchaguzi kwao.

Aidha Mkuu wa Wilaya amempongeza Mh Cecil kwa kuamua kukaa na viongozi wa vyama vya msingi.

Mwisho
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2024-01-22 at 23.40.57.jpeg
    WhatsApp Image 2024-01-22 at 23.40.57.jpeg
    84.9 KB · Views: 1

Similar Discussions

Back
Top Bottom