Kifo cha ACT Wazalendo ni "Poor parenting"

Suphian Juma

Senior Member
Apr 2, 2019
133
546
KIFO CHA ACT WAZALENDO NI "POOR PARENTING."

ACT wazalendo ina kila sababu ya kuwa Chama Kikuu cha Upinzani Tanzania, na kuongoza idadi ya madiwani na Wabunge Chaguzi zijazo kulinganisha na CHADEMA.

Udhaifu wake mkuu ni kwenye "Parenting", iwatengeneze Vijana mapema kama CHADEMA ilivyowaibua akina Zitto, Lissu, Halima, Mnyika, Heche n.k

Siasa za ACT wazalendo ni "Siasa za muktadha", ni Siasa zinazoendana na wakati, mahitaji ya wakati, na zinazojikita kwenye "masuala" makhususi ya watu tofauti kabisa na CHADEMA ambao muda mwingi mtaji wao ni Siasa za kuzodoa dola, kufitini na kushambulia watu, kitu ambacho si hitaji la wananchi wengi kwa sasa kwani mahaba yao ni Siasa za kuunganisha watu, na kutoa majawabu mbadala ya shida zao kama ambavyo Falsafa ya 4R ya Rais Samia inavyofunda.

ACT wazalendo imefanya vema Zanzibar kwasababu ilipata ngekewa ya wafuasi wa CUF ya Hayati Maalim Seif, Swali je, Wamebaki hai akina Maalim Seif wangapi Zanzibar kuelekea 2024/2025? Je, Tanzania bara ina akina nani zaidi ya Zitto na labda Ado na Nondo? Na hata hao Ado na Nondo wanalelewa na Chama kama Taasisi kwa kiwango gani kuelekea Chaguzi zijazo? Au wanaisubiri miujiza?

ACT wazalendo itambue kusifiwa kuwa na Siasa za kisasa zinazovutia wengi haitoshi kuwa Sifa ya Chama Kikuu cha Upinzani wala kete ya kushinda Chaguzi.

Majimbo na Kata zipo je, mna wawakilishi gani, mmewaandaje na mmewawezeshaje kuleta ushindani wa kushinda Chaguzi au mnafikiri ushindi ni kutoa matamko bora Twitter na WhatsApp?

Panahitajika uwekezaji wa kimkakati wa kuwaibua, kuwainua, kuwalea na kuwasimamia kisiasa na kiuchumi vijana wenye sifa za kiuwakilishi, lasivyo Chaguzi zitafika Taasisi itabaki na mtu mmoja, Zitto Kabwe mbele ya Macho ya Wananchi, na kusababisha Chama kukosa wawakilishi na hivyo kudumaa kisiasa kwa "kujitakia".

Kama kujifunza "Parenting"; ACT wazalendo, CHADEMA na vyama vingine vya Upinzani virejee Chama chetu cha Mapinduzi CCM ambacho tuna mamia kwa maelfu ya watu wenye haiba ya Uongozi kuanzia nafasi ya Urais hadi Balozi wa nyumba kumi.

Chama cha Siasa makini chochote duniani kinachotaka kuishi umri mrefu hujikita kuandaa makumi, mamia kwa maelfu ya viongozi. Ndio maana kuna siku Twitter niliwaambia CHADEMA kama kuna kosa kubwa la kihistoria walifanya tangu kiumbwe ni kuwafukuza akina Halima Mdee, maana kufukuza ni rahisi ni siku moja tu, ila kuwatengeneza wanasiasa brands za akina Halima Mdee itachukua miongo kwa miongo.

Rais Mstaafu, "role model wangu" Mzee Kikwete alishawahi kusema "wazo halipigwi rungu", hivyo ACT wazalendo wana uhuru wa kufanyia kazi mawazo yangu au kuyapuuza.

Nimeyaandika haya baada mara kadhaa watu wengi, na hasa kipekee asubuhi ya leo kukutana na mtu fulani na kuniomba nitoe tathmini yangu kama mwanasiasa na mchambuzi wa siasa juu ya mwelekeo wa Siasa za ushindani kati ya ACT wazalendo dhidi ya CHADEMA, na hivi ndivyo nilivyomjibu.

Suphian Juma Nkuwi.
Kada- CCM
Octoba 02, 2023.
FB_IMG_1696231261805.jpg
 
Hali ya CHADEMA ingekuwa hivyo unavyojaribu kuwaaminisha watu, naamini hata usingeandika huu uzi.
Ila, kwa kuwa kuwa unatamani ACT na CCM viwe katika ubora wa CHADEMA, ndiyo maana umeitea kuiongelea ACT dhidi ya CDM.
 
Andiko zuri sana kaka 💪
Lugha iliyotumika✅
Hoja ulizotoa✅
Hadhira kusudiwa✅
Wakati wa kutoa ✅
Aina ya uwasilishaji✅
Hoja makini sana kutoka kwako,barikiwa 🙏🏼
 
Hii ni ajabu Act wazalendo kushauriwa na mccm namna ya kukifanya kiwe bora ili kuishinda misisiyemu.Ukiwa na hekima lazima udoubt na uone there is something wrong
 
Kinachoisumbua ACT ni kuwa inaipenda Zanzibar kuliko Tanganyika, mapenzi ya chama hicho yako biased ndiyo maana kamwe haitokuja kutoboa Tanganyika.

Kila siku inazungumzia mamlaka kamili ya Zanzibar, lakini haijawahi kuitetea Tanganyika kwenye huu muungano

Hata kwenye ishu ya bandari, ACT inatetea bandari isibinafsishwe ila za Tanganyika inasema zibainafsishwe tu!

Zitto akifa hicho chama kinahamia mikononi mwa Wazanzibar rasmi.
 
Wewe ni mnafiki. Ulihama ACT kisa imeingia kwenye serikali ya umoja kitaifa huko Zanzibar. Cha kishangaza wewe nawe ukahamia huko huko CCM.
 
Back
Top Bottom