Hahaaaaaa.......Haya bana....
Na mpira umekwishaa.....Mpira umekwisha ndugu wana JF.....
Tanzania bara, Kilimanjaro Stars wanaondoka na ushindi wa magoli mawili kwa bila dhidi ya Rwanda......Magoli ya Tanzania bara la kwanza limefungwa na Amri Kiemba dakika ya 34 baada ya kupata pasi kutoka kwa Mwinyi Kazimoto aliyeiwachambua mabeki wa Rwanda kutoka kona ya kushoto na kutoa V pasi ambayo ilimkuta Amri Kiemba ambaye bila ajizi alimuangalia Jean Claude Ndoli amekaaje na kuujaza mpira wavuni, goli la pili limefungwa na John Bocco ambaye alitumia vizuri uzembe wa kipa Jean Claude Ndoli ambaye aliutema mpira(shuti kali) uliopigwa na mtaalamu Mwinyi Kazimoto.......
Kwa ujumla timu zote leo zimecheza vizuri na zilikuwa zikishambuliana kwa kupokezana na kwa maoni yangu Mwinyi Kazimoto ndiye MOTM kwa mchezo wa leo....
Pia pongezi ziwaendee makipa wote wawili Juma Kaseja wa Tanzania bara na Jean Claude Ndoli wa Rwanda ambao wameokoa michomo mingo iliyoelekea katika magoli yao......
Kwa matokeo haya Tanzania imesonga kwenda Nusu Fainali na wanasubiri mshindi kati ya Uganda na Ethiopia hiyo kesho ambaye ndiye watapambana naye katika mechi ya Nusu fainali......
Hongereni sana watanzania....
Kwa niaba ya mtangazaji/mchambuzi mwenzangu
watu8 , msimamizi wa matangazo haya
Eqlypz na Fundi mitambo
Invisible nawarudisha moja kwa moja studio namba moja ya JF kuendelea na matangazo ya mechi kati ya Intamba Murugamba ya Burundi na Zanzibar Heroes......Kia la heri Zanzibar Heroes.....
Wakatabahu.....
Bala.