CCM yapasuka? Kinana ang'atuka...

1.Kaka nape naomba kuuliza hivi ww ni katibu mkuu au mwenezi kwenye chama chetu mie huwa sielewi duties zako nahisi unaingilia hadi nafasi za watu wengine

2. Na pia vipi zile siku 90 za mafisadi ndania ya chetu.. Au ni ulmaansha miezi 90?
- sorry kwakuwa ofpoint but naomba ufafanuzi jembe
 
Nape,
Kinana anaweza kutumia maneno yoyote yale kuhakikisha kuwa haeleweki vibaya. Nia yake moyoni haiwezi kuwa reflected na maneno, ni yeye mwenyewe anafahamu kwanini ameng'atuka.
Kama ilikuwa ni kupokezana vijiti basi angetoa kijiti hicho kati ya 10-15, lakini anaposubiri robo ya karne inatia shaka sana.

Kwa kuliangalia jambo hili kisiasa, ukweli ni kuwa Kinana ameamua kuungana na wazee wengine kukaa pembeni ili kulinda legacy yao. Ni wazi kuwa chama kipo katika hali na wakati mgumu sana kisiasa na watu waliojenga heshima zao wasingependa kuwa sehemu ya 'kamati' za kuandaa maziko ya chama. Huu ni ukweli usiohitaji fikra nawe unaufahamu.

Kwa upande wa pili, inaweza kuwa amejiuzulu kugombea akijua kuwa kuna mahali patamrudisha katika kamati hiyo.
Mathalani, akipewa ukatibu mkuu basi anaingia kwa kofia hiyo. Kuna mchezo unachezwa hapa, guess what, Tanzania ya leo si ya jana. Time will tell!
 
Mbona nasikia kaamua kuachia ngazi kwa hiari kuwapisha wengine? Huko mbele kuna taflani na wengine hawataki kuwa sehemu ya historia ya yatakayotokea.

Tunachotaka ni uthibitisho wa habari, tusije tukawa tunajadili habari za vijiwezi ambazo hazijahakikiwa ukweli. Tunachotaka kuhakikishiwa ukweli wa habari hii ndio uandishi unaotakiwa, na hata kama mleta mada kakonyezwa na mshikaji wake atueleze hivyo ili tuijadili kadiri ya uzi ulivyopatikana.
 
Huko mbele ya safari the race shall be very tight...probably he doesn't want to be part of the unfolding new history....labda ameaona kweli sasa ni wakati muafaka wa kupumzika. But time will tell...
 
Naona suala la mzee kungatuka ni kweli ila Nape anasema sababu alizoziandika mtoa mada sizo
 
Nashukuru kwa kujitokeza haraka kuweka kumbukumbu sawa katika jukwaa hili.

dr f.ndungulile ni mapema sana kumshukuru Nnauye Jr kwa madai ya kuweka kumbukumbu sawa kwani hajaainisha chanzo cha hayo maneno anayodai ni ya Kinana.
Hata hivyo Kinana atakuwa amewahi kusoma alama za nyakati hataki jumba bovu lianguke nae akiwemo. Wewe tu ndio bado umeshindwa kufanya maamuzi magumu pamoja na kuzibwa mdomo na chama chako cha ccm, mbunge uliyechaguliwa na wananchi unazuiwa kufanya mikutano na wewe umeridhika kama vile mambo yako shwari!
 
Last edited by a moderator:
Utaratibu wa kupokezana vijiti CCM umeanza lini? Kangatuka huyo kaka kubali ukweli
 
Tunachotaka ni uthibitisho wa habari, tusije tukawa tunajadili habari za vijiwezi ambazo hazijahakikiwa ukweli. Tunachotaka kuhakikishiwa ukweli wa habari hii ndio uandishi unaotakiwa, na hata kama mleta mada kakonyezwa na mshikaji wake atueleze hivyo ili tuijadili kadiri ya uzi ulivyopatikana.

Ni kweli mkuu...especially kwa sisi tusio kwenye inner circle ya hizi siasa zinazoendesha nchi yetu, habari kuwa kamili bila kutiwa chumvi inatusaidia zaidi kuliko longolongo na story zisizo na tija.
 
Uamuzi mzuri wa Kinana. Kila lenye mwanzo halikosi mwisho.

Kweli! Ila nataka niamini, maneno aliyoyatoa ametumia busara na uzalendo zaidi ya kuonyesha hisia halisia ndani ya nyoyo zake Kama bado anazo!

Nape, asante kwa kutudhihirishia Yale yaliypkuwa yanatuzonga ndani mwetu! Huwezi ukafanya utawala aw Jamhuri ukawa wa kifamilia! Tanzania has never been a monarchy and shall never be! This is notwithstanding the emerging practice of politician offsprings, the kind of Napes taking over their dads roles in politics!
 
Ukweli ni kwamba Kinana hakugombea kwa sababu ameshindwa kuendana na kasi ya kuendesha chama ki majungu na kujikomba kama wanavyofanya kina Nape! Hapa swala sio kupokezana vijiti! Kijiti gani kinapokelewa mkimbizaji akiwa kachoka huku chama akiwa amekiacha ki hoi!? Hapo anae pokea anakikimbizia kijiti mochwari au Lumumba.

Ukweli utajulikana tu mbele ya safari kama jinsi tulivyo ambiwa hakuna fedha za Epa zilizoibiwa lakini baadae wenyewe wakaja kusema kuwa EPA kilinuka sasa kinatoa harufu! Time and history are the best teachers I ever had.

Sent from BlackBerry 8520 authorized by JamiiForums.
 
Kitendo cha mtu aliyeongoza kwa robo karne kukaa pembeni kinatoa fursa kwa vijana kushiriki katika uongozi. Uamuzi wa Kinana unapaswa kupongezwa na vijana wanaoitakia mema nchi yetu...
 
dr f.ndungulile ni mapema sana kumshukuru Nnauye Jr kwa madai ya kuweka kumbukumbu sawa kwani hajaainisha chanzo cha hayo maneno anayodai ni ya Kinana.
Hata hivyo Kinana atakuwa amewahi kusoma alama za nyakati hataki jumba bovu lianguke nae akiwemo. Wewe tu ndio bado umeshindwa kufanya maamuzi magumu pamoja na kuzibwa mdomo na chama chako cha ccm, mbunge uliyechaguliwa na wananchi unazuiwa kufanya mikutano na wewe umeridhika kama vile mambo yako shwari!

Mwita Maranya nitafanya na kukukaribisha. Vuta subira. Nimeanza ziara na kufanya mikutano.Ijumaa nilikuwa Kiburugwa, wiki ijayo Pemba Mnazi, Kigamboni na kata nyingine kufuata.
 
Last edited by a moderator:
Jambo moja lipo wazi.....Mzee Kinana ni mpinzani wa waziwazi wa mafisadi waliopo CCM! Tofauti ya Kinana na Sitta ni kwamba, wakati Sitta hana uwanja maalumu wa kuongelea, Mzee Kinana analinda maadili ya chama chake na hivyo kufanya harakati zake za upinzani dhidi ya mafisadi ndani ya vikao halali vya chama!!

Hapa naweza pata hisia kwamba wakati Mzee Kinana alizani watu kama akina Lowassa wangetoswa, kinyume chake inaelekea wana-shine mbaya! Nape, nafahamu ili kulinda heshima ya chama ni lazima uje hapa na kauli kama hiyo ingawaje nafahamu unafanya hivyo shingo upande......kumbuka kauli yako tamu na ya kupendeza "ukiwa mnafiki ujanani, uzeeni utakuwa mchawi....!"
 
Ile thread nyingine Nape anayoiita ni uzushi,inaelezea Kinana kujiuzulu nafasi zote ndani ya CCM, sasa sijui hilo ni sawa na kuamuwa kutokugombea?

Nape wewe unazungumzia barua ya kutokugombea ama ni ya kujiuzulu kutokana na kile wanachosema "Siasa Uchwara"?
Al sadat said:
Mjumbe wa Almashauri kuu na kamati kuu ya ccm captain Abdulharaman kianana amejiuzulu nafasi zota alizonazo ndani ya ccm kwa madai ya kuachana na siasa uchwara.
 
avatar11941_3.gif

icon1.png
Uzushi dhidi ya Kinana kutogombea unasikitisha!

Uamuzi wa Kinana kutogombea umepokewa kwa hisia tofauti lakini kuna watu wanajaribu kupotosha ....ETI NI KUACHANA NA SIASA UCHWARA...!!!!! hii hapa chini ndio sehemu ya maneno yake binafsi juu ya uamuzi wake huu....

"SIJAGOMBEA KWAKUWA MIAKA 25 YA KUSHIRIKI KATIKA KAMATI KUU NADHANI INATOSHA NA NI VIZURI KUNG'ATUKA. NAAMINI KUNA WANACCM WENGI WAZURI WENYE SIFA NA UWEZO WA KUONGOZA CHAMA. UONGOZI NI KUPOKEZANA VIJITI NA NI WAKATI WANGU KUKABIDHI WENGINE KIJITI HIKI"

Sasa wanaosema eti siasa uchwara wanayatoa wapi........ Uzushi mwingine ni wa ajabu sana..

##nakuomba mods msiunganishe hii thread na ile ya uzushi tafadhali!

:target:Kwa kauli hiyo ya Nape, najihakikishia kuijadili hii mada sasa, ndicho nilichokitaka:target:​
 
dr f.ndungulile ni mapema sana kumshukuru Nnauye Jr kwa madai ya kuweka kumbukumbu sawa kwani hajaainisha chanzo cha hayo maneno anayodai ni ya Kinana.
Hata hivyo Kinana atakuwa amewahi kusoma alama za nyakati hataki jumba bovu lianguke nae akiwemo. Wewe tu ndio bado umeshindwa kufanya maamuzi magumu pamoja na kuzibwa mdomo na chama chako cha ccm, mbunge uliyechaguliwa na wananchi unazuiwa kufanya mikutano na wewe umeridhika kama vile mambo yako shwari!

Kuna wakati tunashindwa ku appreciate professional za watu na kuishia kutowaelewa vizuri. Yule bwana ni askari haswaaa...anajua anachofanya ndio maana unaona amesimama imara dhidi ya dhoruba nyingi juu yake. Kusema kweli ni mtu anayetumia vizuri kichwa chake....Ameona yale wengine tusioyaona.Mabadiliko!
 
Nashukuru kwa kujitokeza haraka kuweka kumbukumbu sawa katika jukwaa hili.

@Dr F. Ndugulile ni mapema sana kumshukuru Nnauye Jr kwa madai ya kuweka kumbukumbu sawa kwani hajaainisha chanzo cha hayo maneno anayodai ni ya Kinana.

Back
Top Bottom