CCM yanguruma Busanda; Wapinzani chali!


Well presentes; wenye macho waone na kujifunza haya sasa kuelekea 2010
 
CCM imeshinda Busanda, hilo halina ubishi. Kwamba nilitarajia Chadema kushinda hilo nalo halina ubishi nalo lilitegemea mambo kadhaa na mazingira fulani ya kisiasa (niliyoyaanisha huko nyuma).

CCM imeshinda Ubunge na kutetea jimbo lake kiukweli na kihalisia ilistahili kushinda jimbo hilo. Hata hivyo ukiangalia vizuri utaona kuwa CCM haijashinda kushawishi mioyo ya yawatu zaidi.

Mwaka 2005, vyama vitatu vilisimamisha wagombea Busanda. CCM iliibuka kwa ushindi wa asilimia 79.2 (61,868) waliofuatia ni CUF asilimia 16.8 (13,094) na Chadema asilimia 4 (3,107). Hii ina maana kuwa wapinzani walipata jumla ya kura 16,161.

Wapiga kura waliojiandikisha ni 125886.

Hii ina maana gani?

a. Katika uchaguzi huu mdogo chama kilicho "gain" ni Chadema. Kama tukichukulia wale walioipigia Chadema mwaka 2005 ndiyo wameipigia tena mwaka huu (3107) basi kura hizi zinasema zaidi. Matokeo yanasema chadema imepata kura 22,799. Hizi kura zimetoka wapi? Kama wale wote wa CUF ndio pia wameipigia Chadema ina maana bado Chadema wangepata kura 16,161 lakini ziko 22,799!

Hii ina maana kuwa kuna kura 6638 ambazo zimetoka mahali pengine.

b. Kwa vile kura za CCM ndiyo zimepungua kutoka 61,868 hadi 29,242 ni wazi kuwa CCM haikugain. Kwa maneno mengine, chama kilichokubalika zaidi ni Chadema na si CCM. Kukubalika huko kunaonekana kwenye takwimu.


c. Nilisema huko nyuma kuwa siri ya ushindi iko kwenye kujiandikisha na wale watakaojitokeza kupiga kura. Kilichotokea Busanda ndicho pia kilichotokea Kiteto. Wakati ule nilifanya observation hii hii. CCM haishindi kwa kukubalika zaidi bali kwa watu kutojitokeza kupiga kura. Kama watu wengi wangejitokeza kupiga kura hata kufikiria asilimia 60 hivi au karibu ya sabini na ongezeko la Chadema lingefuata mtiririko wa ongezeko tuliloliona hakuna shaka hata kidogo Chadema ingeibuka na ushindi.

d. CCM inajua siri hii; wanajua kwa sababu wao ni chama kikongwe kinachojua mikakati na utaalamu wa uchaguzi. CCM haikuhitaji kushawishi watu wengi wajitokeze kupiga kura; ilihitaji kuwashawishi wana CCM kukipigia kura! NI kwa sababu hiyo basi ushindi wa CCM umetokana na wana CCM wenyewe; kama itafanyika tathmini tutaona kuwa karibu asilimia 80 ya waliopigia kura CCM watakuwa ni wana CCM au watu ambao wana mapenzi na CCM (kitu ambacho kina mantiki).

e. Wapinzani bado hawajafika kwenye kutegemea wanachama; wanategemea watu wenye kuichukia CCM; Huu ni mkakati wa kushindwa. Zile kura karibu 6000 za ziada (ukiondoa za CUF na Chadema) ni kura za wana CCM ambao hawajaridhika na hali iliyopo au watu wengine ambao na wenyewe wameona waachague vinginevyo. Binafsi ninaamini Chadema wangekuwa makini wangewekeza mtaji wao kwenye hawa.

Sijui muda wote wa kampeni Chadema imepata wanachama wangapi wapya Busanda. Sijui katika mikutano yao ya kampeni walitoa mara ngapi nafasi kwa mtu kujiunga na chama chao na kwa kiasi gani waliwaalika watu siyo tu kuichagua Chadema wakati wa uchaguzi bali kukichagua kama chama chao. Bila kuwa na base ya wanachama huwezi kushinda chaguzi za namna hii.

Hivyo, ushindi wa CCM si wa kupuuzia wala kubeza hata kidogo; ni ushindi wa mzoefu wa siasa ni ushindi wa mtaalamu wa mikakati. CCM ni chama cha kisiasa na kinaelewa majukumu na malengo yake ambayo ni kutawala. Katika hili hawana shida kutumia mbinu zozote za kisiasa kujihakikishia ushindi.

Mshindi ni mshindi tu hata kama goli lake la ushindi limekuja kwa penati! CCM inastahili pongezi zote na wapinzani hususan Chadema wanastahili pongezi kubwa zaidi kwa kuonesha kuwa wanaweza kushindana. Lakini hilo peke yake halitoshi, anayepewa tuzo ni mshindi tu, kuwa namba mbili siyo sifa ya ushindi.
 
Mie sikuwa na muda wa kupita post zote..Nilisoma za juu kwanza!

Kama ulitoa tathmini kabla ya matokeo,sasa hivi yametoka una maoni ganui?

nilitoa maoni baada ya matokeo; kwani kanzi kalishatoa taarifa tangu jana wakati nyinyi mnasubiri. Sasa kama hukuchukua muda kusoma utaniuliza kitu kile kile.
 

Good Analysis!

Unawashauri nini CHADEMA baada ya kupoteza?Nini kifanyike ili kuhakikisha wanashinda jimbo la biharamuro?

Je hauoni kuna haja ya CHADEMA kuinga mkono TLP?yaani chama kimoja cha upinzani ndiyo kisimame huko?
 
Hakuna kitu kilicho good kwenye hiyo analysis ya Mwanakijiji,
Analysis iliyojaa subjective opinions ambazo haziko supported na evidence yoyote itakuwaje good!
 

- Mkulu wangu Malundi, yamekua haya tena ya shetani badala ya siasa na demokrasia at work? Yaani kila mwananchi kuweka mawazo yake bila kujali upande wa pili sasa wote tukiwaza sawa si hata huyo shetani atakimbia mkuu?

Respect.

FMEs!
 
- Mkulu wangu Malundi, yamekua haya tena ya shetani badala ya siasa na demokrasia at work? Yaani kila mwananchi kuweka mawazo yake bila kujali upande wa pili sasa wote tukiwaza sawa si hata huyo shetani atakimbia mkuu?

Respect.

FMEs!

Hayo maneno huw wanaambiwa na wale wakosaji!wanaodhani tunawasababishia Hasara kisiasa...
 

Haya nakubaliana na wewe sasa na hawa wapinzani wafanyenini kuanzia leo ili washinde 2010?
 
Hakuna kitu kilicho good kwenye hiyo analysis ya Mwanakijiji,
Analysis iliyojaa subjective opinions ambazo haziko supported na evidence yoyote itakuwaje good!

Kwa kulinganisha takwimu za kura za 2005 na za sasa huko Busanda, ni chama gani kimekubalika zaidi kwa watu wengi zaidi?
 
wanachama wa mpira wa miguu ni tofauti na wa siasa
wanachama wa mpira wa miguu wakifungwa na timu yao ikishuka daraja hawatakiwi kuisaliti timu wanatakiwa wabaki na kuendelea kuishabikia ie uzalendo

mwanachama wa siasa hutakiwi kuwa kama wa mpira wa miguu
mwanachama wa siasa usiporidhisha na sera za chama chako unatakiwa kukihama na kutafuta mbadala
ni sahihi kwa chadema kuchukua watu wanaoichukia ccm na ndio hivyo inavyotakiwa iwe, wanachama wamechoka wanataka alternative

hata obama alipata watu ambao walikua wana vote republican all their live...
kama chadema wanaweza kuwakamata watu wanaoichukia ccm then the party is in a right direction
watu wanavyofikiria humu JF ni tofauti na watu wanavyofikiria uraini
ukitaka kuisulubisha ccm ndani ya jf ni dakika moja lakini bado utapata upinzani
ukitaka kuisulubisha ccm uraini sio mchezo, bado wa TZ upeo wao ni mdogo sana kwa hiyo mimi naona chadema wanafanya kazi ya ziada na ukizingatia siku hizi viongozi wa TLP na CUF wanasafiri na ccm sio mchezo "ccm wamegundua ukitaka kula vizuri lazima ule na mwenzako" viongozi wa upinzani wanasafiri kimya kimya
 

good analysis kuna kazi kubwa huko mbele na inahitaji akili na uvumilivu. kumbuka ni kazi ya kuwanyanganya watu tonge mdomoni. hivyo si kazi rahisi
 



Kwakweli mwananchi wa kawaida kujua faida ya kura ni kazi kubwa. Kumbuka yeye immediate need yake ni chakula cha siku hiyo na mara nyingi hawawezi ku- associate matatizo yake na mambo ya kupiga kura na viongozi for hawajawahi kuwa na experience ya kusaidiwa mambo yao binafsi. Wakati mwingine democracy is a necessary but not sufficient condition for the peoples welfare.

Inahitaji moyo wa uzalendo na upendo kwa wengine wenye uwezo wa kulink welfare na politics kuwasaidia wale ambao bado wana loyalty ya vyama vilivyoleta uhuru. Naamini watanzania wengi hawapendi kuona haya ila pia siasa za chuki na magomvi ndizo zinazorudisha watu nyuma. Hizo ni mbinu chafu za wachache wanaonufaika na huu mfumo nadhani vijana wengi hawapendi hayo na hii inanipa moyo kwamba mbeleni hii hali itakwisha na tutaamua ku agree to disagree on ideologies bila kumdhania mwenzako vibaya.

Natoa wito kwa viongozi waliopo madarakani wasaidie kukuza upinzani it is also for their well beings. Maendeleo yakipatikana uchumi ukakua haya mambo madogo madogo ya kufuatiliana fulani kala nini ka vaa nini kaenda wapi yataisha. Adui yetu mkubwa ni sisi wenyewe tukubali tumekosea tukijirekebisha hakuna wakupoteza wote tutakuwa washindi. nahapo wengi watatokea kupiga kura bila hata kuelimishwa. Extensionist claim the gud technology is the one which extends itself without extensionist. Waswahili wakasema chema chajiuza chenyewe.........
 

Hapa nimekupata vizuri Mzee Mwanakijiji
badala ya kutumia helkopta (gharama kubwa) hizi gharama zingetumika kutafuta wenyeji vijijini wenye uwezo wa kuzungumza (siasa) waku convice watu (wao kwa wao wanaelewana vizuri zaidi kuliko wazungumzaji wa kutoka "dar" wanaoongelea vitu vikubwa kama ufisadi, nk vitu ambavyo havieleweki kwa vijijini) na kutafuta vikunda mbalimbali mf. NGOs za kuhamasisha watu wapige kura.

tusidanganyane kuwa wanakijiji hawana uelewa. inategemea tunaongelea kitu gani! kwa wale wanaofuatilia kuhusu Indigineous Knowledge (IK) wanavijiji wanaulewa mkubwa sana katika kutatua matatizo yao. ila huenda wasiwe na uelewa wa mambo/ufisadi unaoongelewa kwenye vyombo vya habari (wizi wa kitaalamu) hivyo badala ya kulaumu uelewa wao tunapaswa kuwajue vizuri na tucheze nao kwa step na nyimbo zinazofanana
 
Mabadiliko ya kweli yanahitaji ushiriki wa mimi na wewe ili kuleta maendeleo endelevu,bila upinzani imara chama hiki kitaendelea kutuhadaa kwamba kinatetea maslai ya wengi.Tunajua kwa uhakika kabisa viongozi walio wengi ktk ccm wanapigania maslai yao na hawako tayari kuweka au kujenga demokrasia ya kweli na chaguzi zilizo huru na za haki.
 
Wewe nani kakuambia kuwa una BUSARA?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…