CCM yapasuka? Kinana ang'atuka...

Siku zote kazi ya ofisi ya mtu kama Nape katika chama ni kule KUTIA MAFUTA PALE PANAPOONEKA KUELEKEA KUPAUKA kimaslahi katika taasisi inayompa kula.

Hivyo, mpaka hapo ukweli tumeshaupata kamili humu na kile anachokifanya Nape hapa nacho tumeshakielewa vizuri sana tu.

Hakika ni hizi funika funika za CCM ndizo zilizotufikisha hapa tulipo kama taifa na ht kupamba kisichopambika.

Kesho tu utasikia wamemlazimisha mzee wa watu kwenda Press Conference kukiokolea sura CCM. Karibu Nape, mhadhara huu ni wako tngu sasa endelea kutiririka upendavyo.
 
Niliwahi kuwashauri CCM kuharisha uchaguzi huu wa chama unaotalajiwa kufanyika ili kupisha hatua za kumaliza migogoro ndani ya chama, hawakunisikiliza. Sasa dalili za migogoro hii kukitafuna chama zinaanza kuonekana waziwazi.

................

USHAURI:

Kwa mvurugano huu wa vijana(UVCCM) na upinzani wa wazi wazi baina ya viongozi na makada wa CCM katika baadhi ya mambo ndani ya chama na serikali, ningependa kumshauri m/kiti wa CCM. Mimi ninamshauri Mwenyekiti wa CCM afuate taratibu za chama kuhairisha uchaguzi wa CCM 2012 kwa mwaka mmoja, ili kwanza kupunguza migongano hii,lengo likiwa wanachama waingie kwenye uchaguzi wakiwa kwa kiwango fulani wamoja. Endapo uchaguzi huu utafanyika katika hali hii ya "misuguano hii mikali" baina ya wanachama, huku baadhi ya viongozi wakipuuza kutatua matatizo halisi yanayokigharimu chama na kudandia matatizo ya ''kupikwa" ambayo yanazidi kukisambaratisha chama, basi Uchaguzi huo utasababisha hali ya mbaya zaidi si kwa chama pekee hata kwa serikali yenyewe.

Source>>> https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/182285-ushauri-uchaguzi-wa-ccm-2012-usogezwe-mbele.html
 
Hebu ngoja niulize!
Ina maana kikao cha CCM bado kinaendelea hadi sasa au Nape hayupo serious kwa kile alichokileta hapa?! Ameandika alichokiandika, amesepa zake huyooo! Hakujisumbua kujibu japo post moja na wla Online haonekani!!! Ni nini hii?! Yaani anaamini akiandika tu wadau watameza maandishi yake, au?! Ningekuwa na mamlaka humu jamvini, ningeondolea mbali hii thread na ikabaki ile ile aliyokuja kuikanusha otherwise aje kujibu hoja za wadau.
Hawezi ku multi task? nina uhakika sasa hivi ni mawasiliano ya hali ya juu yanaendelea ndani ya hao magamba, na vikao ili kujaribu kuona kama wanaweza kuliokoa jahazi.Kuna watakaoombwa na kupigiwa magoti,kuna watakaotishwa nk.Ila mwishowe watakuwa na majibu tu na ukweli utafahamika.Hapa ni popcorns tu kwa mwendo wa mbele.

Binafsi ninaamini Nape ndiyo mzushi,na huko alipo anajaribu kufanya "damage control".Usikute usawa huu amemvutia waya JK wanajadili,na kama hicho kipengele cha ufamilia kipo,usishangae hiyo barua ikafanyiwa mizengwe.Hapa wanaliana timing tu.
 
Wanajamvi,
Nnauye jr amekuja hapa haraka kutokana na thread iliyosema ' Kinana ang'atuka.... kuachana na siasa uchwara'.
Alichokifanya Nape ni kukubali kuwa Kinana ameng'atuka na hapo tu amethibitisha kuwa ile thread ina element za ukweli kama si ukweli kamili.

Asichokubaliana nacho ni matumizi ya neno 'kuachana na siasa uchwara'. Amenukuu maneno ya Kinana bila kutueleza yametoka katika kikao, FB au katika barua.

Pasco ameuliza, je ni kweli barua imeandikwa au ni uzushi? Nape amekimbia hataki kujibu hilo wala wapi maneno ya Kinana yanapatikana. Hadi hapo unaweza kuona namna alivyojichanganya.

Kwanini Nape amekuja kwa kasi? Jibu ni kuwa vikao vya chama vinaendelea na habari hizi kuvuja JF zinaufikia umma kwa haraka sana. Kitakachotokea ni wale wenye hati hati ndani ya chama kujipanga kabla ya kumalizika vikao.
Ni kuzuia mkakati uonaonekana kuwa una sababu maalumu. Mtu kama Kinana hahitaji kutangaza, angekuwa na option ya kutochukua fomu basi hilo tu lingetosha kumuondoa katika nafasi.

Kitendo cha Kinana kusema hayo aliyoyasema kinaashiria ujio wa jambo zito. Anaweza kuwa amefanya hivyo kwa kukusudia baada ya kutathmini hali ya chama na mustakabali, au anaweza kuwa amefanya hivyo ili ku-set tone kwa maamuzi yanayoonekana kuwa mazito na yenye madhara 'repercussions'.

Kwahiyo msibabaike sana ujio wa Nape ni katika mkakati wa 'pre-emptive strategy' hasa baada ya JF-Leak.
Nisomeni vizuri, Jumatano na Alhamisi zitakuwa siku zenye habari nyingi za kisiasa, siku zitakazoonyesha hatima ya CCM na wale waliokubali kubeba jeneza na kibao cha R.I.P.

Nasema R.I.P kwasababu damage ya chama ni kubwa sana kiasi kwamba kinachohitajika ni injini mpya na si bodi.
Hilo halitatokea katika makundi yaliyopo na kuparaganyika ni jambo la kwanza hata kama litafunikwa na maneno 'tumeingia wamoja tumotoka wamoja'. Underneath there is a big rift for the part to stand tall as it used to be.
 
Nashukuru kwa kujitokeza haraka kuweka kumbukumbu sawa katika jukwaa hili.
Mh Mbunge wangu, mimi naona ni mapema mno kumshukuru Nape kwa hili, kumbu barua ya Kinana inatambuliwa zaidi kuliko haya maneno mawili ya Nape.

Mimi ningeshauri ajibu vema maswali ya bwana Pasco ndio ashukuruwe au ashutumiwe nasi.

Mwisho kumbuka Nape nimtaalamu wa propaganda chafu, anaweza kubisha/kukanusha chocho i;limradi tu umpe jukwaa.
 
JK alisema Watanzania wana viwanda vya kuzalisha uongo, natamani angeenda mbali zaidi kuwa viwanda vyenyewe havijasajiliwa BRELA, havilipi kodi TRA na mbaya zaidi havichagui vema huduma na bidhaa zao za uongo zinazozalishwa ili kujua kama zitauzika ama zitaWATIA hasara ya mwili

kwa habari hii iliyo hapa mbele yetu, THIBITISHA kwamba ni uongo! Nape katuthibitishia ni ukweli, haya lete uthibitisho wako wa uongo
 
Kinana ni mwanasiasa mzoefu na makini. Miaka 25 ni mingi. Uamuzi wa kupumzika siasa ni wa busara na unafaa kuigwa. Nitamkumbuka kwa ushauri na nasaha zake kama mlezi wa Chama Mkoa wa DSM.

uzoefu wa siasa za kinafiki,fitina na uwongo,angekuwa mtu anayeona mbali angekwisha achana na siasa zaidi ya miaka 5!
 
Ni kuzuia mkakati uonaonekana kuwa una sababu maalumu. Mtu kama Kinana hahitaji kutangaza, angekuwa na option ya kutochukua fomu basi hilo tu lingetosha kumuondoa katika nafasi.
Hapo ndo kwenye mzizi wa fitina,there is no such a thing as "kujiuzulu kugombea",magamba bana.
 
Wanajamvi,
Nnauye jr amekuja hapa haraka kutokana na thread iliyosema ' Kinana ang'atuka.... kuachana na siasa uchwara'.
Alichokifanya Nape ni kukubali kuwa Kinana ameng'atuka na hapo tu amethibitisha kuwa ile thread ina element za ukweli kama si ukweli kamili.

Asichokubaliana nacho ni matumizi ya neno 'kuachana na siasa uchwara'. Amenukuu maneno ya Kinana bila kutueleza yametoka katika kikao, FB au katika barua.

Pasco ameuliza, je ni kweli barua imeandikwa au ni uzushi? Nape amekimbia hataki kujibu hilo wala wapi maneno ya Kinana yanapatikana. Hadi hapo unaweza kuona namna alivyojichanganya.

Kwanini Nape amekuja kwa kasi? Jibu ni kuwa vikao vya chama vinaendelea na habari hizi kuvuja JF zinaufikia umma kwa haraka sana. Kitakachotokea ni wale wenye hati hati ndani ya chama kujipanga kabla ya kumalizika vikao.
Ni kuzuia mkakati uonaonekana kuwa una sababu maalumu. Mtu kama Kinana hahitaji kutangaza, angekuwa na option ya kutochukua fomu basi hilo tu lingetosha kumuondoa katika nafasi.

Kitendo cha Kinana kusema hayo aliyoyasema kinaashiria ujio wa jambo zito. Anaweza kuwa amefanya hivyo kwa kukusudia baada ya kutathmini hali ya chama na mustakabali, au anaweza kuwa amefanya hivyo ili ku-set tone kwa maamuzi yanayoonekana kuwa mazito na yenye madhara 'repercussions'.

Kwahiyo msibabaike sana ujio wa Nape ni katika mkakati wa 'pre-emptive strategy' hasa baada ya JF-Leak.
Nisomeni vizuri, Jumatano na Alhamisi zitakuwa siku zenye habari nyingi za kisiasa, siku zitakazoonyesha hatima ya CCM na wale waliokubali kubeba jeneza na kibao cha R.I.P.

Nasema R.I.P kwasababu damage ya chama ni kubwa sana kiasi kwamba kinachohitajika ni injini mpya na si bodi.
Hilo halitatokea katika makundi yaliyopo na kuparaganyika ni jambo la kwanza hata kama litafunikwa na maneno 'tumeingia wamoja tumotoka wamoja'. Underneath there is a big rift for the part to stand tall as it used to be.

teh teh..nacheza na JF?Jf ni serious business..hata mizaha humu ndani watu wanapewa tasks ngumu kwa hilo.Hapa pasco anaonekana kapata habari nzuri sana kwa mgombea wake.Utajuaje kuwa hii habari inahusiana na hii pic, ama ndio kaitwa kajibu haraka?
Ze komedi kama si machokoraa fulani baada ya abush ndio wanajipongeza kwa kukutana tena wakiwa hai,pengine na msala walioacha ndani hauwahusu.Bongo kuna wapiga picture wana imaginations.pengine wakuu wa kaya wameziona na kuwataka vijana na wazee (watoto) warudi ndani upesi na msala unawahusu.
 
Kinana ni mwanasiasa mzoefu na makini. Miaka 25 ni mingi. Uamuzi wa kupumzika siasa ni wa busara na unafaa kuigwa. Nitamkumbuka kwa ushauri na nasaha zake kama mlezi wa Chama Mkoa wa DSM.

Endelea kumkumbuka lakini njia nzuri ya kumuenzi ni kufuata yale anayoyaamini hasa hili la kuchoshwa na Siasa uchwara ndani ya CCM. Kuna kundi kubwa la wazee wamesayaona haya, wameamua kukaa pembeni. Sidhani kama kuna siasa safi ya kushabikiwa na vijana wa aina yako ndani ya CCM.
 
Kuhusu kujiudhuru sijui kungatuka kwa kinana bila kufata la nape wala la wanaosema siasa uchwara.
Hivi Kinana amejiuzulu ama kung'atuka kitu gani?Alikuwa ana madaraka gani ndani ya chama hadi usawa huu?Msaada tutani tafadhali.
 
Kuna dhoruba inaikumba ccm mda si mrefu sasa kinana hataki kuwa sehemu ya waathirika wa dhoruba hiyo.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums

Mungu ni wa ajabu sana, ana njia nyingi za kuwanusuru waja wake zidi ya madhalimu na udhalimu wao,ata binadamu walipofanya kiburi cha kujenga mnara wa babeli aliwavuruga kila mmoja akaongea lugha yake sasa ameamishia miujiza yake kwenye ukombozi wa watanzania.
 
Kwa statement hii ya Nape,good thing JF is on "another level",na siasa uchwara haziwezi kuiaffect!
Nape Nnauye, ametishia kuwazuia waandishi wa habari watakaotangaza habari ambazo hazijathibitishwa na uongozi wa juu, kuingia ndani ya viwanja vya makao makuu ya chama hicho.
Nape akizungumza na waandishi wa habari alisema kuwa wamewaelekeza walinzi wao kutoruhusu waandishi wa chombo kilichoandika habari za barabarani kuingia ndani ya jengo hilo.
Naona atakuwa anajaribu "kuthibitisha habari hizi na uongozi wa juu",kaazi kweli kweli!
 
Mjumbe wa Almashauri kuu na kamati kuu ya CCM captain Abdulharaman kianana amejiuzulu nafasi zota alizonazo ndani ya ccm kwa madai ya kuachana na siasa uchwara.

Kinana amedai kuachana na siasa uchwara zinazoendeshwa na Nape Nnauye akishirikiana na Chilagati na january makamba.kinana amekuwa mjumbe wa NEC kwa zaidi ya miaka 22 pia amewahi kuwa waziri wa ulinzi na jeshi la kujenga taifa.ktk barua yake ya kujiuzulu kinana pia ametaja kutofurahishwa najinsi jk na familia yakea inavyoendesha chama'' chama ni taasisi hauwezi ukaendesha chama kwa kutumia familia baba , mama na mtoto ,nimefanya kazi chini ya Nyerere ,mwinyi na mkapa hatukushirikisha familia zao'' hayo ni machache yaliyomo kwenye barua ya comrade Kinana

Jumatano ndio mambo yote baada ya NEC viongozi wengi wa CCm watahama peoples powerr!! Peoples powerr

As long ni mechi nzuri kuangalia .mimi nitaangalia kwa makini.CDM wakiohold any more time CCM itakufa kabla hawaajarushiwa konde na CDM.
 
Hivi Kinana amejiuzulu ama kung'atuka kitu gani?Alikuwa ana madaraka gani ndani ya chama hadi usawa huu?Msaada tutani tafadhali.

Kavunja kamati ya kampeni rasmi.Pengine hajasema alivyokereka na kuomba kila sent kwa prince kwa kipindi chote cha kampeni.Halafu leo ndio najikuta akitakiwa jikomba NEC wakati teammates wake wakichuku nafasi NEC.
 
Kwa statement hii ya Nape,good thing JF is on "another level",na siasa uchwara haziwezi kuiaffect!
Nape Nnauye, ametishia kuwazuia waandishi wa habari watakaotangaza habari ambazo hazijathibitishwa na uongozi wa juu, kuingia ndani ya viwanja vya makao makuu ya chama hicho.
Nape akizungumza na waandishi wa habari alisema kuwa wamewaelekeza walinzi wao kutoruhusu waandishi wa chombo kilichoandika habari za barabarani kuingia ndani ya jengo hilo.
Naona atakuwa anajaribu "kuthibitisha habari hizi na uongozi wa juu",kaazi kweli kweli!
jmushi1 hawa CCM ndio wameamua kila kukicha kuongeza at least one enemy kutoka ktk list ya media.By the time wanafikia 2015,watakuwa ktk position ya CUF.

Sasa hivi they are up for something fishy with another media.
 
Back
Top Bottom