CCM wamekosea kutumia M4C kumnadi Magufuli

CCM wamekosea kutumia M4C kumnadi Magufuli

Bro Malisa, do not even waste your energy discussing This Silly misjudgement, Magamba wanajua wamekosea, but they are a desperate lot, no brainers, no ideas, no stratégies, a Silly lot indeed, tantamount to a silent admission of the superiority of brains, ideas nd strategic thinking of CDM/UKAWA, Sasa tunawapeleka chaka kuwafanya kitu mbaya; Stay tuned!!
CDM/UKAWA TUNAONGOZA, MAGAMBA YANATAWALA!!

Tehtehteh mmeshikwa kila kona, hayo mapovu mnayotokwa huwez nambia eti unafurahia ccm kuishiwa BALI ninaona maumivu makali ndani yako... M4C - MAGUFULI FOR CHANGE, upo hapo?? Mtalialia sana mwaka huu.. Tehtehteh.
 
Sioni hoja hapo , hiyo nembo , inatoa maana tofaut na chadema kwanini ulalamike acheni kukurupuka
Abbreviation ndio hutoa tofaut na sio nembo

ndio umeandika nini hiki sasa? ni afadhali ungekaa kimya kuliko kuonyesha upumbaFU wako hadharani.
 
Kwani yule jamaa anayetembea kwenye kampeni na Pombe mwenye tumbo kubwa hivi ambaye jana alisema piga ua galagaza ccm haiwezi waachia wapinzani Ikulu, Elimu yake ni darasa la ngapi vile???

Tehtehteh kwani yule jamaa aliyeuza chama kwa mafisadi papa tena kwa bei chee, Elimu yake ikoje vile??
 
Sioni hoja hapo , hiyo nembo , inatoa maana tofaut na chadema kwanini ulalamike acheni kukurupuka
Abbreviation ndio hutoa tofaut na sio nembo
hee!!! Kweli kila mtu ana uelewa wake.kuna mtu ukimwambia hii ni nyeusi ye anasema ni nyeupe.atatetea na yuko tayari hata kufa....,...NAPITA TU.
 
Jamaa ameeleza wazi ila inaonekana hutaki kuelewa, hilo nalo ni kosa sana.
Sioni hoja hapo , hiyo nembo , inatoa maana tofaut na chadema kwanini ulalamike acheni kukurupuka
Abbreviation ndio hutoa tofaut na sio nembo
 
Akili za Lumumba ni za ajabu sana,yaani hazijai hata mfuniko wa chupa ya bia.

Angalia yanavyojaribu kutetea ujinga humu!!!!,embu kaeni chini muangalie ni jinsi gani mtabadili rangi za nywele zake ziwe za kijani.
Maana mamvi rangi nyeupe za nywele zake zipo kwenye bendera ya chadema.

Mnajenga hoja nyepesi kwenye swala pana.

Hapo hakuna cha hoja nyepesi Mkuu. Kama kweli logo ni mali yenu leteni HAKIMILIKI. Vinginevyo kama mmezoea kufanya mambo kimazoea ndo ishakula kwenu hivyo.. Hao ndo ccm bana, wakongwe wa propaganda na hiyo ndo siasa in case u forgot..
 
Kabla hujaandika habar kama hii ni vema ungejiridhisha na upande wa pili(CCM) kujua kama kweli matumizi ya logo hiyo yameidhinishwa na chama au la? Otherwise kinachoendelea ni ushabiki wa mitandaoni na ccm haiwez kuwazuia watu kufanya wanachojiaikia kiushabiki..

hata kama inatengenezwa na watu wa mitandaoni, hiki ni kiashiria tosha jinsi CCM walivyochoka kufikiri.
 
Hapo hakuna cha hoja nyepesi Mkuu. Kama kweli logo ni mali yenu leteni HAKIMILIKI. Vinginevyo kama mmezoea kufanya mambo kimazoea ndo ishakula kwenu hivyo.. Hao ndo ccm bana, wakongwe wa propaganda na hiyo ndo siasa in case u forgot..

Kukosekana kwa hakimiliki hakuzuii ccm kuonekana vilaza wa kukopi.

Na haiwezi kula kwetu kama unavyoandika,ila inazidi kutupa publicity na kuwavua nguo.

If kweli ni wakongwe kama unavyofikiria,basi mwaka huu hali ishakuwa tofauti sio kawaida yao kabisaaa.
 
Tatizo la CCM imejaa mapoyoyo watupu. Ndio wanamshauri Magufuli.

Unategemea wakina Lusinde na Bulembo, wakishauri vipi chama na mgombea!
 
Unaona jinsi akili kubwa inavyo ongoza akili ndogo? Sisi wa tanzania tunajua kabisa kuwa m4c ni mali ya chadema hivyo John Pombe Magufuli alitakiwa atengeneze yakwake. Angeweza kuiita J4C au P4C au JPM4C au 4CJPM, labda tungemuelewa ila anaposema yeye ni M4C manayake anatuambia watanzania tuichague chadema. Namimi nashauri watanzania tufanye kama anavyotaka magafuli i.e tuichague chadema ili kumufikishia ujumbe kuwa somo lake alilotufundisha wakati wa kampeni tumelielewa.

Mimi najiuliza kitu kimoja yeye anaposema Magufuli for change anataka kubadilika kutoka wapi kwenda wapi kama siyo kutoka ccm kwenda chadema? unajua wazee hawa mara nyingi huwa wanafundisha kwa mifano na mafumbo kama alivyokuwa akifanya Yesu. Amejaribu kutumia njia ya kawaida akaona hatuelewi sasa ameamua kutumia mfano wa M4C kama Yesu alivyotumia mfano wa shamba la mizabibu. Yesu alikuwa akiongea mfano wa shamba la mizabibu akimaanisha watu na magufuli anatumia M4C akimaanisha tuichague chadema.

Magufuli anataka kubadilika kutoka wapi kwenda wapi kama sera anazo hubiri ndio hizohizo ambazo chama chake kimehubiri tangu mwaka 1961 hadi leo na wameshindwa kabisa kuleta matumaini ya maisha bora kwa watanzania.

Mgufuli anataka kubadilika kutoka wapi kwenda wapi kama baba wa taifa alisema ccm siyo baba yangu wala mama yangu hivyo unadhani yeye ndio atapenda ccm awe babayake au mama yake? inamaana magufuli ananguvu kuliko nyerere?

Mgufuli anataka kubadilika kutoka wapi kwenda wapi kama barabara alizotengeneza kwa kiwango kikubwa zinaharibika ndani ya miaka mitatu.


Mgufuli anataka kubadilika kutoka wapi kwenda wapi kama serikali imejaa madeni kila kona ya dunia, inawakopa hadi bibi zetu wanaolima korosho na mahindi

Mimi naona magufuli anamapenzi mema na tanzania ndiyo maana anatuambia watanzania kuwa tutumie nembo ya chadema kuitoa ccm madarakani. Kwamimi ambaye ni mtaaramu wa kuhubiri kanisani ujumbe huu wa magufuli nimeupata na kuuelewa vizuri na nitautumia kanisani kuwaeleza waumini wangu juu ya nia hii njema aliyonayo magufuli.
 
Hao wanasheria wanapotezea mahakama muda.Eti Magufuli kusema Magufuli for change tatizo! Angesema Magufuli nne Change ingekuwaje maana chadema alama yao ni m4c
 
Kesi imekufa kabla ya kuanza.mnajifunga magoli mengi wenyewe.Wala Magufuli hajaishika hiyo nembo ya watu wengi duniani
 
Tangu jana kumekuwepo na mijadala sehemu mbalimbali kuhusiana na matumizi ya logo ya M4C kwa chama cha Mzpinduzi (CCM). Wengine wakisema ni sawa lakini wengine wakisema si sawa.

Sikutaka kulizungumzia hili lakini naona kuna upotoshaji (wa makusudi) unaoendelea, hivyo nimeona nitumie uzoefu wangu ktk taaluma ya Mahusiano (Public Relations) na uelewa mdogo wa Sheria nilionao kutoa ufafanuzi juu ya jambo hili.

Lakini kabla sijaendelea nimpongeze sana mwanasheria wa CHADEMA John Mallya kwa kutoa msimamo wa Chama kuwa wataifikisha CCM mahakamani kwa kitendo cha kurudufu nembo yao.

Kwa uelewa wangu kinacholalamikiwa si logo tu, kinacholalamikiwa ni kitendo cha CCM kutumia nembo ya utambulisho ya chama kingine (Corporate Identity) ya CHADEMA, while are two oponent parties.

Muaasisi wa Taaluma ya Public Relations, Arthur Page alisema ili kutengeneza utambulisho wako kwa jamii (Corporate Identity) unahitaji kuwa alama zitakazokutambulisha.

Alama hizo ni pamoja na Nembo (Logo), Jina (brand name), Rangi (corporate colour), Mundo wa maandishi (designing) kama ilivyo Cocacola, etc.

Vyote hivi ndio vinatengeneza kinachoitwa utambulisho wa kampuni/shirika/asasi/chama etc.

Nembo ya M4C ni Corporate Identity ya Chama cha Demokrasia na maendeleo na imesajiliwa hivyo. Kwa hiyo CCM au chama kingine kutumia nembo hiyo bila ridhaa au makubaliano maalumu na CHADEMA ni kosa kisheria (Criminal Fraud).

KWANINI CCM WAMEKOSEA.

Sheria zinazolinda haki miliki Tanzania (The copyright and neighbouring Act, ya mwaka 1999 na The Trade and Service marks Act, ya mwaka 1986) pamoja na Sheria za kimataifa zinazolinda haki miliki zinataka kuwe na utouti wa utambulisho kati ya asasi moja na nyingine, bidhaa moja na nyingine, shirika moja na jingine etc.

Utofauti huo unakuwa kwenye maeneo mengi lakini kwa uchache ni kama ifuatavyo;

1. Jina/Brand name.
Jina moja haliwezi kutumiwa na asasi mbili tofauti zinazofanya kazi za kufanana. Kwa mfano Kampuni ya bia ya TBL ikizindua kinywaji kiitwacho "Burudani" kampuni ya Serengeti haipaswi kuanzisha kinywaji chenye jina kama hilo. Sheria inazuia ili kutowachanganya wateja na kulinda haki ya mwanzilishi wa hiyo "brand name".

Kwa hiyo kitendo cha CHADEMA kusajili nembo ya M4C kama "operation brand name" yake kinazuia chama kingine cha siasa kutumia jina hilo. Kwa hiyo CCM kutumia M4C ni kosa kisheria.

2. Muundo/Designing.
Muundo wa maandishi una hati miliki kisheria. Kwa mfano muundo wa neno Cocacola ulivyo ni tofauti na muundo wa neno Pepsi. Cocacola wanaandika kwa kucharaza. Hiyo ni designing yao. Pepsi hawaruhusiwi kuiga muundo huo unless kuwe na makubaliano maalumu na Cocacola.

Sasa CCM kwa ujinga wa kiwango cha "PhD" wameiga muundo wa neno M4C. Bora hata wangeandika kwa muundo mwingine, kwa mfano M-FOR-C, au m4c au namna nyingine itakayotofautisha brand name yao na ya CHADEMA. Lakini wamecopy na kupaste. Hapa haihitaji degree ya sheria kujua kuwa CCM wamekosea.

3. Rangi/Corporate colour.
Unaposajili bidhaa yako au kampuni yako ni vizuri kusajili na rangi yako ya utambulisho.

Kwa mfano hati ya usajili ya Chama cha mapinduzi inatambua rangi za kijani na njano kama rangi zao za utambulisho (corporate colour). Chadema rangi zao ni Blue, nyekundu, nyeupe na nyeusi.

Ukisajili rangi yako ya utambulisho ni kosa kisheria kutumia rangi ya mshindani wako hasa kwenye ulimwengu wa leo wa ushindani wa kimasoko wa "Oligopoly Marketing"

Simba hawaruhusiwi kuvaa jezi za Njano kwa sababu sio rangi yao ya utambulisho, vivyo hivyo Yanga kuvaa nyekundu.

Japo Sheria inatoa ruhusa kubadili rangi ikiwa unaona kuna haja ya kufanya hivyo. Yani ukiona "clients" wako au "audience" wako hawaridhiki na rangi yako unaweza kubadili kwa kufuata taratibu za kisheria. Na si rangi tu bali hata logo au muundo (design).

Ndio maana Vodacom ilianza na rangi ya Blue na nyeupe, lakini wakachange na sasa wanatumia nyekundu na nyeupe. Sheria inaruhusu kubadilisha.

Lakini CCM hawakufanya hivyo. Bado hati yao ya usajili inaonesha rangi zao za utambulisho ni Kijani na Njano, lakini leo wamekurupuka kutengeneza logo ya M4C kwa rangi ambazo si zao. CCM hawana utambulisho wa rangi nyekundu, blue, nyeupe wala nyeusi. Wamezitoa wapi?

Haihitaji elimu ya sheria kujua hawa watu wamekurupuka. Yani baba Njano, mama Kijani halafu mnazaa mtoto mwekundu au mweupe.. haya ni maajabu ya 8 ya dunia.

Haiwezekani baba awe Punda, mama awe Nyumbu halafu mnazaa mtoto Twiga?? Hakuna "cross genetics" ya aina hiyo. CCM u have proved failure.

Nisiwachoshe sana lakini kwa kifupi CCM wamekurupuka mno. Ni kukosa umakini kwa kiwango kikubwa. CCM ina wataalamu wa Sheria, ina wataalamu wa PR and Marketing, ina wataalamu wa Communication, kwanini wanafanya "Technical Mistake" ya kitoto namna hii? Hizi ndio akili za kushauriwa na kina Lusinde (standard seven) na kupuuza wataalamu. Poor u.!

Malisa GJ.

Mkuu hawo wote unaowataja sijui wanasheria, wasomi etc. Walikuwa wameonja mzigo wa 'unga' wa chama ulioingia kwa hiyo hawako vizuri upstairs kwa sasa! Maana wametupa bao hapo, ila mi niliwahi kusema magufuri ni wetu, angeachwa angehamia ukawa, wao wakampitisha, huyu ukawa damu wacha atupigie kampeni,
 
jahnuary makambakamba ni mwizi wa mitihani,aka mzee wa kudesa mwenye uzoefu mkubwa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom