Mikael Aweda
JF-Expert Member
- Dec 17, 2010
- 2,973
- 3,901
Kwa mtu yo yote mwenye ufahamu wa kawaida anajua kuwa, Nyoka akijivua gamba hawi Chura au Mjusi, kama anasuma wala sumu yake haipungui makali. Sana sana anajipanga kutenda yale yale ya siku zote kwa kasi zaidi.Habadili chakula, wala habidili tabia, umri wa kuishi au kitu chochote. Ni yule yule Nyoka hata jina lake halibadiliki. Kilichobadilika ni ngozi tu imekuwa nzuri zaidi, mpya zaidi inayovutia.
CCM wamebadilisha sura za secretariet, wamebadili pia baadhi ya wajumbe wa kamati kuu. Hivi kumweka mkama nafasi ya makamba kunaleta nafuu gani kwa watazania? Hawa wote walikuwa ni viongozi wa CCM na Serikali yake kabla ya uteuzi wa jana. Mkama alikuwa katibu wa wizara ya afya miaka kadhaa akikumbwa na tuhuma kibao zilizohusu dawa ya ukimwi. Magazeti yaliandika sana tu. Chiligati alikuwa waziri wa ardhi. Hakufanya lolote zaidi ya kuharibu na kurudisha nyuma kazi nzuri aliyoanzisha magufuli katika wizara ile. Je, kubadili secretariet inawafaidije watanzania? Au itawasaidiaje CCM? Ina punguzaje mikataba ya feki kama IPTL. Je, itaibuka na kauli ya kutokulipa Downs? Itatoa tamko la kuridhia mabadiliko makubwa ktk mswada wa mabadiliko ya katiba yanayopigiwa kelele kila kona wakati mkiti wake ni Rais JK aliyeuleta mswada huo? Au kumtosa Fisadi mkubwa kuliko wote RA kwenye CC wakati mfanyakazi wake wa zamani/Swahiba wake ni waziri wa Nishati na Madini (Ngeleja) kwa kupigiwa debe na RA mwenyewe kunaleta jipya gani?
HII ni danganya toto, tatizo la CCM ni la kimfumo, halibadiliswi kwa kubadili sura za watedaji.
My take,
Maisha bora hayawezi kuletwa na Chama kile kile, chenye sera zile zile kikiongozwa na Kikwete yule yule aliyeleta ombwe la uongozi ktk nchi yetu, eti kwa kubadili nafasi za baadhi ya viongozi na kuwa hadaa wananchi kuwa kimejivua gamba CCM kingali na sumu ile ile ya Ufisadi