CDM wamesusia sherehe za uhuru

Kama Kikwete mwenyewe alijua kuwa watu watamkimbia uwanjani kwa nini ahutubie? CDM walilijua hilo na wao wakaamua kutokwenda kabisa. Hawakagui gwaride, hawapigiwi salute, sasa ya nini waende? Ila mwakani, lazima CDM wafanye sherehe yao ya UHURU.

Nina imani hatakuja kuhutubia tena umati wa watu, labda waje CCM na wawalipe hela....

Sidhani kama anajali sana kuwa mnampenda au hamumpendi. Yeye ni Rais wenu na hamna mwingine.

Mlie au msage meno, Rais ni yeye. Labda mwaka 2016 mje mumpandishe Kizimbani ........

Ningelitamani sana kuona mwaka 2016 Zito Kabwe akiwa Waziri wa mambo ya ndani ......



Safi sana: Hapa Zitto anamwita Dr. Slaa Ndugu Rais.
 
Last edited by a moderator:
Tutatue haya kwanza ndio tusheherekee uhuru wa tanganyika
1. Tuondoe ujinga vijana wetu wasome bila ubaguzi elimu kwa wote bila kodi
2. Tuondoe maradhi, afya bure kwa wote serikali igharimie kwa kodi za wananchi
3. Tuondoe nyumba za tembe na mbavu za umbwa
4. Tuondoe huu umaskini wa kutupwa kwa kuweka serikali makini ituongoze kwa manufaa ya umma, wizi wa rasilimali za nchi hii inatufanya maskini wa kutupwa.
5. Tuondoe mafisadi na ufisadi

tulete katiba mpya
 
Viongozi wa CHADEMA hawakuwa na haja ya kwenda maana hamna nchi inayoitwa Tanzania bara iliyopata uhuru toka kwa Waingereza bali ipo nchi inayoitwa Tanganyika ambayo ilipewa uhuru na Ndugu Nyerere akawa waziri wake mkuu wa kwanza. CCM walikuwa wanasherekea uhuru wa Tanzania Bara kitu ambacho hakipo duniani wala ahera wala motoni!
 
Binafsi nimetazama ITV na TBC1 nichoona ni viongozi wa CCM na uongozi wa juu wa CUF akiwemo Maalim Seif ila sikuona kiongozi yeyote wa juu wa CDM yaani Mbowe, Arfi, Slaa, Lissu, Zitto wala Mnyika. Ndiyo tuseme walimaanisha walichosema?

Hivi kwani ni uhuru wa nchi gani?? Je hiyo nchi bado ipo?? Na wananchi wake wanatambua kuwa hiyo nchi ipo???

Isije kuwa kusherehekea nchi ambayo haipo??? Tuirudishe hai kikatiba na wananchi wake tuhakikishiwe uhuru wetu kisha ndipo tutasherehekea.

Mi nashukuru ipo maana jana imenisaidia kujifungia ndani kwangu na familia kujipooza na hectic za job
 
Hizi sherehe zingesitishwa mpaka tuwe na tafsiri halisi ya ni maadhimisho gani tunayafanya ya nchi ipi kwa sababu uhuru ulikuwa wa Tanganyika leo Tanganyika haina hata bendera sisi tunaadhimisho kwa nchi isiyokuwepo kwenye uso wa dunia ajabu kweli
 
Binafsi nimetazama ITV na TBC1 nichoona ni viongozi wa CCM na uongozi wa juu wa CUF akiwemo Maalim Seif ila sikuona kiongozi yeyote wa juu wa CDM yaani Mbowe, Arfi, Slaa, Lissu, Zitto wala Mnyika. Ndiyo tuseme walimaanisha walichosema?

Sasa watu waliochanganyikiwa unafikiri watakuja uwanjani ????? kushindwa kubaya sana !!!
 
Binafsi nimetazama ITV na TBC1 nichoona ni viongozi wa CCM na uongozi wa juu wa CUF akiwemo Maalim Seif ila sikuona kiongozi yeyote wa juu wa CDM yaani Mbowe, Arfi, Slaa, Lissu, Zitto wala Mnyika. Ndiyo tuseme walimaanisha walichosema?

Kama kawaida yao , kwenye uwanja hawakuonekana ila kwenye party walikuwepo kama kawa, wazee wa NEVER MISS !!!
 
Maalim Seif sawa si kiongozi wa serikali. Wapinzani wengine ni kina nani wameenda? Mimi nilisahau kama ni siku ya uhuru, nilipoona sijaenda kazini nilifikiri ni J'mosi. Hata TV tu sijaangalia.
wewe kama mimi nilistuka asubuhi kwanini sikwenda kulinda shamba langu.nikagundua kua dogo alienda maana jana hakwenda shule.
 
Uhuru ulikuwa kwa wale waliovaa suti nyeusi,walikuja na maVX,halafu jioni kula dhifa ya Uhuru..
 
Na ndio maana hata alisusa kutoa hotuba akabaki kukagua gwaride tu Duh jamaa hii miaka 5 mbona anashughuli Pevu!
 
KWANI NINI MAANA YA siku kuu ya UHURU??
KUSHUHUDIA KIONGOZI ALIYESHINDA URAIS KWA KUCHAKACHUA AKIPIGIWA MIZINGA 21??
Ole wenu wanafiki ile mizinga itakuja kugeuka sauti za mabomu na vifaru kuwashambulia nyie.
Mumekwisha.

Afadhali mbwa koko wa porini aliye huru, kuliko mbwa wa polisi mtumwa.
 
Kwa hiyo subirini 2015, kwani kwa sasa JMK ndie anaetakiwa na wengi.

Sijui akili zako unakuwa umezikalia?? watu hapa wanajadili SIKU NYERERE alipokabidhiwa nchi mpaka watanzania watakapoweza kujitawala, we ulivyo kilaza unajadili kuhusu huyo mpuuzi wenu ambaye hana hata muda wa kusoma badget ya nchi yake.
 
KUSUSIA SHEREHE ZA UHURU NI UTOTO......... karibia kila tendo wanalofanya linazidi punguza imani ya wananchi(HASA MIMI) NADIRIKI KUSEMA MSHAURI WA CHADEMA ANAWAPOTEZA

Kila linalo isha ni dogo zaidi ya lile linalokuja-Mpoto. Endelea kusubili
 
Hivi leo si ndio siku ya uhuru wa zanzibar? maana tumekuwa tukisherehekea mapinduzi tu, uhuru je? au ndio tunaharalisha mapinduzi?
 
wa tz wameruka mkojo waka kanyaga mavi, hakuna uhuru ni unafiki mtupu, uhuru ni wa ccm kupokea nchi kutoka kwa wokoloni na sio wa tz

Bora ya mkoloni kuliko serikali ya CCM, na Tanzania haitaendela milele. lazima kuingia kwenye mfumo wa vyama vingi iwe ni dhamira ya kweli. kama CCm wanasema watatwala 100 years ijayo, unadhani watafanya vizuri wakati wanajua hakuna ushandani wowote?
 
Back
Top Bottom