CCM yapasuka? Kinana ang'atuka...

Kwa habari zisizo rasmi wapo wengi sana wataitisha press kesho na kesho kutwa
either majina yao yamekatwa mkoani ama na halmashauri lakini watatangaza kung'atuka
na ni watu prominent. hasira zao hatujui zitaushia wapi
 
Napela, kama lengo lako ni kuleta ufafanuzi pale palipopotoshwa ingefaa ulete maneno yake yote aliyoyasema ama kuyaandika huyo Bwana mkubwa Kinana. Ukituletea hapa jamvini kitu ambacho wewe mwenyewe umekiita sehemu tu ya maneno yake, tunaanza kuhofu kwamba sehemu uliyoiacha bila kuinukuu ndiyo yenye hayo yenye kuhusu "uchwara".

Ukweli utajulikana tu ni suala la mda tu!
 
naona katosheka na wizi wa mali ya umma, huyu si yule meli yake ilikuwa inabeba meno ya tembo! Shame on you Kinana!
 
Nape kwani kila kitu mpaka usikie wewe?kwako atasema hivyo lakini unaweza ukakuta kawambia watu wengine!

Kumbuka ccm si mama wala baba yake, kwa hiyo lolote lina wezekana.ni kweli siasa uchwara zimemchosha na yule ni mtu mzima ndio maana kaamua kukuridhisha hivyo!

Sito shangaa na wewe kuachana na siasa uchwara za sisiemu na ukajiunga kwenye kilimo na ufugaji kama Babu Makamba!

Watu wa sisiemu ni wagumu kuacha kula mali za uma ukiona kaacha na kaamua kujitoa ujue kuna jambo bila Ndug kinana kachoshwa na kasikitishwa na siasa uchwara za sisiemu hivyo ameona hajiweke pembeni.
 
Mh Nape..usipende tuonesha jinsi gani ulivyo Novice au ulivyo tayari tudanganya..HEMBU TUAMBIE LUGHA GANI NZURI ZAIDI ANGEWEZA TUMIA ILI KUTUNZA DIPLOMASIA?Sioni unachopinga hapo zaidi ya kuonyesha kutoelewa bigger picture au kudanganya makusudi.
 
Mimi sio Nape na siye uliyeniuliza swali, lakini naomba nitoe ufafanuzi kidogo.
Kinana hajagombea nafasi za uongozi katika uchaguzi. Hii ni tofauti na mtu aliye madarakani anapoyaacha madaraka hayo. Madaraka ya Kinana yamemalizwa kwa mujibu wa katiba ya chama na sasa ni uchaguzi ambao angeweza kuamua kugombea au kutogombea.
Katika hali kama hiyo hakuna sababu ya kuandika barua.
Sijasema kuwa hakuna barua iliyoandikwa ila sioni umuhimu wa kuchimbachimba na kutafuta barua iwapo mtu ameamua kutogombea nafasi fulani ya uongozi.
Mkuu Ze Marco', thread ile inahusu contents za barua ya Kinana kung'atuka. Kanusho la Nape ni kauli ya Kinana, hivyo ni vitu viwili tofauti!.
Ili kanusho la Nape, liwe valid, then Nape aseme, hakuna barua, yaani hata hiyo ya uwepo wa barua ni uzushi!. Pili Kinana hajang'atuka bali hagombei!. Hivyo swali langu bado lipo, barua ipo, au haipo?, endelea kumjibia!.
P.
 
Uamuzi wa Kinana kutogombea umepokewa kwa hisia tofauti lakini kuna watu wanajaribu kupotosha ....ETI NI KUACHANA NA SIASA UCHWARA...!!!!! hii hapa chini ndio sehemu ya maneno yake binafsi juu ya uamuzi wake huu....

"SIJAGOMBEA KWAKUWA MIAKA 25 YA KUSHIRIKI KATIKA KAMATI KUU NADHANI INATOSHA NA NI VIZURI KUNG'ATUKA. NAAMINI KUNA WANACCM WENGI WAZURI WENYE SIFA NA UWEZO WA KUONGOZA CHAMA. UONGOZI NI KUPOKEZANA VIJITI NA NI WAKATI WANGU KUKABIDHI WENGINE KIJITI HIKI"


Sasa wanaosema eti siasa uchwara wanayatoa wapi........ Uzushi mwingine ni wa ajabu sana..

##nakuomba mods msiunganishe hii thread na ile ya uzushi tafadhali!

Vitu vingapi Nape mwenyewe amepindisha na kupotosha umma aw Watanzania. Atashindwa mini katika hili kufanya anavyofanya siku zone kwa manufaa anayoyajua eye na watu wengine wanaofurahia na kumwacha kujisemea anavyotaka. Hata hapa katika hili, kutokana na tabia hiyo, watu wana haki ya kutokumuamini. Lakini pia, Mtanzania yupi anayefuatilia taarifa na maarifa mbali mbali hajui kwamba Kinana hakuwa akifurahishwa na siasa uchwara za Chama Cha Mabwepande.

Lakini pia Nape tayari amekiri mwenyewe hapa kuna uamuzi wa Kinana kutogombea umetafsiriwa au kupokelewa kwa hisia tofauti, sasa kwa nini hapo hapo tafsiri za wengine anasema in upotoshaji wakati ameshakiri kuwa kuna hisia tofauti katika uamuzi huo?!

Lakini pia vipi tukisema kuwa aliyeanzisha lie topic ya awali amenukuu sehemu ya kauli ya Kinana kama ambayo tu Nape naye kanukuu sehemu nyingine ya kauli hiyo hiyo. Kwamba kila mtu inawezekana kanukuu anapotaka yeye kutokana kwa mtu huyo huyo.

Of course kitu genuine kuhoji kwenye lie topic ya awali ni kwamba kama Kinana kajiuzulu kwa nini anashiriki vikao vinavyoendelea huko Dom?

Lakini pia kwani lie kauli ya Rostam Aziz kuwa ndani ya CCM kuna siasa uchwara iliwahi kukanushwa popote na chama hicho. Kwa hiyo zipo Kama kawa. Lakini pia jana SItta si kasema tote, kuwa chama hicho kimetekwa na mafisadi. Waliomo ndani ni mateka wa ufisadi na mafisadi. Sasa wengine wanaweza kuwa wanajiepusha na hapo ambayo Akins SItta wanatusaidia kuthibitisha.
 
Mkuu Ze Marco', thread ile inahusu contents za barua ya Kinana kung'atuka. Kanusho la Nape ni kauli ya Kinana, hivyo ni vitu viwili tofauti!.
Ili kanusho la Nape, liwe valid, then Nape aseme, hakuna barua, yaani hata hiyo ya uwepo wa barua ni uzushi!. Pili Kinana hajang'atuka bali hagombei!. Hivyo swali langu bado lipo, barua ipo, au haipo?, endelea kumjibia!.
P.

Sawa mkuu, hapo namuachia Nape mwenyewe katika kuzingatia itifaki...
 
Leo tuko pamoja Elizabeth Dominic,


Hii speed ya mwanga aliyokimbia nayo Nape siyo ya CCM tunayoijua......

Labda kama alitokea kwa Mch Rwakatare kuombewa!

Sana tu Dark City
It leaves much to be desired..................hivi kweli kwa kauli hizi za rejareja za makanusho Nape anaweza zuia the inevitable? kuna mtu alisema shimo la panya alizibwi na mkate............
 
Last edited by a moderator:
Hapo umenena mkuu pasco!
Nape anatakiwa akanushe kwa kuleta barua yote ya kinana anayo ijue yeye! Au hakanushe uwepo wa barua!

Kinyume na hapo ile thread bado ina ukweli.

Mkuu Ze Marco', thread ile inahusu contents za barua ya Kinana kung'atuka. Kanusho la Nape ni kauli ya Kinana, hivyo ni vitu viwili tofauti!.
Ili kanusho la Nape, liwe valid, then Nape aseme, hakuna barua, yaani hata hiyo ya uwepo wa barua ni uzushi!. Pili Kinana hajang'atuka bali hagombei!. Hivyo swali langu bado lipo, barua ipo, au haipo?, endelea kumjibia!.
P.
 
Kila kheli mzee kinana kwa utumishi hulio tukuka nakuombea mafanikio ktk kipindi iki cha mapunziko, ukwel chama chako umekiacha ktk milima na mabonde laiti mwalim ungelikuwa hai.
 
... Mbiki Msumi tunamfahamu vizuri sana tu; baba yake alikua Jaji hapo nyuma kidogo na mdogo wake yuko njiani naye kuelekea huo huo ujajia akitokea mahakama kanda ya Arusha. Ndio, yawezekana kabisa ikawa ni BASHE KAMA KANUMBA vile vile.

Hata hivyo, mwelekeo wowote juu ya Bashe, Kinana pamoja na Rage itakua na ujumbe mzito sana nyuma yake kama ambavyo ilivyowahi kufikirika hapo nyuma kidogo.

Mzee Kinana, kama Bashe, pole sana na yaliokupata kisiasa leo upenuni mwa jumba hili linalokimbiwa kwa jina la CCM. Laiti ungalijua mapema ....


Ukweli utajulikana tu ni suala la mda tu!
 
Sio vya uongo tu vilivyopo nchini , nadhani hata vya kuzalisha ARVs bandia navyo angevitaja angekua ametusaidia sana!

magamba kwisha habari yao hata campaign manager? kwa kauli ya nape kwamba wanaoondoka ni magamba wabajivua . Je kinana ni gamba ndani ya ccm?
 
Hata Asha Rose Migiro hakufukuzwa kazi UN kwa poor performance bali muda wake wa utumishi ulikuwa umekwisha. Hao ndio CCM Uspika tukaambiwa ni zamu ya Wanawake.
 
Kuna makundi mengi sana ccm hivi sasa,halafu sasa ishakuwa kama miluzi mingi ambayo itamchanganya mbwa.

Kuna wanaojiita wapinga mafisadi,ambao wanakubaliana na mafisadi kuwa kuna mambo ya familia(yani wale waliopita bila kupingwa nk) ndani ya chama,sasa sijui hii vita yao itakapokwisha nani atakuwa msindi?wenye kutetea ufamilia wako kundi gani kati ya mafisadi vs wanaowapinga?very interesting...
 
Mh lakini ni vyema kuthibitisha ukweli zaidi nikumtakia kila la kheli ukweli na usio pingika ccm kuna milima na mabonde hakita baki salama kwa mtindo huu.
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom