CCM may lead for decades! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM may lead for decades!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kasheshe, Mar 16, 2009.

 1. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #1
  Mar 16, 2009
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Kwa mtaji huu wa kukubali kukosolewa CCM yaweza ongoza kwa miaka makumi yajayo....


  TahaririHabari zaidi!
  Waraka wa CCM uwe mfano​

  Mhariri
  Daily News; Monday,March 16, 2009 @19:14


  Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimetoa waraka maalumu kwa ajili ya kuwaonya na kuwabana viongozi na wanachama wake wanaoendesha kampeni za chinichini kinyume na ratiba ya uchaguzi.

  Hatua hiyo inapiga marufuku mgombea na kiongozi wake yeyote kuingiza wanachama wapya kwa ufadhili binafsi kwa kuwanunulia kadi au kuwalipia ada za uanachama, kwa lengo la kutaka wampigie kura.
  Hiyo inatokana na uamuzi wa chama hicho kubadilisha utaratibu wa kura za maoni kwa kupanua wigo, ambapo sasa kura hizo zitapigwa katika matawi yake badala ya utaratibu wa zamani wa wajumbe wa mkutano mkuu.

  Hii ni hatua mabayo kwa kweli itatoa viongozi wanaotakiwa badala ya zamani ambapo fedha zilitumika kwa majina tofauti tofauti na wagombea, kwa lengo la kurubuni na hatimaye kupitishwa.

  Hali hii ndiyo imefanya baadhi ya watu wanaotaka kuwania uongozi kwa tikiti ya chama hicho, kujipitisha kutafuta kuungwa mkono kwa mashinikizo mbalimbali yakiwamo ya kununuliana kadi na kulipiana ada.

  Tunaipongeza CCM kuwa imeliona hili na haikutaka kulifumbia macho na mara moja imetoa waraka, ambao utakuwa mwongozo ili kuhakikisha yale inayoyapitisha na kuyasimamia, ndiyo yanayoheshimika na kufuatwa.

  Malalamiko ya rushwa yamekuwapo siku zote wakati wa uchaguzi hali ambayo imekuwa ikiichafulia CCM jina na kuonekana kana kwamba ni chafu kupindukia na hivyo kuwapo na haja ya makusudi ya kuhakikisha kuwa haiko hivyo.

  Sasa basi hatua hii ya kutoa waraka wa kujibana yenyewe, inaonyesha kuwa inakubali kujisahihisha kwanza kwa kukiri tatizo kuwapo na kulitafutia dawa ya kudumu. Tunaviomba vyama vingine vya siasa nchini vinavyoshiriki uchaguzi na hata visivyoshiriki, kuiona hatua hii ya CCM kama mfano bora wa kuigwa katika mapambano ya rushwa na ufisadi mwingine.

  Hivyo navyo havina budi kuja na mwongozo wao kuhusu uchaguzi wa Serikali za Mitaa na hata uchaguzi mkuu mwakani, kwa sababu navyo si visafi kama ambavyo vitataka wananchi waelewe. Uchaguzi ni uchaguzi na nguvu nyingi halali na haramu hutumiwa na si kwa CCM bali kwa vyama vyote vya siasa na si tu nchini bali duniani kote, hivyo ili kujitoa kimasomaso, vyama vya upinzani navyo havina budi kuweka mambo yao wazi katika hilo.

  Kama utoaji fedha na zawadi nyingine wakati wa uchaguzi utadhibitiwa, ni wazi kuwa uchaguzi utafanyika kwa uhuru na haki na kuondoa malalamiko yasiyo ya msingi na hakika watapatikana viongozi wenye uwezo na waadilifu. Kama vyama vya upinzani vitaendelea kudhani kuwa rushwa ya uchaguzi imo ndani ya CCM peke yake, vitajidanganya na kwa upofu huo, rushwa itavitafuna vyenyewe na kujikuta vinakosa viongozi wanaostahili.
   
 2. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #2
  Mar 16, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,650
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  God forbid...........
   
 3. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #3
  Mar 16, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Siamini kama habari hiyo imo kwenye gazeti la serikali, au ni habari iliyoppo kwenye uhuru na aliyepost amekosea. Au bado tuko kwenye muongo ule wa chama na serikali kuwa kitu kimoja. Hata hivyo kuna uwezekano mkubwa huyo anayetoa kaluli hiyo kwa niaba ya chama, aliingia kwenye nafasi hiyo kwa njia anayojaribu kuikemea sasa.

  Ni njia nzuri kama watu wakipata uongozi kwa njia ya halali kuna uwezekano kuwa hata ufisadi kwenye serikali utapungua.
   
 4. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #4
  Mar 16, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Wataendelea kubaki madarakani kwa hila zifuatazo:-

  1. Katiba inayokipa upendeleo CCM na kuvinyima vyama vingine haki na usawa.
  2. Tume ya Uchaguzi inayotekeleza matakwa ya CCM na kuwahakikishia ushindi.
  3. Vyombo vya Dola vinavyolinda CCM na kuvinyanyasa vyama pinzani.
  4. Serikali inayofumbia macho utawala wa sheria na haki.
  5. Bunge linaloweza kugeuzwa kikao cha kamati ya CCM.
  6. Mahakama inayoogopa kutafsiri sheria na kufuta sheria mbovu.

  Lakini kila kinachovuma, hufikia tamati.
  Kudumu kwa CCM ni sawa na kudumu kwa umasikini Tanzania !! Watu hawatakubali kudumu kwenye umasikini milele
   
 5. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #5
  Mar 16, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,691
  Likes Received: 82,582
  Trophy Points: 280
  Hayo ndiyo mambo yatakayoifanya CCM iendelee kubaki madarakani kiharamu kwa miaka nenda miaka rudi
   
 6. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #6
  Mar 16, 2009
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145

  Je unaona strategy zozote effective kutoka kambi ya upinzani kuondoa hayo mambo haramu... au inabidi tuishie kualaamu.
   
 7. Pundamilia07

  Pundamilia07 JF-Expert Member

  #7
  Mar 17, 2009
  Joined: Oct 29, 2007
  Messages: 1,433
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Wa mbili katu havai moja
   
 8. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #8
  Mar 17, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,691
  Likes Received: 82,582
  Trophy Points: 280
  Kulaumu pekee hakutoshi maana tutalaumu miaka nenda miaka rudi lakini CCM bado watakuwa wanapeta madarakani na kukingia kifua mafisadi. Tumewashauri mara chungu nzima vyama vya upinazani kwamba wakati umefika wa kuweka ubinafsi wao na tofauti zao pembeni ili waunde chama kimoja chenye nguvu ambacho kitakuwa tayari kuchukua madaraka, hata Waziri Mkuu wa Kenya Odinga katika ziara yake ya hivi karibuni aliwashauri wapinzani kwamba kama wanataka kufanikiwa kuing'oa CCM madarakani hawana busi kuungana, lakini sikio la kufa halisikii dawa maana bado wameweka mbele maslahi yao na ubinafsi badala ya yale ya Taifa. Kwa hiyo kwa maoni yangu wapinzani inabidi na wao tuwabebeshe lawama za CCM kuendelea kuwepo madarakani. Labda watasikia vilio vyetu na kuamua kuunda chama kimoja chenye nguvu na hatimaye kuing'oa CCM madaraani.
   
 9. J

  Jamco_Za JF-Expert Member

  #9
  Mar 17, 2009
  Joined: Jul 14, 2007
  Messages: 1,315
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Hata kiundwe chama gani hakitapewa madaraka hata siku moja kwani wamejiandaa kwa nguvu zote kuendelea kuiba. lakini wanatakiwa kuchukua mfano wa nchi kama Kenya ambazo wananchi wake walichoka wakaamua kufanya kweli kwani mwenye njaa hatajali kufa hatafanya linalowezekana kuakikisha kuwa hali inabadilika.

  Amani tunayojivunia haina muda mrefu tutazalisha wakimbizi halisi badala ya wakimbizi wa kujitakia waliotokea zanzibar ndani ya miaka 10 ijayo kama hali haitabadilika na kuleta manufaa zaidi kwa wananchi walio wengi.
   
 10. J

  Jamco_Za JF-Expert Member

  #10
  Mar 17, 2009
  Joined: Jul 14, 2007
  Messages: 1,315
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  tunaogopa kusema kuwa wanchi watariot lakini kitu cha msingi ni kuwa hatuna muda mrefu kwani nchi imekuwa na matatizo mengi wakati wao wanakura rundo la pesa za wananchi.

  Ndio maana nimekuwa nikimshauri mkuu wa kaya naamini kuwa anaingia ukumbini hapa mwenyewe bila kuwatuma hakina Salva, njia sahihi ni kujiuzuru na kuitisha uchaguzi upya nina uhakika kwa wakati tulionao atashinda tu, lakini tunavyosogea mambo yanaharibika zaidi na kuleta mgogoro kwa CCM kuingia madarakani bila wizi wa kura.
   
 11. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #11
  Mar 17, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Eeeeeeeeeee Mungu we, usijaalie kabsaaaaa, ziraili -watu, hawa wakatawala miaka yote hiyo.Amin
   
 12. A

  Atanaye Senior Member

  #12
  Mar 17, 2009
  Joined: Oct 31, 2007
  Messages: 153
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Maoni yangu
  Hakuna mbaya kwa hili. Ikiwa bado upinzani unalegalega nani aongoze?
  (Sio watu bali Chama)

  So long ndani ya Chama chenyewe kuna demokrasia inayoeleweka, nafikiri Chama bado kina nguvu cha kuongoza kwa mda mrefu.

  Atanaye
   
 13. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #13
  Mar 17, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Lepidus Atanaye,
  Chama kimeshatekwa na mafisadi. Demokrasia unayozungumzia ni ile ya
  kuwalinda mafisadi. Mwulize Chenge.
   
 14. M

  Malila JF-Expert Member

  #14
  Mar 17, 2009
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Kwa mparaganyiko wa viongozi wetu wa upinzani tunazidi kuipalilia ccm.
   
 15. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #15
  Mar 17, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,566
  Likes Received: 18,532
  Trophy Points: 280
  Ni ukweli usiofichika, CCM itatawala kwa miaka mingi ijayo mpaka litimie lile neno la Baba wa Taifa lisemalo "Upinzani wa Kweli Utatoka CCM". Mwalimu aliona mbali sana na akasema wazi "Utitiri wa Vyama Haujengi Upinzani Imara".

  Kwa lugha rahisi, mpaka sasa, Tanzania hatuna chama cha upinzani, hivi vilivyopo sio vyama, ni 'mfano vyama'. Kama hakuna vyama vya upinzani, na CCM kilichokuwa Chama Dola, ndicho chama tawala, basi kitaendelea kutawala mpaka kitakapotokea chama cha upinzani kukipinga. Hivi mfano vyama vilivyopo bado vinacheza makidamakida kuganga njaa za kushibisha matumbo yao.
  Angalizo, kwa upande wa Zanzibar, CUF ni Chama cha Upinzani.
   
 16. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #16
  Mar 17, 2009
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Politics have many dynamics. What you see today can absolutely be omething else in just a month. Mimi siamini kama kweli CCM itakaa madarakani zaidi ya miaka 10 from now. Why?

  1. Mpaka sasa hatujaona mikakati yeyote ya maana ya kuiwezesha CCM kukaa madarakani muda wote huo. Hicho kilichotajwa hapo juu ilitakiwa kifanyike kabla CCM haijawa infested na rushwa iliyokithiri. At least those days muheshimiwa Kolimba aliposema CCM haina dira. Pia the no. of people who used to love CCM whole-heartedly especially vijijini wanapungua siku hadi siku.

  2. Kuna wapiga kura watakaopioga kura say mwakani wamezaliwa 1992 and therefore what they know about CCM is not the same like us the old guards who did Siasa from kindergarten to uni.

  3. Shule za kata zitasaidia mno kureplace minds za jamii into open ones.

  4. Kwa kuwa CCM sasa ni chama cha matajiri na si wakulima na wafanyakazi tena. You bet how many rich pple we have in the country.

  5. CCM have told lies and yes if you tell lie thousands times people will believe you. But wait a second!!!!!!! if you have failed to deliver clean and safe water since independence how do I believe the lie even if it is told million times?

  6. Watanzania wengi sasa hivi wanaamini CCM is something we can live and prosper without.

  7. Ngome kuu ya CCM (viijini) hawaiamini tena CCM na ahadi zake maana pembejeo zimepanda bei maradufu na bei za mazao kushuka maradufu vile vile tofauti kabisa na wanachokuwa wakikinadi kama ilani kila uchaguzi unapofika.

  8. The in-fightings zilizopo CCM and I am sure si muda mrefu kuanzia sasa kuna watu watajump-ship

  9. Serikali ya CCM imedisappoint walimu ambao ndiyo hasa wamekuwa wakitumika kuinjinia matokeo ya uchaguzi.

  10. Kwa kadri uchafu wa wafadhili na baadhi ya viongozi wa CCM unavyozidi kuanikwa haiyumkini haitaweza tena kurecruit watu safi, wenaojiheshimu na wenye intergrity katika jamii.

  Mimi binafsi naamini kabisa anaeidekeza CCM na maybe adui wa taifa hili ni the so called middle class ya bongo. hawa wengi ni educated, wana reliable income, wanaweza kupambanua mambo but they enjoy the status quo. Hawaishi kulalamika lakini hawahamasiki kama anavyosema Mkjj. Kundi hili lina influence kubwa mno katika jamii thru extended families. Lakini linashindwa kuitumia fursa hiyo kuisensitize jamii na kuhamasika pamoja nao. Imagine You have parents to take care of, wadogo zako say wanne, kuna hausigeli, shamba boy, kuna fundi na wasaidizi wake wa kagari kako sekandi hendi, kuna wale wafanyakazi wa baa unayokunywa pale mtaani kwako au memba wa kanisani kwako.Hawa ni watu kama 20 per a middle class disposal. Sasa basi kama middle class ya bongo ina watu say 500,000 wanaweza kurecruit not insurgents but wazalendo na wanaoipenda nchi yao 20 kila mmoja. Total ni 10 Million. CCM hapo itapenya wapi?????
   
 17. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #17
  Mar 17, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Mpaka sasa mimi naridhika kwa kiasi na jitihada zinazofanywa na upinzani. Upinzani umedai mabadiliko ya katiba, umeomba kuundwa kwa tume huru ya uchaguzi, umeomba kufutwa kwa sheria mbovu zinazominya fursa sawa mbele ya sheria, umelalamikia upendeleo wa vyombo vya dola, umelaani vitendo vinavyodidimiza haki n.k. Kwa ufupi kwa nchi inayohubiri amani na mshikamano, upinzani umejitutumua lakini jitihada zimekwamishwa na ubinafsi wa CCM.

  Ombi langu kwa CCM ni kuwaomba wasisahau historia ilivyo na tabia mbaya sana ya kujirudia, haki haiombwi na kama haitolewi kwa hiari ina tabia mbaya zaidi ya kupatikana kwa shari. Marehemu Nicolae Ceausescu wa Romania alikuwa akichaguliwa na asilimia kubwa ya wapiga kura wake lakini hao hao wananchi walipochoka na utawala wa kiimla uliokosa mwelekeo na kuanza kudai haki, nguvu za dola hazikuweza kuwazuia kumwondoa madarakani kwa nguvu na kumsulubu.

  CCM lazima kitambue kuwa ndicho kisiki kinachokwamisha utawala bora na hali hii haiwezi kudumu milele. CCM kama ina nia njema na nchi hii ni lazima ishike hatamu katika harakati za kuandika katiba inayokidhi matakwa ya demokrasia ya vyama vingi. CCM kama chama kinachounda serikali ni bidi ionyeshe kwa vitendo kuwa ipo kwa maslahi ya wananchi wote na si kikundi cha watu.

  Ikifanya haya CCM siyo tu itakuwa imeikwamua nchi yetu na machafuko ambayo yanaweza kutokea bali itaonyesha kukomaa kisiasa. Lakini isipoitikia wito huu CCM ijitayarishe kuvuna kile ambacho waliolewa madaraka huvuna wananchi wanapochoka na utawala wa kilaghai. Narudia ombi langu kwa CCM kuwa wakati wa kusimamia haya mabadiliko ni sasa na kuzidi kujivuta vuta ni kuhatarisha amani.
  Mwenye macho na aone, mwenye masikio na asikie ili tuweze kujenga taifa la amani ya kweli.
   
 18. M

  Mama JF-Expert Member

  #18
  Mar 17, 2009
  Joined: Mar 24, 2008
  Messages: 2,858
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 0
  Maneno matupu hayavunji mfupa!
   
 19. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #19
  Mar 17, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Ni kweli - kwa sasa bado ni maneno matupu... Kaburu De clerk wa Afrika Kusini aliwahi kusema hivyo hivyo. Hata tarumbeta tu ziliwahi kuporomosha ukuta wa Babylon. Kumbuka wimbo wa marehemu Salum Abdallah....Hayawi, hayawi sasa yamekuwa. Oneni wenyewe.............
   
 20. Recta

  Recta JF-Expert Member

  #20
  Mar 17, 2009
  Joined: Dec 8, 2006
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  CCM inatakiwa kujua kuwa, endapo upinzani ukishinda uchaguzi kwa Katiba iliyopo sasa, itakuwa vigumu kwao pia kushinda katika chaguzi zinazofuata (same way as Upinzani wa sasa). Katiba yetu inabidi ibadilike kwa manufaa yetu sote.

  Siku za karibuni tumeona wanasiasa wakongwe (wastaafu) waliokuwa na uwezo wakufanya mabadiliko haya muhimu wakilalamikia utendaji wa serikali. Walipokuwa madarakani, na wenye nguvu za kufanya mabadiliko hawakuona umuhimu wa kubadili Katiba. Sasa wanajidai kuona mapungufu yaliyopo. Mapungufu mengi yaliyopo kwenye utendaji wa serikali yanatokana na Katiba isiyotosha. Si ajabu baadae, wakaongezeka viongozi hao wenye lawama tele kuhusiana na Katiba. Huwa inanishangaza sana kuona wale wale waliokuwa wakisema Katiba iko sawa na haina mapungufu, wakilalamika baada ya kutoka madarakani. Ni usaliti, uzandiki na unafiki mkubwa kwa viongozi wetu hawa.
   
Loading...